Munishi
Group: Members Posts: 77 Joined: Nov. 2003
|
 |
Posted: Nov. 22 2003,12:20 |
|
 CCM WENGINE WANAKIITA CHAMA CHA MAJAMBAZI
SIKU YA KUFA NYANI MITI YOTE HUTELEZA
http://www.munishi.com
Siku ya kufa nyani, Miti yote huteleza. CCM ni sawa na nyani ambaye siku ya kufa kwake imekaribia. Kila mti wanaojaribu kuuparamia unateleza. Ujuzi wa CCM kuparamia miti ni wa miaka mingi. Lakini sasa miti yote inateleza na kufa watakufa.
Utafiti uliofanywa na BBC Tanzania unaonyesha kwamba ukimwi umesambaa Tanzania kwa kiwango cha kutisha. Nchini Tanzania inasadikiwa kwamba wenye madaraka ndio wanaoongoza katika kuusambaza ukimwi. Kwingine wanadai ngono kama hongo, na mara nyingine wanapewa kama zawadi kwa sababu wana pesa nyingi walizojipatia wakiwa madarakani. Usijali kama walipata kwa halali mapesa wanayotumia, lakini ukweli unabaki kwamba wenye madaraka Tanzania ndiyo wanaoongoza katika kuusambaza ukimwi. Nani wamekuwa kwenye madaraka Tanzania kwa zaidi ya miaka arobaini kama siyo CCM?
Hao ndio nambari wani kwa kila kitu, hata kuusambaza ukimwi ni nambari wani. Hata bila upinzani, ukimwi unatosha kuisambaratisha CCM. Msidanganyike kwamba CCM ni chama imara. Kama kuna chama kisicho na matumaini ni CCM.
Ni ukweli walikuwa wamejiimarisha katika kila kona ya nchi, lakini nguvu zao ndizo zimegeuka kuwa maangamizo yao. Huzuni yetu ni watanzania wasio na hatia ambao itawabidi wapoteze maisha yao.
Nchi nyingi barani Afrika wameutangaza ukimwi kama janga la kitaifa, Lakini Tanzania ndio kama hakuna ukimwi kabisa. Vigogo wanaokufa kwa ugonjwa huo wanatafutiwa majina ya kitaalamu kufunika isieleweke walikufa kwa Gonjwa la Ukimwi.
Utasikia kwamba ilikuwa ni kansa ya damu, wengine watasema kwamba moyo ulishambuliwa, na siyo ajabu ukasikia wakisema kwamba damu za waadhirika zilitengeneza mabonge ya barafu ya damu, na ilipokataa kuyeyuka ndipo kifo kikatokea. Kwamba nchi imekataa kukubali ukweli kwamba ukimwi unaua hata viongozi hilo ndilo linalotisha kuliko Ukimwi wenyewe. Hatulifurahii, kwani hatujui wanaosambaza wamefikia wapi katika zoezi lao. Siyo ajabu miaka kumi ijayo Tanzania ikawa na watu wachache sana.
Kama CCM wanaongoza kueneza ukimwi? KANISA NI SALAMA? Lakini tusisahau kwamba maaskofu na mapadri wanakufa kwa ugonjwa huo wa UKIMWI. Kwamba hata hao wanaondoka tena kwa kasi ya ajabu, huo ni ushahidi tosha kwamba wengi katika jamii hawawezi kuachana na UFUKSA. Sasa je tuwaache waende kaburini kichwa kichwa? Wanaohubiri kwamba KONDOMU inakinga kwa asilimia mia moja wanakosea, na wanaosema kwamba watu wasitumie kondomu kabisa wanakosea zaidi. Mbaya zaidi ikiwa wanaosema hivyo ni kanisa Katoliki ambalo linajulikana kwa mmomonyoko wa maadili kuanzia makadinali maaskofu mapadri na watawa wa kike.
Siyo siri tena kwamba ufuksa kwenye kanisa hilo ni wa hali ya juu, hasa ule unaohusisha watu wa jinsia moja. Kisa na sababu ni sera ya kanisa ya kutowaruhusu watumishi wa kanisa kuoa na kuolewa. Ikiwa wenyewe ni MAFUKSA YA KUTUPWA, kuna kosa gani mtu akiwapa mipira kujikinga angaa kidogo? Kwa wale waliowahi kupanda ndege, kila siku ni lazima atokee msaidizi katika ndege hiyo ili kuwaelezea jinsi ya kutumia mpira wa kujiokoa wakati wa ajali. Watu wote husikiliza kwa makini sana maneno yake, japo hakuna ukweli ni kwamba inapotokea ajali ya ndege wengi hufa. Na wale wanaopona mara ngingi huwa hawakusaidiwa na mipira hiyo. Japo kuna wachache ambao imewasaidia. Pointi hapa ni kwamba tusikatae kabisa kondomu. Nakataa kwamba kondomu itachochea ufuksa. Kuna majaketi ya kujikinga na risasi, na sioni watu wakiyanunua ili waende mahali polisi na majambazi wanapofyatuliana risasi.
Kwa kuwa ushahidi wa kutosha upo kuonyesha kwamba watu wameshindwa kuacha ufuksa, tusipinge kila juhudi zinazochukuliwa kuwasaidia wale walioshindwa kujizuia. Ukimuona mtu kapanda kwenye jengo ndefu na anataka kujirusha chini, siyo vibaya kutafuta magodoro mawili matatu ili akifika chini asijipigize sana kwenye lami. Nani ajuae? unaweza kuyaokoa maisha yake hata kwa kujaribu kumdaka kama mpira.Ninachotaka kusema hapa , ni kwamba kila juhudi zifanywe kujikinga na janga hili la ukimwi. Niliwahi kuimba na kusema kama polisi wanawashika wauza bangi, kwa nini wasiwakamate wauza miili wanaoeneza ukimwi? Wengine walisema BOLTI nne zimefunguka kichwani mwangu. Cha ajabu niko hapa, na hakuna aliyejaribu kukaza hizo BOLTI kama alivyosema Bwana Njiraine. Pengine hawana spana saizi ya bolti hizo. Lakini hata PLAYAS inaweza kujaribu kukaza.
Suala siyo nani aliyeleta UKIMWI. Ila kwa kuwa uko nasi, tusizuie kila juhudi zinazofanywa na kila taasisi au watu binafsi kujaribu kupigana na janga hili ukimwi. Unafiki kama unaoonyeshwa na kanisa katoliki hautosaidia chochote. Wale wanaoweza kuachana kabisa na ufuksa hawawezi kushawishiwa na kondomu kujiingiza tena kwenye ufuksa. Wakifanya hivyo, wajilaumu wenyewe na siyo makampuni yanayotengeneza KONDOMU. Tuelezeni nini kitumike badala ya kondomu lakini siyo kukazania mambo ambayo hatuna hakika kama kweli mnayaweza mnayosema. Hata kama tuna hakika mia kwa mia kwamba Moshi na Mdada hawajihusishi na ufuksa, hiyo haitufanyi tuache kuwasaidia wale ambao hawakubahatika kushinda mtihani huo.
Kila la kheri na mjichunge jamani!!! Mambo siyo mazuri. kumeharibika. Hizo ndizo ligha za mitaani siku hizi.
|