Ukurasa wa mbele
Gazeti la injili
Nyimbo za Munishi
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail
Tuma SMS duniani
Sema nami
Sikiliza waongo

Twende kanisani

CNN
TBN
BBC
Times
Islamtz.org
Winners
Maranatha
Intergrity

China Today

Japan Times

Korea Online

China Site

China Maps

USA Today

Google Seach

China English

Gv China

China view

China news

China
Natinal
News

China Tech

India News

India Times

India Daily

Gospel of
Jesus

USA Gospel

Gospel
Church

Dubai news

Africa News

Gospel Music

US VISSA

BBC
Bush
Curches
Gospeltv
munishi
Mkapa
usgospel
Times
GTV
GTVGOSPEL
Jesus
God
Faith
Life
Kenya
Tanzania
Uganda
Africa
Japan
Toyota
China
Korea
India
Nation
News
Online
Nyerere
Kibaki
Museveni
Mugabe
KOFFI ANNAN
Nairobi
Dar
Goverments

 


Wamasai wanaohubiri kwenye Redio Biblia Husema maarufu kama Shonara Ole Riambati na Samiet Ole Leteipan wameigiza kipindi "Hakuna nuru gizani" Bonyeza hapa chini usikize kipindi.

MASAI: Hakuna Nuru Gizani!!

Serikali Kenya yatishia kubomoa Kanisa

Wanasema Kanisa pamoja na majengo mengine yako barabarani na ni lazima yabomolewe. Ni amri ya serikali. Tunaomba iwe siyo kulipiza kisasi. Mke wa Muiru alikuwa na bado ni kipenzi cha chama kilichotolewa madarakani KANU. Wakati wengine walilipa kutumia ukumbi wa KICC, Yeye alipewa bure kuutumia ukumbi huo apendavyo. Hata kama alilipa basi ilikuwa sawa na bure.

Lakini hii haiwapi haki serikali ya sasa kulibomoa kanisa la MAXMAM MIRACLE CENTRE. Pamoja na kwamba Muiru amekiri kutokuwa na hati ya kumiliki eneo lilipojengwa kanisa, kama walipata kihalali hakuna mwenye haki ya kuwanyanganya kwa kisingizio cha barabara. Picha inaonyesha wazi kwamba barabara ziko mbili na kuna nafasi kubwa katikati na pembeni kuiongeza barabara husika bila kuharibu mali za raia na hasa makanisa ambayo ni mahali pa kumwabudu Mungu.

Dunia na Vyote ni mali ya Mungu.

Inashangaza kuona kwamba ili wahubiri wapatiwe sehemu za kujenga makanisa, lazima wajipendekeze kwa wanasiasa. Tatizo ni wakati wanasiasa wanapotolewa madarakani na wengine kuingia. Dunia ya Mungu chini ya sheria za wanasiasa. Mpaka lini tutaendelea kunyanyaswa kwenye dunia ya muumba wetu? Hivi kweli sehemu za kuabudia zinaweza adimika kiasi ni lazima tuwapigie magoti wanasiasa? Wao waliumba dunia gani mpaka kibali cha kujenga mahali pa kuabudia watoe wao?

Hatupingani nao, ila wafanye waonavyo ni vyema. Lakini wajue Mungu mwenye dunia na kila kitu mpaka maisha yao anawatizama. Hawawezi kutudanganya kwamba tuna UHURU wa KUABUDU wakati kupata sehemu ya kuabudia ni kitendawili. Sheria hutungwa na watu kwa ajili ya watu. Sheria zinapotumika kuwabomolea watu mali zao, ni wakati wa watu kutunga sheria nyingine za kuwajengea watu mali zao. Amri za Mungu hazibadiliki kwani hazina makosa. Sheria za wanadamu zinatakiwa zibadilishwe kila mara kwani wanadamu wana makosa mengi. Nini kinachowafanya mfikiri kwamba sheria za sasa hazina makosa?

