![]() ![]() |
![]() |
|
|
Gazeti
INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com Or fmunishi@hotmail.com Majira Wamzuia Munishi kutoa Maoni Gazeti la "MAJIRA" kwenye mtandao kitengo cha mijadala limempiga marufuku mwinjilisti Munishi kutoa maoni katika safu hiyo. Akieleza sababu za hatua hiyo msimamizi wa ukumbi huo wa maoni alisema: "Lengo lake kubwa ni kuijenga, kuikomboa na kuiendeleza jamii yetu kiuchumi, kisiasa, kielimu, kibiashara, kiutamaduni n.k." Kwamba gazeti la majira linawazuia watu kutoa maoni tena ndani ya mtandao siyo tu ni ajabu, bali inashangaza. Gazeti hilo limekuwa likipigwa stop na serikali mara kwa mara kwa kile serikali ilichodai habari zinazokiharibia chama tawala sifa. Na limekuwa likilalamika hata kwenye safu hii ambayo sasa wao ndio wanaowapiga wengine STOP. Naye Munishi akieleza masikitiko yake alisema:" Internet ni bahari pana kuliko bahari ya Hindi. Inashangaza kuona kwamba huku baharini kuna watu wanaosema usinywe maji hapa!!! Ajabu . Basi mimi naenda zangu lakini usisahau kwamba barabara ninayoitumia kwenda ni maji, na kila kilichonizunguka ni maji. Nitakudanganya nikikuambia kwamba nimehuzunishwa na kitendo chako cha kunizuia kunywa maji hapa. Ila ninakushangaa!! Kumbuka ulisema:"Lengo lake kubwa ni kuijenga, kuikomboa na kuiendeleza jamii yetu kiuchumi, kisiasa, kielimu, kibiashara, kiutamaduni n.k." Tufafanulie hiyo kadhalika maana yake nini kwani kwa wengine inaweza kumaanisha chochote. Unanikumbusha siku moja niliingia hotelini hapo bongo na akaja jamaa mmoja aliyetaka kujua kuna chakula gani hapo hotelini. Baada ya wahusika kumtajia kwamba kuna wali maharage na ugali nyama mtori na ndizi na kadhalika, jamaa alisema apewe hiyo kadhalika. wahusika walimcheka, lakini alikuwa na haki ya kutaka kula hiyo kadhalika kwani kwake kilikuwa chakula kipya. Kwenye ukumbi huu sitaki kuchangia mawazo kuhusu kadhalika, ila naomba nifafanuliwe kuhusu utamaduni, elimu siasa, zinatofautiana nini na dini? Haya ninayouliza yakisomwa yana tofauti gani na publications? Sasa unapomzuia yeyote kunywa maji hapo na sababu unazozitoa ni: "Nisingependa, wala sitarajii kama kuna mtu atafurahia kuona baadhi ya wachangiaji wanautumia vibaya ukumbi huu. Dhumuni la ukumbi huu sio kuweza kuwapa nafasi waheshimiwa watoe publications zao au kuhubiri dini zao. Mheshimiwa Munishi nafikiri umenielewa" Ukweli sijakuelewa ila nimekushangaaa!!! Wakati wa kuwachagulia watu habari, na kuwalazimishia maoni umepita. ikiwa hujaelewa hilo nakusikitikia. Bado niko baharini, ninaondoka sehemu uliyosema nisinywe maji, lakini barabara ya kuondoka kwako ni maji , mimi mwenyewe nimezama majini siwezi kukudangaya kwamba nitaacha kunywa maji hapa au popote, na isitoshe nikihema natoa maji. Kwa hiyo ndoto zako kwamba utakuwa na watu hapa baharini
ambao hawajaloa maji hizo ni ndoto za mchana. haiwezekani. Wanachama wa ukumbi wachachamaa Sawa imeeleweka lakini kama tukiwafukuza hao wapinzani basi na sisi tutabakia mbumbumbu bila ya kujua mambo jinsi yanavyokwenda.Kwa hiyo through hao wapinzanzani ndio tutajua njia gani ya kufuata . Kuna ndugu kama Mheshimiwa Munishi kwa kweli kaandika na kaweza kuchangua matatitizo yanayotukabili lakini mimi kama mkereketwa wa mwalimu Nyerere sikupendelea sana wakati ama kama mzee akizungumzwa sana kwani ninaamini kuwa alitufikisha alipoweza na hivi sasa ni jukumu letu kuendelea mbele na kujaribu kubadilisha makosa yaliyo fanywa hapo nyuma na sio kumlaumu Mzee Nyerere. Mimi nafikiri tunatakiwa ku deal na hawa viongozi tulionao
sasa kwani huo ndio ukweli, mzee Nyerere hayupo tena . Nandani mpango wako ndugu webmaster ni mzuri tu ila ningeomba kujulishwa majukumu yao. Na mawazo yangu ni badala ya kuacha malumbano ni vyema hoja zisizofaa zikaondolewa moja kwa moja, kama ile niliyoiandika ya machimbo ya dhahabu. Sikuelewa ulivyosema Puplication ulimaanisha nini labda ungefafanua ni nini hoja na ni ninipublication. Mwisho nafikiri hakuna sababu ya kuogopa baadhi ya hoja kwa sababu ya uzito wake kama kweli tunataka kujenga nchi. Ndiyo maana wengine tumetumia majina halisi. au
vingine huu ukumbi utakuwa wa kupoteza muda. Mimi hayo ni maoni
yangu. Aika Asema Asante lakini !!! Pope wa Tanzania
Asema kusema kweli mh munishi inaonekana kuwa una uchungu na mabadiliko ya jamii yetu watanzania . Bila shaka mh umepata fursa ya kutembelea sehemu mbali mbali ulimwenguni kupata exposure .... katika jamii nyingine wanavyokabiliana na maisha . Ila mheshimiwa kama ni mjumbe au (mtu uliyepata fursa) hiyo unashidwa kufikisha ujumbe kwa wahusika . unachofanya ni kutuchanganya tuu ,,,,,,, Jaribu ku summari za point zako na hii itatupa uwezo wa kutafakari unachoandika ... ASAALAM ----- BY MCHUNGUZI Madevuu Atafuta Kinyozi mchungaji munishi! si vyema kumkuza kuwa ni mchungaji kiutendaji munishi ni muimbaji tena muimbaji asiye faata umaana wa uimbaji kila linlomuijia hulitoa katika kinywa chake na kuwa ni sehemu ya wimbo wake kwa wakati huo!hivyo mimi simshangai na mjadala wake ambao naona umeniacha hoi bin taaban kwani hana anasema hiki mara hiki bila kuelewa anasema nini au bila mpangilio wa maudhui anayozungumza utafikri anaimba!na pengine mimi sishangai haya yote aliyoandika pengine ni moja ya nyimbo zake mpya zisizo kuwa na mpangilio wowote lakini si injili hii kwa watu bali upotoshaji wa watu! ----- madevuu |
||||||||||||
|
|
|
|