1 Next Page

Pages:  2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18  
  Topic: CCM IMESHUSHA JEHANAMU TANZANIA, HOTUBA YA MCHUNGAJI KWA TAIFA < Next Oldest | Next Newest >  
Munishi



Group: Members
Posts: 78
Joined: Nov. 2003

  

"Maovu ya CCM sasa basi" Mwinjilisti Faustin Munishi http://www.munishi.com/

CCM imeleta Jehanamu Tanzania. Watanzania watakaoingia Jehanamu, Itabidi Mungu awapunguzie ukali wa moto kwani tayari wameungua vya kutosha chini ya utawala dhalimu wa CCM. CCM ni wanyanganyi. Walianza kuwanyanganya wananchi mali zao wakitumia azimio la Arusha, na sasa Mkapa anatunyanganya mali akitumia ukusanyaji wa kodi. Anatumia TIN kama nambari 666 ya mpinga Kristo kutunyanganya mali zetu. Je Roho ya mpinga Kristo inafanya kazi ndani ya CCM? Kila dalili zinaonyesha hivyo.

Wananchi wapendwa yangu ni machache sana leo. Maisha yetu na watoto wetu ni muhimu kuliko chama chochote cha siasa. Hakuna sababu ya kuwa mwanachama wa chama cha kisiasa, wakati chama husika ndicho sababu ya kuharibika kwa maisha yetu ya sasa na baadaye. Nazungumza kuhusu CCM. Inasikitisha kuona kwamba wananchi Tanzania wameyazoea maovu ya CCM kiasi cha kukata tamaa ya kujikomboa.

Kwao maovu wanayofanyiwa ni kawaida iliyozoeleka, na hawaoni sababu ya kufanya chochote kujitoa kwenye makucha ya CCM. Niko hapa kuwapa sababu za kuanza harakati za kujikomboa. Tunataka ukombozi kwa sababu ni haki yetu. Lazima tujikomboe kwani tusipofanya hivyo hakuna atakayefanya kwa ajili yetu. Maisha yetu ndiyo yanayoharibiwa, kwa hiyo hakuna mhadhiriwa nambari moja kama mwananchi wa Tanzania. CCM inawatesa Watanzania, wengine inawaua kosa lao ni kusema CCM itoke madarakani kwani sera zake zimeiharibu Tanzania.

Maumivu Mateso Dhuluma Uonevu, na uchungu wote tunausikia, na mwisho wa kuvumilia umefika. Kifo mara nyingi huwa ndio mwamuzi kati ya uchungu na maumivu makali, huupumzisha mwili usiteseke tena. Tusipochukua hatua kwa kuogopa kuuawa, mateso na maumivu ya CCM yatafanya kile tunachokiogopa. Tayari yameua wengi, na wengi wako mbioni kufuatia mkondo huo.

Swali langu kwenu ni hili: Mnataka CCM iue wangapi ndipo mseme imetosha liwalo na liwe? Kwangu naona imetosha, SASA BASI. Liwalo na liwe, tutachukua hatua za haraka kujikomboa. Je tuchukue hatua gani? Kwamba tumefikia mahali pa kujiuliza swali hilo, hiyo ni hatua nzuri ya mwanzo. Nani anayeweza kusema kwamba mateso ya CCM hayajamhadhiri kwa lolote? Atakuwa anasema uongo. Kila Mtanzania mdogo kwa mkubwa, ameonja maovu ya CCM.

Siyo nia yangu kuamsha hisia zenu kinyume na CCM bali nia yangu ni kuwafanya muipende kiasi cha kuitoa madarakani. Kuitoa CCM ndani ya mawazo yenu ni rahisi kama ilivyoingia. Swali la kujiuliza ni Je CCM iliingizwaje kwenye mawazo na fikra zetu? Jibu lake ndiyo njia ya kuitoa na kuisahau. Sitaki tufanye kosa la kuitoa CCM kwa mbinu wanayoitumia kubaki madarakani. Tutakosea kwani tutakuwa tukifanya kile wanachokijua zaidi yetu. Kwa hiyo mawazo kwamba tutaitoa CCM kwa mtutu wa bunduki msahau.Tena hatuwezi kutumia chama kingine cha siasa kuitoa CCM, kwani hakutakuwepo na tofauti.

TUTAITOA CCM MADARAKANI BILA SIASA
" Siasa ni uongo, kwa hiyo hatuwezi kuutumia uongo kuwatoa waongo."

Siasa ni uongo, kwa hiyo hatuwezi kuutumia uongo kuwatoa waongo. Ndugu wananchi, asiwadanganye mtu. Hakuna siasa nzuri. Wanasiasa wote duniani mbinu zao zinafanana tofauti ni mahali mbinu hizo zinapotumika. Kwa hiyo rais wa Amerika hana tofauti yeyote na wanasiasa wetu hapa Tanzania sema kiwango cha uongo wanachotumia wanasiasa wa nchi zilizoendelea kinazidi kile kinachotumiwa na wanasiasa wa nchi zinazojaribu kuendelea.

Kifupi hakuna nchi iliyoendelea duniani.Kilichoendelea ni mbinu za kuwaibia wananchi walio wengi mali yao ambayo ni haki yao, na kuiingiza kwenye mkondo wa kisiasa ambao unalindwa na uongo pamoja na silaha kali. Kwa hiyo mbinu ya kwanza kuwatoa CCM madarakani ni kutambua kwamba wanasiasa wote duniani ni waongo. Pili ni kutokusikiliza uongo wao ambao hupeperushwa na vyombo vya habari kila siku. Ni vizuri mjue kwamba hakuna vyombo huru vya habari katika dunia inayoongozwa na siasa. Kwa hiyo someni habari magazetini, pia sikilizeni redio. Lakini mjue asilimia tisini ya yale mnayoona na kusikia kwenye vyombo vya habari ni takataka kama siyo uongo na mbinu za kuwafanya mnunue bidhaa. Kwa sababu wanasiasa wengi siyo waandishi wa habari, kazi hiyo hufanywa na wanataaluma hiyo kwa malipo.

Kwa hiyo hamtakosea kama mtasema kwamba waandishi wa habari wameshirikiana na wanasiasa kuifikisha hali yetu kimaisha ilipo. Uzuri wa waandishi wa habari, ni kwamba wanaweza kirahisi kurudiwa na fahamu zao, na kuwageuka wanasiasa na kuungana na sauti ya wanainchi. Tatizo ni kwamba walikuwa hawajui kama mnajua. Wakijua kwamba nimewaambia na mbaya zaidi wajue kwamba sasa mnajua yale waliyowaficha muda mrefu, watajikomba kuwaumbua wanasiasa. Hapo tuwe tayari kusikia mengi. Watakapogeukana hiyo ni furaha tele upande wetu.Tutakuwa tumempata msaidizi katika vita yetu ya kuwatoa CCM madarakani.

WANASIASA HUTUMIA VYOMBO VYA DOLA KUWANYANYASA WANANCHI "Kila inapobidi majeshi yote hutumika kulinda maslahi ya wanasiasa. "

Siyo rahisi wanasiasa warudiwe na fahamu zao, hasa ukitilia maanani kwamba wamezoea ukubwa na kutaka kuabudiwa kama 'miungu' wadogo. Kwa hiyo watatumia kila mbinu kubaki madarakani. Mbinu wanayoijua zaidi ni ile ya kutumia vyombo vya dola kama polisi na majeshi yote ya angani nchi kavu na majini, bila kusahau vikosi vya siri ambavyo hutumiwa kuwanyamazisha wapinzani.

KAZI IKO HAPA.

Wananchi wapendwa sipendi kuwaficha niwaambie kibarua kilicho mbele yetu ni rahisi. Nitakosea sana nikifanya hivyo. Jukumu langu ni kuweka wazi mbele yenu kila pingamizi tutakalokutana nalo, na kuwaeleza mbinu na njia sahihi ya kupambana na adui yetu. Majeshi yote yameundwa na wananchi wa TANZANIA. Polisi kwa lengo la kulinda mali zetu wananchi, na majeshi yale mengine wanasema lengo lao ni kulinda mipaka ya nchi yetu.

Hiyo ndiyo lugha wanayotumia wanasiasa kutuonyesha kwamba majeshi yako kwa ajili yetu wananchi kumbe ni kinyume chake. Kila inapobidi majeshi yote hutumika kulinda maslahi ya wanasiasa. Mnakumbuka yaliyowapata wananchi wa Zanzibar walipojaribu kuipinga CCM. Wananchi zaidi ya sabini walipoteza maisha yao, huku wengine wakikatwa viungo vya miili yao ili kuwafundisha adabu.

