Gazeti INJILI Kwenye Internet
http://munishi.netfirms.com

Tel. 254722602445 E-mail: munishifaustin@yahoo.com
Or fmunishi@hotmail.com

MUGABE NA ZIMBABWE TUNAJIFUNZA NINI?

Mr. Mugabe na sera za Mashamba

ZANU PF Chama kinachotawala Zimbabwe hakina tofauti na CCM inayotawala Tanzania. Kwamba Mkapa amekuwa wa kwanza kumuunga mkono MUGABE hiyo ilitarajiwa. Sera za ardhi alizotumia Mugabe siyo kwa manufaa ya wananchi wa zimbabwe bali ni kwa ajili ya kulinda maslahi yake kisiasa.

Mkapa alikuwa wa Kwanza kumuunga mkono Mugabe.

Inasemekana kuwa Mugabe ameshinda uchaguzi, lakini mimi nasema Afrika hakuna chaguzi zinazofanywa. Kama hazitaingiliwa na mataifa ya magharibi, basi vyama vinavyodai kupigania uhuru vitauza sera za kuwaadaa wananchi kwa malengo yao ya kuendelea kuwatawala.


Mheshimiwa Benjamin William Mkapa

Kiongozi wa UPINZANI Zimbabwe pia simuungi mkono kwani alionekana kama kibaraka wa kulinda maslahi ya mataifa ya mahgaribi na UINGEREZA ilikuwa ikiongoza katika hilo. Ni ukweli usiopingika kwamba Zimbabwe inahitaji mageuzi ya kweli, lakini watu wa kuleta mageuzi hayo ndiyo waliokosekana. Sambamba na Tanzania ambayo kama Zimbabwe inahitaji mageuzi ya kweli lakini watu wa kuyaleta mageuzi hayo ndiyo ambao walikuwa hawajapatikana.

Tunamshukuru Mungu kwamba ametukumbuka na kutupa kijana Faustin Munishi ambaye ataleta mageuzi ya kweli Tanzania na Afrika kwa ujumla. Sera za Munishi kukataa kuwa kibaraka wa nchi za magharibi ili asaidiwe kuingoa CCM madarakani ndizo zinazothibitisha kuwa huyu ni mwanamageuzi ya kweli. Kila mara Munishi hutufundisha kwamba huwezi kuwa mtumwa ili uwatoe watu utumwani. Ukifanya hivyo utakuwa umebadili watawala tu na siyo kwamba umeleta mageuzi .

Mwinjilisti Munishi: Nimepewa jukumu kuiongoza Tanzania

Upinzani ungeshinda Zimbabwe bado wananchi wa Zimbabwe wasingeona mabadiliko katika maisha yao kwani wangetoka katika makucha ya chama tawala na MUGABE na kuingia kwenye makucha mengine ya ukoloni wa wazungu ambao ndio mbaya zaidi.

Lakini je sasa wameepuka ukoloni wa nchi za magharibi Hasha hawajaepuka nasikitika kusema kwamba mambo sasa ni mabaya kuliko awali.

Wanasiasa wamewadanganya wananchi kwamba wanafanya kitu kinachoitwa uchaguzi ili maisha yao yawe mazuri zaidi. Ni waongo. Wamepoteza muda wa WAZIMBABWE na kilichopatikana ni chuki zaidi kati ya wazungu na waafrika, chuki kati ya wanachama tofauti wa vyama vya kisiasa, na mbaya zaidi uchumi wa nchi yao umeharibiwa zaidi.

Wazungu waliokuwa wakiunga mkono upinzani kwa kisingizio cha kutaka kuwasaidia wananchi wa Zimbabwe ndio watakaokuwa wa kwanza kuiwekea vikwazo vya kiuchumi nchi hiyo ili wananchi waendelee kuteseka.

Mugabe aliyewaahidi wananchi kwamba atawapa mashamba ya wazungu, sasa atajitahidi sana kurekebisha sera ili aondolewe vikwazo vya kusafiri alivyowekewa kwani utawala bila kwenda ulaya kuponda raha na kununua nguo za bei mbaya huo siyo utawala tena kulingana na mawazo finyu ya viongozi wengi wa kiafrika.

Wananchi wataachwa na shida zao, na Mugabe na wazungu wake watarudiana kama mwanzo. Sitoshangaa kusikia wazungu walionyanganywa mashamba wakirudishiwa na kuruhusiwa kuwanyanganya wananchi wa Zimbabwe mashamba zaidi.

Hiyo ndiyo siasa. Ndiyo maana mimi Munishi siwezi kuwa mwanasiasa. Nitawakomboa Watanzania bila siasa. Kwa Mungu yote yawezekana. Sitokubali kutumiwa na nchi za magharibi ili niwalindie maslahi yao Tanzania kama anavyofanya Mkapa. Angalia kila kitu Tanzania kimeuzwa. Hata wananchi wenyewe sasa wameuzwa. Yote hayo ni matunda ya msingi mbovu alioujenga Nyerere ambao nawaomba mnisaidie ili tuubomoe. WANANCHI nisaidieni kwa hili.

