NATION
News |
http://nation.netfirms.com Rodnat Mwenda Attacks Munishi Hi
Munishi, whoever you are but get ready to defend the truth...
Munishi, you have been in Kenya for along time right? You know
nothing about tanzania considering your bad education background..
Look at this "Ninaujua ugumu wa kazi hiyo hasa ukitilia maanani
kwamba Nyerere alitumia muda wote wa utawala wake kujikita katika
nyoyo za watanzania ili wamkumbuke miaka 100 ijayo. Mwaka mmoja
tangu afe kwa ugonjwa wa MKANDA WA JESHI{na sijui ni ugonjwa
gani huo.}Tayari hisia za watu juu yake zimeanza kubadilika
ghafla." It shows your ignorance if not stupidity of analyzing
things... Hey, guess what, I thought you are Christian, you
stated by your fake songs, don't you remember Munishi you were
one one the Majambazi sugu?" Do you want us to make a followup
and as one of the person you killed my relative during that
time and I am convinced you are still jambazi sugu under the
cover of christianity. We warn you to stop writing these stupid
ideas about the late Nyerere, this man used to be the one who
was making peace internationally and you cannot even compare
any these stupid ideas and his. Yes, if you think he was wrong,
who is right? I know you think Tanzanian will listen to you,
but we will put your issue open Ok... GO ON>>> mrodnat@uccmail.co.tz
Munishi Ajibu Mashambulizi Mwambie Mkapa.....Eti Muafaka? Hakuna muhafaka bila CCM kutoka madarakani.Iliwaweka watu kizuizini kinyume cha sheria, na sasa inataka kuwaachia kama sharti la kutimiza muafaka.Walioachiwa ni haki yao maana hawakufanya kosa.Ikiwa kusema uchaguzi urudiwe ni kosa la jinai basi hakuna muafaka bila uchaguzi kurudiwa.Wanajua wako madarakani isivyo halali.Dawa ni kutoka. Anguko la Amerika litakuwa kubwa, na kishindo chake kitasikika dunia nzima.Ole wake atakayejaribu kuishikilia Amerika isianguke!! Atasagwa kama panzi. Mungu ameikataa Amerika kwa kujiinua kwao na kiburi.Lakini wakijirudi,warekebishe sera zao Mungu mwenye huruma atawasamehe.Wasipofanya hayo,Ole wao Amerika ilimsaidia Mkapa ashinde uchaguzi kwa njia zisizo halali.Masharti ilikuwa awathibiti waislamu, na hasa wa Zanzibar. Kwa kiburi serikali ya CCM iliwaua waislamu zaidi ya 70 huko Zanzibar.Amerika ilimkingia kifua Mkapa, badala ajiuzulu aliwapandisha vyeo polisi walioua.Sasa Amerika maji yako shingoni.Mkapa anataka mapatano na waislamu bila kutoka madarakani.Sawa hiyo? Amerika walimjenga Osama Bin Laden wanataka sisi tumbomoe? Hatutaki, hatuwezi,tumekataa.Walimjenga kwa damu ya Warusi,Siyo vibaya wakimbomoa kwa damu yao wenyewe.Wamezoea kujenga kwa damu.Walimjenga Saddam Hussein kwa damu ya Wairan na sasa wanambomoa kwa damu ya Wairaq.Walianza kumjenga Mkapa kwa damu ya waislamu huko Zanzibar, Huyu tutambomoa bila kumwaga damu. Mkapa alisema atatumia nguvu za dola kuwaweka sawa wale anaowanyanyasa. Kama ni nguvu za dola Amerika ni zaidi ya TZ mara mia moja.Tunasubiri tuone atafika wapi na nguvu