Yaani watanzania wako tayari kuua wenzao kwa ajili ya wanasiasa. Hiyo ndio kazi iliyo mbele yetu. Mjue kuna watu walio tayari kuua kwa ajili ya CCM na viongozi wake. Na tayari walifanya hivyo mchana jua linawaka bila kuogopa kamera za TV. Inataka moyo, lakini msisahau nguvu iliyo katika KWELI. Ukweli utatuweka huru mbali na wanasiasa waongo. Kweli ni NENO la Mungu ambalo ndiyo silaha yetu yenye nguvu zote.

TIINI MAMLAKA HATA CCM?
"Tuna haki na uhuru wa kuikataa CCM, na Mungu aliyetupa hawezi kutunyanganya haki na uhuru huo. Ni mali yetu, aliyetupatia ni Mungu na tumeamua kutumia haki na uhuru huo kuikataa CCM ya wauaji. "

Wacheni waje wakitumia silaha, sisi tutawakabili kwa NENO la Mungu. Kwa imani yote yawezekana kwa waaaminio. Imani yetu kwa Mungu tusikubali iyumbishwe na chochote. Siyo matisho ya CCM wala kejeli zao.Mara zote wananchi ndio wengi kuliko risasi zote CCM walizojilimbikizia. Sauti ya wengi ndiyo sauti ya Mungu.

Tukisema kwa sauti kubwa kwamba 'CCM CHAMA CHA MAJAMBAZI HATUKITAKI,' hiyo ndiyo itakayokuwa sauti ya Mungu. Na hakuna awezaye kushindana na MUNGU. Tuna haki na uhuru wa kuikataa CCM, na Mungu hawezi kutunyanganya haki na uhuru huo. Ni mali yetu, aliyetupatia ni Mungu na tumeamua kutumia haki na uhuru huo kuikataa CCM ya wauaji. Watakaopingana na uamuzi wetu kuikataa CCM, hao ndio watakaokuwa wakipingana na agizo la Mungu. Ndiyo watakuwa wameasi mamlaka ya Mungu. Kwa hiyo lazima waitii mamlaka yetu wananchi, kwani hiyo ameiweka Mungu mwenyewe. CCM iliwekwa na mtu mmoja, ni sawa ikitolewa na watu.

Walitudanganya kwamba wanafanya uchaguzi ili iwe kana kwamba iliwekwa na watu, lakini tumegundua janja yao.Maoni ya wengi hayajawahi kuheshimiwa katika uchaguzi wowote ule tuliowahi kuwa nao. Kwanza tulikuwa tukichagua nini kinyume cha nini? Uchaguzi lazima uwe kati ya Shetani na Mungu, na siyo kati ya shetani na mashetani. Chaguzi tulizowahi kuzifanya kabla ya vyama vingi vya siasa, zilikuwa kati ya Shetani na kivuli. Chaguzi tulizofanya wakati wa vyama vingi vya kisiasa, zimekuwa kati ya Shetani {CCM}na vijishetani {vyama vya upinzani} ambavyo navyo vitakua kumfikia Shetani mwenyewe. Sasa tunataka uchaguzi wa kweli. Tuchagua kati ya Shetani na Mungu. Duniani hakuna uchaguzi zaidi ya kuchagua MUNGU na Shetani. Hakuna kitu cha tatu wananchi msidanganyike.

GIZA NA NURU
" Msije mkanilaumu kwamba nilisema siasa ni dini ya shetani."

Dunia imekuwa na historia ya kupenda giza kuliko NURU, ndio maana wengi wanapenda siasa ambayo ni giza nene. Nuru ya injili sasa inaangaza duniani kote. Inatufundisha kuikataa siasa ambayo hutumiwa na shetani kuyatekeleza malengo yake ya kuharibu, kuchinja na kuua. Msije mkanilaumu kwamba nilisema siasa ni dini ya shetani. Lakini hata kama ulimi wangu ungeteleza niseme hivyo, ningekuwa nimekosea nini? Je sasa nimesema hivyo? Hapana. Nilichosema ni kwamba siasa ni chombo anachotumia sana Shetani. Hatuwezi kumkataa Shetani na kuikubali SIASA chombo anachokitumia. Tumkatae jongoo na mti wake. Wananchi! Siasa ni mbaya na hilo mnalijua fika. Wengi mtaniuliza nini mbadala wa siasa? Jibu langu ni KWELI. Neno la Mungu ndiyo KWELI.

UJAMAA NA UBEPARI
"Ujamaa ulisikika mzuri masikioni, lakini kwa sababu aliouleta alikuwa Nyerere mwanasiasa muongo, kila kilichovutia hakikutekelezeka."

Watu tofauti kwa nyakati tofauti wamekuwa na mawazo tofauti kuhusu mfumo gani unaofaa kumwongoza mwanadamu. Wengine waliufuata mfumo wa ukomunisti kama akina Nyerere, wakashindwa kabisa. Mbaya zaidi walitumia miaka zaidi ya 30 kuyajaribu mawazo yao ya ujamaa Tanzania. Matokeo yake yalikuwa kuiacha Tanzania ikiwa imeharibiwa na sera zao mbovu, na hata sasa hatuna sera kamili tunayoifuata.

Tanzania siyo mabepari wala siyo wajamaa kama alivyotaka Nyerere. Sisemi ubepari ni bora kuliko ujamaa, kwani sera zote hizo ni za kisiasa. Kwangu zote ni mbovu kwani zinakosa KWELI ndani yake. Ujamaa ulisikika mzuri masikioni, lakini kwa sababu aliouleta alikuwa Nyerere mwanasiasa muongo, kila kilichovutia hakikutekelezeka. Badala ya aliyeanzisha kukiri kwamba alikuwa amesema uongo, alitumia uongo mkumbwa kuutetea uongo mdogo aliouanzisha. Miaka ikapita na tulichoambulia watanzania ni umaskini wa kutisha.

Nyerere alitutaka tuamini kwamba dunia yote inapita kwenye matatizo kama yetu watanzania, na wakati huo huo polisi waliwakamata wananchi waliopatikana na sabuni, dawa za meno na mafuta ya kupikia kutoka Kenya. Ilikuwa ni sawa na kukamatwa na madawa ya kulevya. Wengi wakati huo tuilijiuliza: Ikiwa dunia yote ina mateso kama yetu, mbona hapa Kenya wao wanaogea sabuni? Tofauti na sisi tunaotumia maziwa ya mpapai kuogea? Tena mbona wenzetu wanatumia dawa za meno wakati Nyerere anaziita anasa? Kweli kuogea sabuni ya REXONA au kutumia dawa ya meno ya COLGET ni anasa? Nyerere mwanasiasa muongo alitutaka tuamini hivyo.

Wengi walimuamini na mpaka leo hawataki makuu. Waliukubali umaskini, na hawataki kuchukua hatua zozote kupambana nao. Japo Nyerere alisema adui zetu ni umaskini ujinga na maradhi, alitufundisha kuwapenda na kuwakubali maadui hao. Nasikitika kusema kwamba kuna watu waliomwamini Nyerere kinyume cha Amin wa Uganda. Waliomwamini Nyerere walikosea sawa na waliomwamini Amin. Watu hao wawili walileta madhara kwa nchi zao, lakini ya Nyerere Tanzania yalizidi.

Ninachotaka kusema ni kwamba mifumo yote ya siasa ilishindwa. Sasa tuufuate mfumo wa Injili ambao hauwezi kushindwa. Injili ni uwezo wa Mungu, sioni haya kusema Injili ndio mkombozi wa dunia. Itaikomboa dunia kutoka katika minyororo ya uongo ya wanasiasa. Lazima tuiamini Injili kama kweli tunataka ukombozi. Dunia ni ya Mungu na haiwezi kuongozwa kwa siasa za watu ambazo ni uongo. Dunia itaongozwa na KWELI ya neno la MUNGU.

WANASIASA NA MFUMO WA BIASHARA NCHINI
"Inasikitisha kuona wananchi ndani ya nchi yao wakiteseka, huku wanasiasa na wageni wachache wakimiliki njia zote kuu za uchumi."

