![]() ![]() |
![]() |
|
|
Gazeti
INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com Or fmunishi@hotmail.com Mazuri ya Nyerere na mabaya wa Mwinyi
Mazuri ya Nyerere? Alikuwa msemaji mzuri aliyeweza kuutetea uongo ukafanana na kweli.Aliwatisha viongozi waliokuwa chini yake na kuwafanya wamwabudu kama mungu wao. Alikuwa na nguvu ya kushawishi akaitumia vibaya kuwashawishi watu wahamie kwenye vijiji vya ujamaa. Alikuwa msomi aliyengangania sera zake hata kama sera hizo zinaonyesha kila dalili ya kushindwa. Kwa hili alikuwa mpumbavu. Ni wapumbavu tu ndio wasiobadili mawazo. Ubaya wa Mwinyi? Alibambikizwa uongozi ambao hakuwahi kuuota. Alifanywa kama robot inayofanya kile inachoamriwa kufanya, Mpaka siku alipofanya kosa la kujiamulia mambo kama rais wa nchi, ndipo Nyerere alipomkemea hadharani kwamba anaongozwa na mkewe.
Huo ndio uliokuwa ubaya wa Mwinyi AL HaJI. Napatwa na kichefuchefu ninapowasikia watu wakisema Nyerere alileta amani Tanzania. Aliileta kutoka wapi? Watanzania walikuwa na amani ambayo haikuwahi kupotea hata siku moja. Nyerere aliwaogopesha watanzania na wala hakuwaunganisha kama alivyotaka ulimwengu uelewe .
Kwangu mimi Nyerere ni mtu aliyekufa bila kufanya kile alichofikiri
kuwa alikiamini. Hakuwa na mawazo yake mwenyewe, bali alijikita
zaidi katika kuwaiga akina Mao na wakomunisti wengine duniani. Baada
ya miaka mitano Nyerere hatakumbukwa kwa lolote Tanzania, na huo
ndio utakaokuwa ushahidi wa kutosha kwamba waovu wanapokufa na mambo
yao yanakufa. Mpaka sasa nawasikitikia akina Mkapa kwani wanatumia
mawazo yaliyokufa ya Nyerere kuiongoza Tanzania ya walio hai. Ndio
maana ninasema kuwa CCM imezeeka na haifai kuiongoza Tz.
You are sick Asema Ben
Twende na wakati! Asema Ochieng Nyerere "aliwabrainwash" Watanzania wote.Tunashukuru
Munishi kutufahamisha hayo. Unaonekana wewe ni mmoja wa hao ambao
bongo zao zilikufa na Nyerere. Wewe ndiye unayetakiwa kwenda na
wakati.Ujue kwamba kutoa maoni siyo kosa la jinai kama Nyerere alivyowafundisha.
Munishi Amjibu Mlawa Ikiwa kwa miaka zaidi ya 40 ya CCM Tanzania imekuwa kama ilivyo, hawahitaji muda mwingine kuendelea kuiharibu Tanzania. Mbwa mzee hawezi kujifunza mbinu mpya. CCM imezeeka haitufai Tanzania. Nyerere aliwatisha watanzania akawatawala, sasa tunataka kiongozi aiongoze Tanzania. Mkapa si lolote wala chochote, kwani aliteuliwa na wala hakuchaguliwa. Watanzania wangepewa nafasi huru ya kuchagua wasingemchagua Nyerere. Tuache ukweli ubaki ukweli. Sasa hivi CCM ikiacha kutumia vyombo vya dola na iitishe uchaguzi kesho watanzania hawawezi kuirurisha madarakani. CCM na akina Mkapa wanabebwa na porojo za Nyerere, hata hawaoni haya maana hawana maneno yao wenyewe kwa Watanzania. Kila siku wanasema tumuenzi baba wa taifa, ili waendelee kula kwa jina lake. Ikiwa Mr.Mlawa ni Mtanzania basi utajua kwa nini Mwinyi anaheshimiwa na wananchi na siyo viongozi wa CCM.Kwao Mwinyi ni sawa na msaliti. kisa? Alithubutu kutumia ubongo wake wakati pipa la kufikiri lilikuwepo.Mwinyi ni mwanaume aliyeamua kutofautiana na Nyerere wakati wa uhai wake. Aliruhusu vitu vingi ambavyo Nyerere alikuwa amevipiga marufuku. Mwinyi wanamwita mzee ruksa.Siyo kwa ruksa ya Nyerere, bali wanatumia uhuru wao wa kumpima mtu. Mungu anapima watu, lakini watu wa Mungu wana uwezo wa kupima na ndiyo maana Nyerere walimwita mzee kifimbo. Yaani kuacha fimbo iliyokuwa inasadikiwa kuwa ya kishirikina, hakuna jambo jingine wanaloweza kumkumbuka kwalo. Unasema ukifanya mema watu hawakumbuki? wanakumbuka sana. Ndiyo maana wanamwita Mkapa jitu la jazba au bwana kodi.Wananchi wanasema Mkapa anairudisha njaa ya Nyerere.Ukiyachunguza majina hayo utajua wananchi ni kioo kinachomuona Mkapa kuliko anavyotaka kujionyesha. CCM haiwezi kun'gan'gania madaraka na kwa unafiki
iseme tuwatoe watanzania kwenye umaskini aliowaachia Nyerere. Itoke
Leo na inipe miaka miwili ione maajabu. Hawatayaamini macho yao.