KWAMBA TAFSIRI YA SHERIA INAWEZA PINDISHWA ILI IWAADHIBU WANAOTAKIWA KUADHIBIWA NAYO HILO NDILO LINALOTUPA MASHAKA. JE! NIA YA SERIKALI NI KWELI KULINDA SHERIA NA UTENGAMANO AU KUWATAFUTA WALIOIUNGA MKONO SERIKALI YA AWALI ILI WAADHIBIWE. SERIKALI YA SASA INATAKA KUUNGWA MKONO. JE INATAKA WANAOWAUNGA MKONO SASA NAO WAJE WAADHIBIWE NA SERIKALI IJAYO? AU WATATAWALA MILELE? KILA LA KHERI.

Pastor Pius Muiru Wahubiri wanampiga vita, na sasa SERIKALI? Lazima tusimame na Mtumishi huyu wa Mungu wakati huu wa mateso kutoka SERIKALINI. Wanasema ukiona mwenzako ananyolewa kichwa tayarisha. Hujui zamu yako ni lini. Hata kama Rais ni MKATOLIKI, hatuwezi kulazimishwa wote tuwe wakatoliki. Haiwezekani.


Tangaza Biashara yako Bure
Tuma picha na maelezo kwa munishi@munishi.com

http://munishi.com
FREE!

Send photo and information to munishi@munishi.com


Redio Injili FM
Sasa unaweza kuisikiliza Redio INJILI FM OnLine. Bonyeza Hapa

Wimbo mpya CCM imewatesa wengi
Wanahabari Wanafiki
MASAI: Hakuna Nuru Gizani!!
Hotuba ya Munishi kwa TAIFA


Redio Injili FM

Sasa unaweza kuisikiliza Redio INJILI FM OnLine. Bonyeza Hapa

Hii ni redio Injili FM, inayokutangazia katika masafa ya INTERNET www.munishi.com Yesu ni nuru ya ulimwengu, Alikuja tutoke gizani. Giza na nuru hazikai pamoja. Yaani hakuna nuru gizani. Mungu anakupenda jinsi ulivyo. Ukimwamini na kutubu makosa yako utaokoka. Huwezi kuokoka ndipo uamini baadae. Hapana. Kwanza unaamini, kisha unatubu, na ndipo Mungu anakusamehe na kukupa uwezo wa kufanyika mwana wa Mungu. Uwezo wa Mungu ndani yako ndio wokovu. Unaendelea kuisikiliza redio Injili FM, inayokutangazia katika masafa ya INTERNET www.munishi.com

Ukisha pokea msamaha wa dhambi, omba lolote kwa Mungu na maombi yako yatajibiwa. Katikati yako na Mungu ni Yesu peke yake. Siyo Mchungaji wala Askofu. Omba mwenyewe kwa jina la Yesu, na Mungu atakujibu maombi yako. Baraka za Mungu hazinunuliwi kwa pesa. Huwezi kumhonga Mungu ndipo akubariki. Mungu ni tegemeo letu sote. Wachungaji na washirika, tunatakiwa kumtegemea Mungu kwa baraka zetu. Siyo wachungaji wawategemee washirika kwa baraka zao, huku wakiwaambia washirika wamtegemee Mungu. Nani walio katika nafasi nzuri zaidi kumtegemea Mungu? Unaendelea kuisikiliza redio Injili FM, inayokutangazia katika masafa ya INTERNET www.munishi.com

Je baraka za Mungu zinawezaje kumpita mchungaji ziwaendee washirika ili washirika wambariki mchungaji? Siku hizi washirika wanawinda baraka zao kutoka kwa wachungaji, Wanasahau kwamba hata wachungaji wanawinda baraka zao kutoka kwa washirika. Wanajiunga na makanisa yaliyovuma ambayo wachungaji wake wanatembelea magari makubwa na kuishi kwenye mitaa ya kifahari. Lengo ni ili na wao wafanikiwe kimaisha. Wakifika wanashangaa kukuta mchungaji anawategemea ili wayalipie maisha yake ya kifahari. Walienda kutafuta mafanikio, wanarudi wakiwa masikini kuliko walivyokuwa. Walikosea lengo. Tunatakiwa kumtafuta Mungu kwanza, na hayo mengine tutazidishiwa. Hiyo ndiyo INJILI. Jiunge na kanisa kwa lengo la kuutafuta uhusiano wako na Mungu. Usijali kama kanisa hilo lina watu wengi au la. Nani alikudanganya kwamba wengi hawawezi kuwa wamepotea njia? Jiunge na wale wanaomtafuta Mungu kwa moyo wao wote hata kama ni wachache. Sikiliza sauti yake

