Ukurasa wa mbele
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail

 



Gazeti la INJILI
Kwenye Internet

http://www.munishi.com

Tel. 254722602445 E-mail: munishi@munishi.com Or
info@munishi.com
 

Wanajeshi wako kambini, CCM na polisi wanakula nchi


Hawa wote ni waandishi wa habari. Wanajivuna kwamba walisomea uandishi wakati wa ukoloni. Wanawaita waandishi chipukizi "MACHINGA" Taipreta ziliwaumiza mikono, wanaona vigumu kuwaita wale wanaotumia kompyuta waandishi. Sio kosa lao walifundishwa hivyo. Wamepitwa na wakati bila wao kujua. ni watumwa kimawazo na hawajui.

Mmoja wao alinukuliwa na gazeti la "RAI" akisema kwamba waandishi habari siku hizi hawawezi kulinganishwa na enzi zao. Anasahau kwamba alipojaribu kumkosoa Mkapa, alitishiwa kuhamishwa nchini na kupelekwa kwao Rwanda. Tangu wakati huo aliufunga mdomo asije akahamishwa. Jenerali Ulimwengu alijali maslahi yake zaidi kuliko kuusimamia ukweli.Hiyo ndiyo aina ya waandishi wa nyakati za Ulimwengu. Vibaraka wa kulinda maslahi fulani. Hakuna walichokiamini bali walitumika kama bomba la kupitishia mawazo ya Nyerere. Kama mwandishi msomi anatakiwa kuwa wa aina ya kina Ulimwengu na Mkapa, basi hawa wa sasa ni afadhali. Wananusa, wanapapasa, wanaona kisha wanasikia, na wanasema hisia zao. Kwangu hawa ndio waandishi hata kama hawana shahada ya chuo kikuu. Ndio maana hata siku moja hawakuwahi kuandika kuhusu mateso wanayopata wanajeshi kambini au vitani. Ukimya wao umewafanya wanajeshi waendelee kuteseka huku wanasiasa na Polisi pamoja na waandishi wa habari aina ya Mkapa na Ulimwengu wakiendelea kuila nchi kiulaini.

Wakuu wa polisi mikoa walipokutana na Mwanasiasa Karume kupongezwa kwa kazi nzuri waliyoifanya Zanzibari mwaka 2000 na kutakiwa wafanye vivyo hivyo mwaka ujao

Umewahi kujiuliza kwa nini wanajeshi hawasikiki kwenye vyombo vya habari? Je hawana maswahibu yao na Serikali au chama kinachotawala? Wananchi wanapoteswa na kuuawa na Serikali iliyo madarakani wanajeshi hawawezi kufanya chochote? Je kazi ya wanajeshi ni kulinda mipaka yetu ili wanasiasa na polisi waendelee kuwanyanyasa wananchi ndani ya nchi yao? Ikiwa wanalinda mipaka ili adui asiingie, mbona wasitulinde na adui aliye ndani ambaye anafanya madhara kuliko adui kutoka nje?Wengine wanasema wanajeshi wataua kuliko CCM.Siyo kweli kwamba wanajeshi wakichukua madaraka wataua. Tena siyo lazima waue.

Hawa ni baadhi ya wakuu wa polisi wa mikoa Inasemekana wao na wanasiasa lao ni moja
Polisi wanaamrishwa kuua kila kukicha kulinda maslahi ya wanasiasa.Mjini Arusha Polisi wamemweka Mchungaji Nnko KIZUIZINI. Hawezi kusafiri nje ya Mkoa wa Arusha, Lazima aripoti polisi mara tatu kwa wiki, Haruhusiwi kuwasiliana kwa njia yeyote ile iwe simu au barua, Haruhusiwi kuwa na simu, Polisi wanaweza kuingia kwake wakati wowote, Wanamfuata kila aendako akijua au bila kujua. Mchungaji amenyimwa karibu haki zote za kibinadamu, Kisa ni kwamba aliilalamikia serikali ya CCM. Wanadai alitoa malalamiko yake kuihusu serikali katika GTV chombo cha habari kinachomilikiwa na mchungaji Faustin Munishi. Je kuna kosa gani kwa mchungaji kufanya hivyo?

Mchungaji Emmanuel Nnko Ambaye yuko kizuizini mjini Arusha. Haruhusiwi kusafiri nje ya mkoa wa Arusha. Serikali Tanzania walivunja kanisa lao, Uinjilisti mikoani ambao ndio uliokuwa umebakia kwa mchungaji Nnko, nao amefungiwa. Bora kufunguliwa mashitaka kuliko kuwekwa kuzuizini. Alisema mchungaji Nnko kwa rafiki yake aliyetuletea habari hizi.

Ilidaiwa kwamba mnamo mwezi wa saba mwaka 2004 Mchungaji Nnko alilalamika kuhusu kitendo cha serikali kuvunja kanisa lao katika maeneo ya Kaloleni Arusha.Pamoja na kuvunjiwa kanisa, pia serikali ilibeba mali za kanisa hilo na kuzihifadhi katika bohari la manispaa ya Arusha.Inakisiwa kwamba mali zilizobebwa ni za thamani ya zaidi ya milioni kumi za kitanzania.CCM walitarajia kwamba mchungaji Nnko angelinyamazia suala hilo. Kilichowaumiza zaidi ni pale Mchungaji Nnko alipokwenda Nairobi na kuituhumu serikali kwenye Gospel Television, ambao nao waliweka malalamiko yake kwenye mikanda ya video yaani VCD na kuanza kuzisambaza kwenye maduka ya nyimbo za injili Tanzania.Kilichofuatia ni serikali kupiga marufuku hizo kanda na kuamuru wahusika wakamatwe. Iwe walimaanisha au ilikuwa kuwatisha watanzania waogope kuzinunua kanda hizo, Yaliyofuatia kutoka hapo ni polisi kupewa amri ya kuwatesa, kuwanyima haki za kibinadamu wachungaji waliohusika katika kutengeneza mikanda hiyo. Mchungaji Nnko alikamatwa alipojisalimisha POLISI, na kwa sababu hakuwa na kosa linalostahili kufunguliwa mashitaka, Polisi waliamua kumtesa kisiri kwa kumpa adhabu ya kuripoti kituoni mara tatu kwa wiki. Huo ndio unyanyasaji ambao tunaulaani kwa nguvu zetu zote. Pamoja na kwamba suala zima la mchungaji Nnko tumekwisha liwasilisha kwa Mungu, Siyo vibaya kuyangojea majibu ya maombi yetu. Mungu anaweza kutumia chochote kujibu maombi yetu, na hatuwezi kushangaa akilitumia jeshi kutuondolea kero za CCM.

