![]() ![]() |
![]() |
|
|
Gazeti
INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com Or fmunishi@hotmail.com "Nisaidieni Nioe"-WACIAMA
Majina yake ni Jeff Njiraine Macharia. Maarufu kwa jina la Waciama, kanda iliyovuma Kenya nzima. Maprojuza wajanja walitajirika na kanda yake, lakini yeye bado yuko kijiweni. Projuza wake alitajirika mpaka akaongeza wake wakawa watano, na Jeff hata mke mmoja ameshindwa kuoa. Hakuzaliwa Moranga, pengine ndiyo sababu hana ujanja wa Kikikuyu. Alizaliwa Narok, na ukimuona ana tabia za kimasai kuliko zile za kabila lake Kikuyu. Alikulia na kusomea Narok, na kimasai anakijua kuliko Kikuyu.Akiongea na gazeti la INJILI Jeff alisema ameamua kutunga wimbo kwa jina "NISAIDIENI NIOE" Bila kuongeza chumvi nawapa nafasi ya kusoma maneno ya wimbo wake mpya. mimi ulinigusa nikaamua kuandika STORY yake, na wewe utakugusa umsaidie aoe.
NISAIDIENI NIOE Nimejitahidi bila mafanikio, kuifanikisha mipango yangu ya kuoa. Msichana nimemuona mzuri wa kunifaa. Pesa zinanipiga chenga, na miaka hainingoji. Nimekumbuka nina ndugu, tuliozaliwa pamoja. Siyo kwa mwili na nyama, bali kwa roho wa Mungu. Mimi Jeff Njiraine, nisaidieni nioe. Hata kama hujaokoka, usisite kunisaidia. Ni jambo la kijamii, Naomba msaada wako. Sitaki ya kifahari, ni harusi ya kawaida. Sanduku kumi za soda, zatosha kuwa vinywaji. Gunia moja la mchele, latosha kuwa vyakula. Ngombe wawili wa kimo, watosha kwa kitoweo. Mimi Jeff Njiraine Nisaidieni nioe. Nimechoka na ukapela, kukaa bila ubavu. Usingizi wa shida shida, baridi kali usiku. Hata nikiwa Mombasa, bado baridi ni kali. Joto la huko mwambao, haliupambi usingizi. Laiti angalikuweko, kiumbe nimpendaye. Usingizi ungenoga, hata bila blanketi. Mimi Jeff Njiraine, nisaidieni nioe. Bila suti sitojali, ikipatikana nitavaa. Na kandambili ni sawa, kama hakuna viatu. Mkokoteni ni sawa, mkikatalia mabenzi. Mradi nibebe kiumbe, niende naye nyumbani. Ya nyumbani nachieni, sitaki mnisaidie. Nitajaribu kila njia, natumai nitaweza. Hapo sitowasumbua, niachieni mwenyewe. Mimi Jeff Njiraine Nisaidieni nioe. Nisiwachoshe wapendwa, kwa mengi yangu maneno. Machache niliyosema, naomba mnielewe. Ukiguswa kusaidia, niandikie barua. Ya umeme ni haraka, itanikuta mapema. jeffwaciama@ yahoo.com hiyo ni anwani yangu. Ningewapa 072 lakini bado sijaipata. Hata 0733 nazisikia kwa watu. Mimi Jeff Njiraine Nisaidieni nioe. Mwandishi ni mwinjilisti na mwimbaji wa nimbo za INJILI Faustin Munishi. |
||||||||||||
|
|
|
|