Ukurasa wa mbele
Gazeti la injili
Nyimbo za Munishi
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail
Tuma SMS duniani
Sema nami
Sikiliza waongo
Twende kanisani
Gazeti INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com
Or fmunishi@hotmail.com

Wanasiasa Ni Wezi

 

Wanasiasa ni wezi wanaotaka walindwe na sheria, ileile waliyoivunja wakiingia madarakani. Waliingia isivyo halali, wanataka watolewe kihalali. Walipitia dirishani, wanataka kutokea mlangoni. Hawaoni haya kuitumia sheria wasiyoitii iwasaidie kuwaweka kizuizini wote wanaowataka watoke madarakani kama walivyoingia.

Wanasahau sheria ni Msumeno unaokata kuwili. Wanataka sheria iwazuie wengine wasiibe, lakini waibe wao. Mwisho wao umefika, wametuibia vya kutosha. Sasa tunataka mapinduzi ya kuwatoa wezi kama walivyoingia. Ikiwa waliingilia dirishani wakiwa wembamba, watatokea hapo hapo baada ya kunenepa kwa mali za wizi.

Wananchi tumeanza mapambano ambayo hayatanyamazishwa na mtutu wa bunduki, bali haki kwa kila binadamu itakapotendeka, ndipo vita yetu itakoma. Wanatumia sheria walizozitunga wenyewe wakashindwa kuzitii, sisi tutatumia sheria za Mungu atupaye uwezo wa kuzitii. Kinyume na sheria za wanadamu zilizo na upungufu, sheria za Mungu ni kamili. Yeye hana upendeleo kwa mtu awaye yote.

Mungu alisema tuzitii mamlaka, lakini zile tu zinazotoka kwake. Torati na manabii wote walikuwa kinyume na mamlaka dhalimu, sioni kwa nini sisi tunaohubiri Injili ya Yesu Mwokozi tukubaliane na udhalimu huu.

Yesu mwenyewe aliwaita wanasiasa mbweha sioni sababu ya sisi kuwaita waheshimiwa. Wanaheshimiwa kwa nini? Eti walianzisha taifa? Mungu ndio mwanzo wa kila kitu. Eti walitutoa katika minyororo ya wakoloni? Ni nini ikiwa walipotutoa minyororo walitufunga ya kwao? Wanasema walitujengea vituo vya afya? Mbona havina dawa? na zile zilizoko mwananchi hawezi kumudu gharama zake? Mbaya zaidi wao wenyewe hawatibiwi huko.

Lakini Mungu hana upendeleo, kwani anahakikisha kuwa wanasiasa wanapokwenda ngambo wakiwa moto kutafuta huduma nzuri za kiafya, wanarudi wakiwa baridi pamoja na juhudi zote za kujaribu kuyaokoa maisha yao. Na wananchi walioachwa na zahanati ambazo hazina dawa, Mungu anahakikisha kuwa chochote watakachokitumia kama dawa kinawatibu na wanapona kabisa, ili Mungu abaki kuwa Mungu, na wanasiasa wabaki kuwa wanadamu waongo.

Kuna uvumi kuwa siasa duniani zinaendeshwa na makundi ya watu waovu ambao hutegemea mapato haramu kutoka katika biashara ya madawa ya kulevya, pamoja na magendo ya kila aina. Ni makundi hayo ndiyo yanayoamua nani awe kiongozi wapi ili mradi maslahi yao haramu yalindwe. Wanatumia mabilioni ya pesa kushinikiza chaguzi zote duniani. Wanaoshinda uchaguzi siyo wale wanaopendwa na wananchi wa nchi husika, bali ni wale ambao sera zao zinalinda maslahi ya majambazi hao wa kimataifa.

CCM chama kinachotawala Tanzania kwa sasa, siyo kwamba kinapendwa na umma wa Watanzania, bali ni chama cha majambazi wa Tanzania kilichofadhiliwa na wenzao wa kimataifa ili kulinda maslahi yao. Ndio maana tunasema kwa ujasiri kuwa siasa ni uongo na dunia haifai kuongozwa kisiasa. Dunia ni ya Mungu, na inafaa kuongozwa kidini. Na huu ndio wakati unaofaa kufanya mageuzi hayo.

Wanasiasa pamoja na waandishi wa habari wanaojiita Third Estate, wameshirikiana kuifikisha dunia mahali ilipo. Sasa ni wakati wetu watumishi wa Mungu au kama tunavyojulikana First Estate, kuiokoa dunia isiangamie.

Ameandika Munishi Faustin

 
| http://munishi.netfirms.com |
 
<<Back  |  Home |  Gazeti La Injili | Injili2 | Nyimbo Za Munishi | Next >>