Duniani kuna vita nyingi na tetesi za vita. Yote hayo ni matunda ya wanasiasa. Shetani anawatumia kuua na kuharibu maisha ya watu. KWELI imekuja ili tuwe na uzima, kinyume na shetani aliyekuja kuua. Utajiri wa dunia uko mikononi mwa wanasiasa. Mnajua ni kwa nini? Ili utajiri huo utumike kununua kila wanachokihitaji. Nanyi wananchi ni moja ya bidhaa ambayo wanasiasa hupanga kuinunua. Mnanunuliwa wakati wa kura ili kutia saini chaguzi ambazo washindi hujulikana kabla ya siku ya kura.

Hawataki mjiendeleze ili muwe rahisi kununuliwa. Ndio maana wengi wenu hamjiwezi kimaisha na hiyo haiwasumbui wanasiasa kwani wanapenda mbaki kama mlivyo ili wawatumie. Hata wale wanaojaribu kujipatia riziki zao za kila siku kwa kuanzisha biashara ndogo ndogo, bado wanasiasa hawaachi wafanye hivyo. Kila siku tume ya jiji hupewa kazi ya kuusafisha mji, na wafanyabiashara ndogo ndogo ndio uchafu unaotakiwa kusafishwa mijini. Siyo ajabu kwani huo ni mpango kamili unaolenga kuwanufaisha wafanyibiashara waliounganishwa kisiasa. Hawa ndio wale ambao hupewa tenda za serikali ili wagawane mapato na wanasiasa.

Kuna wengine wa asili ya kiasia ambao nao hupewa kumiliki maeneo yote muhimu ya kibiashara. Makubaliano ni kwamba mapato wayagawane na wanasiasa. Inasikitisha kuona wananchi ndani ya nchi yao wakiteseka, huku wanasiasa na wageni wachache wakimiliki njia zote kuu za uchumi. Hali hii haipaswi kuwa hivyo. Wananchi wanatakiwa wapewe uhuru wa kufanya biashara popote katika nchi yao. Udogo wa biashara usiwe ndio sababu ya kumsumbua mwananchi, kwani hata hizo biashara kubwa ziliaza zikiwa ndogo. Wananchi wanaoiamini KWELI wanatakiwa waruhusiwe kufanya chochote chema katika nchi yao.

Hali hiyo ndio itakayochochea ubunifu utakaopelekea kugunduliwa kwa vitu vingi kwa ajili ya maisha ya kila siku ya mwanadamu. Ugunduzi huo ndio unaoweza kuinua uchumi wa nchi husika kinyume na nchi nyingine, kwani "akili ni nywele na kila mtu ana zake." Na wale wanaogundua vitu, wanapaswa kulipwa sawa sawa na ugunduzi wao. Hapo taifa litakuwa limejitengenezea wanasayansi wake, wanaoweza kuvumbua vitu ambayo wengine hawana, na wakiviitaji taifa linapata pesa za kigeni kuinua uchumi wa nchi.

Sekta ya elimu nayo itakuwa imeboreshwa kwani elimu kwa watoto wetu itazingatia zaidi vitu tulivyogundua wenyewe, kinyume na elimu ya sasa ambayo misingi yake ni mengi yaliyofanywa na wengine, huku tukipima uwezo wetu katika kuyaiga. Ndiyo maana maisha ya waalimu katika nchi nyingi ni duni. Wanasiasa hufundishwa na waalimu, lakini kimaisha wametofautiana sana. Waalimu mishahara yao ni midogo sana kulinganisha na wanasiasa ambao kila kukicha hujiongezea mishahara na marupurupu mengi.

Katika nchi ambayo inaongozwa na KWELI bila siasa, waalimu ndio wanaotakiwa kupata mshahara wa kuwatosha kumudu maisha yao kama siyo uliowazidi wanasiasa. Hata kama watawazidi wanasiasa kimshahara kuna ubaya gani? Hilo ni swali tu. Msije mkasema niliwaambia mishahara ya waalimu izidi ya kila mtu. Lakini waalimu ndio humfundisha kila mtu. Sasa inakuwaje kila mtu anampita mwalimu kimshahara? Hapo nimetoka maana naona maswali hayaishi kichwani mwangu. Mengine mtajijazia wenyewe.

RAIS BILA WALINZI?
Watalinda nini wakati KWELI inajilinda yenyewe?

KWELI na uongo ni kama mafuta na maji. Huwezi kuvichanganya hata kama utajaribu kufanya hivyo. Kweli inajilinda yenyewe na haihitaji kulindwa na silaha kali. Uongo lazima ulindwe kwa kutumia silaha kali, kwani hawajui wale waliodanganywa wakierevuka watafanya nini. Ndio maana dunia nzima inafikiria kuhusu silaha kali kuliko chakula cha wanadamu wanaoikaa. Waangalie wanasiasa wanavyolindwa. Watu zaidi ya mia moja hawafanyi kitu kingine duniani ila kumlinda mwanasiasa.

Naheshimu kila taaluma ya mtu, lakini siwezi kumshauri yeyote awe mlinzi wa mwanasiasa. Kwa nini ufe kwa ajili ya uongo ambao hukuusema? Tena kwa mshahara gani basi? Yaani wenzio wako ndani wanakula vinono nawe unaungua jua nje? Sawa ni kazi yako. Unaipenda. Sina la kuongeza. Lakini ikiwa mimi ndiye nitakayekuwa kiongozi katika nchi itakayokuwa ikiongozwa na KWELI bila siasa, basi sitaki walinzi. Watalinda nini wakati KWELI inajilinda yenyewe?

Unamkumbuka mmoja wa wanafunzi wa Yesu aliyejaribu kufanya kazi ya kumlinda? Alikata sikio la mmoja wa askari waliokuwa wanamkamata Yesu. Aliambiwa aurudishe upanga wake kiunoni kwani YESU ni KWELI iliyotoka kwa Mungu na hakuhitaji kulindwa na mapanga au bunduki. Pesa wanazotumia wanasiasa kununulia silaha za kujilinda, zinatosha kumaliza baa la njaa duniani kote.

Yaani nina maana kila mtu duniani anaweza kula milo mitatu kwa siku. Tena chakula kizuri. Lakini pesa zote wanatumia wanasiasa kununulia silaha kali za kujilinda na wale waliowadanganya. Mwisho wao umefika. KWELI itawatoa madarakani bila kutumia silaha. Ole wao. Silaha walizojiwekea watazifanyia nini? Mbinu za vita zimebadilika. Hatutatumia mbinu walizozizoea.

Nguvu ya kweli ya INJILI itawakata makali yao. Injili ni NENO la Mungu ambaye ndiye KWELI yenyewe. Je wanasiasa watashindana, au kupigana na Mungu? Kila la kheri katika vita yao hiyo. Watatoweka mmoja baada ya mwengine. Hawatajua ilikuwaje, wala hawaruhusiwi kujua. Pesa na utajiri havitawasaidia wakati huo. KWELI haipimi uzito wa mtu kulingana na vitu alivyo navyo. Mtu ni mtu hata kama hana vitu. Mtu huunda vitu, lakini vitu haviwezi kuunda mtu. Vitu ni kwa ajili ya mtu, lakini siyo mtu kwa ajili ya vitu.

WANASIASA HUTUMIA DINI KUTAWALA
Makanisa mengi yameanzishwa na kufadhiliwa na wanasiasa kwa kwa lengo la kuyatumia kisiasa, wakati lugha yao ni kwamba chama na serikali havina dini.



Dini ni imani kwa Mungu wakati siasa ni imani kwa watu. Zote mbili ni itikadi zinazohitaji watu kufanikisha malengo yao. Ndio maana nawataka watu wa dini zote tuungane pamoja kuitoa siasa madarakani. Suala kwamba dini gani itatawala hilo lisitusumbue kwa sasa. Muhimu ni wote tutambue kwamba wanasiasa wanatutumia vibaya. Baada ya kutambua hayo tuachane kabisa na siasa. Kitakachofuata ni kila dini inayowania uongozi kujitokeza hadharani na kutangaza nia yao ya kutaka kuongoza. Wananchi wa dini husika, pamoja na wale wasio na dini, bila kuwasahau wale wa dini nyingine watakaoamua kujiunga na dini yenye sera nzuri kutoka kwa Mungu, Watachagua dini gani iongoze kwa kipindi kilichozoeleka cha miaka mitano.