Munishi Akienda zake Nyumbani


Makao Makuu ya Magazeti ya Nation



City Hall Annex
sms Messages
Gospel tape banned by Dar officials

Nina Ukimwi: Asema KENEDY OCHIENG


KENEDY OCHIENG Bonyeza HAPA kwa picha zaidi 2 3 4

Biblia Inasemaje? Ukimwi Unaua Jiadhari- KENEDY Wewe Unasemaje? Mwinyi Aliibadili Tanzania Wewe Unasemaje? Nation TV Yakosa Mwelekeo Wewe Unasemaje? Siasa na Dini Zitenganishwe? Kweli serikali haina dini? Wewe Unasemaje? Waislam Wampora Mkisto Nyumba Wewe Unasemaje? Nyerere Msingi aloujenga Haufai Tuubomoe? Wewe Unasemaje? Mjue Kaka Paul Wewe Unasemaje? "Nisaidieni Nioe" Asema Jeff WACIAMAWewe Unasemaje? Mkapa Hatoki Muda Ukiisha Wewe Unasemaje? Marandu T.L Ajitoa Kwenye "FORUM"Kisha Akarudi TenaWewe Unasemaje?MUNISHI AZINDUA HERALD Wewe Unasemaje? Majira Wajaribu Kumzima Munishi? Wewe Unasemaje? Professor Oloo Amlaumu Mwinyi Wewe Unasemaje? Taliban Wamefanya Kiungu, Amerika walifanya kishetani Wewe Unasemaje? Philip Ochieng attacks Mkapa- Wewe Unasemaje?Moi Aombewa Amalize Vizuri Wewe Unasemaje?Rodnat Mwenda Amshambulia MunishiWewe Unasemaje? SIKU TATU BAADAYE Majambazi Wamvamia Munishi NyumbaniWewe Unasemaje? NYERERE ALISHINDWA MENGIWewe Unasemaje? Leila Asema Alikuwa ShujaaWewe Unasemaje? Wengi Wampinga Leila Wewe Unasemaje? EAGT Dodoma kunafuka Moshi Wewe Unasemaje? ASKOFU KULOLA AMTIMUA MCHUNGAJI ARUSHA Wewe Unasemaje? Mwazembe Amtetea Kulola NAYE MWAKIPESILE ASEMA EAGT IMEOZA Wewe Unasemaje? Kwa Nini Waislamu Wanalalamika? KITABU HIKI MARUFUKU TANZANIA Wewe Unasemaje? Hofu ya Mabomu Imetanda Dar es Salaam SERIKALI YALAUMIWA KUWANYANYASA WAISLAMU Wewe Unasemaje? Amerika Siyo Mungu WENGI WASEMA IJILAUMU YENYEWE. ISIPOBADILI SERA MAMBO BADO Gazeti la Nation Lasema Kenya Ilikosea Kutangaza Msimamo Haraka. Wewe Unasemaje? NALO GAZETI LA An-Nuur Lamwita Osama Shujaa Na Mpigania Haki Wewe Unasemaje? YESU NI MUNGU? Wewe Unasemaje? Haki za Wanaume Wewe Unasemaje? POLISI TANZANIA WALIUA ZAIDI YA70 HUKO ZANZIBAR Serikali Ilihusika Na Mauaji Ya Raia Wasio Na Hatia Wewe Unasemaje? CCM ILIWAITA WALIOUAWA MAGHAIDI Wewe Unasemaje? Serikali Inayoua Raia Haifai WENGI WANAOMBA MUNGU AIANGUSHE CCM Wewe Unasemaje? Mkapa Asema Nguvu Za Dola Zitamshinda Mungu Wewe Unasemaje? Waziri wa Viwanda TZ Amejiuzulu Wewe Unasemaje? WorldSpace Hawajui Wamlenge Nani Wewe Unasemaje? Dani Hagael Amsaga Askofu Habari Katika Picha Wewe Unasemaje? Mrema Awapongeza Afghanistan Wewe Unasemaje? CUF Kujitoa katika muafaka-Wewe Unasemaje? Gospel tape banned by Dar officials Wewe Unasemaje? Bonyeza kichwa cha habari kusoma Habari, au bonyeza "Wewe Unasemaje?" kutoa maoni yako. Kumbuka! maoni yako yatachapishwa hapo kwa hapo kwenye mtandao, na yatasomwa duniani kote sasa hivi.Tembelea Web Site zetu mpya kwa habari zaidi: http://ktn2.netfirms.com http://nipashe.netfirms.com munishifaustin.netfirms.com http://nation.netfirms.com http://munishi.topcities.com

Faustin Munishi Tell. 25472602445 Nairobi Kenya East Africa
E-mail: fmunishi@hotmail.com  |  munishifaustin@yahoo.com

You are Visitor Number

since 14th February 2001
Check mail at Hotmail
Check Mail at Yahoo