za dola.Haki kwa kila mtu ndiyo silaha kwa sasa.Bila haki, Nguvu za dola ni Bure.Waliouawa Zanzibar ni watu, ndugu zao wapo,wanaoendelea kupigwa marungu ya Polisi ni watu,na wanaowekwa ndani na kuteswa bure ni watu.Yakiwafika shingoni sijui watafanya nini.Tunao muda kuyarekebishe yasitufikishe pabaya Walokufa Amerika hawana hatia? Wana hatia kama walikubaliana na sera za serikali yao kuwanyanyasa wengine.Mimi ni Mkristo mwananchi wa Tanzania na sikubaliani na sera za serikali yetu kuwanyanyasa waislamu kwa sababu ya dini yao.Wakati umefika wananchi wa Amerika kupinga kwa nguvu zote sera za serikali yao.Wasipofanya hivyo wana hatia. Tatizo siyo Osama Bin Laden, bali tatizo ni Amerika. Osama na wote wanaodhaniwa kuwa maghaidi wakifa leo tatizo la ughaidi haliwezi kwisha duniani. Ughaidi ni matunda ya sera mbaya.Huwezi kuumaliza ughaidi bila kumaliza sera mbaya.Kila mtu anaweza kuwa ghaidi kulingana na mahali alipo na hasa kama anahisi kunyimwa haki zake za msingi. Sasa Nakujibu..Twende pole pole Mwenda. Unajua Mwenda pole hajikwai. Tayari umejikwaa kwa sababu unaenda haraka. Ikiwa unayajua mazuri ya Nyerere ni vizuri ukayasema bila kujaribu kumzuia huyo unayemwita jambazi sugu kuusema ubaya wa Nyerere. Ikiwa Munishi alikuwa jambazi sugu ambalo halikuwahi kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za ujambazi wakati huo, basi wa kulaumu siyo Munishi bali ni polisi waliozembea kazi yao. Na kwa sababu polisi walikuwa chini ya uongozi wa Nyerere pia utakosea kuwalaumu polisi bila kumlaumu Nyerere aliyemwacha jambazi huyo katili awaue wazazi wako. Naijua Tanzania vizuri, lakini siyo kuliko wewe kulingana na elimu yako.Sikatai kwamba sikumaliza masomo, na ndio sababu mpaka leo nasoma.Unajionyesha kwamba ulimaliza masomo na unashikilia karatasi kwa jina la shahada, ndio maana husomi na ubongo wako umejaa matope. Ninafanya vitu vya shahada, na wewe unaishikilia.Unajifanya kumtetea Nyerere ambaye wala hujui aliamini nini.Unawasiliana nami kwa Kiingereza kwa sababu unafikiri kujua kiingereza ni ishara ya usomi.Nyerere asingefanya ujinga kama wako.Ikiwa pamoja na yote aliyofanya Nyerere kwangu anabaki mpumbavu, basi unajua nimekuweka wapi. Kumbuka nilimwita Nyerere mpumbavu na siyo mjinga.Sina tabia ya kuwashambulia wafu, lakini Nyerere ni mfu anayeitawala Tanzania akiwa kaburini.Kama mkristo siwezi kukaa kimya niitazame nchi yangu ikiongozwa na mawazo yaliyopitwa na wakati ya mfu.Hiyo ndiyo ninayopigana nayo na nitaendelea kupigana nayo kwa nguvu zote .Napoteza muda wangu kujibizana na wewe kwa sababu ulisoma makala yangu na ukashawishika kuninyamazisha maana nimekufanya mwanafunzi wangu.Yale ambayo hukuelewa ndio napoteza muda wangu kukuelimisha.Mjinga akielimishwa huelimika nami sitoacha kukuelimisha. Watanzania
walinyang'anywa haki yao ya kufikiri na kutoa maoni, na unamjua
mnyang'anyi. Nyerere kwangu alikuwa mpumbavu na atabaki hivyo
akiwa kaburini. Siwezi kuacha kuyatoa mawazo yangu, kwani hiyo
