Ukurasa wa mbele
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail

CNN
TBN
BBC
Times
Islamtz.org
Winners
Maranatha
Intergrity

China Today

Japan Times

Korea Online

China Site

China Maps

USA Today

Google Seach

China English

Gv China

China view

China news

China
Natinal
News

China Tech

India News

India Times

India Daily

Gospel of
Jesus

USA Gospel

Gospel
Church

Dubai news

Africa News

Gospel Music

US VISSA

BBC
Bush
Curches
Gospeltv
munishi
Mkapa
usgospel
Times
GTV
GTVGOSPEL
Jesus
God
Faith
Life
Kenya
Tanzania
Uganda
Africa
Japan
Toyota
China
Korea
India
Nation
News
Online
Nyerere
Kibaki
Museveni
Mugabe
KOFFI ANNAN
Nairobi
Dar
Goverments


Gazeti la INJILI
Kwenye Internet

http://www.munishi.com

Tel. 254722602445 E-mail:fmunishi@hotmail.com Or
munishifaustin@yahoo.com
 


Katiba Siyo mali ya CCM
Hakuna Uchaguzi Bila Katiba Mpya

Mchungaji Faustin Munishi Rais Mtarajiwa Tanzania Amesema kwamba Hakuna uchaguzi Tanzania bila ya Katiba mpya. Watakaowaburuza Watanzania kuingia kwenye uchaguzi bila katiba kubadilishwa, wajue wanafanya hivyo kinyume na matakwa ya Watanzania walio wengi. Alisema: "
Nia yangu ya kuwa Rais wa Tanzania bado iko pale pale.Kwamba katiba hairuhusu wagombea binafsi, hiyo hainifanyi nijiunge na chama chochote cha kisiasa ili nitimize masharti ya KATIBA. Kwangu siasa ni uongo, na siwezi kujiunga na uongo niwatoe waongo. Ikiwa CCM hawataibadili Katiba iruhusu wagombea binafsi, basi tutaiasi katiba tuandike yetu. Wakichaguana nasi tutachaguana. Kwa mara ya kwanza Tanzania itakuwa KATIBA ya Injili na serikali ya Injili, Rais wa Injili na Bunge la kiinjili. Hapo ndipo tunapoelekea. Siyo ajabu kwani tayari tuna nyimbo za GOSPEL kilichokuwa kimebaki ni KATIBA ya Gospel Itakayounda tume ya Gospel ya uchaguzi utakaomchagua Rais wa Gospel atakayeunda Serikali ya Gospel akitumia wabunge wa Gospel. Waislamu wakiona vyema wajiunge na Gospel tutawakaribisha. Wakiona waunde yao ya SHARIA, ni sawa. Pia kwa mara ya kwanza Tanzania itakuwa nchi ya serikali zaidi ya kumi. nayote hayo yatafanyika kwa amani. Kikwazo cha amani Tanzania kitakuwa ni CCM pale watakapokataa mabadiliko, na kungangania madaraka.Kama kawaida yao wataanza kuwalaumu wengine. Lakini wananchi safari hii wameerevuka na wanamjua mbaya wao ni nani.CCM ndiye nyoka anayestahili kupondwa kichwa."

KATIBA SIYO MALI YA CCM

Katiba ya Tanzania ni ya watanzania. Siyo mali ya CCM. Lazima kila mtanzania ahusike katika kuirekebisha au kuibadili. Kuna mengi yanayohitaji marekebisho na mengine yatatolewa kabisa. Najua kwamba nikiingia ikulu na katiba ya sasa itanikwamisha mengi. Tanzania ni sawa na gari iliyonoki injini. Inataka  matengenezo kamili ndani ya injini. Siwezi kuifanyia Tanzania MAREKEBISHO INAYOSTAHILI bila ya katiba mpya. Hata kama kipengele kimoja kitabadilishwa niweze kugombea bila chama cha kisiasa, hilo siyo lengo langu.

Lengo langu ni kuleta mabadiliko ambayo ndiyo kiu ya watanzania wengi wakubwa kwa wadogo. Hatuwezi kuwa na nchi yetu, bila katiba yetu. Tena katiba haiwezi kuwa yetu kama haina mchango wa mawazo yetu. Tunahimiza zoezi la kukusanya mawazo kutoka kwa watanzania wote lianze ndipo katiba irekebishwe. Bila hilo kufanyika  hakuna sababu ya kufanya uchaguzi kwani CCM watatumia mapungufu yaliyoko kwenye katiba kushinda uchaguzi kiulaini.