Wanajeshi silaha walizo nazo ni mali yetu wananchi. Ikibidi lazima wazitumie kutulinda na wanasiasa wanaotunyima haki zetu za kimsingi. Jeshi linatakiwa liwe na sauti inayowatetea wananchi. Na sauti hiyo inatakiwa isikike kwa nguvu, hasa wakati huu tunapoelekea uchaguzi mkuu. Jeshi linatakiwa kuhakikisha kwamba uchaguzi ni huru na haki. Tume ya uchaguzi huteuliwa na wanasiasa, kwa hiyo siyo huru. Tunataka tume ya uchaguzi iwe ni jeshi. Iihakikishe kwamba CCM haitumii pesa walizojikusanyia kwa miaka arobaini kuvidumaza vyama vya upinzani. Nasema lazima wanajeshi wetu waamke kutoka usingizi wa miaka mingi. Wasingoje amri ya kuvamia nchi fulani kutoka kwa wanasiasa, bali wao wanatakiwa kuwa chombo huru kinacholinda maslahi ya wananchi kutoka kwa wanasiasa. Kazi ya wanajeshi ni kulinda siyo kuua.

Hawa wote ni viongozi wa vyama vya upinzani, na hakuna siku waliwahi kuwataja wanajeshi kama uvumbuzi wa matatizo ya kisiasa Tanzania. Na wao wakiingia madarakani, sera zao kuhusu wanajeshi zitakuwa zile zile za miaka nenda miaka rudi.

Yaani Wanajeshi wakae kambini wakingojea amri kutoka kwao. Nimeshauri mara nyingi KATIBA ya nchi yetu irekebishwe. Wengi hawanielewi. Siyo lazima wanajeshi wawe kimya hata kwa mambo ambayo wanaweza kuyakemea. Tunataka wawe huru kutoa mawazo yao kuhusu jambo lolote nchini. Wakati mtu kama LIPUMBA anaposema kwamba CCM inavuruga uchaguzi wa mitaa, Anategemea nani amsaidie? MAHAKAMA? Hiyo ni chombo cha CCM. Ni hapo ndipo wataalamu kutoka jeshini wanatakiwa wachunguze malalamiko ya LIPUMBA na wakigundua kwamba chama tawala kinacheza rafu, wakikemee. Mtikila naye amenukuliwa akilalamika kwamba CCM imewanjima wapinzani RUZUKU ndio maana vyama vingi vya upinzani havifurukuti mikoani. Yanasikika kama malalamiko ya swala anayetaka simba ampe pesa za kujiimarisha awe na uwezo kama simba. Mnategemea jibu gani zuri kutoka kwa simba? Lazima kuwepo na mwenye uwezo kuliko simba na swala nchini. Na malalamiko yanapotokea yachunguzwe bila kuupendele upande wowote. Kwangu mimi mwenye uwezo kuliko simba na swala ni Jeshi. AMKENI. TUNAWAHITAJI SASA KULIKO BAADAYE
.

Salim Ahmed Salim Kushoto, na Jakaya Kikwete
CCM wanapanga kumsimamisha Salim awe mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao. Wanadai yeye pekee ndiye mwenye "Pasonalite" ya kuamuru Majeshi yetu na Yatamsikia. Ila Jakaya Kikwete naye hajaacha hamu yake ya kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho. wagombea wanavyozidi kujitokeza CCM ndio upinzani unapojitokeza kwenye chama hicho na unaweza kukigawa vipande vipande.

SUMAYE ATINGISHA KIBERITI CCM Waziri mkuu tayari ameanza kasheshe zake za kutaka kuwania urais pindi Mkapa atakapomaliza muda wake. Wengi ndani ya CCM hawalifurahii hilo, ndiyo maana wameanza kumtaka ajiuzulu wathifa wake wa uwaziri mkuu, ndipo atangaze msimamo wake huo. Naye amekataa na kusema wakati umefika wa CCM kuwa na demokrasia ya kweli. Sasa ngoma iko hapo. Nasikia kuna wengi wanaomuunga mkono waziri mkuu, na hatua hiyo inampa Mkapa kukosa usingizi.Cheo cha waziri mkuu kiko katika katiba yetu ya sasa. Hatuwezi kukiondoa bila kuibadili katiba. Kwa hiyo mjadala huu utakuwa na maana zaidi pale tutakapojadili suala la kuirekebisha katiba. Ni mengi ya kurekebishwa katika mfumo mzima wa uongozi Tanzania. Mkapa naye kwa upande mwingine anataka kumweka mtu atakayelinda madhambi yake hasa ya kuwaua waislamu wasio na hatia Zanzibar.


Makamu wa Rais Dr.Ali Mohammed Shein akitoa hotuba huku wakuu wa chuo kikuu Dar wakimsikiliza. Urais anautaka lakini anaogopa kusema hadharani. Kisa hata yeye anaiogopa CCM.Wanaogopana wenyewe. Chama cha majambazi washirikina, wenye vikosi vya mauaji, watakosaje kuogopana? Ukijifanya kimbelembele, sumu kwenye kinasa sauti inatosha kukuletea shinikizo la Moyo na madaktari wakiifanyia uchunguzi maiti yako ikutwe ulifariki kwa ugonjwa wa Moyo. Ni kama viongozi CCM wana haki ya kuogopana. Lakini mpaka lini? Hayo ndiyo maswali yaliyotinga kwenye kichwa cha mkuu wa chuo aliyeketi balozi Paul Bomani.

