Ukurasa wa mbele
Gazeti la injili
Nyimbo za Munishi
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail
Tuma SMS duniani
Sema nami
Sikiliza waongo
Twende kanisani
Gazeti INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com
Or fmunishi@hotmail.com

Mkapa Hatoki Muda Ukiisha

 

Aliyekuwa mhariri wa gazeti la DAILY NEWS kwenye miaka ya 70 bwana William Mkapa ameanza mikakati ambayo wengi wanaiona kama mbinu ya kiongozi huyo wa CCM kuendelea kubaki madarakani, hata baada ya muda wake kumalizika.

Mkapa alitumiwa na Nyerere wakati wa uongozi wake kuzuia habari kuliko kupeleka habari.Alipokuwa mhariri wa DAILY NEWS alihakikisha kuwa mawazo ya kibepari hayaandikwi kwenye gazeti hilo, jambo lililomfanya Nyerere ampende kama kijana wake aliyeyatetea mawazo ya ujamaa kwenye gazeti hilo lililokuwa likitolewa kila siku.

Akitumia uzoevu wake katika kuhariri habari, Mkapa ameanzisha mjaladala katika mtandao wa kompyuta duniani ili kujadili nani atamrithi. Kwanza kichwa cha habari "NANI ATAMRITHI MKAPA" kinatia kichefuchefu kwa wale wanaoijua Tanzania na hali yake kisiasa ilivyo kwa sasa.

Mkapa katika katika "Forum" hiyo amewaweka watu wa kuchokonoa mada na kuzichangia huku wakihakikisha kuwa mawazo yao ndiyo yanayotawala mjadala. Watafiti wameshaziona kasoro nyingi na wana wasiwasi kama "Foram" hiyo itadumu hasa ukitilia maanani kuwa wahariri wamekuwa wengi na wana uwezo wa kufuta kuhariri au kuipa kichwa cha habari kipya mada ya mchangia mada bila idhini yake.

YAFUATAYO NI MAONI KUTOKA KWENYE "FORUM" HIYO KAMA YALIVYO BILA KUHARIRIWA.

Mchunguzi Afungua Dimba

WANDUGU HABARINI ZA KUTWA...................

NAONA NIJE NA SURA MPYA KATIKA MJADALA HUU. KWANZA NAPENDA KUTOA SHUKRANI ZA DHATI KWA WALE WOTE WANAOCHANGIA MISWALA KATIKA UKUMBI HUU.

PILI NI MATUMAINI YANGU KUWA INGEWEKUWA VYEMA KAMA KUNGEPATIKANA NAFASI KATIKA MAGAZETI YETU AMBAYO ITACHUKUA BAADHI YA MALUMBANO YENYE CHANGAMOTO KUTOKA KATIKA UKUMBI HUU WALAU MARA MOJA KWA WIKI. LENGO LETU NI KUJENGA ,KUONYA ,KUREKEBISHA,NA KUVUMBUA MACHO JAMII .

SASA NAONA NIJE KWENYE HOJA 1. KIPINDI CHA MIAKA MITANO SI KIREFU KATIKA MAISHA HUSUSANI PALE MTU UNAKUWA KATIKA UONGOZI. NASEMA HIVI KWA SABABU KWA KUPIGA PICHA NAONA KARIBU RAISI MKAPA ATAMALIZA MUDA WAKE WA UONGOZI . KWELI KUNA BAADHI YA MAMBO AMBAYO MKAPA AMEJITAHIDI KUYAWEKA SAWA KATIKA NCHI HII AMBAYO MATUNDA YAKE YATAONEKANA BAADA YA MIAKA KUMI IJAYO KAMA KUTAKUWEPO NA MTU THABITI WA KUZILINDA SERA ZAKE MHESHIMIWA HUYU.

LAKINI MTU HUYO LAZIMA AWE FLEXIBLE KATIKA KUPOKEA USHAURI ? SIO KUBANA TUU WANANCHI ....AWE NA SERA WAZI HATA KAMA TUNABANWA LAKINI MATUNDA YAONEKANE BASI... MFANO; EMPLOYMENT,AND MORE INVESTORS ,INFRASTRUCTURES AND SO ON ... SASA SWALI KWA UPANDE WANGU NAULIZA NANI ANAFAA KUCHUKUA /KUSIMAMISHWA NA CCM BAADA YA MKAPA..? NAOMBA KUTOA HOJA.......... .
Wewe Unasemaje?