Tumeliona hilo. Ndiyo maana tunasema kwamba hakuna aliyehitimu kuingia katika uchaguzi na katiba ya sasa. Ina mapungufu mengi, Hatuitaki, Ni batili. Yeyote atakaeingia kwenye uchaguzi na katiba ya sasa ajue anafanya hivyo kinyume cha sheria. Ndiyo ni kinyume cha sheria kwa sababu Watanzania wengi wanataka KATIBA MPYA. Kujaribu kuwaburuza ili waingie kwenye uchaguzi bila ya kuibadili katiba ni mbaya kuliko wao kuchukua silaha na kuanza kudai haki zao kwa mtutu wa bunduki. Hatuombi hali ifikie hapo kwani itatuumiza wote. Lakini ikibidi, Hakuna jinsi.


Kuhusu baraza la mawaziri, nilisema wazi kwamba mimi sitakuwa na uwezo wa kuunda baraza la mawaziri. Katiba ya sasa inamruhusu rais kuunda baraza lake la mawaziri. Katiba mpya italiruhusu bunge kuunda baraza letu la mawaziri. Sifa za watakaogombea nafasi za uwaziri lazima ziambatane na taaluma zao katika wizara husika. Wakati wa kuchaguliwa waziri kwa sababu za kikabila, kiundugu na kirafiki, UMEKWISHA. Hata hapa kuna wengi tayari nimeona wataifaa Tanzania katika baraza la mawaziri. Mtu kama Augostino Moshi ukisoma posti zake utaona uanasheria ndani yake.


Hawa ndio tunaotaka kuwahimiza wagombee nafasi za waziri wa sheria na katiba. Wabunge wakiridhishwa na kuhitimu kwao katika fani husika watawachagua.
Nimemtaja Moshi siyo kwa sababu ni mchagga, bali nipate nafasi ya kujibu swali lake. Aliniuliza kama nakimudu kiingereza. Ukweli ni kwamba kiingereza nakimudu vizuri.

Lakini nilijifunza kwa njia ngumu zaidi. Nikija Nairobi mwaka 1984 nilikuwa siwezi kabisa kuwasiliana kwa kiingereza. Jambo hilo lilinikera sana. Niakaamua kuanzia mahali. Biblia ndicho kitabu kilichokuwa hakibanduki mikononi mwangu. Nilikuwa nimemaliza kuisoma na kuirudia mara tatu. Nikanunua madaftari makubwa ya kuandikia kama matano, halafu nikanunua Biblia ya kiingereza. Nilianza kuandika neno hadi neno, nikamaliza kuandika agano jipya. Mengi nilielewa maana kutokana na ukweli kwamba nilikuwa nimeyasoma katika Biblia ya kiswahili. Yaliyonishinda matamshi ilinibidi ninunue biblia katika kaseti. Yale ambayo sikuelewa kuyatamka, Biblia ya kaseti ilinisaidia kujua yanatamkwa vipi.


Hata kabla ya kumaliza agano la kale tayari nilikuwa na kiingereza kingi sana akilini mwangu. Tayari niliweza kuwasiliana kwa kiingereza kuliko.  Nasita kusema kuliko wasomi wengi Tanzania, lakini ukweli unabaki hivyo. Sasa hivi ndipo kasi ya kujifunza kiingereza imeongezeka Tanzania. Wakenya na Waganda wamefungua shule uchwara na wanaziita za kimataifa kwa sababu tu wanazingatia somo la kiingereza. Ningekuwa najua kutumia kompyuta wakati huo, nisingepitia njia ngumu hivyo kukijua kiingereza.