Siyo Waziri mkuu pekee anayetamani kugombea urais kwa tiketi ya CCM, bali hata makamu wa Rais anataka kuwa RAIS. Kama siyo kubanwa, tungesikia mengi kutoka CCM. Lakini maji ukiyazuia sana, halafu yajikusanye pamoja, yakipata upenyo, nguvu yake haizuiliki tena. CCM wanakataa kuruhusu wagombea binafsi kwa sababu ya wingu zito lililotanda katika chama hicho. Kwa sasa hakuna Nyerere wa kuwakingia kifua watu kama Mkapa. Kila mtu lwake. Mkapa hata akipenda hawezi kuushawishi umma wa watanzania umchague kiongozi ampendaye. Wala asijaribu kufanya hivyo. Watanzania tunayajua madhara aliyotuletea Nyerere pale alipomkingia kifua Mkapa. Alituambia ni kiongozi mzuri tumchague, kumbe ni muuaji na mwizi. Nani angeweza kuamini kwamba Mkapa angeweza kuamuru polisi waue watanzania zaidi ya sabini Zanzibar kwa sababu za kisiasa? Hata Nyerere asingeamini hilo wakati anampigia debe Mkapa. Mwanadamu anaweza kubadilika ushangae. Hasa mwanadamu anapokunywa mvinyo iitwayo madaraka, akianza kulewa hakuna ovu litakalomshinda kufanya. Kwa Nyerere Mkapa alikuwa mtoto mtiifu kuliko Salim Ahmed Salim ambaye watanzania wengi walidhani Nyerere angempendekeza huyo. Madudu aliyofanya Mkapa, yatamfanya Nyerere arudi kaburini, hata kama Mungu angeamua kumfufua leo. Aibu ingemfanya Nyerere akatae muujiza wa Mungu kumrudisha duniani tena kuendelea kuishi. Ndiyo maana tunapendekeza KATIBA ya nchi ibadilishwe ili kila raia anayefikiri anaweza kuongoza Tanzania, aseme hivyo, na watanzania wawe ndio pekee wanaoweza kumkubali au kumkataa.Hakuna sababu ya mtu au makundi ya watu, chama cha kisiasa au cha kidini, kuwa na uwezo wa kumzuia anayetaka kuwania urais.

Karata ya udini ndani ya CCM ndiyo inayowafanya wasiwe na jinsi ila kumchagua mgombea Mwislamu.Waislamu ndani ya chama hicho wanadai kwamba sasa ni zamu yao. Ukizingatia kwamba Zanzibar wana usongo na chama hicho baada ya waislamu zaidi ya sabini kuuawa mwaka 2000, CCM wanaweza kufikiri kwamba kumteua mwislamu mwenzao, kutapooza joto la kisiasa Zanzibari. Hapo ndipo watakapojidanganya. Watanzania wote bila kujali itikadi zao kidini, wanataka mabadiliko.

Wamegundua kwamba haijalishi rais ni wa dini gani, akiwa anatoka CCM hawategemei chochote kipya. Sera bado zitakuwa ni zile zile za kuwaua wanaojaribu kupinga sera za chama hicho hadharani.Kiu ya wananchi ni nani atakayewakomboa kutoka minyororo ya CCM? Wanachotaka ni UKOMBOZI. Ndio maana tunasema lazima katiba ibadilishwe ili iruhusu wagombea binafsi. Kila Mtanzania anayefikiri kwamba anaweza kuwa rais aruhusiwe kuuza sera zake kwa wananchi, na wao ndio wawe waamuzi wa nani atakaewaongoza. Inashangaza kuwasikia watu fulani wakisema fulani hafai kuwa rais kabla mtu huyo hajajieleza kwa wananchi wapiga kura. Wewe ni nani unayemzuia mwananchi wa Tanzania kukutana na wananchi wenzake ajieleze kwa hao? Utata uko hapo.CCM wanafikiri wana uwezo wa kutuchagulia kiongozi nasi tumkubali bila kuuliza swali. Ilikuwa hivyo wakati wa Mwinyi na Mkapa, Hatutaki makosa hayo yarudiwe.

Makosa aliyofanya Nyerere ni kupanga uongozi kwa misingi ya kidini. Alipojifanya amejiengua, alimteua Al Haj Hassan Mwinyi. Baada yake akamleta William Mkapa.

Nyerere alituchagulia Mwinyi ili atutawale akitumia kivuli cha Mwinyi. Mambo yalipogeuka, Pale mwinyi alipojaribu kuongoza aonavyo vyema, Nyerere alimsuta Mwinyi hadharani. Hiyo haikutosha, Bado Nyerere huyo huyo akatuchagulia Mkapa. Ndoto yake ya kuwatawala watanzania akitumia kivuli cha mtoto wake mtiifu Mkapa,ikakatizwa na kifo chake. Mkapa kwa sababu hakuwahi kuota kuwa rais, na aliyemweka kifo kimemwita mapema, Mtoto mtiifu aliyumba kidogo, japo watafiti wanasema aliyumba sana. Bila kujua la kufanya, alianza sera za kukusanya kodi, ambazo wengi walizitafsiri kama wizi. Baadaye akaanza kuyabinafsisha mashirika na mengine akayauza kwa wazungu wenye pesa, Ambao jina la kitaalamu wanajulikana kama wawekezaji. Watanzania wengi waliliona hilo kama kuiuza nchi. Ndio maana Mkapa baada ya miaka kumi anaondoka na jina jipya. MWIZI na MUUZA NCHI. Nyerere aliondoka na jina jipya la MZEE HAAMBILIKI, wakati Mwinyi aliondoka na jina la MZEE RUKSA. Sina sababu ya kukuambia nani aliondoka na jina zuri. Hapo jaza mwenyewe.