Baada ya miaka mitano tutachaguana tena. Pamoja na kwamba kila dini itakuwa na katiba yake, lakini lazima tuwe na katiba moja ya pamoja. Nayo ni ile itakayozingatia Imani kwa Mungu ambayo ndilo lengo la kila dini. Pamoja na kwamba dini fulani itachukua uongozi kwa kipindi cha miaka mitano, bado kila dini itawakilishwa katika baraza la makuhani ambalo ndilo litakalohusika na kuhakikisha kwamba amri kumi za Mungu zinafuatwa kikamilifu. Kwa hiyo hofu kwamba kutatokea michafuko ya kidini msahau kabisa. Badala yake dini zote zitaingia katika ushirikiano ambao haujawahi kuonekana tangu kuumbwa ulimwengu. Bado kila dini itakuwa huru kuendelea kufanya mambo yake yenyewe, bila kuomba kibali kwa wanasiasa kama ilivyo sasa.

Hakutakuwepo na makanisa ua misikiti inayodhaminiwa na serikali. Makanisa mengi yameanzishwa na kufadhiliwa na wanasiasa kwa kwa lengo la kuyatumia kisiasa wakati lugha yao ni kwamba chama na serikali havina dini. Mambo yako hivyo karibu kila dini. Inasikitisha kuona kwamba wengine wanafikia mahali pa kudanganya kwamba watu wamepona kwenye mikutano yao ya kidini, kumbe ni waongo. Tayari tumewangundua kuwa ni wapambe wa CCM. Wanalindwa kama wanasiasa na huku wanajiita maaskofu. Wanatembelea magari ya kifahari na huku waumini wao ni masikini wanaodanganywa kwamba wakitoa watabarikiwa. Tayari viongozi wa dini wanawasaidia wanasiasa katika kuendeleza ukandamizaji na uonevu kwa waumini wao, ili mradi tu waitwe ikulu na wapewe magari na pesa. Hawana tofauti na wanasiasa tunaotaka kuwatoa madarakani. Kweli ya Mungu ni taa. Ikiwamulika, matendo yao yataonekana na kila mtu. Hawa ndio watakaokwenda pamoja na wanasiasa wakati dini ya kweli itakapochukua madaraka.


MAUAJI YA KISIASA SIRI YAFICHULIWA

Wanasiasa kwa makusudi wameziharibu taasisi zote. Duniani taasisi zote hufanya kazi kwa ajili ya wanasiasa. Nchi zilizoendelea wameendelea katika kujaribu kuficho hilo lakini nchi zetu jambo hilo liko wazi. Kwamba wana mbinu kali za kulificha, haiwatofautishi na wenzao katika nchi zinazoendelea. Inabaki kwamba kila taasisi duniani inalinda maslahi ya wanasiasa kwanza. Mahakama mara nyingi zinaonekana kupindisha ukweli, hasa pale ambapo mwanasiasa anahusika. Hebu fikiri kuhusu gari lililotekwa nyara katikati ya mji.

Watekaji wanamlazimisha mwenye gari kuliendesha kuelekea wanakotaka. Baada ya safari ya kama kilomita mbili hivi, wanaacha gari la kwanza baada ya kulizinga jingine kwa mbele. Mwanye gari la pili anapigwa risasi na kuuawa hapo hapo baada ya kisichojulikana kuendelea kati ya watekaji na yeye. Wanayaacha magari yote mawili hapo baada ya kumwamuru mwenye gari la tatu kutoka ndani ya gari lake na kuwapa funguo. Wanaondoka na gari huku wakiwaacha wenye magari wote mahali pamoja, lakini mmoja ni marehemu na mwingine amebaki bila gari.

Baada ya dakika kama tano hivi, Polisi wanawasili mahali hapo. Wakiwa katika kuwahoji wenye magari wawili, waandishi wa habari wa magazeti TV na Redio wanawasili mahali pa tukio. Usijali wataulizana nini hapo, lakini sikiliza redio na utizame TV jioni, halafu usome magazeti asubuhi yake. Utakayemsikia akitajwa kwamba aliuawa na majambazi waliojaribu kumpora gari, ndiye aliyekuwa amelengwa na taaluma zote hizo. Yaani habari yenyewe itasomeka hivi. MAJAMBAZI WAMUUA BWANA XXXX Aliyekuwa mhubiri wa INJILI bwana XXXX amefariki dunia baada ya majambazi kumfyatulia risasi.

Wakiongea katika sehemu ya tukio, bwana JJJJ na bwana SSSS walisema kwamba walishuhudia majambazi wakimfyatulia risasi bwana XXXX baada ya mvutano ulioonekana kama Bwana XXXX alikataa kuwapatia majamabzi fungua za gari lake. Wakisimulia saidi kisa hicho, walisema kwamba walisikia mlio wa risasi mara mbili, na baadaye majambazi walitoka kwenye gari la huyo aliyekuja kujulikana baadaye kama Bwana XXXX. Walimwamuru Bwana SSSS atoke kwenye gari lake na awape funguo. Alitii, na majambazi waliondoka na gari lake ambalo mpaka sasa halijapatikana. Kwa sababu vyombo vyote vya habari vimelipa uzito suala hilo kwenye kurasa zao za kwanza, wananchi wanaiamini hadithi hiyo. Ndiyo lengo lilikuwa ifanyike hivyo ili wananchi waaminishwe uongo. UKWELI wa mambo ni kwamba bwana XXXX alikuwa mlengwa kwenye sakata yote hiyo.

Kuna mtu aliyejua kwamba atapitia barabara hiyo saa hizo baada ya kutafiti nyendo zake kwa zaidi ya miezi mitatu. Taasisi zilizotumika kuwadanganya wananchi nazo zilihusishwa wengine wakijua na wengine bila kujua. Walioporwa magari yao ndio ambao hawakujua nini kilichokuwa kikiendelea. Ilikuwa hivi: Bwana XXXX aliwaudhi wanasiasa kwa kujaribu kuwaambia kwamba wanasiasa hawawatendei mema wananchi walio wengi. Walipochukizwa naye wakaamua kwamba atauawa. Pesa nyingi zikatolewa kwa ajili ya kazi hiyo. Walitakiwa watu kutoka katika taasisi mbili nyeti. Polisi na vyombo vya habari vilitosha kukamilisha zoezi zima.

Kachero mmoja wa polisi alitumika kuzijua nyendo zote za Bwana XXXX, halafu mkuu moja wa kituo cha polisi alitakiwa kuwatoa vijana ambao watafanya kama wafanyavyo majambazi. Na huyo huyo ndiye aliyetakiwa kuvipigia simu vyombo vya habari kuviarifu kuhusu tukio, na jitihada zao za kuwafukuza majambazi.

Lengo likiwa kutekeleza mauaji ya kisiasa, na kuyafanya yaonekane kama ujambazi wa kawaida. Walikosea. Kwanza hakuna ujambazi wa kawaida. Kwamba kuna ujambazi hiyo inaonyesha kushindwa kwa wanasiasa kuwalinda wananchi pamoja na mali zao. Pili: Kwamba wanamuua mtu kwa sababu tu amewakosoa chama tawala CCM huo ni wendawazimu nambari ONE. Wananchi mfano huu unaonyesha jinsi wanasiasa wanavyoweza kuzitumia taasisi kuyaficha maovu yao. Hii ni siri iliyofichuliwa katika mijadala ya Internet huko BCSTIMES .COM baada ya siri hii kufichuliwa na mtu aliyejiita AISHA AIESHI. Unaweza kujisomea mwenyewe kisa hicho kwa KUBONYEZA HAPA. Kuna matukio mengi ya zamani na hivi karibuni yanayofanana kabisa na mfano huu. Mauaji ya watu zaidi ya sabini kule Zanzibar, Kifo cha SOKOINE aliyekuwa waziri mkuu wakati wa Nyerere. Kifo cha KOMBE aliyekuwa mkuu wa kikosi cha usalama wa taifa wakati wa Nyerere, na wengine wengi.


Mchungaji Faustin Munishi ambaye pia ni mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Afrika ya mashariki na kati, ametangaza azma yake kuwania kiti cha urais Tanzania katika uchaguzi ujao. Mengi yamesemwa kuhusu hatua ya mchungaji huyo, na hapa ni sehemu ya mjadala katika mtandao. Inasemekana serikali ilikuwa imeufungia mjadala huu usiweze kusomwa na Watanzania. Gazeti la Injili kwenye internet linakuletea mjadala huo bila kuhariri chochote.

SASA BASI INATOSHA

Ndugu wananchi yangu yalikuwa hayo machache. Msimame imara, wala msikubali kuyumbishwa na hawa wanasiasa. Mkatae kabisa mbinu zao za kutaka kuendeleza maovu yao kwa kuachiana viti. Nyerere alituachia MKAPA ili alinde madhambi yake.Naye Mkapa anataka kutuachia sijui nani ili alinde madhambi yake. Watalindana mpaka lini? Mwisho wao umefika.Sasa tunataka dunia isiyo na kitu kinachoitwa SIASA.