UPONYAJI

Unaisikiliza redio Injili FM, inayokutangazia katika masafa ya INTERNET www.munishi.com Hujambo msikilizaji. Tunamshukuru Mungu kwa ulinzi wake maishani mwetu. Ndiyo maana tunamtukuza na kumwabudu siku zote. Shetani ni muongo. Lazima tupambane naye kila iitwapo leo. Anatumia kila mbinu kuwapotosha watu wa Mungu, Lakini Bwana Yesu asifiwe kwani tumezigundua hila zake. Alifikiri akiwatumia wale wanaojiita wahubiri hatutamgundua. Alijidanganya. Tunajua kwamba yeye huweza kujigeuza na kuwa kama malaika wa nuru. Hatujali atatumia nani, lakini tukiziona dalili zake popote na kwa yeyote tutamkemea arudi kuzimu. Unaendelea kuisikiliza redio Injili FM, inayokutangazia katika masafa ya INTERNET www.munishi.com

Kifo cha Yesu msalabani na hatimaye kufufuka siku ya tatu kilimaanisha mengi kwetu tunaomwamini. Sasa tunapokea msamaha wa dhambi, Wokovu wa roho, Uponyaji wa mwili, na baraka maishani Bure. Mtu asikufanyie sarakasi, mbembwe, vitimbi, eti akusukume uanguke ndipo upokee uponyaji. Injili ya Yesu inasimamisha haiangushi. Shetani kazi yake ni kuangusha kwani mwenyewe alianguka kitambo. Ukiona mahali watu wanaombewa na kuanguka anguka hovyo ujue shetani ana mkono wake hapo. Kama nguvu za Mungu ndizo zinazowaangusha, mbona mhubiri huwa haanguki? Unaendelea kuisikiliza redio Injili FM, inayokutangazia katika masafa ya INTERNET www.munishi.com

Wengine wanasema wanafanya miujiza kumpita Yesu. Sawa. Je kiutakatifu pia wamempita Yesu? Nina mashaka kama hata wanamkaribia.Hii ni mbinu ya shetani kuongeza chumvi kwenye injili. Tunaikemea katika jina la Yesu ishindwe. Ndiyo ninaamini kwamba Yesu anaponya. Tatizo langu ni watu wanaotumia uponyaji wa Mungu kujinufaisha kibinafsi. Mungu ndiye anayeponya na siyo mhubiri. Uponyaji wako unategeme Mungu na wewe kuliko mhubiri. Hata kama ana nguvu za kuangusha watu, na pengine siyo nguvu za Mungu, haina maana kwamba wewe utapona kwa kuitumia imani yake. Haiwezekani. Kama hujaisikia injili vya kutosha imani yako ijengeke, hata ukiangushwa mara ngapi. Haitaleta tofauti yeyote. Utaangushwa uanguke, ukiamka utakuwa umepoteza pochi na viatu, lakini bado utakuwa mgojwa kuliko mwanzo. Ukimuuliza huyo mhubiri wa vituko, mbona hujapona, utaambiwa kwamba hujatoa fungu la kumi. Utauza gari na shamba ulete pesa zote kwa mhubiri huyo tapeli, lakini bado hali yako itazidi kuwa mbaya. Ni mpaka uijue kweli ya Injili ndipo utawekwa huru. Kweli inasema kwamba kwa kupigwa kwa Yesu wewe ni mzima. Siyo kwa kuangushwa chini. Pole sana. Unaendelea kuisikiliza redio Injili FM, inayokutangazia katika masafa ya INTERNET www.munishi.com