Christopher Kidanka Adakia

Mjadala kuhusu nani anafaa kuwa Rais unafaa lakini si vema kujadili majina, kama Mwalimu alivyosema mwaka 1995. *Rais ajaye, inafaa awe na sifa zifuatazo: Achukie umasikini na rushwa na awe na ujasiri ya kupambana nao bila kuopopa mtu. *Asiwe anaumwa ugonjwa wa 'Unyerere', kwamba kwa kila kitu lazima amnukuu Mwalimu na kurejea alivyofanya. Awe na ujasiri wa kuthubutu kupingana na wakubwa (nchi wahisaji) katika mambo yanayodhalilisha uhuru wetu. * Asimamie maadili ya viongozi bila woga, awe sauti ya maskini dhidi ya matajiri wacheche
Wewe Unasemaje?

Hayeshi Apendekeza

Mr Joseph Sinde Warioba !Top choice.
Wewe Unasemaje?

Madevuu atokezea

nafurahi sana kuchangia mada hii kwani inanifanya nijihisi kwamba tumepata rais tayari,kwa maoni yangu ningependelea jaji warioba awe rais,makamu wake awe katibu mstaafu wa oau,waziri mkuu awe jackson makweta,ulinzi awe kikwete,afya sarungi,sheria na katiba awe lamwai,mambo ya ndani awe ulimwengu(najuwa warioba atamrudishia uraia wake)kilimo awe wasira,jaji mkuu awe kisanga,spika wa bunge awe john cheyo,mrema awe msajiri wa vyama vya siasa.nimejalibu kupanga safu yangu kwa kuelewa kuwa hawa wote wawe huru katika chama chochote tanzania tutakomboka. ----- madevuu -------------------------------------------------------------------------------- Total Posts: 31 | Joined Oct. 2001 | Posted on: 7:14 am on Nov. 9,
2001 | IP
Wewe Unasemaje?

Hayeshi Arudi Kwa Uzito

Hapo ndugu yangu madevu umenena sana kwani huyu Joseph Warioba ni muhimu sana kwani hata ukiangalia historia yake ni mtu asiyekuwa wa rushwa,ni mtu mwenye sifa zote za uongozi na mwenye uchungu wa nchi yake .

Taifa letu linahitaji mwokozi ambaye anouwezo wa kuweza kutafsiri matatizo mengi sana yanayotukabili .Ninao moyo mkubwa sana na ndugu Warioba kwani tunahitaji mtu ambaye anayeweza kuja kufagia serikali nzima na kurudisha hali ambayo tuliyokuwa nayo zamani.Kama yeye na Dr Salim Salim watakuwa tim moja basi kunahatima nzuri sana hapo baadaye katika tanzania.Tunataka mtu ambaye ataturudishia power tuliyokuwa nayo zamani .

Huyu ni mtu simple sana ,hana makuu yoyote, ni mtu ambaye anaweza kuleta mabadiliko na maelewano baina ya watanzania wengi ambao wameathirika na udhalimu wa ccm.Mfano ni kidogo sana,hivi sasa kuna aina fulani ya mvutano baina ya waumini wa dini mbili nchini na mvutano huu jinsi ninavyojuwa haukuwepo zamani bali umetengenezwa na viongozi wachache katika utawala na hali jinsi ilivyo ,inaonekana kana kwamba waislam na wakristo wanachukiana jambo ambalo mimi ninalipinga kila siku,kwani hizo ni siasa zao mbovu ili kuweza kuwasahausisha wananchi badala ya kufuatilia masuala ya nchi watu tunabakia kupigana wenyewe kwa wenyewe tukisahau kuwa sisi ni ndugu moja (WABANTU)wote tunaasili moja ndio maana tuko pamoja sana.

Warioba tatizo kama hili ninaamini sana atakuja kuliondoa kwa dakika moja na tutarudia katika hali yetu ya usalama na upendo wetu kama ilivyokuwa kama kawaida yetu.Ndugu Madevu umenifurahisha sana kwa kuweza kumtaja huyu ndugu kwani watu wapende au wasipende ndio huyu ni kama nabii MOSES(Musa)atakekuja kutuondoa katika utumwa na kuturudisha kwenye promise land.Ahsante sana ----- www.lycos.com(/D) -------------------------------------------------------------------------------- Total Posts: 61 | Joined Oct. 2001 | Posted on: 10:41 am on Nov. 9, 2001 | IP
Wewe Unasemaje?