Wametudanganya vya kutosha, wakatuibia vya kutosha sasa tunataka KWELI ya neno la Mungu iongoze Tanzania. Mungu ni pendo na anaipenda Tanzania ndio maana amenituma mtumishi wake kuwaletea ujumbe huu. Msijali kufurukuta kwao kwani wangefanyaje nao wanakata roho? Watawapeleka kwenye madanguro yao kuwatesa lakini msikate tamaa. Watatumia kila mbinu ikiwepo ya kuwafungulia kesi za uongo, msijali kwani hayo yote hayana budi kuja. Nguvu ya dola ni ndogo sana ukilinganisha na nguvu ya wananchi wamoja.Umoja wetu na imani yetu kwa Mungu ndiyo silaha kubwa ambayo kila mmoja wetu lazima awe nayo.

Watahangaika kujua nani anayetupa nguvu tulizo nazo, lakini jibu watakalolipata litawarudisha hatua mia tatu nyuma. Wataanzisha magazeti kwa lengo la kuueneza uongo wao lakini watagonga mawe kwani wananchi tumeyashitukia magazeti ya hivyo. Watatumia pesa walizoiba kwetu kutununua kwazo, nasi tutatumia pesa bila kuwaunga mkono.Pesa ni zetu. Zikirudishwa hatuachi. Tutazitumia. Tuanze mara moja zoezi la kuchoma moto kadi za vyama vya kisiasa. Sisi ni waumini wa dini na hiyo inatutosha. Hatuwezi kuamini katika dini mbili, yaani siasa na INJILI. Moja ni ya shetani na nyingine ni ya Mungu.Sisi tumeamua kuwa upande wa Mungu. Mungu hawezi kutuacha watoto wake tuteswe na siasa za yule mwovu.

Hatua ya kwanza tutakayoichukua kuelekea ukombozi, Mungu atachukua hatua mia moja kutulinda na CCM pamoja na wanasiasa waovu. Mara zote Mungu hafanyi chochote kutulazimishia matakwa yake. Lakini tunapoamua kwamba tutaifuata njia hii, na kisha tuombe baraka na ulinzi kutoka kwake, mara moja Mungu hutujibu maombi yetu kwa kuanza kutulinda na kutupa ufunuo zaidi. Nilipochukua kalamu kuanza kuandika haya, ndipo ufunuo wote huu uliponijia kutoka kwa Mungu. Ningengoja ufunuo kwanza ndipo niandike, pengine mpaka mwaka 2080 ndipo ningepata ufunuo huu. Ni muhimu sana kutilia maanani ujumbe huu. Huwezi kuusoma popote kwani lengo kubwa la serikali ni kuwazuia wananchi kujua. Wanajua kwamba mkijua mtawauliza maswali wasiyopenda kuulizwa. Wana mengi ya kuficha na anayejaribu kuyafichua ni adui wao nambari moja. Kama hawatammaliza kibiashara au kisiasa, basi watapanga njama za kuutoa uhai wake. Wameuawa wengi ndiyo maana hatuchukulii kama mzaha matisho yao ya kuua. Bonyeza hapa usome yale waliyokusudia kumfanyia mwandishi wa hotuba hii.[/B][B]


Mchungaji Faustin Munishi.


   
s.carter



Group: Members
Posts: 32
Joined: July 2003

Posted: Nov. 17 2003,19:45   

Mwinjilisti  Munishi!
Nadhani nchi yetu ina utawala wa haki na sheria na ni utawala/serikali iliyochaguliwa kwa ridhaa ya wananchi(watanzania) kwa hiyari yao wenyewe.Katika hii kama inavyofahamika ni kwa wanachi wote-wenye dini na wasio na dini.Nimesoma kwa kirefu na umakini maelezo yako(ingawa umerefusha mno!;) lakini what i failed to see a logic ni kwa madai kuwa tumechoshwa na ccm tuiondoe madarakani hata kwa nguvu....sijui unazungumzia jamii gani?pamoja na walio-ichagua?).Kama kwa harakati za kuiondoa nadhani tuna mfumo wa vyama vingi na kwa watu wenye kuitumia haki yao ya kikatiba ni sehemu nzuri ya kuweka mifumo yao yeyote waipendayo.
 Umegusia suala la kodi na kwa jinsi ninavyofahamu mimi hio ndio inayoongoza serikali yeyote duniani(anzia ya vatican.....)Hii ilikuwepo toka enzi ya kaisari.....Haiyumkiniki uwashawishi watu eti ni ushetani..kumbuka umpe kaisari yale yake...na uheshimu na kuufuata utawala uliowekwa duniani kwani yote yatokana nami asema bwana..
 Nilitegemea kwako mtu wa mungu ungekuwa wa kwanza kushawishi utawala bora na sio kuhimiza vurugu na machafuko..kiasi nahamini utatuweka sawa zaidi kwani nakufahamu kuwa u-mtu makini sana,
ubarikiwe!
(lastly i take this opportunity to welcome u-here but behold its not going to be that easy)

--------------
S "dot" Carter

   
Augustine Moshi



Group: Members
Posts: 332
Joined: May 2003

Posted: Nov. 18 2003,02:58   

Mchungaji Munishi,

Mimi sisemi "ubarikiwe", ila nasema "ulaaniwe", kwani ni wazi kabisa kwamba kuna mkono wa ibilisi kwenye usemayo!

Wewe sio mhubiri wa habari njema kwani unashawishi vurugu na ghasia. Umemruhusu ibilisi akaingia kwenye roho yako, na sasa anatumia kinywa chako. Unahubiri mauti badala ya uzima. Ibilisi huwa anatumia njia mbali mbali kuvuruga amani na mshikamano tulionao Watanzania, na ni hakika kabisa kwamba wewe Munishi ni mojawapo wa mbinu hizo za ibilisi.

Tunamkataa shetani wa vurugu unayetaka kutuletea. Mhatamie tu huyo ibilisi hapo Nairobi, sisi tunamkataa na mambo yake yote, nguvu zake zote!

Augustine Moshi

   
Mizambwa



Group: Members
Posts: 250
Joined: May 2003

Posted: Nov. 18 2003,09:23   

Mchungaji Munishi,
Utabiri wako ni mzuri kwa mtazamo wako tu. Chama siyo kinachoongoza na kuweka sheria katika sehemu yoyote, bali watu ndio wanaoongoza na kuweka sheria katika sehemu. Hivyo hata tukikiondoa chama tawala madarakani bado kama tutawachagua viongozi wale wale haitasaidia kitu.

Kiongozi yeyote anapochaguliwa kuna mambo ambayo anafikiri ni mazuri katika uongozi wake, yaani anaweka mikakati ya uongozi, hivyo inategemea mingine inaweza kuwa mizuri kwa jamii au mibaya kwa jamii, hiyo ni kawaida.

Pia elewa kamwe Duniani kama kiongozi huwezi kuwaridhisha watu wote, lazima tu lawama itatokea katika kundi moja la waongozwa.

Ndugu Minishi ukiwa kama Mchungaji bila shaka unaelewa kuwa hata Mungu hawezi kuwatimizia watu wote katika maombi yao kwa muda ule ule. Mfano katika maisha kuna watu ambao hawapendi kabisa MVUA INYESHE na kuna wengine wanataka mvua. Utaona hapa Mungu ana kazi sana katika kuwaridhisha hawa Viumbe wake. Ndivyo inavyokuwa na kiongozi lazima lawama ipo tu.

Na wakati unamuomba Mungu akusaidie upone ugonjwa unaokusumbua, bila shaka na wewe hukai tu kusubiri miujiza ya Mungu, lazima unatafuta njia ya kujitibu ama kwenda Hospitali.

Nasi wakati tunaomba Viongozi watufanyie mambo fulani kwa kupitia Serikali lazima na sisi tutafute njia za kutatua lile jambo tusisubiri Serikali tu.

Mfano mzuri wa kujisifu ni ujenzi wa shule za msingi mpya hasa pale DSM, Serikali inatoa fungu fulani la pesa na kisha wananchi nao wanachangia katika ujenzi wa yale madarasa. Na kwa mtindo huu sasa hivi shule nyingi sana DSM zimejengwa ama kukarabatiwa na zinapendeza.