Yesu katika mahubiri yake hakufanya maonyesho tunayoyaona na wahubiri leo. Alihubiri na kufundisha kweli ya Mungu, walioamini walimwendea ili awaponye, aliwaambia wapokee kadiri ya imani zao.Yesu hakuwahi kuwaombea wagonjwa wakakosa kupokea uponyaji wao. Tena Yesu hakutumia imani yake kuwaponya wagonjwa. Kila mara aliwauliza waliomwendea kama wanaamini anaweza kuwatendea wanayohitaji. Walipojibu ndiyo, aliwaambia wapokee kadiri ya imani zao. Leo hii wahubiri wanawaita wagonjwa waje wawaombee siyo wawahubiriwe injili. Ndiyo maana wengi hawaponi. Huwezi kupona kwa kuitegemea imani ya mhubiri.Unatakiwa uwe na imani yako. Imani kwako itakuja baada ya kusikia Neno la Mungu. Unataka mafundisho ya injili uijue kweli ikuweke huru. Wacha kuwa na imani tegemezi kwa wahubiri. Imani zetu zinatakiwa kumtegemea Mungu pekee. Ukiiamini Injili, Utubu usamehewe, halafu Mungu akupe uwezo wa kufanyika mwana wa Mungu, Huwezi kuangushwa kwa madai kwamba unaombewa. Utamuomba Mungu kwa imani yako, na Mungu atakuponya. Soma neno la Mungu kila siku, kwani ndilo litakalokujenga kiimani. Imani yako ikikua, utawaona wengine wakiangushwa na kudanganywa lakini wewe utasimama imara. Yesu alipomfufua Lazaro ilibidi atumie imani yake kwani Lazaro hakuwa hai kuamini. Wewe uko hai. Imani yako inahitajika sana katika kusababisha muujiza wako. Sikiliza sauti yake

Wimbo mpya CCM imewatesa wengi

Wanahabari Wanafiki

MASAI: Hakuna Nuru Gizani!!

Hotuba ya Munishi kwa TAIFA

Washirika Nairobi wa nani?

Nairobi washirika ni sawa na Kondoo waliokosa Mchungaji. Walitoka kwa Mchungaji Mwarandu wakajiunga na Pius Muiru. Sijui waliona nini kwa Muiru, wakahama kwenda kwa James Maina Nganga. Sasa Pastor Nganga anawatingishia funguo za Benzi aliyonunua kwa pesa zao. Nasikia kwamba hata kwa Nganga hawakai. Safari hii sijui wanataka kuhamia kwa nani? Muiru ambaye alikuwa akitamba kuiteka Nairobi na Injili, amejikuta bila wathamini baada ya kundi kubwa la matajiri kulihama kanisa lake. Hata mbinu za kuhubiri imembidi abadilishe. Badala ya mahubiri watu waliomzoea kwayo, sasa Muiru anatabiri kama mganga wa kienyeji. Anakaa mbele ya Camera ofisini kwake, na kuanza kutaja mambo ambayo ni kawaida na ni lazima apatikane mwenye matatizo anayoyatabiri. Mfano akisema kwamba kuna mtu mwanamke mwenye matatizo ya kizazi, na Mungu atamponya kama atatoa shilingi elfu tatu kusaidia huduma ya NURU GIZANI, Lazima watatokea wanawake wengi wenye matatizo kama hayo. Kinachowasumbua wengi akili ni kama baada ya kutoa pesa hizo kweli watapona.

Kundi linalowafadhili wahubiri si watu wengi. Wakiamua kuhama itakuwa vigumu kwa wahubiri kumudu gharama za juu kuendeshea huduma zao.Inasemekana kwamba wahubiri wanaoonekana kwenye TV gharama zao ni Kshs.500,000 kwa juma moja. Sasa matajiri wazito wakihama kama walivyomhama Muiru, Sishangai kumsikia akisema kwenye TV kwamba Bwana amemwonyesha kwamba yule mtu ambaye kanisa limejengwa kwenye shamba lake, asarende hati za kumiliki shamba hilo kwake mara moja, kwani hiyo ni amri kutoka juu kwa Mungu mwenyewe. Wengi walishitushwa na kauli hiyo na wakabaki wakijiuliza nini kitafuatia baada ya kusarenda hati za kumiliki mashamba? Pengine kitakachofuata ni kusarenda wake zetu kwa wahubiri. Mungu asaidie tusifike hapo, lakini kila dalili zinaonyesha tunaelekea hapo. Maisha ya hali ya juu yamewalewesha wahubiri na hawataki kushuka. Lakini Mungu atawashusha.