ni haki yangu. Rodnat Ajirekebisha Aweka Uzungu Chini Ndugu mwanasiasa Munishi, Kwa kisio langu nilidhani nitanyamaza kwa maana nilidhani malumbano na kundi la wasioelewa ni kujipaka matope lakini nimeona nikujibu kulingana na jinsi ulivyoamua kunisakama... 1- Ninapenda kukuhakikishia kuwa baada ya siku kadhaa utatujia kuwa umepata vitu ulivyoibiwa kwa maana pengine umejiibia ama wenzio waleee wa zamani wamekuja kugawana vitu kadhaa mlizozichuma kwa njia hiyo hiyo.. Kwa kifupi nadhani mimi kama mkristo, nilikusamehe kwa sababu ulisema umeokolewa lakini tangu majuzi nimepata picha halisi ya ulivyo kwa hiyo bora nikukumbushe tu kuwa hivyo ulivyojisikia ndivyo ulivyokuwa ukiwaacha wenzako midomo yao wazi kipindi kilee ukiwa kama hao wageni wako wa usiku wa jana... " Actually, I am pretty sure kuwa hawajamaliza na lazima waje tena very soon probaby within this week or by the end of the next week" 2-Munishi Tanzania hii unayoiona ni ya watanzania, tena inaongozwa na watanzania, Ni lini uliwahi kupiga kura Tanzania? Ina maana unatufanya sisi tuliopiga kura mara mbili hata baada ya huyo unayedhani alimchagua Mkapa kufa, ama hujui kuwa mwaka 2000 tulikuwa na kura na hao wanaokutumia walishindwa na kwa taarifa yako wataendelea kushindwa for couple of coming decades. Ninajua wazi kuwa hii Tanzania ambayo wewe unadhani kuwa ilichaguliwa na Nyerere na wewe kwenda Kenya japo ulitoroka kwa kudhani utakamatwa na polisi kwa makosa yako ya ujambazi, ndiyo Tanzania tuliyoichagua na tunaipenda ndiyo maana hatujaikimbia kwa sababu ni salama. 3-
Kwa nia ya kuijenga Taifa hili la amani ambayo wewe huitaki,
ukiingiza mbegu za chuki ukijua kuwa hata kama huyo unayemtaka
aingie madarakani bado utakuwa yule yule Munishi wa porojo za
hapa na pale.. Nakushauri ujikaze kwa kila namna iliyohalali
uijenge taifa lako, lakini kwanza pata mafunzo ya kujua taifa
hili kabla hujalisakama.. Hata inatia kichefuchefu kuwa hunajaribu
hata kumkosoa Mkapa, Ndugu munishi Mkapa na Mrema wako ni sawa
na wewe na mimi. Nadhani utajitahidi kuwa mwangalifu kwa kipindi
hiki kwa maana Huyo Mkapa unayemsema ni Raisi wa Tanzania, na
wa Mrema pia. Mungu akubariki ndugu Munishi upate ufahamu na
ujuvi wa Taifa hili. Mungu Ibariki Tanzania, na walaaniwe wanaoiombea
Tanzania maafa na vita kama akina Munishi.. Kennedy Greyson Atoa Mpya SI WAKATI MWAFAKA WA MALUMBANO. Ndugu Mhariri Munishi, Nimefuatilia kwa karibu sana malumbano baina yako na Bwana Mwenda nilikiwa najaribu kujua wapi mnaanza na kufikia lakini naona mgongano wa mawazo, kwanza napenda kumfahamisha bwana mwenda kuwa si jambo la busara hata kidogo kutoa hoja za haraka katika mambo nyeti kama ya siasa hasa katika nchi kama Tanzania kwa sababu mbalimbali: Kwanza, Mwenda Munishi si mtanzania kimsingi, yeye yuko Kenya, lakini pia anatumiwa, hata ikiwa kweli lolote analosema liwe limetimia atakavyo bado hatahathirika lolote kwa kulingana na kuwa yeye na familia yako wako kule