Wana kila sababu ya kufanya hivyo. Wanasema Salim ana "pasonalite" ya kuwa amiri jeshi mkuu mtarajiwa. Hatuna ugomvi na uamuzi wao ikiwa tu wataruhusu wapinzani wawe huru kufanya mipango yao ili na wao waweze kumteua yule wanaefikiria kwamba anaweza kuwa amiri jeshi mkuu. Mpaka lini Jeshi litatishwa na "pasonalite" Wakati umefika kwa wanajeshi kusema kwamba hawajali mtu ana "pasonalite" gani, Mradi tu amechaguliwa na wananchi katika uchaguzi huru huyo anafaa. NI matumaini yangu kwamba Jeshi letu Tanzania litahakikisha kwamba hilo linatendeka katika uchaguzi mkuu unaokuja. Ikiwa Katiba haiwaruhusu kufanya hivyo, basi uchaguzi usimamishwe, hadi katiba irekebishwe irwaruhusu wanajeshi kuhusika katika kuyasimamia mambo ya kisiasa nchini.


Chadema wamefikiri. Lakini wanajeshi ambao hawasikiki wala kuonekana kwenye TV ni vigumu kujiuza kwa muda mfupi kwa wananchi wakubalike.Isitoshe wanayemwandaa ni mwanajeshi mstaafu.Ninachozungumza hapa ni kuhusu wanajeshi wanataaluma walioko kazini sasa. Silaha tulizowanunulia wasingoje mpaka nchi jirani itushambulie, bali wazitumie kutulinda na maadui wa ndani. CCM ni adui mkubwa wa wananchi Tanzania na hawezi kutolewa kwa njia za kawaida. Ila wakijua kwamba jeshi liko tayari kuchukua madaraka kama watacheza rafu, nadahani watajirekebisha kama sio kuacha mbinu chafu za kisiasa moja kwa moja.



Wachungaji kama KAKOBE na MTIKILA wamefanya kazi kubwa kuikemea CCM. Lakini nani asiyejua kwamba huwezi kuikemea CCM ukaishi salama Tanzania?
Kama hawatakusakama kwa kodi za ajabu ajabu, basi wanaweza hata kukuwekea sumu ya kukuua polepole. Askofu Kakobe alipowakemea CCM mwaka 2000, aliandamwa kila kona mpaka akainua mikono.Inasemekana kwamba CCM walitaka kulisambaratisha kanisa lake, na nani ajuae? Hata KAKOBE haonekani akiwa na afya nzuri kwa sasa. Pengine ni tunguri za CCM Huyu hapa siyo Kakobe yule wa mwaka 2000. Anaonekana amechoka, uzee usio wa kawaida unamnyemelea, kifupi anaonekana mgojnwa. CCM wanaweza kujisifu kwa kuwanyamazisha wapinzani wake kwa nguvu zote, Lakini hakuna lisilo na mwisho. Siku ya kufa NYANI miti yote huteleza. Haijalishi umaarufu wa nyani kuparamia miti, lakini iko siku miti yote huteleza na nyani hubamiza chini kwa kishindo na kufa.Iko siku CCM itakufa.Tunaomba siku hiyo ifike haraka.


Mchungaji DR Rwakatare Yeye na CCM wako sambamba.
Usishangae kwa nini biashara zake zinashamiri kila kukicha. Ni fundisho kwamba ukitaka kufanikiwa Tanzania lazima uwe "mpambe" wa CCM. Lakini mafanikio yanayokingiwa kifua na chama tawala, huyeyuka mara chama hicho kinapoachia madaraka. Mama Getrude Rwakatare aombe CCM watawale milele.Siyo kosa kuwa mwanachama wa chama ukipendacho cha siasa, lakini kwangu msemo kwamba adui wa adui yangu ni rafiki yangu, unatimia. CCM ni adui wa watanzania wengi. Kwa hiyo yeyote atakayekuwa adui wa CCM lazima awe rafiki wa watanzania walio wengi. Ndiyo. Ni haki ya kila mtanzania
kuwa mwanachama wa chama halali cha kisiasa, lakini CCM siyo chama halali. Tulijikuta Tanzania tuna CCM bila kuichagua. Kwa kuwa sasa ni haki ya watanzania kuchagua chama wakipendacho, CCM hawatuachi tufanye hivyo. Wanadai wao ni baba na mama wa Taifa. Sawa. Lakini baba mwizi, muuaji, mkorofi, mtoto gani atakayejivunia baba wa hivyo? Ni kweli watoto hawana uhuru wa kuchagua wazazi, Lakini sivyo kwa vyama vya kisiasa. Katiba yetu "kinadharia"inaruhusu watanzania wawe huru kuchagua chama chochote cha kisiasa, Tena wanaweza kuchagua kutokuwa wanachama wa chama chochote. Kimatendo CCM hairuhusu hilo litokee.Wanatumia mbinu zote halali na haramu kuhakikisha kwamba watanzania wanabaki na CCM ya kulazimishiwa kwa namna moja au ile nyingine. Hilo ndilo linalotuumiza na kutufanya tutumie silaha pekee tuliyo nayo. Yaani KALAMU na bongo ZETU. Mungu tusaidie ili tuweze kufanikiwa kuitoa CCM madarakani. Pesa na dhahabu hatuna, lakini tulicho nacho ndicho tunachowapa watanzania. Kwa jina la Yesu, CCM washindwe PEPO MBAYA. Ishindwe.

