![]() |
![]() |
|
|
|
||
|
Gazeti
INJILI
Kwenye Internet
http://munishi.com Tel. 254722602445 E-mail: munishifaustin@yahoo.com Or fmunishi@hotmail.com Nairobi Leo
Maoni yetu kuhusu mzozo wa Israel na Palestina Mwanadamu aliyenyimwa haki zake za msingi na akawa hana la kufanya ila kujiua na wale anaowaona kama wakandamizaji, ni makosa kuwahurumia wale aliokufa nao kuliko huyu aliyejitoa mhanga, kwani wote wamekufa. Muhimu ni kujiuliza kwa nini huyu kijana wa kike miaka 18 ameamua kufanya kitendo hicho cha kuyatoa maisha yake mhanga? Bila kuangalia chanzo, tunaweza kusema au kutenda mambo yatakayochoche wengi kujitoa mhanga na hali ikawa mbaya zaidi. Vyombo vya habari pamoja na kazi nzuri vinavyofanya huko mashariki ya kati, nasikitika kusema kwamba vinaonyesha kuwahurumia zaidi raia wa Izraeli waliouawa kuliko wanaharakati wanaojitoa mhanga. Tusijidanganye tatizo la Wapalestina na Wayahudi ni kubwa kuliko linavyotangazwa kwenye vyombo vya habari na hasa vile vinavyowaunga mkono Amerika na sera zao mbovu za kumwita kila mtu Ghaidi.
Waandamanaji wakiwa wamebeba bendera na picha ya kiongozi wa Palestina Yasser Arafat karibu na ubalozi wa Amerika Beirut Lebanon. Laiti waandishi wangechimba kiini cha tatizo lenyewe na wakemee pale inapostahili, tatizo sasa lingekuwa katika hatua za mwisho kumalizika. Lakini kwa mtaji huu wa vyombo vya habari kujifanya kuwa havifungamani na upande wowote, tatizo ndio kwanza linaanza. Kwenye suala kama hili ni hatari sana kujifanya uko katikati. Mimi nimeamua kuwa upande wa Wapalestina labda nishawishiwe vinginevyo. Majeshi ya Israeli yakitumia vyombo vya kisasa vya kivita wamezikalia sehemu za Wapalestina wasio na silaha. Mnategemea Wapalestina wafanye nini? Wamekata tamaa ya kuishi wameamua kujiua, na wanapojitoa mhanga waandishi mnawaona Waisraeli ni bora kuliko Wapalestina waliojitoa mhanga? Basi waundiwe jeshi lao lenye nguvu sawa na lile la Israeli ili vita ya kweli ianze. Mambo yakiwa hivyo nami nitabadili msimamo wangu niwe katikati bila kufungamana na upande wowote. Lakini kwa hali ilivyo sasa, nawaunga mkono Wapalestina katika juhudi zao za kupambana na wavamizi.
Nairobi Cty
Invesment & Morngage House
KBC
Maneno yao ni kweli hata kama kuna kasoro za hapa na pale, Ukweli unabaki kwamba wasanii wengi wa nyimbo za injili walisaidiwa na KBC kuwafikia walengwa. Karanja Kimwere akitumia vipindi kama "Sing and Shine" na "Joy Bringer" aliwatumia wasanii kwenye vipindi hivyo na ikawa ndiyo njia ya kusikika nchi nzima na hata nje ya mipaka ya Kenya. Watangazaji wa redio nao walichangia pakubwa katika kuwafanya wasikilizaji wasikize nyimbo za Injili kuliko zile nyingine za kidunia. Ilifikia mahali ambapo nyimbo za Injili ndizo zilizotawala anga la Muziki Kenya na Afrika mashariki, na mpaka sasa bado zinatawala.
Wito wetu ni kwa vituo vipya vya redio na Tv: Igeni mfano wa KBC wa kuwainua wasanii wa humu nchini na Afrika kwa ujumla. Inashangaza kuona redio nyingi mpya bado zinacheza nyimbo za wasanii wa nchi za magharibi na kuwaacha wasanii wetu bila chombo cha kuinua sanaa yao. Kuna mtu aliyeanza kuwainua hao mnaopenda kucheza nyimbo zao sasa. La kama hakuanza msingewasikia kama na wasanii wenu wasivyosikika huko katika nchi za magharibi. Wanajiuliza kama vyombo vyao vya habari haviwatambui, sisi tutaanzia wapi hata kugusa sanaa yao?
Na mkifanya fujo mtapambana na hawa ambao hawapokei kitu kidogo. Hawa wote wameokoka. Kwa hiyo ukikutana nao ni mawili uende ndani au wakusamehe baada ya kukusomea maandiko matakatifu ya Mungu. Bwana Asifiwe anayeokoa hata Polisi wa Kenya.
Safaricom ndio waliofungua dimba la simu za mikononi Kenya. Bei zao wakati huo zilikuwa kuanzia Kshs. 130,000 ili uweze kuwa na simu pamoja na laini yake. Bei za juu zilifanya huduma hiyo kuwa ya watu wanaojiweza kimaisha hasa wauza madawa ya kulevya pamoja na wanasiasa. Kampuni ya pili ilipoingia kushindana na Safaricom bei zilishuka ghafla kutoka Kshs.130,000 mpaka Kshs. 4,500 tu. Sasa hivi kila mtu anaweza kuwa na simu ya mkononi. Wengi wanaishukuru Kampuni ya KenCell kwa kuiona kama MKOMBOZI, japo Safaricom wanaweka bei zao chini kinafiki ili kuwapa ushindani KenCell ambao hawakuwahi kuuza huduma yao kwa kiwango cha juu kama walivyofanya Safaricom. Wengine husema kwamba hata kama Safaricom watatoa huduma zao bure, hiyo ni kama kurudisha zile nyingi walizochukua hapo awali.
KenCell pamoja na kuwa na mtandao wa kisasa usio na matatizo wakati wa kuunganisha simu, lakini bei zao kwa dakika moja ya mawasiliano ni ghali kulinganisha na kiwango cha mapato ya wengi. Wengi wanalazimika kwenda Safaricom bila kupenda kutokana na malipo rahisi , lakini hatujui ni mpaka lini.KenCell waliangalie hilo kwa makini na hakika wateja wengi watawaunga mkono kwani wao ndio walioleta MAGEUZI ya simu za mikononi Kenya.Wanasema kutangulia siyo kufika. Lakini aliyekutangulia akitumia kutangulia kwake kuchuma kwa wingi, anaweza kukupa ushindani na mapato yake ya awali ambayo sijui kama niyaite haramu au halali. Hapo misaidie kuamua.
Bonyeza hapa kwa picha zaidi NAIROBI LEO 2 Gospel
tape banned by Dar officials
|
||
|
Faustin
Munishi Tell. 25472602445 Nairobi Kenya East Africa
E-mail: fmunishi@hotmail.com | munishifaustin@yahoo.com You are Visitor Number since 14th February 2001 |
||