nchini Kenya. Labda tungemuomba Munishi arudi Tanzania aikosoe Tanzania akiwa nchini, hapo mimi na wewe tutakuwa pamoja. Pili, Munishi ni mwana injili ( entertainer ) kwa hiyo njia kama malumbano ndiyo aliyokolea nayo tofauti na wewe ambaye ki msingi naamini kuwa siyo kulingana na namna unavyojieleza na hata maelezo yako yanaonyesha kuwa pengine taaluma yako haiusiani na watu. Tatu, Tanzania inahitaji kuwa na wakati maalumu tena wa mpito (transition period) ambapo kwa njia zote za mawasiliano itumike kuelezea wananchi wa Tanzania hasa walioko nje waelimishwe nini kinaendelea nchini. Hebu fikiria mtu anaongelea watu kupanga mstari wa sukari eti Nyerere aliwarithi watanzania! Amazing. Hebu chukua mfano wa Leila anayedai madai ambayo hata hayana msingi, Kwanza Leila angejua kuwa maelezo haya si ya kweli, "Sasa mambo yakiwa hivyo najiuliza kwa nini alipoteza muda kwenda Makerere kupata shahada ya DR." Nyerere hakupewa PhD. Makerere, hilo si kweli kwanza. Pili, Nyerere alikuwa anawaongoza wananchi wa Tanzania waiweke Tanzania iwe mahali pazuri na si Nyerere mwenyewe yeye si Mungu! kama kuna alilopaswa kufanya Leila ni kujiuliza amefanya nini Tanzania imekuwa mahali pazuri pa kuishi? Kama hakuna labda ajiulize kama ana ndoa halali, kama anayo, nyumba yake ni mahali pazuri pa kuishi ama ni wale wa perrrr kama tunavyowajua na mume wake anampenda kweli? Ama Nyerere hakufanya kwake kuwa pazuri pa kuishi. Leila ujue, Tanzania ni mahali pazuri sana na wengi wanpalilia, labda wale wasiojua wanachofanya na wasiojua huko nje pana nini. Tuseme rwanda ndipo pazuri pa kuishi? ama Sudan ndipo pazuri pa kuishi? ni wapi unataka tuseme ni pazuri kama si Tanzania? Napenda kukujibu swali lako unasema; "Bado nasita katika njia mbili, sijui nimpeleke mtoto wangu Makerere apate shahada kama ya Nyerere" Mmmh, Leila uliza walio na PhD. hawapelekwi huko. Si Form Four hiyo dada. Wanafika huko wale wanaoelewa na wala si kupeleka mtoto. Mtoto utampeleka mwisho kidato, ukimaliza hapo ndo unaanza Degree ya kwanza, ambayo si mwaka moja pengine sita hata saba kama si minne na mitatu, kisha kuna Masters hii si tena masihara kisha ndo hiyo Dr. ambayo imekutoka mdomoni. Hiyo si chini ya miaka kadhaa kama si mitatu basi mitano. Tena
basi hapo si mtoto tena ni mama kama wewe, swali sijui tukupeleke
ama tuache.. Kwa elimu tuache kwa maana hata huyo Nyerere hakuipata
kwa darasani bali alionekana anafaa kupata hiyo kwa taaluma
yake. Leila jina lako linanishawishi kuwa unauwezo wa kuelewa
ukieleweshwa ungekuwa Shayo, ma Arawa ningesita kukusemesha.
Madai yako "Yoshua alifanya makuu kuliko Musa Na Yoshua wa Tanzania
ni mimi Faustin S. Munishi" Sina jibu hilo ni la Munishi anaweza
kukuita Yoshua sina jibu hapo kwako japo ungeuliza umma ningekwambia
enda shule uje uongoze nchi. hata hivyo nakushauri uanze kuongoza
japo akina mama tuone kabla siku hajijaja utakapo sema sina
nguvu tena maana utakuwa mzee tena.. NAWATAKIA KILA LA KHERI.