Sijivuni lakini Mungu amenihakikishia kwamba kwa kipindi cha miaka
miwili Tanzania itabadilika kutoka nchi inayojaribu kuendelea na
kuwa taifa la kutegemewa duniani. nipeni nafasi muone. Mpinga ampinga Munishi Ndugu Munishi nimefurahi sana kuona sasa unaweza kuzungumza mambo bila uchambuzi wa kihistoria. Chukua mfano ya ylae yanayotokea zimbabwe halafu utayaona mwenyewe ni jinsi gani Afrika bado inadhulumiwa!!! Wakati wa Nyerere ilikuwa kosa kwa mkoloni kumilikishwa ardhi ya Waafrika. Hii ni pongezi ya kwanza na muhimu. Mambo haya ya kumilikisha ardhi wazungu na waarabu na mwisho wahindi na kuwauwa wazalendo imeanza wakati wa Mwinyi mtu ambaye sasa unamtetea karibu kumlamba miguu. Mimi ninapokumbuka wakati wa mwinyi na haya ya wakati wa Mkapa karibu machozi yananitoka. Wakati wa MWinyi kama ulivyosema sera ya ruksa, Waarabu walikuwa huru kuingia na ndege pamoja na silaha nzito kwenye mbuga zetu na kuua wanyama ovyo na kisha kufaidi wao. Mimi mzalendo nimekula nyama pori wakati wa utawala wa nyerere pekee lakini hadi leo hii siajaonja hata kiapande ya nyama ya nyumbu. Sasa waulize watawala mbuga zetu zinafaidi nani zaidi badala ya kukaa na shutuma dhidi ya nyerere kwani wanyama wanazidi kuzaliana na kujaza mbuga lakni nyama yake hatuioni. Sera ya ujamaa ndugu yangu ilikuwa nzuri sana ila tafsiri yake bado huielewi vizuri. Kwa mfano Yesu alifundisha watu wote kushirikiana pamoja na kuishi vizuri lakini ikatokea watu walitofautiana naye kwa tamaa ya pesa ndipo wakamuua ili kupata pesa na hadi leo hii kila anayekuja na wimbo wa shutuma haeleweki vizuri kwa watu. Kwa mfano, unaposema kuwa sera za Nyerere zilikuwa mbovu hakuweka sera hizo mwenyewe walikwepo pia na hata Babu yako ambao baada ya kufaidika na sera hizo wamegeuka!!! Ndugu Munishi naomba sana badala ya kuendelea kumshutumu Nyerere uanzishe mfuko maalum itakayosaidia kuwaendeleza walemavu. Yesu alisema hivi, atakayewatendea mmoja wa wadogo
zangu hawa mema atakuwa amemtendea yeye, bali yule atakayekuwa akipiga
parapanda njia nzima atakuwa sawa na kipofu anayefaa kuelekezwa
njia kwa kushikiwa fimbo. Thanks you very much having this excitement
site? I will be with you again. Bwana Mpingwa utapingwa sana. Kwanza unatutisha na American University of Rochester ili tukubaliane na mawazo yako. Unafanya kama baba yako Nyerere aliyejifanya mwalimu, akawafundisha watanzania kukumbatia umaskini. Ikiwa msomi kama wewe bado unalalamika kwamba matatizo ya Tanzania yanasababishwa na watu wengine nje ya Tanzania, na mbaya zaidi huna suluhisho, basi unajiaibisha kutaja kwamba uliwahi kwenda American University of Rochester. Unapomlaumu Mwinyi na Mkapa ndio umemlaumu Nyerere. Ninapousifu ujasiri wa Mwinyi na kumlaumu Mkapa bado nimemlaumu Nyerere. Unaposema wakati wa Nyerere Mwinyi na Mkapa unakosea. Tanzania tumekuwa na wakati mmoja tu wa Nyerere na ndio ninaotaka kuubadilisha. Namsifu na nitaendelea kumsifu Mwinyi kwa sababu alijaribu kuuleta wakati wake japo Nyerere alimzuia kwa nguvu zote. Kwa mabadiliko kidogo ambayo Mwinyi alifanikiwa kuyaleta japo siyo kwa ruksa ya Nyerere, yalimfanya apendwe na umma wa Watanzania ambao wengi hawajui IMF ni