Mkapa miaka kumi Tanzania anaondoka bila mafanikio ya maana. Hakupaswa kuwa Rais ukilinganisha uwezo wake kiuongozi na ule wa Salim Ahmed Salim. Nyerere aliujua uwezo wa Salim, na ndio maana hakupenda awe rais. Alimpendekeza Mkapa kwa sababu alikuwa MR. "YES SIR" Kwa asili Mkapa si mbunifu. Ndio maana miaka kumi inakatika na hajabuni chochote kipya Tanzania. Anaondoka kama alivyoingia. Alipoingia alikuwa hajulikani, na anaondoka akiwa hajulikani.Nyerere aliyemkingia kifua na kumpigia debe sasa hayuko. Madaraka aliyokunywa yakamlevya mpaka akaanza kuwaua raia wa Tanzania waliosema kwamba hawaitaki CCM, sasa atavuliwa.Aliowauzia nchi wanawezamgeuka kwa kigezo kwamba walimlipa yakaisha. Waliokuwa wakimdanganya kwamba ni waaminifu kwake atapatwa ugonjwa wa moyo watakapomgeuka wote. Pengine atajenga makumbusho ya Mkapa, na ndani aweke mifupa ya waislamu zaidi ya sabini aliowaua Zanzibar. Au ajenge nyumba chini ya daraja la Rufiji awe akiishi huko. Sioni maisha baada ya Mkapa kuvuliwa urais wenye madaraka mengi ambayo CCM hawataki yapunguzwe na katiba mpya. Wakifikiri ni kwa faida yao, kumbe ni kwa hasara yao. Ukijua ni miaka kumi, kwa nini uwe na madaraka makubwa karibu ya Mungu kwa miaka kumi pekee? Miaka mingine ya maisha yako utaishije ukiwa huna madaraka hayo? Maswali hayo Nyerere hakujiuliza na ndiyo maana maisha nje ya madaraka yaliishia Kaburini. Tena yeye (Nyerere alihadhirika zaidi kwani madaraka yalimlevya kwa muda mrefu kuliko Mwinyi na Mkapa.Tuombe Mungu iwe Mkapa alikuwa hajalewa madaraka chakari. Wachunguzi wa kisiasa wanasema kwamba Mkapa aliitawala Tanzania kibabe tu. Hakuwa na uwezo wa kutetea hoja, bali alilazimishia hoja akitumia nguvu za dola. Ole wake.Waandishi wa habari sijui kama watamkaribisha kwenye meza za habari, kwani alipoingia ikulu aliwaona hawafai. Aliwadharau, wengine alifungia kazi zao, Pengine watakaomkaribisha ni wauza madini ambao walifanya biashara ya kuiuza nchi pamoja. Je umma wa watanzania utamsamehe aendelee kula pesa alizowaibia? Tunasubiri tuone. Huku mifupa ikisagana, na uzee ukimnyemelea, hakuna kilichobaki kwa Mkapa kusheherekea. Atakuwa mtu mpweke sana. Madaraka ya hivyo mara nyingine ni mateso. Pole Mkapa.

Mwanzo wa mwisho wenu

Farijianeni, lakini huu ndio mwanzo wa mwisho wenu. Tunataka mawazo mapya. Muungano tutaujadili. ukitufaa sawa. Tukiona haufai, tutauvunjilia mbali. Na hapo hatuhitaji maoni ya Chissano wala Mkapa.


Muungano uliwafaa na unaendelea kuwafaa hawa. Sisi lazima tuujadili. tuutupilie mbali.
Mkapa anajipigia debe aagwe kwa heshima huku akijua wazi kwamba alifanya makosa mengi sana katika uongozi wake. Serikali ya Mkapa Tanzania inaamini kwamba Munishi na nyimbo zake ni mwanzo wa kuvurugika kwa amani Tanzania. Kinyume chake ndio sahihi. Amani ilivurugika pale Mkapa alipowaamuru Polisi wawaue Wazanzibari zaidi ya 70 kwa sababu za kisiasa. Majeshi Tanzania walikasirishwa sana na jambo hilo,na walikuwa tayari kuipindua serikali ya Mkapa. Munishi akaimba wimbo "MPENDE ADUI YAKO", Mkapa badala ajue kwamba wimbo huo ulikuwa ukimsaidia yeye ili serikali yake isipinduliwe na kisha afunguliwe mashitaka ya kuwaua raia wasio na hatia, Aliupiga marufuku wimbo huo na kuamuru polisi wamsake Munishi. Iko siku Mkapa atamkumbuka Munishi. Ngoja kipindi chake cha urais kimalizike, na tunaomba kimalizike salama, halafu Mkapa awe raia wa kawaida. Kombe aliyemwamuru amsake Munishi, ndiye atakayeamriwa amtie Mkapa mbaroni ili ajibu mashitaka ya kuua na kupora mali ya umma pamoja na kuiuza nchi kwa makaburu. Habari zaidi

Uchungu wa mwana aujua mzazi. Mkurugenzi wa shule za St. Mary's Mchungaji Getrude Rwakatare Katikati, akiwa na wanafunzi waliokuwa wamekwama Kenya kwa kukosa kulipiwa ada. Cha kushangaza walirudi nchini kwa ndege. Wanasema Mkapa ameboresha elimu. Mbona watoto wa vigogo hawasomi nchini? Dr. Rwakatare aliitumia nafasi hiyo kuzipigia debe shule zake pale alipoahidi kuwasomesha watoto hao bure kwenye shule zake.Hivi karibuni mama huyo aliandamana akidai anahamasisha umma uwalipie watoto yatima, na hapa anaahidi kuwasomesha watoto wa vigogo bure. Malimwengu hayaishi duniani.

Muulize Anti Lisa


Wengine wanakiita Chama Cha Majambazi. Washirikina Wachawi, Wauaji. Chama kilichoharibu maisha ya watanzania kwa zaidi ya miaka arobaini.CCM wanatumia mbinu zote kubaki madarakani. Pesa walizoiba miaka zaidi ya arobaini ndizo wanazotumia kununua kila anayekubali kununuliwa., Je Anti Lisa. Tufanyeje kuitoa CCM madarakani?
FANYENI HIVI:


Yalianzia viwanja vya KARIMJEE Dar es Salaam, na kumalizikia Mnazi Mmoja. Yalikumba wa kila rika.Walisema ni maandamano ya kuchangia watoto yatima, Lakini ujumbe kutoka mioyoni mwao ni kwamba CCM OUT.Watanzania wengi wamechoshwa na KERO za CCM. Woga unawafanya waseme wasiyomaanisha.Siku ya kufa nyani, miti yote huteleza. CCM ni Nyani ambaye siku ya kufa kwake imefika. Haijalishi ujuzi wa miaka arobaini kuparamia miti, Lakini safari hii miti yote inateleza. Watapigiza chini kwa kishindo, na ndio mwisho wao. Watanzania tunataka ENZI MPYA bila CCM. Habari Zaidi

