Ukurasa wa mbele
Gazeti la injili
Nyimbo za Munishi
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail
Tuma SMS duniani
Sema nami
Sikiliza waongo
Twende kanisani
Gazeti INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com
Or fmunishi@hotmail.com


Nation TV Wakosa Mwelekeo

 

Waliingia kwenye uwanja wa TV Nairobi kwa vishindo. Na matangazo mengi kwenye gazeti lao "DALY NATION" yaliwafanya wapinzani wao wakubwa KTN kuonekana kama simba aliyenyeshewa. Wananchi walisubiri kwa hamu kuona uwanja wa TV Kenya ukibadilishwa na magwiji wa habari Afrika Mashariki na kati. Baada ya kuanza na kasoro nyingi, wananchi waliendelea kusubiri kwani wengi walisema mwanzo wa kila kitu ni mgumu. Roho za watu wengi zilipoa kidogo wakati NATION TV walipoanzisha kipindi kilichowaonyesha viongozi wa Kenya kuwa ni kichekesho kitupu. Kipindi hicho kilijulikana kama REYDICULAS "Mnisamehe kama sikuandika vizuri jina hilo." Hii ni kwa sababu binafsi sikuwahi kukiona kipindi hicho japo watu wengi walionekana kukisifu na kukipenda sana. Pengine hamu ya kuona watu weusi kwenye TV zetu ilichangia kuwafanya watu washabikie kipindi hicho.

Matumaini hayo yaliendelea kufifia kila kila siku baada ya NATION TV kufuata mkondo ule ule ambao TV za awali ziliufuata. Vipindi vingi vilikuwa vya nchi za magharibi, Habari pamoja na usomaji wake haukuwasisimua wengi, kwani badala ya NATION TV kuwatumia wakongwe wake wa habari katika magazeti yao, waliaza na watu wapya jambo ambalo mpaka sasa sijui nani aliyefanya maamuzi hayo yasiyo ya busara hata kidogo.

Kila tunachokiona kwenye TV ni kazi ya uandishi halafu ikapatiwa sauti na picha. Kwa NATION hawakuhitaji waandishi wapya wa TV, bali walihitaji wasomaji wa yale ambayo tayari yameandikwa na waandishi wao waliobobea katika fani hiyo. Kwa maneno mengine walihitaji KAMERA nzuri na studio ya kisasa kuweza kuwa na vipindi vya kutosha masaa 24 kila siku kwa muda wa miaka ishirini. Cha ajabu ni kwamba pamoja na kuwa na studio ya kisasa kama hii inayoonekana hapa, bado NATION TV haina vipindi vya kutosha masaa sita kwa siku.



Studio ya kisasa NATION TV, Ila vipindi ni kiwango cha chini sana.

Akiongea na Gazeti la Injili, aliyekuwa mhariri wa gazeti la NATION Bwana Ogova Ondego ambaye sasa analifanyia shirika la habari la Kenya KBC alisema alijiondoa NATION baada ya kuona kuwa hawataki kuitumia taaluma yake vizuri. "Niliwaambia nianzishe kipindi cha TV ambacho kitatumia makala zangu ninazoliandikia gazeti la NATION lakini wakubwa walikataa." "Walisema siwezi kulipwa na gazeti halafu tena nilipwe na TV." Alimaliza Ogova ambaye mbali na kuifanyia KBC, ameanzisha WebSite yake inayohusiana na mambo ya sanaa na inapatikana katika http://artmatters.netfirms.com

Inawezekana kuwa uongozi wa NATION ulikuwa sawa kumzuia Ogova kupata mishahara miwili, lakini ikiwa hakuna mtu mwenye uzoevu kama wa Ogova kuandika makala za TV sioni kwa nini wamkataze. Lakini kuna minongono NATION kuwa Mkurugenzi wa shirika hilo la habari Bwana Kiboro anataka mwenyewe awe ndiyo habari. Tena wako wanaosema kuwa hata wale wanaoajiriwa kushika nyathifa mbali-mbali katika shirika hilo, huchaguliwa kwa misingi ya undugu au ukabila na siyo uwezo wa mtu kitaaluma. Katika enzi hizi za mtandao wa Internet itakuwa vigumu kwa NATION kuwazuia waandishi wake kupata zaidi ya mishahara miwili kwani kila mwandishi anaweza akawa na WebSite yake na kuandika "story" zake hapo na kuziuza kwenye chombo chochote cha habari ulimwenguni.

Ogova amefungua mlango kwa waandishi kuwa huru, sijui wengine wanasemaje. Waandishi wengi huwa msitari wa mbele kutetea wanaoonewa katika jamii, lakini hakuna wa kuwatetea wakati vyombo vya habari vinapowaonea na kuwanyanyasa waandishi. Kwa mwandishi yeyote anayetaka kuanzisha WebSite, niko tayari kusaidia.

Ameandika Munishi Faustin
E-Mail fmunishi@hotmail.com

 
| http://munishi.netfirms.com |
 
<<Back  |  Home |  Gazeti La Injili | Injili2 | Nyimbo Za Munishi | Next >>