Wakati unalipa kodi elewa kuwa ndiyo inayojenga shule hiyo, ukienda Muhimbili usifurahie kupata dawa na huduma kwa gharama nafuu ile ni kodi yako, usifurahie kupita katika barabara nzuri za lami, ni kodi yako ile. Pesa hazitoki Mbinguni kama umande wa asubuhi!!!!!!!!!!

Hivyo mchungaji Munishi jaribu kuwahubiria waumini wako mabo ya kweli na usiwapotoshe. Utaunguzwa na motot wa Jehanamu!!!!!!

INANIUMA SANA!!!!
Jina Kubwa

   
Munishi



Group: Members
Posts: 78
Joined: Nov. 2003

Posted: Nov. 18 2003,11:19   

HOTUBA YANGU HAIKUMAANISHA VURUGU http://www.munishi.com/

Jamani Hamjambo? Mimi siyo mtu wa kuchochea vurugu na sipendi kabisa vurugu. Nisemayo ni kwamba CCM aliyoanzisha Nyerere sasa imezeeka. Sera zake zimeiharibu nchi yetu ya Tanzania. Ujamaa ulishindwa kabisa na haifai kurudishwa madarakani.

Nakubaliana na hoja kwamba huwezi kuwaridhisha watu wote. CCM haijawaridhisha watanzania kwa lolote. Imekuwa ikitumia mabavu kwa kila kitu. Mbaya zaidi Nyerere alisema CHAMA KINASHIKA HATAMU ZOTE NA KUUA TAASISI ZOTE. Kila kitu Tanzania kilifanywa siasa na siasa kuwa kila kitu.

Hakuna mabadiliko Tanzania bila kuitoa CCM madarakani. CCM ni sawa na kansa kwa watanzania. Dawa yake ni kukata sehemu iliyoharibiwa na kansa hiyo na kuzuia isiendelee kusambaa. CCM walitumia pesa za umma kujitanua kila kona ya Tanzania kuendeleza maovu yao. Michango ya lazima kutoka kwa wananchi ndiyo iliyowafikisha CCM walipo. Wanaoridhika na CCM ni wale wanaokula kwenye sahani ya CCM iliyojaa pesa za wizi.

Watanzania tunachotaka ni mabadiliko ya kuitoa CCM madarakani. Tutafanya hivyo kulingana na sheria lakini siyo sheria za CCM. Ikiwa CCM wakitumia mwenyekiti wake wa zamani Nyerere, Waliweza kucheza na katiba ya nchi ili ilinde maslahi yao, nani atakayeweza kusema kwamba Tanzania kuna sheria? Sheria Tanzania ni CCM na CCM ndiyo sheria. Katika mazingira kama hayo mnategemea  watanzania wafanye nini? Waendelee kukaa chini ya utawala dhalimu? HAPANA. Liwalo na liwe. CCM sasa basi.Wametuibia vya kutosha, Wametuchangisha kwa nguvu vya kutosha, Tumetozwa pesa za michango ya mafuta ya mwenge vya kutosha, Sasa tunataka mabadiliko. Tusiibiwe tena, tusilipe pesa za mafuta ya mwenge tena.

Umewahi kuhudhuria tamasha la mahali mwenge unapolala? Mambo yote ya kishetani hufanyika hapo. Ulevi wa kupindukia usiku kucha, Ubakaji, na mambo mengi maovu hufanyika kwa kisingizio cha mbio za mwenge. Walitudanganya kwamba Mwenge unaleta amani pasipo na amani. Mbona wasiupeleke Rwanda na Burundi? Tena kwa nini hawakuupeleka Somalia ukaleta amani huko? Nani wanaouhitaji mwenge zaidi, Watanzania au nchi ambazo hazina amani? Sasa tunakubaliana na wale wanaosema kwamba Mwenge ulikuwa uchawi wa kizanaki kuwafumba macho watanzania. Tunakemea pepo hili la Mwenge pamoja na shetani mwenyewe CCM  kwa jina la Yesu washindwe.

Mwisho wa kuwanyanyasa watanzania umefika. Nuru ya Mungu imeanza kuiangazia Tanzania. Wanaosema hakuna kiongozi atakaweza kuongoza bila kulaumiwa, waachie ngazi nichukue hatamu za uongozi na watakaolalamika ni vigogo wa CCM waliozoea vya bure.

Uongozi wangu utaheshimu Taasisi na kila mtu atapewa uhuru wa kufanya kazi kwa bidii na alifurahie jasho lake. Kinyume na ilivyo sasa Watanzania wengi wanatumia msemo usemao MPANDA NGAZI HUSHUKA. Hawataki kufanya bidii ya kujitoa katika umaskini, kwani serikali inawasaidia kuwashusha waliopanda ngazi kwa njia ya kuwatoza kodi. Kodi siyo mbaya. Lakini inapotumika kama ujamaa mamboleo ndipo tunapokuwa na kila sababu za kuwakosoa watoza kodi.

Mkapa ni mwanafunzi mzuri wa Nyerere. Na itakumbukwa kwamba Nyerere hakuwahi kuukana  ujamaa hadharani. Mkapa pamoja na na kuyauza mashirika ya umma kwa mabepari, mwenyewe ni mjamaa mpaka ndani ya  mifupa yake. Hajawahi kuukana ujamaa hadharani. Kutokana na hayo Tanzania inabaki na sera  kama za popo ambaye siyo mnyama wala siyo ndege. Sera za Tanzania Siyo wajamaa wala siyo mabepari, Lakini watanzania wenyewe walilazimishwa kuwa wajamaa kwa miaka yote ya utawala wa Nyerere. Na mniambie kama Tanzania sasa inaongozwa na nani kama siyo Nyerere akiwa kaburini.

Baada ya kuyasema hayo naomba nieleweke kwamba mimi sipingi kodi. Ninachopinga ni kuitumia kodi kama kama njia ya kuwakomoa matajiri. Na ndivyo kodi inavyokusanywa Tanzania. Nikisema inatumika kuwakomoa matajiri inasikika vizuri. Lakini ukweli ni kwamba kodi inatumika kuwazuia watanzania kuwa matajiri. Mtanzania anayeuza vitu vidogo vidogo kwenye duka lake dogo, anapotozwa kodi za ajabu ajabu, basi lazima atafunga duka lake. Kwa sababu ya kasumba za kiujamaa alizotuachia Nyerere, Mtanzania mwenye kaduka ka nguo na gari moja TOYOTA CHASER pamoja na nyumba ya kulala na familia yake, huyo ni tajiri kulingana na serikali ya Tanzania. Ataandamwa na maofisa wa kodi mpaka afunge duka lake.

Je huo ndio utawala wa kufuata sheria au ni kunyanyasana? Nchini Kenya walifuata sera za kibepari tangu wapate uhuru, jambo linalowapa uwezo wa kupambanua nani tajiri na masikini. Nchini Kenya ukiwa na viduka vya nguo hata kumi pamoja na vigari hata vitatu, kisha uwe na vinyumba hata kumi vya kupangisha bado unawekwa kwenye kundi la Jua kali, yaani watu wanaojitafutia maisha, na siyo matajiri. Tatizo la Tanzania ni kwamba Nyerere hakuruhusu matajiri wawe matajiri. Serikali inapowasumbua walalahoi wanaojitafutia maisha kwa kodi kibao, huo ni ukandamizaji.

Serikali yangu haitafanya hivyo. Sera za serikali yangu zitakuwa kuwaruhusu wananchi watajirike wawezavyo mradi tu wanafanya kazi au biashara halali. Matajiri wataruhusiwa kuchangia mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na ustawi wa jamii. Kodi zitatozwa kulingana na mapato ya wahusika na siyo njia ya kujipatia pesa za kampeni za uchaguzi. CCM weanafanya kila wawezalo kupata pesa za kuwanunua wananchi katika uchaguzi ujao. Lakini watashangaa kujua kwamba wananchi safari hii watapokea pesa lakini watachagua mabadiliko. Pesa siyo kila kitu, Msemo huo utakuwa na maana kubwa kwa CCM watakapowekwa BENCH.


   
Mizambwa



Group: Members
Posts: 250
Joined: May 2003

Posted: Nov. 18 2003,15:41   

Quote (Munishi @ Nov. 18 2003,11:19)
Umewahi kuhudhuria tamasha la mahali mwenge unapolala? Mambo yote ya kishetani hufanyika hapo. Ulevi wa kupindukia usiku kucha, Ubakaji, na mambo mengi maovu hufanyika kwa kisingizio cha mbio za mwenge.
Mwisho wa kuwanyanyasa watanzania umefika. Nuru ya Mungu imeanza kuiangazia Tanzania. Wanaosema hakuna kiongozi atakaweza kuongoza bila kulaumiwa, waachie ngazi nichukue hatamu za uongozi na watakaolalamika ni vigogo wa CCM waliozoea vya bure.