Wengine wamefikia hatua ya kujitengenezea kile watakachokiita miujiza kwenye TV. Wanachaguliwa watu watakaosema kwamba wamepona ili kuvuta umati kanisani. Wakija wasipone, wanaondoka kimya kimya. Kwa sababu TV bado inatumika kuwatapeli, kila siku hawakosi watu wapya. Wanakamuliwa, wakikauka wataondoka wapishe wengine. Yaani mtindo wa makanisa umegeuzwa na kuwa kama gari la abiria. Linabeba likishusha na hakuna abiria wanaoweza kusema gari ni lao. Makanisa nayo hivyo hivyo yamekuwa ni mali ya wachungaji na familia zao. Washirika hawana lao. Wanachopata ni mafundisho yenye chumvi nyingi, ikiwashinda kumeza, wanaambiwa wameze kwa lazima ya Mungu. Wanatoa na hawaruhusiwi kuuliza pesa hizo zinatumika vipi. Yani Kanisa ni kama KIOSK ya Mchungaji. Anafungua KIOSK asubuhi saa kumi na mbili. Wanaingia kwa maombi ya asubuhi, maarufu kama "Morning Glory" Sadaka asubuhi lazima watoe. Mchana wanakuja maombi ya mchana maarufu kama "Lunch Time Meeting" Hapo pia wataahidiwa ahadi za baraka kutoka kwa Mungu, lakini wao wanapaswa kumbariki Mchungaji wao anunue BENZ ya milioni kumi na tano. Jioni bado watakuja kuombewa baraka pamoja na kupakwa mafuta, kisha wataulizwa kutoa ili kiwanja cha kanisa kinunuliwe. Bei ya kiwanja wataambiwa ni milioni 30 pesa za Kenya. Kila mtu atatoa mpaka akose nauli ya matatu kurudi wanakoishi. Usijali kama kweli kuna kiwanja kinachonunuliwa, au pesa hizo zinatumika kujenga nyumba ya kibinafsi ya mchungaji katika mtaa wa Karen, na hata kama kiwanja kikinunuliwa, na tuna mashaka kama kitanunuliwa, kitakuwa kimesajiliwa kwa jina la mchungaji na siyo Kanisa. Hata washirika wakiamua kumtimua Mchungaji, Hawawezi kulipa madeni ya mamilioni ya shilingi kanisa linayodaiwa na vyombo vya habari ambavyo hurusha vipindi vya mchungaji huyo. Watajiuliza mbona tunachangishwa kila siku kulipia vipindi? Kumbe kwa makusudi Mchungaji halipii vipindi hivyo ili kuwazuia washirika wasije wakawaza kumtimua wachukue usukani Kanisani hapo. Kwa Mchungaji mkimtimua atachukua mkoba wake aondoke awaachie kiwanja ambacho siyo mali yenu, Tena hakuna dalili zozote kuonyesha kwamba kiwanja husika kinatarajiwa kuwa mali ya kanisa, Nadhani wengi watazimia kuambiwa kwamba kiwanja hicho hakijalipiwa chochote. NI ugumu huo ndio unaowafanya washirika wakose nguvu ya kudai haki zao. Nasi tunauliza. Mpaka lini wahubiri matapeli wataruhusiwa kuwaibia watu mchana machoni pa Serikali na kila mtu?

