
Gazeti INJILI Kwenye Internet
-

http://www.munishi.com
Tel.
254-722-602445 E-mail:
munishi@munishi.com

Waki ametibua maji.
Sioni yakitulia karibuni.Kibaki atakuwa wa kwanza kwenye ndege inayoelekea
kwenye mahakama ya kimataifa.Katika kipindi cha uongozi wake alichochea
cheche za kikabila zilizopelekea hali ya kisiasa Kenya kuzidi kuegemea
misingi ya kikabila.Mbaya kuliko yote ni kukiuka MoU ambayo alikubaliana
na viongozi wenzake. Alipoingia madarakani siyo tu alikiuka MoU, bali
aliwatimua serikalini wale walioonekana kuuliza kulikoni. Yote hayo
ndiyo yaliyozaa upinzani uliojulikana kama ODM. Uchaguzi ulifanyika
huku kura za maoni zikionesha ODM ni maarufu na watashinda uchaguzi
kwa kishindo. Kibaki anajua alifanyaje ikawa ilivyokuwa. Wakenya walihisi
kuibiwa haki yao ya kupiga kura. Hasira yao na ya wale waliotaka kubaki
madarakani kwa gharama yeyote, ilipelekea watu zaidi ya 2000 kupoteza
maisha yao.Jamii ya kimataifa iliingilia kati na kumlazimisha Kibaki
kugawa madaraka kati kati. Kichwa upande akakubali. Asijue ameingia
kwenye mtego wa Amerika. Ofisi ya waziri mkuu ililazimishiwa kwenye
katiba ya Kenya. Japo wanaoigharamia ni Amerika, sasa wanataka mapendekezo
ya tume ya Waki kutekelezwa. Walioorodheshwa kwenye bahasha ya siri
aliyokabithiwa Kofi Annan, lazima washitakiwe kwenye mahakama ya kimataifa.
Hayo ni kwa mujibu wa Amerika, japo baadhi ya wabunge Kenya wameanza
kuimwagia maji baridi ripoti hiyo. Je itapoa? Hilo ndilo swali la
wengi. Inaonekana Marekani wamepania kuwachukulia hatua wote waliohusika
kusababisha ghasia za kisiasa Kenya.Haishangazi kuona watu wa kabila
fulani Kenya hawafurahii sana Obama kushinda uchaguzi wa Amerika.
Wanauona huo kama mwisho wao.Mungu ibariki Kenya.Je Marekani wana
haki gani kumkamata KIBAKI na kumfurusha kwenye mahakama ya kimataifa?
Wanadai wao ni wanademokrasia halisi. Mbona na wao walikuwa wakiunga
mkono ODM na inadaiwa walikuwa wakiwamwagia pesa za kampeni? Hilo
siyo kosa kwani PNU nao walikuwa wakiungwa mkono na kupewa pesa nyingi
kutoka CHINA.Hata hilo siyo kosa kwa mtizamo wa wengi. Kwangu hayo
ni makosa makubwa. Na kama tume ya waki haikuyaangalia hayo, basi
wanaopaswa kushitakiwa watabaki na wanyonge watasulubiwa badala yao.
Haki na uhuru wa uchaguzi ni pale wananchi wanaporuhusiwa kuchagua
bila kushawishiwa kipesa wala kutapeliwa na MEDIA zilizonunuliwa.
Huwezi kutumia nafasi yako kama rais wa Jamhuri ya Kenya kuvuruga
uchaguzi, Halafu utumie nafasi hiyo kuunda tume ya kuchunguza yaliyojiri
baada ya uchaguzi kutoa matokeo yenye utata, kisha utegemee matokeo
ya tume yatakupendelea na kuyafunika makosa yako. Kwamba tume ya waki
ilimtaja KIBAKI kama kiongozi aliyevuruga siasa za Kenya na kupelekea
wakenya kuuana kwa misingi ya kikabila, hilo ndilo ambalo wengi tunalipongeza.
Kazi ya rais ni kulinda katiba ambayo ndiyo mhimili wa nchi. Haki
za kisiasa hupatikana wakati sheria kulingana na katiba zinapofuatwa.Rais
akiikiuka katiba, atumie vyombo vya dola kubaki madarakani kwa gharama
yeyote, Anategemea nani afuate katiba? Kila mtu itakuwa mguu niponye,
wengine itakuwa pesa niponye, na kwa wanasiasa itakuwa majeshi binafsi
niponye.Ilikuwa hivyo Kenya wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi.Mbaya
zaidi hata vyombo vya dola ambavyo hupaswa kuwalinda wananchi wote,
navyo vilijikuta vikiegemea upande wa amiri jeshi mkuu ambaye alikuwa
KIBAKI kwa wakati huo. Ndiyo maana tunasema kwa ujasiri kwamba, kama
kweli haki itaonekana kutendeka, basi bahasha nyingine yenye majina
ya KIBAKI, WAHARIRI WA MEDIA KARIBU ZOTE KENYA lazima apewe Annan.
Vinginevyo jamii ya kimataifa ijitayarishe tena, kwani Kenya inaweza
kurudi ilipokuwa na mambo yakawa mabaya zaidi.Mungu apishe mbali.
Hayo ni maombi yetu.Tena bahasha ya tatu lazima iwe na majina ya AMERIKA