mdudu gani. Wananchi walikuwa hawana bidhaa muhimu wakati wa Nyerere, wakaziona madukani kwa ruksa ya mwinyi. Wananchi waliogopa kuwa na pesa wasiitwe wahujumu uchumi, Mwinyi akawapa ruksa ya kufanya biashara na kuwa na kiasi chochote cha pesa. Wananchi hawahitaji hizo taminoloji za IMF, ila wanataka watu wenye bongo ya kupambana na IMF maana wanahoji IMF ni ya watu na Tanzania kuna watu wenye bongo za kutosha kujibu mashambulizi ya IMF. Munishi niko hapa na sera za IMF hazitakuwa tishio kwangu kwani tayari nimetayarisha mfumo wa kupambana na sera hizo. Siku moja Mwinyi aliitwa Butiama kukemewa kama ilivyokuwa kawaida ya Nyerere kumwita kila aliyetaka kumkemea. Alipofika alikaribishwa sebuleni na kukalia sofa seti ya Nyerere kwa muda wa saa moja bila Nyerere kutoka chumbani. Siyo kwamba alikuwa hajui kuwa Rais wa Tanzania Mheshimiwa ALI Haji Hassan Mwinyi alikuwa sebuleni akimngoja, lakini masista wa kikatoliki waliokuwa wakihudumia hapo nyumbani hawakumpa hata kikombe cha chai wakati wote huo. Inasemekana kwamba mama Maria mke wa Nyerere hakupewa heshima yake kuwahudumia wageni nyumbani kwake na kazi hiyo waliifanya watawa wa kanisa katoliki. Alipotokea kutoka chumbani Nyerere alianza kumkemea Mwinyi."Umegeuza ikulu yangu kuwa mahali pa biashara? Kwa nini unaongozwa na mwanamke? Kama kazi imekushinda sema nitaweka mtu mwingine." Mwinyi alisimama na kusema."Ndugu yangu kwa nini unanitukana matusi ya nguoni mbele ya wanawake hawa ambao kwa muda wote nimekuwa hapa hawajanipa kikombe cha chai? Ikiwa mimi naongozwa na mwanamke basi ukija kwangu unaweza kukaa sebuleni saa nzima bila huyo anayeniongoza kukuletea angaa kikombe cha uji? Ikiwa unataka kunifuta kazi nifute, lakini huwezi kunipa nchi uliyoiharibu halafu uniambie nisirekebishe chochote bila ruksa yako. Ijulikane leo nani Rais wa Tanzania." Inasemekana kwamba Mwinyi aliondoka kwa hasira
na kurudi Dar. Tangu siku hiyo uhusiano wa Mwinyi na Mzee kifimbo
ulianza kuharibika kiasi kwamba Nyerere alianza kumkemea Mwinyi
hadharani. Ndio maana nausifu ujasiri wa Mwinyi na nitaendelea kufanya
hivyo. "Professor" Oloo Akasirika
Vibaya Munishi Amtuliza "Professor" "Professor" unaonekana una yako majambo. mimi sijatumia lugha ya kihuni ila nilisema: "Bwana Mpingwa utapingwa sana. Kwanza unatutisha na American University of Rochester ili tukubaliane na mawazo yako. Unafanya kama baba yako Nyerere aliyejifanya mwalimu, akawafundisha watanzania kukumbatia umaskini. Ikiwa msomi kama wewe bado unalalamika kwamba matatizo ya Tanzania yanasababishwa na watu wengine nje ya Tanzania, na mbaya zaidi huna suluhisho, basi unajiaibisha kutaja kwamba uliwahi kwenda American University of Rochester." Sijali nani alikulipia masomo, lakini unapotanguliza American University of Rochester, halafu ukasema mambo ya kawaida ambayo hayalingani na elimu unayotaka tuamini kwamba unayo, siyo vibaya tukikuambia unajiaibisha. Lakini kwa sababu umeandika tena ninaendelea kulijua tatizo lako. Umeniita "kiongozi wa Mungu" siyo kwa sababu nilitaja seminary niliyosomea, lakini sijui kwa nini unaniita mimi mwanadamu "kiongozi wa Mungu. Sikia ulivyosema:"Wewe kama kiongozi wa Mungu