 


Bonyeza hapa usome zaidi

Nyerere Msingi aloujenga Tanzania haufai, Tuubomoe.
Ujamaa ulishindwa, kwani CCM alioanzisha Nyerere sasa imezeeka. Sera zake zimeiharibu nchi yetu Tanzania. Tunataka mapinduzi tuitoe CCM madarakani ili tusinyanyaswe tena. Tumeonewa vya kutosha. sasa basi. CCM hatuitaki, imetufika shingoni. Tutaitapika.Mungu bariki Watanzania, wape hekima ya kutosha kuiweka CCM kapuni. Chukua usukani sasa kuiongoza Tanzania kwani kwa kipindi kirefu nchi yetu iliwekwa wakfu kwa shetani mpinzani wako. Tunamkataa shetani na CCM chama anachotumia kuwatesa watanzania, na tunaiweka nchi yetu mikononi mwako. Tumeomba machache hayo katika jina la Yesu Mwokozi wetu. Amen HABARI ZAIDI



GOSPELGTV.COM
.com

TV ya INJILI
Kwenye Internet
-
WWW.GOSPELGTV.COM

Tel. 254722602445 E-mail:
munishi@munishi.com or info@munishi.com


Hakuna Uchaguzi Tanzania bila Katiba mpya

GOSPELTV WATCH PRO-LIFE VIDEOS


GTV Online

Gospel Television ambayo Studio zake ziko Nairobi Kenya, Sasa itaanza kurusha matangazo yake kutumia Internet. Mipango yote imekamilika na tuko mbioni kukamilisha ile ya kiufundi ili tuwe Online ulimwenguni kote. Endelea kuutupia macho ukurasa huu. Kwa sasa unaweza kuisikia sauti ya GTV. Habari zaidi

Gospel Redio FM
Sasa unaweza kuisikiliza Redio INJILI FM OnLine.
TAHARIRI: Wahubiri Tegemeeni Mungu

Wimbo mpya "Nateseka Natukuza"
"Wanahabari Wanafiki" Wimbo
MASAI: "Hakuna Nuru Gizani" VICHEKESHO
Hotuba ya Munishi kwa TAIFA
"Yesu atakuponya bure" TAHARIRI
Wimbo mpya "Mpende Adui "
GUMZO"Aibu wanahabari!! "


Habari za hapa na pale

Kenedy Ochieng Asema ana UKIMWI Mugabe na Mkapa lao moja
Gospel tape banned by Dar officials Vituko Makanisani Sokoni Gikomba
Munishi Magazetini

Hotuba ya Munishi kwa TAIFA

Ajali ya Kutisha


Moja kati ya ajali mbaya Tanzania HABARI ZAIDI
Gazeti la "MWANANCHI" Tanzania lafichua
www.mwananchi.co.tz

Umewahi kujiuliza kwa nini mabalozi wa Tanzania nchi za nje karibu wote ni wanajeshi wastaafu? Je Serikali huwatumia kufanya ukachero kwenye nchi hizo? Au hujihusisha na mambo ya kidiplomasia kama yalivyo? Je wanajeshi na wanadiplomasia ni taaluma moja? Kwa nini Serikali zote tangu Nyerere zimekuwa zikifuata desturi hiyo? Je ni mbinu ya kuwatawanya wanajeshi ili wasiweke vichwa pamoja kuitoa serikali dhalimu ya CCM? Hayo na mengine mengi, Mwandishi wetu atayaangalia katika makala haya. Habari zaidi

"Standard" Kenya Latoboa siri


Kikwete siyo Wetu!

Wakati Waislamu wameanza kumshuku Kikwete, Wakristo nao wanasema Kikwete siyo wao. Magazeti yenye misimamo mikali ya Kiislamu yamemtaka Jakaya Mrisho Kikwete atangaze msimamo. Ama aachane na Uislamu abatizwe awe Mkristo, au abaki Mwislamu. Walihoji kwamba Kikwete hawezi kuwa na dini zote mbili. Yaani hawezi kuwa Mwislamu Mkristo. Nao Wakristo kwa upande ule mwingine wanashindwa kabisa kumwamini Kikwete kwani wanajua wazi kwamba yeye ni Mwislamu. Habari Zaidi