CCM wameanza tena kuua
Kana kwamba hawakutosheka na mauaji ya waislamu zaidi ya sabini Zanzibari wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, Mkapa amewaamuru polisi wake waanze kuua tena. Safari hii wameanzia Dar er Salaam na wamemuua kijana mdogo wa miaka 18. Mengi zaidi linaarifu gazeti la "Guardian"
Angry opposition condemns boy killing
Dar Er Salaam 2004-11-30 09:48:54
By Peter Tindwa

Opposition parties have condemned the police for allegedly killing a 18 year-old pupil, Khalid Omar Mfaume, in Dar es Salaam last Sunday and have formed a probe team. The deceased was among people waiting to cast their votes in the just ended local government elections.

Addressing reporters after a meeting of leaders from nine opposition parties yesterday, NCCR-Mageuzi Chairman James Mbatia said the Standard Six pupil at Mbande Primary School, on the city outskirts was gunned down by police at the school grounds. “Political tyranny coupled with use of excessive force have deprived Mfaume of his right to life.

His blood will inspire change in this country,” Mbatia said.He warned that ‘dictatorship’ would turn the country into another Rwanda or Kosovo. “We condemn the killing of Mfaume with strongest possible terms,” Mbatia said.


NCCR-Mageuzi Chairman James Mbatia holds a photograph of primary school pupil Khalid Omar Mfaume who was allegedly killed by police in Mbagala Kiburugwa, Dar es Salaam, during disturbances in Sunday’s local government elections.(Photo: Tryphon Mweji)

A relative of the deceased, Uwesu Seif Magenge, told The Guardian that a group of armed policemen invaded Mbande Primary School and ordered people to disperse. “It was 5pm and many had not cast their votes. They defied the police order. Candidates were ordered to get into a police van.

Tension mounted and police opened fire,” Magenge said. But a police statement released at Muhimbili National Hospital where the deceased’s body was preserved alleged that Mfaume died mysteriously. Mbatia told reporters that a four-man team had been formed to establish the cause of the pupil’s death.

The team comprises Joseph Selasini, Msafiri Mtemelwa, Fahmy Dugutwa and Khamis Hassan. The four would also work with the family of the late Mfaume in the preparation for the funeral. Leaders who took part in the emergency meeting were from NCCR-Mageuzi, Civic United Front (CUF), FORD, NRA, UMD, NLD, TLP, UPDP and CHADEMA.

Meanwhile, opposition leaders have called on the government to repeal the Political Parties Act. “We don’t know what would happen in the general elections next year,” Mbatia said. CUF National Publicity Secretary Tambwe Hiza blamed the Temeke District Commissioner, Baraka Konisaga, for interfering with the voting exercise. “The DC called off polling at National Stadium and seized ballot papers and boxes,” Tambwe charged.

He also claimed that the polling station had registered 604 voters but the results indicated that 820 people voted at the National Stadium. CUF National Council would meet on Saturday to assess the civic polls. Both Ilala and Temeke municipal directors John Lubuva and Idi Nyundo respectively declined to comment but promised to announce the results today.

In another development, twelve people have been injured in a clash between Morans and villagers during Sunday’s elections, reports Joyce Mkinga. The cause of the fight was not established but eye witnesses told The Guardian that the Morans clubbed voters who were waiting for the polling results at Olopoponyi Village, Njoro Ward. One of those seriously injured, Athuman Hassani, who was hit on his head told The Guardian that some of those assaulted were flushed out of their homes and beaten.

According to Hassani, a commotion ensued when results showed that the Maasai candidate, one Makoo Nangolo of CCM, had lost to the opposition. Ten morans were arrested according to Kiteto District Commissioner Lt. Lepillal ole Molloimet.
SOURCE: Guardian


Mchungaji Faustin Munishi Rais Mtarajiwa Tanzania

Sijuti kugombea kiti cha urais Tanzania, Bali namshukuru Mungu kuniwezesha kufanya hivyo. Mungu ni HAKI tupu na ndani yake hakuna hata chembe ya udhalimu. Hatuwezi kudai kumcha Mungu huku tukiunga mkono udhalimu wa CCM. Wanaoiunga mkono CCM dhalimu, watuambie wanamwabudu nani kama siyo shetani baba wa udhalimu wote.

Tusidanganyane. Huwezi kuwa mtumishi wa Mungu na ukose kuyaona MAOVU ya CCM. Watumishi wa shetani ndio wanaoyafurahia maovu kwani, yanatimiza lengo la shetani la kuchinja, kuharibu, na kuua. Tunaipinga CCM Tanzania sawa na tunavyompinga shetani duniani kote.

Dunia ni mali ya Mungu, na Tanzania ni sehemu ya dunia. Hatuwezi kumpinga shetani duniani huku tukimruhusu aweke kambi Tanzania, akitumia Chama Cha Majambazi CCM. Haiwezekani, Tumekataa, Hatutakubali, na hatutaki. Ni agizo la Mungu kwamba wale wanaomtumikia, Wayahubiri maneno yake kwa walimwengu wote. Kila atakaeyaamini maneno ya Mungu, Sifa ya kwanza ni kuyakataa maovu yote. Atafanya kila lililo ndani ya uwezo wake kuwasaidia, Kuwatetea, na kuwakomboa wanadamu wanaonyanyaswa chini ya utawala dhalimu wa CCM. Akifanya hivyo, anatimiza agizo la Mungu.