KENEDY ALIILA GREYSON Rodnat Mwenda ni Mwenda Wazimu: Asema Munishi Mtu mwenye akili timamu hawezi kusema Tanzania ni kisiwa cha amani baada ya jumuia ya kimataifa kusema uchaguzi haukuwa huru na haki.Kilichofuatia ni mauaji ya watu waliokuwa wakidai uchaguzi urudiwe.Tanzania ni mbaya kuliko huko mnakofikiri hakuna amani.Rwanda Uganda Somalia Sudan ndio wimbo wa wanasiasa wa Tanzania kwamba sisi siyo kama wale wasio na Amani.Sasa wimbo umebadilika. Waganda wanasema Nyerere alipoteza pesa za watanzania kupigana na Amin kwa sababu hakumwamini, Lakini madhara ya Amini uganda yameisha japo yuko hai, wakati madhara ya Nyerere Tanzania yanaendelea kuwaathiri Watanzania japo Nyerere alikufa. Ikiwa huo ndio unaouita uchaguzi ndani ya kisiwa cha amani anayotaka kuivuruga Munishi, Basi nitakuwa na kosa gani nikikuita Mwenda Wazimu? Utulivu wa Watanzania hauna maana ya amani. Jela wametulia lakini hawana amani wao wenyewe.Paka ni mtulivu, lakini utulivu wake unaisha wakati unapompiga huku umefunga mlango.Serikali ya CCM inawapiga Watanzania huku imefunga milango yote ya mawasiliano.Tunaishukuru nishati ya kisasa inayotuwezesha kutoa maoni yetu japo Mwenda Wazimu anasikia kichefuchefu. Cha ajabu ni kwamba wananiomba nafasi ya kusikika kwenye mtandao wa kompyuta duniani, Na tayari nimewapa, wakati wao wanaizuia kaseti yangu isisikike Tanzania.Watanzania wenzangu waliwekwa ndani kwa kosa la kuwa na kanda ya Munishi toleo la saba iliyokuwa na maneno CCM imezeeka isirudishwe madarakani. Wengi walipewa dhamana baada ya kuwahonga polisi laki tatu wengine laki mbili.Kitendo hicho ndicho kilichonipa uchungu mkubwa wa kuandika yote niliyoyaandika.Isitoshe maofisa usalama wa taifa walikuwa wakitunga uvumi wa kuniharibia sifa yangu na kuusambaza Tanzania nzima.Kwanza walisema mke wangu ametoroshwa na mzungu, wakaona haitoshi wakasema Munishi alikuwa jambazi, sasa wamekuja na mpya wanasema Munishi siyo Mtanzania kwa sababu alikwenda Kenya. Nashukuru kwamba watu wamekuwa wakipuuza uvumi huo kwa uzito unaostahili kwani ni uongo mtupu.Mke wangu hajawahi kutoroshwa na yeyote wakati wowote.Pia mimi sijawahi kuwa jambazi wa kawaida wachilia mbali kuwa jambazi sugu.Nilizaliwa Moshi Kindi chini Muyuni, Nikaishi Dar es Salaam kwa miaka mitatu nikifanya biashara ya kuuza sigara Kurasini nje ya Shirika la usafiri Dar es salaam UDA na kuishi Keko Magurumbasi. Hiyo ni kuanzia 1975 mpaka 1978 nilipohamia mjini Arusha Kaloleni nikiwa mchoraji wa picha na kuandika vibao vya matangazo mbalimbali katika kituo cha mabasi mjini Arusha mpaka mwaka 1980 nilipookoka na kuanza kuimba nyimbo za Injili.Niliishi na watu wengine wako hai na wengine wamekufa. Waulizeni wale walio hai nilimwibia nani? Sijatumwa na mwanasiasa yeyote,wala kikundi chochote cha kisiasa.Nimeokoka na bei yangu ni ghali sana kuweza kununuliwa na wanasiasa. Niyasemayo ni kweli tupu na Mungu ni shahidi. Juzi
majambazi walinivamia nyumbani kwangu na kuiba kila kitu.Huo
pia ni ukweli mtupu.Siwezi kutunga uongo eti nimeibiwa wakati
sijaibiwa.Itanisaidia na nini? Kuna kitu huyu Mwenda Wazimu
anatakiwa ajue.Kwamba mimi siwezi kusema uongo. Ninayoyaimba
na kuandika yanatoka moyoni mwangu na kamwe siwezi kujigeuza
debe la wanasiasa.Inavyoonekana huyu Rodnat Mwenda anafanya
kazi na kikosi cha propaganda cha CCM. Wanakiita Maofisa Usalama
wa Taifa, lakini wanalinda CCM kuliko Taifa la Tanzania.Wanatumia
mabilioni ya pesa ili kuhakikisha kuwa Tanzania hainuki mtu
au kikundi cha watu watakaosikika kuliko CCM. Asitufanye wajinga
barua zote mbili yaani yake Mwenda Wazimu na ile ya Kennedy
Aliila ameandika mtu mmoja. |
Gospel tape banned by Dar officials Majambazi Wamvamia Munishi Nyumbani
|
|||||||||||