Zanzibar Kunaashiria Moto

Pastor Pius Kongo Alaumiwa

Pastor Pius Kongo Aliyekuwa TAG Moshi mjini, kabla ya kufungua kanisa lake ambalo sasa wengi wanamtupia lawama. Mwandishi wetu anajiuliza!
Kwa nini wanamlaumu? Je wanaionea wivu huduma yake inayokua haraka? Yuko Mjini Moshi, katika mtaa wa Majengo, nchini Tanzania. Mwandishi wetu alipata nafasi ya kuzungumza na wakazi wa Majengo na kupata maoni yao kuhusu huduma ya Mchungaji Pius Kongo. Pia Kutoka Meru Kenya, Dada Penina ana mengi ya kusimulia baada ya kuhudumu na Mchungaji P.Kongo. Yeye anasema:,
"Safari yangu Moshi yaashiria Moto"


Mwimbaji wa nyimbo za Injili Kutoka Meru Nchini Kenya Penina Muthoni, Akiwa katika ofisi za GTV Nairobi hivi karibuni. Anasimulia masaibu yake alipokuwa Moshi Tanzania akiwa mgeni wa Pastor Pius Kongo. Nao Waciama Vijana mashuhuri wa kuimba nyimbo za Injili Kenya wanasema Walipokuwa Moshi walijionea Mengi.

Sammy Waciama na Jeff Waciama Habari Zaidi


James Kim Atoa kanda mpya

Waislamu wamlalamikia Mwinyi

Aliyekuwa Rais wa awamu ya pili Tanzania Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi Watanzania wanamheshimu kwani yeye ni nyota ya mabadiliko Tanzania. Alikuwa na ujasiri wa kupinga sera za Nyerere akiwa hai, na kuleta mageuzi Tanzania ambayo Mkapa ameyadidimiza matumaini ya Watanzania. Habari Zaidi

"Kikwete Tosha" asema Mchungaji

Mchungaji Paul M.K. Mduma Akiwa katika Ofisi za GTV alielezea masikitiko yake kwamba, vyombo vya habari vimeanza kumchafua Kikwete aliyemjua tangu akiwa mwanafunzi Kibaha Secondary School. Alidai kwamba walisoma wote kwa muda wa miaka minne. Tangu mwaka 1966 hadi 1969 Habari Zaidi

Waruinge Atawazwa Uchungaji

Alikuwa kiongozi wa kundi la Mungiki ambalo Serikali ya Kenya ililiita "kundi haramu" Aliokoka mwaka 2003 na miaka miwili baadaye alitawazwa kuwa Mchungaji Hezekia Ndura Waruinge

Washirika Nairobi wa nani?

Nairobi washirika ni sawa na Kondoo waliokosa Mchungaji. Walitoka kwa Mchungaji Mwarandu wakajiunga na Pius Muiru. Sijui waliona nini kwa Muiru, wakahama kwenda kwa James Maina Nganga. Sasa Pastor Nganga anawatingishia funguo za Benzi aliyonunua kwa pesa zao. Nasikia kwamba hata kwa Nganga hawakai. Safari hii sijui wanataka kuhamia kwa nani? Habari Zaidi

Kikosi cha Living Water Kawe

Waimbaji wa kikundi cha Living Water wakiimba nyimbo za kumtukuza Mungu

Komba Ajikomba na CCM

Wanamwita "Kapteni" Komba Msanii anayetumia sanaa yake kuwatukuza wanadamu badala ya Mungu. Sasa anajuta kuwapandisha wanasiasa ngazi huku mwenyewe akibaki chini.Anasema kama siyo yeye Mkapa asingeuona Urais na hatimaye awe tajiri wa kutisha Tanzania. Mkapa alimsahau Komba mara tu alipoingia Ikulu. Mungu anamwita Komba amtumikie. Uzee unapomnyemelea Komba, laiti angeona mwanga amtukuze Mungu badala ya wanasiasa waongo.Kila la Kheri Bwana Komba.

