Ukurasa wa mbele
Gazeti la injili
Nyimbo za Munishi
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail
Tuma SMS duniani
Sema nami
Sikiliza waongo
Twende kanisani
Gazeti INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com
Or fmunishi@hotmail.com

Ukimwi Unaua Jihadhari: Asema KENEDY

 

Kenedy Ochieng picha ya mwaka 1999 kushoto, na nyingine ya mwaka 2002 March

Kama kuna kitu wanachokiogopa wanadamu kwa wakati huu ni UKIMWI. Wachache tu ndio wanaothubutu kujadili gonjwa hili hatari.Kwa Kenedy ochieng siyo kwamba ana ujasiri wa kujadili kuhusu ukimwi, bali yeye mwenyewe anakiri kuugua ugonjwa huo.


Kenedy Ochieng 26

Msikie Mwenyewe asemavyo. "Niliugua bila kujua naugua nini, nikalazwa Kenyata Hospital na baada ya kupimwa damu nilikutwa na virusi vya ukimwi. Madaktari walianza kunishauri kila siku jambo lililonifanya niwaulize nilikuwa naugua nini. Walinituma kwa wanataaluma ya kushauri watu na kwa mwezi mmoja nilikuwa nashauriwa tu bila kuambiwa nina maradhi gani."

Alieleza Kenedy Ochieng ambaye ukimuona hana tofauti na vijana wengine wanaokata mitaa ya Nairobi. Anaonekana mwenye afya mchangamfu, furaha tele. Nini siri ya yeye kuwa hivyo wakati anaugua ugonjwa ambao wengi hawapendi kuusikia?

Aliendelea na kulielezea gazeti la injili alipozitembelea ofisi zetu RIVER ROAD tarehe 27. 2. 2002. "Ilifika siku ya siku wakati mmoja kati ya madaktari aliponiuliza kama ningependa kujua hali yangu ya kiafya. Nilipomjibu ndiyo, alimwaga maneno mazito kwenye masikio yangu, ambayo uzito wake niliusikia mwili mzima. Ni maneno matano KENEDY UNA VIRUSI VYA UKIMWI. Kwangu ilikuwa ni kama hukumu ya kifo. lakini ushauri niliokuwa nikiupata ulinisaidia kuubeba uzito uliokuwa kwenye yale maneno matano." waliendelea kunishauri kwamba kuwa na virusi vya ukimwi siyo mwisho wa maisha. Itategemea mgonjwa atakavyoishi baada ya kujua kwamba yeye ni mgonjwa. waliniambia kwamba nikifuata maelekezo yao na nisikate tamaa ya maisha , naweza kuishi maisha marefu hata miaka 50 baada ya kuugua. Nilijua ni faraja tu, na hawakuniruhusu kutoka hospitalini mpaka walipohakikisha kuwa wamenishauri vya kutosha ili nisijiue kwa kuogopa kuishi na ukimwi.


Kenedy Ochieng

"Lakini wakati wote huo mimi binafsi nilijiuliza ni nini maisha baada ya kufa? " Nikajiuliza nitakuwa wapi baada ya maisha haya yanayotaka kukatishwa na virusi vya ukimwi? Ndipo nilipoamua kuwatafuta wahubiri wanihubirie nitengeneze maisha yangu na Mungu muumba wangu. Niliwapata wahubiri wakaniombea na nikampa bwana yesu maisha yangu. Nikatubu dhambi zangu zote na kuomba msamaha kwa Mungu na wanadamu wenzangu. Nimeamua kutangaza hadharani kwamba nina virusi vya ukimwi, na bado nina matumaini makubwa kwamba Mungu anaweza kuibadili hali yangu kiafya, lakini asipofanya hivyo niko tayari kuihama dunia hii na kwenda kuishi na Yesu milele. " Ndiyo maana nina furaha kila siku ninayopewa kuishi duniani kwani kwangu kila siku ninayoiona tangu niambiwe kwamba nina virusi ni nyongeza tu.

Alipoulizwa nini mipango yake ya baadaye, alianza kwa kusema. "Sina FUTURE kabisa duniani. Sina mpango wa kuoa na kulea watoto.Lakini nina jukumu zito la kuwalea ndugu zangu wadogo ambao nao wananitegemea mimi kwani wazazi wangu wote waliaga dunia mwaka 1994. Kibarua nilichokuwa nikifanya bandarini kiliota miguu baada ya mimi kuwa naugua mara kwa mara. Sasa naishi kwa misaada ya watu kanisani mwangu NEW LIFE SDA CHURCH Kayole. Daktari alinishauri kula vizuri, lakini umasikini ndio unaotuua haraka sisi ambao tuna virusi ya ukimwi. Alisema tusile vyakula vilivyokaangwa na mafuta na badala yake tule vyakula halisi kutoka shambani kama vile mboga za majani na matunda kwa wingi.CHIPSI na kila kilichokaangwa na mafuta mengi Daktari alinishauri nijiepushe navyo. Lakini ukosefu wa pesa unanifanya nile CHIPSI ambazo ndio uwezo wa pesa kwa siku hiyo.Shilingi 30 najipatia chipsi sahani moja na siku hiyo inapita. Siku nyingine nakosa kabisa pesa na inabidi nilale njaa. Siulaumu umasikini kabisa, lakini kama siyo Mungu ningekuwa nimekufa kitambo. Pia daktari alinishauri ninywe maji yaliyochemshwa kila mara kuepuka kuambukizwa magonjwa kama TAIFOID kwani mwili wangu hauna nguvu za kupambana na magonjwa. Najitahidi kuyafuata masharti ya daktari lakini wakati mwingine STOVU yangu inakosa mafuta na inabidi ninywe maji ambayo hayajachemshwa. Nimeamua kujitokeza hadharani ili yeyote popote anisaidie. Kwa siku chache nilizoruhusiwa kuwa chini ya jua, nisaidieni kwa hali na mali.Kwa nini mje kuninunulia sanduku la bei ghali kuulaza mwili wangu wakati mimi siko hapo? Ya nini mikutano mingi ya kupanga mazishi yangu na mimi niko kwa Yesu wakati huo? Nisaidienio sasa.


Ochieng Kenedy

Alimaliza Kenedy Ochieng ambaye anaweza kupatikana katika E-Mail kenbicco@yahoo.com au simu ya mama anayemsaidia kwa sasa Bi Petronila Njeri 072519995 Muombe huyo mama uzungumze na Kenedy ochieng.

Na mwandishi wa Injili Munishi.

Miezi minne baadaye Kennedy aaga Dunia
Tunasikitika kwamba Kenedy ametuacha na kwenda kupumzika alikokujua zaidi yetu sisi. Alifariki mwezi wa sita tarehe 15 mwaka 2002. Alijiandaa vizuri kwa safari hiyo kuliko wengi wetu. Na tunaweza kumwambia "Nenda Kennedy Nenda" Aliacha mausia kwa maandishi, akiwashukuru wote walioweza kumsaidia baada ya kusoma habari zake kwenye Internet. Amewaacha ndugu zake wawili ambao walimtegemea kwani wazazi wote waliaga dunia.

Endelea kututembelea hapa kwa habari zaidi.

 

 
| http://munishi.netfirms.com |
 
<<Back  |  Home |  Gazeti La Injili | Injili2 | Nyimbo Za Munishi | Next >>