Akifanya kinyume na hayo, Atakuwa hatimizi wajibu wake kama mtumishi wa Mungu. Watumishi wa Mungu ni wale wanaomwamini Mungu. Haijalishi wanatoka dini gani, hata kama ni dini za kienyeji, Ilimradi wanamwamini Mungu, Basi wamehitimu kuitwa watumishi wa Mungu. Hatuwezi kuwahukumu watu kutokana na tofauti za kidini, Badala yake tunawahukumu kutokana na matendo yao. Wakitenda mema ambayo asili yake ni Mungu, Tutawaita watumishi wa Mungu. Hata kama dini zao ni za kiasili. Huwezi kuwaita vinginevyo. Ni watumishi wa Mungu.

Wakitenda maovu ambayo asili yake ni Shetani, Tutawaita waabudu Shetani hata kama dini yao inatoka Marekani. Katika hilo watumishi wa Mungu ni dhahiri. Yaani wale wanaochukia maovu na kuyakemea, hata kama maovu hayo ameyafanya Mkapa na serikali yake inayowaua wale wanaosema kwamba CCM imezeeka, Iliharibu Tanzania, hawaitaki. Kuna kosa gani kusema hivyo wakati ni ukweli usiopingika?

Wakati umefika kwa watumishi wa Mungu kuwakomboa watu wa Mungu. Wameteseka vya kutosha. CCM imewaibia, na hata wengine imewaibia uhai wao. Mungu anasema "IMETOSHA. LAZIMA WATANZANIA WAKOMBOLEWE KUTOKA MAKUCHA YA CCM."

Kwa Mungu hakuna lisilowezekana. Mungu siyo sawa na mwanadamu. Akisema saa imefika Watanzania wakombolewe ANAMAANISHA NA ITAKUWA HIVYO. Nilianza kuyasema haya mwaka 2000, wengine wanauliza mbona ni muda mrefu na hakuna dalili za njia ya kuwakomboa watanzania?

Mungu hatawaliwi na muda. Muda wote ni wake. Kifupi ni kwamba Mungu hachelewi wala hawahi. Hufanya vitu kivyake ili abaki Mungu nasi tubaki wanadamu. Mwaka elfu mbili nilisema ole wao wanaosimama kuyazuia mapenzi ya Mungu Tanzania. Mkapa alisema yeye ni mbabe na akashupaza shingo. Leo hii anatembelea magongo akielekea kaburini. Haijalishi watatumia pesa ngapi kujaribu kumtibu, Lakini lazima mapenzi ya Mungu yatendeke ili iwe funzo kwa wengine wasijaribu kushindana na Mungu.

CCM mwisho wake umefika. Mungu anajua atatumia njia gani kuzima kiburi cha CCM. Kazi yangu ni kuwatayarisha watanzania wawe tayari kuyaona makuu ya Mungu Tanzania. Baada ya kila kitu kutendeka na CCM iwe ni historia, Watanzania tutayainua macho yetu juu na kumtukuza Mungu aliyetenda maajabu machoni petu. Kuna wengi hawataishi kuyaona hayo.

Sera za Mungu ni "ANZENI NA MIUJIZA ITAWAFUATA." Ni vigumu watu kuifuata miujiza ya Mungu, Lakini ni rahisi watu walioamua kufuatwa na miujiza ya Mungu. Kwanza wanaihitaji kuliko wale ambao hawajaamua. Tangu tulipoamua kuipinga CCM na sera zake mbovu, Mungu ametenda miujiza mingi. Mkubwa kuliko yote ni ule wa kumwangusha mbabe wa CCM DIKTETA Nyerere pamoja na Nduli Benjamin Mkapa ambae atafuatia karibuni.

Kwa sasa CCM ni sawa na nyoka aliyekwisha pondwa kichwa na kilichobaki ni kutisika kwa mkia. Suala kama la kuibadili katiba ili iniruhusu kugombea bila chama cha kisiasa, siyo tatizo kubwa kama linavyoonekana. Wengine wanaliona hilo kama bahari kubwa mbele yetu. Yangu ni kuwaambia kwamba waamini tu na watauona muujiza wa Bwana. Kama wana wa Izraeli walivyopita katikati ya bahari ya Shamu kama nchi kavu, Ndivyo Watanzania tutakavyolivuka tatizo la katiba. Mungu mwacheni abaki Mungu.
Censorship turning systematic in Tanzania

Hii ni kanda mpya ya video katika VCD, ambayo Mchungaji Munishi aliitoa mapema mwaka 2004 na ilipoanza kusambaa Tanzania serikali ikaipiga marufuku. Ndani ya video hiyo kuna maneno kama CCM chama cha majambazi na wauaji.Pamoja na nyimbo mpya. Jipatie kanda hiyo uonje UHONDO.

Upande wa nyuma wa kasha la video mpya ya Munishi.

Hii pia ni moja ya Kanda mpya ya video katika VCD. Ndani yake kuna vichekesho vya kuvunja mbavu. Bwana Godfrey Gathena Kuniara maarufu kwa jina la kisanii Ole Soipei ndiye msanii katika kanda hii.Usiikose.

Hapa kuna VCD mpya ya Waciama. Nyimbo ni kwa lugha ya KIKUYU. Picha pamoja na kuhariri vimefanyika Gospel Television.Utaipenda.

Contact us/ Tuandikie

Full Name
E-mail
Subject
Message
   
   


Name: Nzua Mukende
E-Mail: prince_moses@juno.com
Subject: Munishi
Him,
Mr. Munishi, I'm deeply disapointed by what Mr Munishi is trying to accomplish through unwise and foolish methods of political empowerment. Mr. Munishi seems not to even understand what our country has been going through and even the direction it is currently going.

Mr Munishi, one thing i would advise you and your friends who are encouraging you to run for that high position in the Tanzania Government, you all ought to be smart and wise, because so far you are propagating foolish ideas, empty stupid promises that you would never even manage to accomplish in your presidency if you are elected(something that would never happen in your lifetime).

I would strongly advise you to study history and see where tanzania was, and where it is going in terms of economic, politics and even spiritual. Mr Munishi you as a pastor you need to have God's wisdom and not talking flatout lies and precipitate hatred toward our government because it is God who was pleased and currently pleased to have Mr. Benjamin Mkapa to be our current President.