Padre Atuhumiwa kwa UBASHA

Padre Sixtus Kimaro Akiwa mahakamani Kisutu Dar.
Ameshitakiwa kwa tuhuma za kumlawiti mvulana wa miaka 17
Sisi tunasema "Lisemwalo Haliko, Kama liko, Lilikuwepo." HABARI ZAIDI

Simbeye Mchawi Aliyeokoka


Bwana Zebius Mulingwa Simbeye Akiwa na Joyce Wairimu Maina Kericho Kenya


Mtoto apatapo Mtoto


Siri za Kakobe



Askofu Nnko ailalamikia Serikali


Kuishi Amerika ni haki yako


Samples. 6 second of every song

SIDE A

  1. Mpende Adui
  2. Wahariri Watubu
  3. Yesu Bima Tosha
  4. Kuhubiri ni Taluma
  5. Maji Yana Mdudu
  6. Gazeti Siyo Ugali

SIDE B

  1. Yesu Aponya
  2. Jirani Mchokozi
  3. manabi.wav
  4. Rushwa Adui
  5. Msiabudu Amerika
  6. Baba Nakuabudu

SIDE A

  1. Malebo
  2. Usichanganye
  3. Yesu Mambo Yote
  4. Ukimwi Na Maisha
  5. ? Wanamwabudu Nani ?

SIDE B

  1. Yesu Nakupenda
  2. Mageuzi Na Injili
  3. Kazi Na Wanawake
  4. Maombi
  5. Yesu Mwanzo Na Mwisho

SIDE A

  1. Yesu Aliniita
  2. Bwana Nashangaa
  3. Tuonane Milele
  4. Wamwendea Yesu
  5. Msalabani Pa Mwokozi
  6. Yesu Kwetu Ni Rafiki

SIDE B

  1. Bwana Uliyewaita
  2. Kumtegemea Mwokozi
  3. Sioni Haya Kwa Bwana
  4. Yesu Unipendae
  5. Yesu Nakupenda
  6. Ati Tuonane Mtoni

SIDE A

  1. Makosa Ni Kosa
  2. Fikiri Mwanadamu
  3. Dhambi Ni Nini
  4. Yesu Anaokoa

SIDE B

  1. Ajirekebishe
  2. Kaka Ananitesa
  3. Christmas
  4. Anarudi Yesu

SIDE A

  1. Chini Ya Mwamba
  2. Paulo Na Sila
  3. Kifo Mapatano
  4. Nimekukimbilia Nisiaibike
  5. Upendo Ule Wa Kwanza

SIDE B

  1. Salama Rohoni
  2. Hakuna Mungu Kama Wewe
  3. Nimuogope Nani
  4. Huna Cha Kujivunia
  5. Amua Mwenyewe

SIDE A

  1. Ninyime Vyote Niachie Yesu
  2. Maisha Yalitisha
  3. Fashoni Ni Yesu
  4. Anakuita
  5. Waokoe Vijana
  6. Uliyaona Zamani?

SIDE B

  1. Ulimi
  2. Pesa
  3. Dhambi
  4. Siku Za Mwisho
  5. Nielezeje

Gospel Television Moto wa kuotea mbali

Ikiwa ndio kwanza inajitayarisha kurusha matangazo yake, GTV imekuwa tishio kwa Serikali Tanzania. Aliyekuwa Rais wa kimabavu nchini humo William Benjamin Mkapa aliamuru polisi wawatie mbaroni wote watakaopatikana na VCD za GTV. Kisa ni kwamba Gospel Television ilikuwa imezungumzia uwezekano wa Mkapa kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa kutumia madaraka vibaya. GTV ilikuwa imedai kwamba, Mkapa akiwa madarakani aliwaamuru POLISI wawaue Wazanzibari zaidi ya 70 kwa kosa la kusema CCM Chama Cha Majambazi hawakitaki. Pamoja na mambo mengine GTV ilipendekeza tume ya kumchunguza Mkapa iundwe na akipatikana na makosa sheria ichukue mkondo wake. Pia GTV ilidai kwamba Mkapa aliitawala Tanzania kama mali yake binafsi kwani hakutaka ushauri wa mtu yeyote. Bado msimamo wa GTV ni huo na hatuombi msamaha kwa Mkapa wala CCM. Habari Zaidi
Hotuba ya Munishi kwa TAIFA

Twende nikutembeze Nairobi

 

 
| http://www.munishi.com |