Ukurasa wa mbele
Gazeti la injili
Nyimbo za Munishi
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail
Tuma SMS duniani
Sema nami
Sikiliza waongo
Twende kanisani
Gazeti INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com
Or fmunishi@hotmail.com

Nyerere Hakuwa na Dini.

 

Miaka 40 ilitosha kumpima Nyerere na kumkuta kuwa alikuwa hafai. Ukurasa wa Nyerere Tanzania haujafutika ndiyo maana bado kuna watu wanaofikiri kuwa Nyerere alistahili sifa zozote.

Aliharibu Tanzania na lawama ndizo zinazomstahili. Najua kwamba kumlaumu marehemu hakusaidii, lakini kuuvunja msingi alioujenga kutawasaidia wale wanaojaribu kujenga juu yake. Haijalishi mbinu gani watakazotumia, lakini kwa sababu msingi wa Nyerere ni mmbovu tena haufai, kila kitakachojengwa juu yake kitabomoka.

Wengine wanasema ana mawazo potovu anayejaribu kuwaonya watu wasifanye kazi bure ya kujenga juu ya msingi mbovu. Naona kuwa wao ndio wamechoka kufikiri. Miaka yao haikubali mawazo mapya. Wanafikiria kufa kuliko kuishi. Kila kitu kwao ni "HAIWEZEKANI." Wanamshuku hata Mungu mwenyewe. Ni watu wa ajabu sana.


Hayati Marehemu Nyerere akionea haya matendo yake

Wanaogopa msingi ukivunjwa tutaanzia wapi kujenga msingi mpya? Hawaioni nishati ya kisasa kwani wao waliishi nyakati giza. Nuru pekee kwao ilikuwa Nyerere. Alifikiri na kuwaza kwa ajili yao. Aliwaambia wasifanye chochote kwani serikali itafanya kila kitu. Wakamwamini walikosea. Wanaogelea kwenye dimbwi la umasikini ambao Nyerere aliwafundisha kukubaliana nao.

Yeyote aliyejaribu kujitoa katika dimbwi hilo, aliitwa mhujumu wa uchumi ambao uliharibiwa na sera zake mbovu. Aliziamini sera zake na kuwataka watanzania waziabudu kuliko Mungu ambaye ndiye muweza wa kila kitu.

Mawazo yake potovu aliyaweka kwenye kibuyu kwa jina TANU na sasa CCM. Aliwafanya watu waumini wa CCM kwa lazima kuanzia vijijini hadi mijini. Kwenye mashirika ya umma wimbo ulikuwa CCM. Majeshi yote saluti ilikuwa CCM.

Na kuna wendawazimu wanaosema kuwa huo ulikuwa uzuri wa mwendawazimu mwenzi wao NYERERE. Sawa na iwe hivyo. Wana haki ya kuamini kiwazimu bila kuwazuia wengine kuamini KIUNGU.

Mimi Faustin S. Munishi, nina maono na Tanzania. Kwamba Mungu anataka kuibariki Tanzania endapo tu watakubali kuyasikia mausia yake. Anasema kuwa kwa watanzania kumwamini Nyerere kuliko yeye walikosea. Watubu na waanze kumwabudu yeye, waone yale atakayowafanyia.

Wasijali nani, wapi, aliyejaribu kuongoza kidini akashindwa, kwani yeye ni Mungu asiyeshindwa. Mungu hutumia watu, na katika maono haya ananitumia mimi. Binafsi mimi ni Mkristo, na siwezi kuukana ukristo kinafiki kama alivyofanya Nyerere. Alivaa kibagalashia cha kiislamu kuwadanganya waislamu kwamba yeye naye yumo. Kumbe Nyerere hakuwa Mwislamu wala Mkristo. Mwenyewe alijua kuwa alikuwa nini.

Kwamba Tanzania kuna dini nyingi zinazomwabudu Mungu hiyo hainizuii mimi kusema maono yangu kwa Tanzania. Kwa sababu dini zinamwabudu Mungu na mimi nina maono kutoka kwa Mungu, sioni shida hapo. Dini zote zinazomwabudu MUNGU wa kweli tutakubaliana.

Watakaoshindwa kunielewa ni wale wanaomwabudu shetani, na hao "TUTAPAMBANA" siyo kwa silaha, au mwili na nyama, bali katika ulimwengu wa kiroho. Uwezo wa kupambana nao tumepewa na Mungu. Uwezo wa kuwageuza mioyo ili warudiwe na fahamu zao wajue kuwa hakuna anayestahili kuabudiwa duniani wala mbinguni isipokuwa MUNGU peke yake tunao.

Sasa hapo ni akili kichwani mwetu tujue nini kianze! Kushawishi ? au MAPAMBANO? Lakini watu waliomwabudu Nyerere hao tayari ni wafuasi wetu. Wanahitaji kuoshwa kidogo bongo zao, ili kutu ya Nyerere itoke.

Na mwandishi wa Injili Munishi.

Habari Katika Picha

 
| http://munishi.netfirms.com |
 
<<Back  |  Home |  Gazeti La Injili | Injili2 | Nyimbo Za Munishi | Next >>