Uongozi wangu utaheshimu Taasisi na kila mtu atapewa uhuru wa kufanya kazi kwa bidii na alifurahie jasho lake. Kinyume na ilivyo sasa Watanzania wengi wanatumia msemo usemao MPANDA NGAZI HUSHUKA.

ALASIRI - 18/11/2003

WAISLAMU: RAIS MPYA ATOKE Z’BAR
Waionya CCM isilete ujanja wa kuteua ‘Mgalatia’

Na  Badru Kimwaga, Kigogo

Wanaharakati wa Dini ya Kiislam wamekitahadharisha Chama Cha Mapinduzi, C.C.M, kutojaribu kufanya ujanja katika uteuzi wa mgombea wa nafasi ya urais wa chama hicho kwa uchaguzi mkuu ujao vinginevyo yataibuka machafuko makubwa.
Wanaharakati hao wakakitaka chama hicho kuzingatia kanuni na sheria zinazotumika katika uteuzi wa mgombea wa nafasi hiyo kwa kubadilishana baina Tanzania Bara na Zanzibar.
Waislam hao, wametoa msimamo huo katika mkutano wao wa hadhara uliofanyika mwishoni mwa wiki, katika msikiti wa Kigogo CCM, Jijini, Dar es Salaam, ambapo walisema wanataka kuona rais ajaye ni lazima anakuwa Muislam kwa vyovyote vile.
Walisema iwapo CCM itataka kutumia ujanja kuendelea kupandikiza Kanisa katika utawala wa nchi hii, basi ni wazi yatatokea machafuko makubwa yasiyozuilika.
Wanaharakati hao ambao wanatoka katika Baraza la Habari la Kiislamu Tanzania, BAHAKITA, walisema wanatoa tahadhari hiyo baada ya kupata fununu kwamba kuna mbinu chafu zinafanywa ili kulirejesha kanisa madarakani kupitia mlango wa nyuma.
“Tunatoa tahadhari mapema, kwa vile rais wa safari hii ni Mkristo, yule ajaye ni lazima awe Muislam tena atoke Zanzibar kama utaratibu ulivyo,” alisema Sheikh Sadiq Kassim, Katibu Mtendaji wa BAHAKITA.
Sheikh Kassim alisema kwa vile Tanzania imetawaliwa na marais watatu waliobadilishana kulingana na uhalisi wao na dini zao basi wanataka kuona rais ajaye anatoka Zanzibar na anakuwa Muislamu na si vinginevyo.
“Iwapo kutafanywa ujanja wowote kwa kuteuliwa mgombea toka Zanzibar ambaye ni ‘Galatia’, tunaapa hatutokubali, tunaitahadharisha CCM kufuata kanuni zake katika uteuzi wa wagombea” alisema Sheikh huyo.
Aliongeza kuwa anafahamu kuwa uchaguzi mkuu ni wa vyama vingi na ni wazi vyama vingine vitashiriki, lakini wanadili na CCM kwa kuamini kuwa chama hicho ndicho chenye nguvu na kinachoweza kurejea madarakani.
“CCM ndio chama tawala na tumekuwa tukivutiwa na utaratibu wake wa kuteua wagombea wake, kutokana na hilo ndio maana tunakionya chama hicho kuacha ujanja wa kulirejesha kanisa madarakani” alifafanua.
Sheikh Kassim aliyekuwa akiungwa mkono na mjumbe wake Ustaadh Hussein Msopah, alisema kuwa waislam hivi sasa hawana imani na CCM kutokana na kufanya mambo mengi ya hujuma dhidi yao kwa kutumia Baraza la Waislam nchini, BAKWATA.
Akithibitisha madai yao alionyesha nakala ya barua ya mwaka 2000 ya BAKWATA mkoa wa Dar es Salaam, inayowaelekeza viongozi wa wilaya na Kata kuwashawishi Maimamu wao kuipigia kampeni ya nguvu CCM kama walivyoagizwa na chama hicho.
Nakala ya barua hiyo pamoja na nyaraka nyingine za siri ikiwemo kikao cha Siri cha viongozi wa Serikali kilichojadili na kutoa maazimio ya mauaji wa Mwembechai, gazeti hili imezihifadhi.
Mkutano huo wa BAHAKITA, uliofanyika mara baada ya swala ya Ijumaa msikiti hapo, ulilaani masheikh wa BAKWATA wanaosahau wajibu wao kidini na kutekeleza hujuma dhidi ya Uislam ka masilahi yao.
Pia walilaani hatua ya kuundwa kwa ushrikiano baina ya waumini wa Kiislam na Wakristo unaofahamika kama UWAWARU, ambao walidai una lengo la kuwahadaa waumini legelege kwa masilahi ya Kanisa na kuwaponda masheikh wa BAKWATA wanaounga mkono.
Wanaharakati hao pia waliwashangaa masheikh wa Kiislam kupenda kukimbilia futari zinazoandaliwa na mabalozi ambao ni magalatia na kusema hiyo ni kuonyesha ni jinsi gani masheikh wengi wanavyosumbuliwa na njaa.
Mwisho kabisa mkutano huo umepanga kongamano kubwa mwishoni mwa mfungo huu wa Ramadhani kwa ajili ya kuijadili CCM na hatimaye kuitisha maandamano ya nchi nzima kuwashawishi wananchi kutokipigia kura chama hicho kama hakitabadili msimamo wake wa kulikumbatia kanisa.

........................................................................................
NDUGU MUNISHI UNAWEZA KUJIBU HAYA MASWALI!!!!!!!

Ndugu Munishi wewe ni Dini gani? na unatoka upande upi wa Muungano????????

Je, kwa mpango huu unaweza kuiondoa CCM.

Vitendo viovu vinavyofanya katika mikesha ya Mwenge nafikiri ni sisi raia ndio watendaji. Sidhani kama ni Chama ndicho kinabaka, au kinafanya mabo ya uovu!!!!!!

Dawa nafikiri ni kuwachagua viongozi ambao hawapo madarakani sasa katika awamu hii. Lakini kuna viongozi wengine ambao wanafanya kazi nzuri sana katika Majimbo yao, sioni sababu ya kuwaondoa tuwape kipindi kingine cha uongozi.

INANIUMA SANA!!!!!
Jina Kubwa.

   
s.crony



Group: Members
Posts: 79
Joined: July 2003

Posted: Nov. 18 2003,20:19   

ndg Munishi,
Inaniwia vigumu kukuita mchungaji kwani kiasi naona msimamo wako ni kama wa kuwapotosha kondoo...
Umegusia yanayofanyika kwenye mikesha ya mwenge..sijui kama unayajua ya mikesha ya cristmass na new year?kiasi sioni kama yana tofauti.Hayo yote mwanzo sikupata picha halisi kuwa upo vipi lakini sasa ingekuwa vizuri tu ungeweka wazi kuwa unatarajia kuomba kura toka kwa wananchi-just a tip-usiende na mbinu hizi-Kushambulia kuwa hakuna mfumo unaofaa wala hakuna uongozi mpaka uwe wewe nadhani hio ni kama kurubuni watu wazima kwa peremende-luckly watanzania sasa wamekuwa watu makini wa kupembua pumba na mchere jaribu lakini sipendi kukukatisha tamaa you have one #### of a mountain to climb on!

--------------
s.crony

   
Augustine Moshi



Group: Members
Posts: 332
Joined: May 2003

Posted: Nov. 19 2003,03:41   

Ndugu Mizambwa,

Hao BAHAKITA  ni watu wenye siasa kali, wasikutishe sana. Nadhani wanatumia Uislamu kutekeleza mikakati yao ya kiharamia. Huenda hiyo BAHAKITA ni tawi la Al Qaeda nchini kwetu. Na hawaelewi katiba ya CCM, kwani si kweli kwamba katiba ya chama hicho ina kipengele cha Urais wa mgao. Tukikubali kupeana zamu kwa msingi wa kidini, basi zitafuatia zamu za msingi wa kikabila. Matokeo ya migawanyo ya aina hiyo ni mauti ya vita vya kidini na kikabila. Na zingetokea vurugu za kidini hao BAHAKITA watakuwa wa kwanza kuadhirika kutokana na ufinyu wao wa elimu.  