naomba sana ujiepushe na lugha za kihuni hii ni kwa sababu kiongozi wa Mungu ni lazima aonyeshe maadili mema mbele ya jamii ili wale anaowaongoza wawe na imani kwake." Kwa sababu yote niliyoandika yapo kwenye safu hii siyo vizuri nipoteze muda kuitetea lugha niliyotumia kwani kila mtu anaweza kusoma na kujionea hiyo lugha mbaya unayodai niliitumia. Unapotoa hoja kwenye safu hii ni vizuri uwe umejiandaa kujibiwa, na mara nyingi majibu siyo lazima yawe kama ulivyotarajia. Maoni yako yatasomwa na watu wa kila aina ulimwenguni kwa hiyo ikiwa ya Munishi yanakutoa povu mdomoni kwa hasira, sijui "Malebo Rasta" akikujibu itakuwaje. Nasema hivyo kwa sababu uliandika hivi:" Mimi ni kiziwi na unaponitukana kwenye magazeti siwezi kukuvumilia hata kidogo. Nilichozungumza yalikuwa ni maoni yangu. Kila mtu Duniani ana rafiki na Adui na ikatokea wewe unamchukia Nyerere halafu mimi namchukia Mwinyi." Sikumbuki mahali popote niliposema ninamchukia yeyote kati ya Nyerere Mwinyi na Mkapa. Lakini kwa sababu wewe umesema wazi kwamba unawachukia Mwinyi na Mkapa basi toa dukuduku lako la chuki kwao. Mimi sina chuki na mtu kwa hiyo usiniingize kwenye chuki zako. "Professor" Ulipotaja American University of Rochester nilifurahi kwamba safu hii imempata mtu anayeweza kuhimili uzito wa hoja, lakini nasikitika kusema kile ninachokisoma kutoka kwako kinaonyesha kwamba huwezi kuhimili uzito wa hoja. Unataja mambo mengi ambayo unadhani yatakujengea hoja badala yake yanakubomolea. Sikia ulivyosema:"Mimi ni kiziwi na unaponitukana kwenye magazeti siwezi kukuvumilia hata kidogo." Sasa ya kiziwi yametokea wapi? Na aliyekutukana ni nani? Au unataka kuhurumiwa? Basi nyamaza usitoe hoja. ikiwa hunyamazi basi jitayarishe kupokea makombora ya hoja kutoka kila kona ya ulimwengu. Sipambani na Nyerere mfu, bali napambana na mawazo ya Nyerere ndani ya Mkapa. Simchukii Mkapa wewe unamchukia, na kumpenda Nyerere. Kwamba unaweza kumpenda Nyerere na ukamchukia Mkapa aliyeteuliwa na huyo unayempenda ili ayaendeleze mawazo yake ya ujamaa na kujitegemea, hiyo ndiyo tofauti yangu na wewe. Basi fanya hivi. Nisaidie katika mapambano yangu ya kuyatoa mawazo ya Nyerere ndani ya Mkapa. Mimi niyachukue hayo mawazo nikayazike pamoja na Nyerere uliyempenda, halafu nikuachie Mkapa unayemchukia ujue utamfanya nini. Suala la walemavu na kanisa au walemavu na jamii unalijua fika.Wewe ni mwafrika na unajua mila za kiafrika zinaamini nini kuhusu ulemavu. tunajaribu tuwezavyo kuielimisha jamii iache mila potovu za kuamini kwamba ulemavu ni laana au kuusisha ulemavu na ushirikina. Katika hilo "Maprofessor" kama wewe mtatusaidia maana mnatufundisha kwamba mwacha mila ni mtumwa, na hapa kuna mila inayowabagua walemavu katika jamii. Mtuambie tuache mila zipi na tudumishe zipi. Huwezi kuwalaumu wakristo wote kwa sababu Askofu fulani alikataa kukusaidia wewe binafsi. Kuhusu hili la mwisho ulilosema:
"Zaidi ni kuwa hata hao Waislamu unaowatumia kuna siku watakuua
kama wanavyosema kuwa wakiristo ni makafiri hata wewe uko humohumo."
Hapo umenichanganya sikuelewi. Labda ufafanue nawatumia waislamu
vipi, na wataniua vipi na kwa sababu gani. |
||||||||||||
|
|
|
|