Ima Aimarisha

Waheshimiwa, nadhani Tz inahitaji sura mpya kabisa. Hao waheshimiwa wliopendekezwa au kutajwa hapo chini wamekuwa kwenye system kwa muda mrefu. Naamini kuna wa-Tz wenye uwezo zaidi ya hao. Nadhani wasiwasi wa wa-Tz wengi ni kwamba tunafuata ile methali " Zimwi likujualo ...". Naamini tunahitaji damu mpya kabisa ktk uongozi wa Tz. Cha maana ni kuwa na Bunge zuri litakalo kuwa na uwezo wa kumfunga paka kengere anapotaka kwenda nje ya yale yaliyo mema kwa nchi yetu. -------------------------------------------------------------------------------- Total Posts: 5 | Joined Nov. 2001 | Posted on: 3:26 pm on Nov. 9, 2001 | IP
Wewe Unasemaje?

Mchunguzi Aweka Mambo Sawa
Kumbuka kuwa huyu ndiye aliyeanzisha

mh hayeshi nakupata... ila kwa upande wangu nina doubt kidogo na mh warioba nadhani unashidwa kutofautisha kati ya MTEKELEZAJI na KIONGOZI ..kwangu mh warioba anafaa sana kama akiwa mtekelezaji i mean kama waziri wa wizara maalum ya kuzuia rushwa na sio nafasi ya uraisi. Kwa upande wangu naona mh PAUL KIMTI anafaa kuwa raisi wa baadaye wenzangu mnalionaje hili? ----- BY MCHUNGUZI -------------------------------------------------------------------------------- Total Posts: 33 | Joined Oct. 2001 | Posted on: 10:11 pm on Nov. 9, 2001 | IP
Wewe Unasemaje?

POPE Aingilia Kati
Lakini siyo baba mtakatifu mnayemjua

Bwana ima nakubaliana nawewe m,oja kwa moja na hoja nzito hapa ni kuwa tunahitaji damu mpya ambayo hitafumbia macho nani alinifanyia nini wakati uleee sio toka tunazaliwa Kingunge, tunasoma Kingunge, Tuanaanza kazi Huyo huyo hadi tunaoa na kuzaa kwani hakuna wengine? nafikiri kuna haja ya kuwa na damu changa mtu mpya ambaye anweza kumnyoshea mtu kidole tofauti na sasa wote wanaogopana, kulindana kwingi, Serikali inanuka Rushwa, Tiujadili tu kuwa tunataka Rais wa Namna gani na sio jina gani Mkilipendekeza leo akafa kesho? Cha maana ni kuwa Guidelines kuwa mtu wetu awe hivi kama vile mtu unavyokuwa na Dream husband wako au dream wife wako kabla hujaoa....(joke) -------------------------------------------------------------------------------- Total Posts: 46 | Joined Oct. 2001 | Posted on: 10:58 am on Nov. 10, 2001 | IP
Wewe Unasemaje?

Munishi Atibua Maji

Hatuwezi kuzungumza kuhusu nani awe rais badala ya Mkapa wakati Mkapa na CCM wako madarakani isivyo halali. Tusizungumze nkana kwamba tuko kisiwa kingine. Tanzania kuna hali mbaya kisiasa tangu serikali iwaue watu zaidi ya 70 huko Zanzibar. Tusidanganyane hali ya kisiasa Tz siyo shwari. Kwangu mimi naona ni vizuri tuweke kwanza hali ya kisiasa shwari kwa CCM na MKapa kutoka madarakani, halafu tufanye uchaguzi huru na kutoka hapo tunaweza kuzungumza nani awe rais baada ya huyo aliyechaguliwa na wananchi. ----- Http://munishi.netfirms.com -------------------------------------------------------------------------------- Total Posts: 33 | Joined Nov. 2001 | Posted on: 9:02 am on Nov. 23, 2001 | IP
Wewe Unasemaje?