Serikali yetu haina dini. Rais wetu anaweza akawa na dini au asiwe na imani yoyote ya kidini. Ni vema vyombo vya dola vikawathibiti maharamia hawa wa BAHAKITA kabla hawajafanikiwa kufanya Tanzania ikawa na vita kati ya Waislamu na Wakristo kama ilvyotokea huko Lebanon miaka ya karibuni.

Nikirudi kwa Munishi, nasema hivi: hata mimi sio mpenzi wa CCM, na mbio za Mwenge nazidharau. Mipango iliyokuweko zamani ya kulazimisha watu kutoa fedha za mafuta ya mwenge ilikuwa ni ya kionevu.  Kama unataka kujitosa kwenye siasa na kugombea  Urais, basi hiyo ni haki yako. Nashauri ujiunge na Mtikila kwani mnafanana mawazo. Lakini, wote wawili mnapashwa kuacha kabisa kuhubiri vurugu na mauti kwani sisi Watanzania tunapenda sana amani tuliyonayo.  Msitushushie jehanamu!

Augustine Moshi

   
Munishi



Group: Members
Posts: 78
Joined: Nov. 2003

Posted: Nov. 20 2003,12:08   

MUHIMU NI MABADILIKO SIYO UDINI NA UKABILA

http://www.munishi.com/


http://www.munishi.com/

Dini Kabila. itikadi za kisiasa siyo muhimu kwa sasa. Muhimu ni kuitoa CCM madarakani.Wengine wanasema ni mlima mrefu kupanda. Watanzania tumeamua kuupanda mlima huo. Nia sababu na uwezo tunao. Hakuna litakalotuzuia. Tunataka mabadiliko ya kuitoa CCM madarakani TOSHA. Mengine tuongee baada ya kibarua hicho. Hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Tukimwachia Mungu, kwa imani yote yawezekana.

Vipingamizi ni vidogo. Kama KATIBA ni moja ya vipingamizi. Tunajua wazi kwamba serikali ya CCM haitakubali kuirekebisha KATIBA waliyokwisha iharibu ilinde maslahi yao. Lakini nguvu ya wananchi kuamua ni sawa na maji mengi ambayo yamefurika mabadiliko. Yatazoa kila kitakachojaribu kuyazuia yasiende yalikokosudia. Nchini Kenya wananchi waliamua wamechoka na KANU. Hawakujali kwamba KATIBA yao inasema hakuna ruksa muungano wa vyama kuunda serikali. Nia yao ya kuitoa KANU madarakani, ilifanikiwa japo katiba inasema wako madarakani isivyo halali. Nani anajali? Hata KANU ilikuwa na uhalali gani kuwa madarakani kuwatesa Wakenya?

Siyo kwamba hatupendi kufuata sheria. Ndiyo maana tunapendekeza kwamba KATIBA yetu lazima irekebishwe kabla ya uchaguzi. Tunajua wazi kwamba CCM hawawezi kutengeneza mazingira ya kufanikisha hilo. Hata wakijaribu, ni kununua muda tu na kutafuta sababu za kukwamisha zoezi zima. Je katika mazingira hayo mnatarajia Munishi na watanzania wanaotaka mabadiliko wafanyeje? Lazima tuanze mikakati ya kujikomboa hata kama ni kinyume na KATIBA ya CCM ambayo ndiyo wanayoiita KATIBA ya Tanzania.

Ni kweli kwamba Tanzania kuna mfumo  mbaya wa utawala na siyo mfumo wa uongozi. Tunataka mabadiliko tuwe na mfumo mzuri wa uongozi. Siyo lazima mimi niwe Rais ndipo hayo yatekelezeke. Mtanzania yeyote mwenye mawazo ya kutengeneza mfumo mzuri wa uongozi Tanzania nitamuunga mkono.Na kuna ubaya gani kama Watanzania watasema ni mimi? Lakini siyo CCM. Sijali dini au kabila la kiongozi husika lakini najali chama kisiwe CCM. Wamekuwepo miaka zaidi ya arobaini, kama kutengeneza muda waliokaa madarakani ungetosha kufanya hivyo. Kwamba matunda ni umasikini na hali duni za kutisha, inanipa sababu ya kesema CCM wamezeeka na hawawezi kujifunza mbinu mpya.


Mimi siyo mwanachama wa chama chochote cha kisiasa na sitarajii kujiunga na Mtikila wala chama chochote cha kisiasa. Wala sitarajii kuunda chama cha kisiasa. Lakini nataka mimi na Watanzania wengi wasio wanachama wa vyama vya kisiasa wawe huru kugombea uongozi wa nchi yao bila kuzuiwa na chochote kama katiba ya CCM. Tunataka katiba irekebishwe iseme hivyo. Tanzania ni ya Watanzania na siyo mali ya Rais aliyeko madarakani. Tunataka KATIBA irekebishwe ili madaraka mengi aliyo nayo rais yapunguzwe. Madaraka yote yawe kwa wenye nchi ambao ni watanzania, halafu lifuate Bunge na ndipo rais. Tunataka katiba inayompa Rais nguvu za kuwaongoza watanzania wapendavyo na siyo apendavyo Rais. Marais watakuja wakienda, na wengine watakufa, lakini Tanzania itabaki. Tutengeneze katiba inayowalenga watanzania na vizazi vijavyo. Katiba tuliyo nayo inalenga CCM na rais anayetawala. Ndiyo maana Rais ana mamlaka ya kuvunja Bunge, isitoshe anaweza kuwapeleka vijana wetu vitani apendavyo. Nyerere aliwapeleka vijana wetu Uganda kujaribu kumsaidia rafiki yake Obote arudi madarakani. Hatutaki upuuzi kama huo urudiwe na Rais yeyote Tanzania. Ndiyo maana kuyapunguza mamlaka ya Rais ni Muhimu kwa Tanzania na vizazi vijavyo.

Siombi kura kwa mtindo huu, lakini sera zangu naziamini kiasi kwamba masanduku ndiyo yatakayokosekana. Katiba irekebishwe, na nguvu ya hoja ndiyo itakayomimina kura upande wangu.  Nataka niwe kiongozi nisiye na madaraka mengi kama ya Mkapa. Hivi amelazwa Watanzania matumbo ni moto japo wana Bunge na viongozi wengine. Haipaswi kuwa hivyo. Ndiyo maana mara nyingi tunafichwa hali za kiafya za watawala wetu. Wana madaraka mengi, kiasi kwamba walitakiwa wasiugue. Hata wakiugua tunafichwa. Tunapoambiwa ni wagonjwa ni wakati maji yamezidi unga. Walipokubali kwamba Nyerere anaumwa ambaye hakupaswa kuugua kulingana na madaraka yake, Mwezi haukwisha aliaga dunia. Tunataka katiba irekebishwe tuwe na rais mwanadamu anaeugua na kuuguzwa kama wanadamu wengine. Kwani kuna kosa gani mtu kuugua? Watanzania tupo. Ndiyo maana walimwomboleza Nyerere kwa muda mrefu. Hawakuamini kwamba kweli yule mwenye mamlaka karibu ya Mungu ametuacha. Tunataka Tanzania mpya na KATIBA mpya tusiyarudie makosa ya awali. Ikiwa makosa yaliyofanywa na wingi wa madaraka ya Rais wa kwanza Nyerere yametufikisha tulipo, Je akitokea mwendawazimu mwingine Tanzania itakuwa wapi? Mwenye sikio asikie neno hili ambalo Roho wa Mungu anawaambia Watanzania.


   
Uwazi



Group: Members
Posts: 176
Joined: July 2003

Posted: Nov. 21 2003,08:30   

Munishi

Kutuambia kuwa lengo iwe kuindoa CCM madarakani bila kutupatia alternatives haitoshi. Kenya waliweza kuiondoa KANU kwasababu walikuwa na mbadala ambaye ni NARC, wakaona kuwa viongozi wa NARC watafaa kuwaongoza wakenya kuliko KANU ya Baba Moi. Sidhani kama wewe una uwezo wa ki-muungu wa kuongoza watanzania milion 35 peke yako.

Ninaomba unieleze kwa mifano kama tukiiondoa CCM madarakani ni watanzania gani unafikiri utaweza kuongoza nao nchi kwa haki na uhuru kama "unavyojimbwafai"? Je hao watanzania wako tayari kugombea hizo nafasi za kisiasa? Usisema watanzania wapo wengi hata bila kunitajia jina moja la hao wengi!!
Uwazi
1 Next Page

Habari News