Mr. Munishi you as a pastor also need to spend a considerable amount of time in praying for our nation (Tanzania) as well as our leaders, something I think you don't even do it, rather than that you are promoting hatred(which is totally unbiblical, shame on you). You need to be ashamed of yourself of critizing Mr. Mkapa for the wonderful job, he's doing in handling the economy, trying to promote peace among our neighboor countries, as well as doing his best to improve public services like education and freedom.

Honorable Mr. Benjamin Mkapa, we born again christian who are praying for this nation, we want to let you know that we love you and always praying that God would heal you, protect you and give you wisdom in your task. It is hard work, but we stand together with you asking God for his help in country and we would make Tanzania a better place and freedom would endure, public services would improve and God's glory would be seen in our beautiful country. Cheers for our government!!

" The supernatural Grace of the Almighty God is greater and more unfathomable than anything we can imagine with our very inteligent minds. His strength is made perfect in our weakness and forever more, enabling us to outdo our performances for anything in our lives...."

Huyo anajiita Nzua Mukende.Usijali hayo ni moja ya majina Mengi ya Mkapa. Na hayo ni maoni yake. Wewe unasemaje? Tuandikie.

Name: James
E-Mail: jim@yaoo.com
Subject: MKAPA NA MUNISHI WAPATANISHWE


Malumbano yanayoendelea kati ya Mchungaji Munishi na Mheshimiwa Rais Mkapa siyo mazuri kwa nchi yetu. Afrika tunajua kuitisha mikutano ya upatanishao wakati damu nyingi sana imeshamwagika. Hatuna hekima ya kuzuia kabla ya madhara makubwa kufanyika. Mizozo yote huanza na malumbano kama haya mnayoyaona hapa. Kila upande ukidai kunyimwa haki na upande wa pili. Tusipoziba ufa hapa tutajenga ukuta. Malumbano yakizidi na yakomae kabisa, huzaa magomvi ambayo nayo huzaa vita.

Hakuna vita inayoanza kama vita. Huanza kama maneno ya chokochoko kama hizi mnazozisikia hapa. yasipozimwa au kupatanishwa huzaa vita. Ni muhimu sana kuwapatanisha Mheshimiwa Mkapa na Mchungaji Munishi. Nionavyo mimi Munishi hana historia ya kulumbana na serikali. Malumbano yalianza pale serikali ilipoipiga marufuku kanda toleo la saba ya mchungaji Munishi. Sababu hasa zilikuwa kisiasa kuliko vinginevyo.

Sijui serikali walisikia nini kwenye kanda hiyo na kuamua kuipiga STOP, Lakini mimi sioni chochote ndani ya kanda hiyo ambacho kingeifanya serikali kuhamaki kama ilivyohamaki. Baada ya kukurupushani za kuweka watu ndani na habari za kutafutwa Munishi kusambaa, ndipo Munishi alipotoa taarifa kwa vyombo vya habari kwamba maisha yake yalikuwa hatarini kufuatia zoezi la serikali kuzikamata kanda zake.

Sina data zaidi ya hapo, lakini nafikiri kuwa malumbano yalianzia hapo. Kama sikosei pia ndio sababu kubwa ya Munishi kuanzisha Web Site yake ambayo wengi tunaiona kama mahali pa kutolea malalamiko yake kuhusu hatua ya serikali. Anahisi kaonewa. Serikali nayo kwa upande wake imeendeleza ukimya ambao siyo wa kawaida. Ni kama wanadharau.

Kama kanda tulizuia na watu tukawaweka ndani, SO WHAT? Mtaifanya nini serikali yenye ridhaa ya wachache ambayo siyo butu? Kwangu msimamo huo hauisaidii serikali. Unathibitisha jinsi ambavyo viongozi wa Tanzania wanavyodhamini ubabe wa vyombo vya dola.Wanaweza kumfanyia mwananchi chochote na wasipelekwe popote. Hata kama simba aliumbwa ale nyama ya swala, lakini swala hawajui hilo. Ndio maana kila inapobidi, swala hutimua mbio. Vinginevyo kizazi cha swala mwituni kingekuwa kimemalizika. Kwamba swala bado wapo mwituni pamoja na wingi wa simba, hiyo inaonyesha serikali haina nguvu inazofikiri kuwa nazo.

Nashauri kwamba Munishi na Mkapa wakae pamoja kutatua tatizo ambalo linakua kila kukicha. Ubabe hautasaidia katika hili. Msisahau kwamba nchi za magharibi huifurahia mizozo ndani ya Afrika. Huitumia kama soko lao la kuuzia silaha. Ninachosema hapa ni kwamba ni rahisi sana kwa nchi za magharibi kutoa misaada ya silaha kwa yeyote anayeonekana mpinzani wa serikali. Siyo ajabu wakatumia mzozo huo kumpa mpinzani silaha bure, huku wakiidanganya serikali inunue silaha kwao kupambana na mpinzani. Mwisho wa kila kitu mnauana wenyewe, na silaha mnazilipa kwa njia moja ama ile nyingine. Tuyatatue matatizo yetu wenyewe. Tena kabla hayajatuletea madhara. Hii ni tathmini yangu mwenyewe kuhusu malumbano kati ya Munishi na Mkapa.


Name: Kim
E-Mail: kin@yahoo.com
Subject: Yes, you are right man!!
I think Nzua Mukende is totally right and very aware of what he's written about. Thats very true, that we as born again christian need to pray for our nation and not standing out to criticize our leaders. But mind you, we need to condemn sin in the nation!

Name:mugo
E-Mail:mugo@kilikenyans.com
Subject:WATCH OUT
Sina nia mbaya lakinin website yako in uowongo mwingi kama vile piccure mixing and pasting wewe ni mtu wa dini. Kama unataka kupambana na CCM rundi Tanzania ukafanye hivyo lakini kuwatukana CCM ukiwa Kenya sio Ungwana


Contact us/ Tuandikie

Full Name
E-mail
Subject
Message
   
   
 
| http://munishi.com |