na CHINA kwa kosa la kuvipatia vyama vya kisiasa pesa za kufanya kampeni
za uchaguzi.Watakaoshitakiwa lazima wawe wengi ndipo haki ionekane
kutendeka. Kama mtumishi wa Mungu, kusameheana ndiyo njia muafaka
kwa Kenya.Pendekezo langu ni katiba ibadilishwe iwaruhusu wananchi
wote kugombea uongozi bila kuwa wanachama wa vyama vya kisiasa. Pia
katiba iwazuie watu kutumia pesa zao binafsi kufanyia kampeni.Halafu
katiba ishurutishe Media kuwaangazia wagombea wote sawa.Kama kulipwa,
vyombo vya habari vilipwe kiwango sawa na serikali.Katiba tena ipige
marufuku AMERIKA na CHINA kuvipa vyama vya kisiasa au watu binafsi
pesa kwa lengo la kufanyia kampeni.Hayo yakifanyika, Mzee au kijana
wa KIBERA au KILELESHWA, atagombea kiti chochote popote Kenya na atachaguliwa
kwa misingi ya uwezo wake kuongoza na siyo vinginevyo.Wanahabari watakuwa
na matumbo makubwa siyo kwa sababu wamehongwa na wanasiasa, bali wamelipwa
kulingana na ujuzi wa kufanya kazi zao sawa na maadili ya taaluma
yao.Waimbaji wa INJILI wataacha kutunga nyimbo za kuwasifu wanasiasa
na watatunga nyimbo za kumsifu Mungu na kueneza injili. Naona nilikuwa
nasahau bahasha ya nne. Hii inatakiwa iwe na majina ya wasanii pamoja
na wanariadha wote waliotumiwa na wanasiasa kuwagawa wakenya katika
misingi ya kikabila.Sasa si mnaona? kama kushitakiana, kila mtu atashitakiwa
Kenya. Jela zote zitajaa waandishi wa habari, Polisi, maofisa wa tume
ya uchaguzi, Rais Kibaki na rais mstaafu MOI, Wanasiasa karibu wote,Waimbaji
wa nyimbo za injili pamoja na wanariadha. Je tuna magereza yenye uwezo
wa kubeba watu wote hawa? Msururu bado ni mrefu. Hata balozi wa AMERIKA
Kenya atakuwemo.Je mtampeleka KAMITI au SHIMO la TEWA? Kwao jela ni
sawa na hoteli ya kifahari. Kuna jamaa nimemsahau. Nafikiri hata WAKI
alisahau kumweka kwenye bahasha.RAILA AMOLLO ODINGA. Hivi kweli hakuchangia
kwa lolote kuifikisha Kenya ilipokuwa wakati wa ghasia za baada ya
uchaguzi? RUTO je? UHURU KENYATTA? Niache nisije nikataja mhariri
wa KBC na NTV waache kucheza nyimbo zangu.Lakini CITIZEN na KAMEME
hawakuwatetea wakikuyu kwa hali na mali? Je K24? KTN siogopi kuwataja
maana hata hawachezagi nyimbo zangu. Hawa walikuwa ODM damu.Jeff Koinange
sijui awekwe bahasha gani. Kelele zake zilikuwa zikiishia Nairobi
pekee. Kama K24 ingekuwa nchi nzima, Basi JEFF KOINANGE alipaswa kuwa
kwenye ile bahasha ya kwanza ya WAKI. Mnaona? majina ni mengi. Na
bado mtasikia mengi.Basi tuache tusameheane yaishe. Lakini nani mwenye
uwezo wa kunyamazisha ripoti ya WAKI? Ni Kibaki? Ama RAILA? Au ni
BUNGE? Pengine MAHAKAMA? Au tuseme maandamano ya halaiki. Yanaweza
kweli kusimamisha ripoti ya waki isitekelezwe? Au ni Amerika? Pengine
CHINA. Nani hasa mwenye uwezo wa kuzima pima joto hii??? Hicho ndicho
kitendawili kigumu. Mwandishi ni mwimbaji wa nyimbo za injili Faustin
Munishi.Sijui naye atakuwa kwenye bahasha gani?
VIDEO
2/3/4/5/6/7/8/9/10/11/12/13/14/15/
Tangaza
Biashara yako Hapa
Kwamba uko hapa, maelfu ya wengine
duniani wako hapa. Tatizo siyo kuwa na Web Site, ila swali ni wangapi
wanaoifahamu na kuitembelea? www.munishi.com sasa inatembelewa na
watu zaidi ya elfu mia nane kwa mwezi, na wengi wao wakiwa kutoka
Afrika mashariki na kati. Ni kweli Internet haijafanyika kuwa njia
kuu ya mawasiliano kwa wengi, lakini tunaelekea hapo. Tofauti na kutangaza
kwenye gazeti ambalo kesho litafungia nyama, Bora uigundue njia hii
ya kuweka tangazo lako hapa na litakaa kwa muda mrefu mpaka lisomwe
na kila mtu. Bei zetu ni sawa na bure. Tuma picha na maelezo kwa munishi@munishi.com

http://munishi.com
Send
photo and information to munishi@munishi.com

Delmonte Thika Kenya

NAKUMATT Kenya. Mabingwa wa kuuza kila kitu. Ukitaka kanda za nyimbo
za injili, utazipata NAKUMATT






Kasanga Music Store
Click the picture for www.coexistkenya.org