Marandu T.L Ajibu Munishi

Uhalali gani Mheshimiwa Munishi, Ni kweli kumekuwepo na matatizo makubwa nyakati za uchaguzi. Matatizo ya zanzibar yana mapana na marefu. Naweza nisiwe nampenda Mkapa lakini sii Kweli nikisema Mkapa sio Rais wa Tanzania, Kama Id Amini aliyepindua serikali aliitwa rais. Iweje Huyu wetu ambaye aliwekwa kwa uchaguzi (uwe ulivyokuwa) tuseme si rais halali? Kama kuna udhaifu mkubwa Kupita wote Kisiasa ni kukataa kumtambua rais. Vyama thabiti vinatakiwa kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru, sio kungoja achaguliwe "ashinde" halafu mumkatae. Mfano katika nchi fulani kubwa tu, Kulitokea mizegwe sana wakati wa uchaguzi. Kile chama kilichoshindwa kiliapa hakitaruhusu kasoro zile kutokea tena. Hivi sasa kinapeleka maelfu ya wanasheria kuhakiki uchaguzi kila unapotoke. Tunachohitaji Tanzania ni kukuza Democrasi Kuanzia katiba yenyewe na sio kuota mchana. -------------------------------------------------------------------------------- Total Posts: 60 | Joined Oct. 2001 | Posted on: 9:15 am on Nov. 23, 2001 | IP
Wewe Unasemaje?

Hayeshi Amchokonoa Munishi

Ndugu Munishi ni lazima utambue kwamba Mheshimiwa Benjamin Mkapa ni rais halal wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,alichaguliwa na wananchi kupitia demokrasia .Kwa hiyo huwezi kumweka pembeni katika mjadala huu . ----- www.lycos.com(/D) -------------------------------------------------------------------------------- Total Posts: 61 | Joined Oct. 2001 | Posted on: 1:01 pm on Nov. 23, 2001 | IP
Wewe Unasemaje?

Munishi Bado Yumo

Uchaguzi ni mwamuzi wa mwisho kuamua nani amechaguliwa na wananchi wa nchi husika. Tanzania mwamuzi huyo hakuamua. Sababu mnazijua na wale waliotaka kuuliza kwa nini tunaonewa mnajua serikali ya mabavu iliwafanya nini.

Kosa limefanyika na badala ya kulirekebisha na njia ya kulirekebisha mnaijua, mnalifumbia macho na kuanza hoja ya nani awe rais badala ya huyo aliyeingia kimakosa. Hiyo ni kutetea kosa kwa kufanya kosa. Na matokeo yake siyo mazuri hata kama itakuwa ni baada ya miaka 100.

Uchaguzi wa Tanzania haukuwa huru hiyo siyo siri. lakini kwa sababu wanaojiita wakubwa wa dunia hii walikuwa na maslahi yao ya kulindwa na walimuona Mkapa anafaa kwa kazi hiyo basi wakamkingia kifua. Lakini taifa likishaanza kuongozwa bila misingi ya haki kwa raia wake basi mwisho wa taifa hilo huwa siyo mzuri.

Amerika ilimsaidia Mkapa ashinde uchaguzi kwa njia zisizo halali.Masharti ilikuwa awathibiti waislamu, na hasa wa Zanzibar. Kwa kiburi serikali ya CCM iliwaua waislamu zaidi ya 70 huko Zanzibar.Amerika ilimkingia kifua Mkapa, badala ajiuzulu aliwapandisha vyeo polisi walioua.Sasa Amerika maji yako shingoni.Mkapa anataka mapatano na waislamu bila kutoka madarakani.Sawa hiyo?

Eti Muafaka? Hakuna muhafaka bila CCM kutoka madarakani.Iliwaweka watu kizuizini kinyume cha sheria, na sasa inataka kuwaachia kama sharti la kutimiza muafaka.Walioachiwa ni haki yao maana hawakufanya kosa.Ikiwa kusema uchaguzi urudiwe ni kosa la jinai basi hakuna muafaka bila uchaguzi kurudiwa.

Wanajua wako madarakani isivyo halali.Dawa ni kutoka. Mkapa asidanganywe na Amerika. Sera za hawa jamaa ni kujenga na kubomoa. Amerika walimjenga Osama Bin Laden wanataka sisi tumbomoe? Hatutaki, hatuwezi,tumekataa.Walimjenga kwa damu ya Warusi,Siyo vibaya wakimbomoa kwa damu yao wenyewe.Wamezoea kujenga kwa damu.Walimjenga Saddam Hussein kwa damu ya Wairan na sasa wanambomoa kwa damu ya Wairaq.Walianza kumjenga Mkapa kwa damu ya waislamu huko Zanzibar, Huyu tutambomoa bila kumwaga damu.