Lakini sijuti kwani maneno mazito ndani ya Bibilia yamekiongezea uzito kiingereza ninachotumia kuzungumza na hata kuandika. Sitaki nijisifu kwamba Kiingereza changu ni sawa na kile cha malkia wa UINGEREZA, lakini nitakuwa mpumbavu gani nishindwe kujieleza kwa lugha rahisi kuliko zote duniani? Kiingereza kwa sasa ndiyo lugha rahisi kuitumia kuliko hata kiswahili. Haya niliyoyaandika hapa hakuna mahali  katika kompyuta naweza kufanya "SPELL CHECKING", sababu ni kiswahili.  Lakini ingekuwa kiingereza, bila kujali natumia programu gani nitapata mahali pa kuisahihisha kazi yangu kiulaini.

Ni urahisi huo ndio unaonipa mashaka kwamba wengi hawajui kiingereza. Kuna rafiki yangu simtaji. Ni mwandishi wa habari katika gazeti la NATION lichapishwalo kwa kiingereza kila siku nchini Kenya. Ukisoma makala zake, utapenda. Mpangilio wa lugha, usahihi wa maneno, NK. Lakini wacha akuandikie barua ya mkono, Au akutumie ujumbe mfupi kwa simu za kipepesi. Utashangaa mbona kiingereza chake kibovu?

Kumbe amelemazwa na kompyuta ambayo inamfanyia kila kitu kuanzia "SPELL CHEKING" mpaka na mtiririko wa lugha. Je ni kitu cha kujivunia kujua kiingereza? Hapana. Hata wanaokiongea au kukiandika vibaya siyo makosa yao. Siyo lugha yao ya kwanza maishani.

Pamoja na umuhimu wa kiingereza duniani leo, Siungi mkono kasi watanzania waliyo nayo katika kukikimbilia kiingereza. Wengi wanalipa pesa za kutisha kwenye shule ambazo zinatilia mkazo kiingereza, Wengine wanawapeleka watoto wao nje Kenya Uganda, Na hapo nimetaja sehemu chache sana. Yote ni watoto wajue kiingereza. Kuna tofauti kati ya kuelimika na  kujua lugha. Lakini kwa watanzania wengi hilo hawalijui. Wanafikiri kuelimika ni kujua Lugha. Kuna uwezekano wa kuzijua lugha tofauti bila kuwa na elimu. Lakini kiingereza tu, sioni ulazima wa wazazi Tanzania kwenda kasi wanayokwenda kukifukuzia kiingereza. Kuna njia nyingi za kuweza kuijua lugha yeyote bila kuingia gharama kubwa wanazoingia watanzania.Nimalize kwa kusema kuna njia nyingi za kumuua panya. Ukiweka mtego utamnasa atakufa. Ukiweka dawa ya sumu jikoni, panya atakula na atakufa. Lakini ole wako mtoto wako akidhani hiyo uliyoweka jikoni ni peremende. Uliyotarajia yampate panya yatampata mtoto wako.

Watanzania wengi wameamua kumuua panya wa kiingereza wakitumia sumu jikoni. Tayari nimeiona hatari mbele yao. Nani awaambie njia nyingine rahisi ambayo ni kumchagua Munishi awe rais wa Tanzania chini ya katiba mpya nitainua kiwango cha elimu. Kiwango cha elimu kikiinuka Lugha zozote hazitakuwa ngumu watanzania kuzitumia. Naujua ugumu nilioupata kujua niyajuwayo, sitopenda mtoto wa kitanzania apitie niliyoyapitia kupata elimu.


Bwana Moshi nafikiri nimekujibu. Nashukuru kuniuliza hilo, kwani CCM wamekuwa wakimtesa sana Mrema kwa hilo. Najua hata mimi wataanza kutumia hilo kama mtaji wa kunipinga nisiwe rais. Lakini hata Mkapa kiingereza chake ni cha kubabaisha pamoja na kwamba alisomea lugha ya kiingereza kama somo ili aweze kuwa mhariri wa DAILY NEWS. Kwa mtaji wa lugha tena ya kiingereza hapa wamefika. Watafute jingine. Ikulu nitaingia tu. Nia na sababu ninazo. Kama walifikiria kwamba uwezo ni kiingereza, basi hata uwezo ninao.  

Kuhusu swali la uraia, maoni yangu ni kwamba Mtanzania anayetaka kurudi kuuchukua uraia wake, itabidi aukane uraia aliouchukua ugenini. Ni maoni yangu binafsi. Lakini kwa sababu tutabadili katiba, sijui maoni ya watanzania yatakuwaje kuhusu hilo. Kulingana na katiba ya sasa, Rais anakuwa kila kitu. Ndiyo maana maswali kama utafanyaje kuhusu hili na lile yanajitokeza kwa wingi. Lakini KATIBA MPYA mambo hayatakuwa hivyo. Kila jambo litashughulikiwa na wizara husika na wanataaluma husika.