Mheshimiwa Hayeshi ameniuliza nitafanya nini kumaliza matatizo tuliyo nayo. Matatizo tuliyo nayo siyo ya vitu bali wananchi wanajua kuwa serikali haiwatendei haki.Haki huinua Taifa lolote kutoka popote kwenda juu sana.

Wananchi wanajua wanaibiwa na Serikali ambayo kwa uzoevu walio nao wanajua kujiweka madarakani na kuwatumia wananchi kama muhuri wa kuionyesha dunia kuwa kulikuwa na uchaguzi na wananchi walimchagua Mkapa.

Wangekuwa wakweli wangesema nguvu ya dola imewatisha wananchi kufanya kitu kinachofanana na uchaguzi na kumbe wenyewe wanajua walifanya nini.

Mkapa alisema atatumia nguvu za dola kuwaweka sawa wale anaowanyanyasa. Kama ni nguvu za dola Amerika ni zaidi ya TZ mara mia moja.Tunasubiri tuone atafika wapi na nguvu za dola. Haki kwa kila mtu ndiyo silaha kwa sasa.Bila haki, Nguvu za dola ni Bure.

Waliouawa Zanzibar ni watu, ndugu zao wapo,wanaoendelea kupigwa marungu ya Polisi ni watu,na wanaowekwa ndani na kuteswa bure ni watu.Yakiwafika shingoni sijui watafanya nini.Tunao muda kuyarekebishe yasitufikishe pabaya Munishi ----- Http://munishi.netfirms.com -------------------------------------------------------------------------------- Total Posts: 33 | Joined Nov. 2001 | Posted on: 3:39 pm on Nov. 23, 2001 | IP
Wewe Unasemaje?

Marandu Asalimu Amri

Hizo ni poit Rev. Munishi, Kama uliona nilisema, uchaguzi uwe ulivyokuwa. Ni kweli uchaguzi wa 95 haukuwa huru na ulikuwa wa kuudhi sana. Walioishi Ubungo kama mimi wanajua tulipiga kura saa 11 jioni ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kupiga kura. wakati wa kurudia uchaguzi nikaona huu ni ushenzi sikupiga tena kura.

Uchaguzi wa urais makaratasi ya kupigia kura yalizidisha wino sura Mgombea mmoja kiasi hakuoinekana. 2000 sikuwepo lakini nilifuatilia kwenye magazeti, Sii kweli CCM huwa inashinda kihalali na hili linaudhi sana. Hayeshi anasema Mkapa ni Rais Halali, Lakini Mimi nasema Tu kuwa Mkapa ni Rais kwamba ana uhalali nina shaka. ( The result of unfair Election can not be legitimate) Hiyo ndiyo tofauti.

Kuna Msemo usemao "dawa yako iko jikoni" Kinachotakiwa sasa sio kusema Mkapa sio Rais. Ni kuanzisha kampeni isio ya kichama ya kuuelimisha uma nchi nzima juu ya Haki yao kikatiba. Tuhakikishe katiba inabadilika kabla ya uchaguzi 2005. Tukumbuke kazi ya Kumkomboa Mtanzania kwa sasa ni kubwa kuliko ile ya Kudai Uhuru, lazima ifanywe kwa jasho, ujasiri na juhudi zisizokoma.

Mwisho Rev. Munishi Ulikuja na gear mbaya lakini sasa naona uko fit kwa nini unasema ukweli. Ila acha hiyo Habari ya Kusema Mkapa sio Rais. Wacha hiyo kitu Munishi. (Edited by MaranduTL at 7:09 pm on Nov. 23, 2001) -------------------------------------------------------------------------------- Total Posts: 60 | Joined Oct. 2001 | Posted on: 7:01 pm on Nov. 23, 2001 | IP

Wewe Unasemaje?

Endelea Sehemu ya pili

 
| http://munishi.netfirms.com |
 
<<Back  |  Home |  Gazeti La Injili | Injili2 | Nyimbo Za Munishi | Next >>