Swali la uraia litashughulikiwa idara ya uhamiaji. Katiba mpya itawatengenezea mazingara mazuri ya kufanya kazi yao bila kuingiliwa kisiasa. Kwanza kutakuwa hakuna chama cha kisiasa madarakani.

Maswali mengi niliyatarajia, na bado nayatarajia. Wengi wamezoea sana utawala wa CCM wala hawajui itakuwaje bila CCM. Mimi naiona Tanzania mpya bila CCM. Picha hiyo iko akilini mwangu. Niko tayari kuendelea kuwafafanulia zaidi picha ya Tanzania mpya. Naiona iko nami. Mungu ameiweka maishani mwangu. Hakuna kitakachonitenga na Tanzania mpya iliyo maishani mwangu, labda maisha yenyewe ndiyo yanaweza kunitenga na Tanzania mpya na katiba mpya, halafu MAISHA MAPYA YA WATANZANIA.
Mungu bariki watanzania. Waonyeshe Tanzania mpya bila CCM.




Gazeti la "MWANANCHI"
Walichokosea ni kutosema kwamba Munishi nitagombea Urais Tanzania. Nia yangu ya kuwa Rais wa Tanzania bado iko pale pale.Kwamba katiba hairuhusu wagombea binafsi, hiyo hainifanyi nijiunge na chama chochote cha kisiasa ili nitimize masharti ya KATIBA. Kwangu siasa ni uongo, na siwezi kujiunga na uongo niwatoe waongo. Ikiwa CCM hawataibadili Katiba iruhusu wagombea binafsi, basi tutaiasi katiba tuandike yetu. Wakichaguana nasi tutachaguana. Kwa mara ya kwanza Tanzania itakuwa KATIBA ya Injili na serikali ya Injili, Rais wa Injili na Bunge la kiinjili.
Hapo ndipo tunapoelekea. Siyo ajabu kwani tayari tuna nyimbo za GOSPEL kilichokuwa kimebaki ni KATIBA ya Gospel Itakayounda tume ya Gospel ya uchaguzi utakaomchagua Rais wa Gospel atakayeunda Serikali ya Gospel akitumia wabunge wa Gospel. Waislamu wakiona vyema wajiunge na Gospel tutawakaribisha. Wakiona waunde yao ya SHARIA, ni sawa. Pia kwa mara ya kwanza Tanzania itakuwa nchi ya serikali zaidi ya kumi. nayote hayo yatafanyika kwa amani. Kikwazo cha amani Tanzania kitakuwa ni CCM pale watakapokataa mabadiliko, na kungangania madaraka.Kama kawaida yao wataanza kuwalaumu wengine. Lakini wananchi safari hii wameerevuka na wanamjua mbaya wao ni nani.CCM ndiye nyoka anayestahili kupondwa kichwa.



Juu ni "Kenya Times" Gazeti la Kenya likiripoti kwamba "Munishi Matatani". Wakati chini Gazeti la Nipashe linaripoti kauli ya Munishi kwamba ana ugomvi mkubwa na CCM. Munishi anakifananisha chama hicho na NYANI ambaye siku ya kufa kwake imekaribia. Haijalishi ujuzi alio nao kuparamia miti, Lakini siku hiyo miti yote huteleza. CCM wana uzoevu wa kuiba kura, na kila aina ya ujanja ili wabaki madarakani, lakini safari hii miti yote inateleza. Hawatayaamini macho yao, wakati Munishi atakapochukua hatamu za kuiongoza Tanzania katika ENZI MPYA.



Gazeti la Nipashe linaripoti kauli ya Munishi kwamba Yeye ndiye aliyeimba nyimbo zinazosemekana ni kashfa kwa CCM na serikali yake. Haombi msamaha kwa yale aliyoimba na haoni sababu yeyote kwa nini serikali iwabuguthi wenye maduka ya kanda za injili Tanzania.. Kama mtanzania, ana haki ya kutoa maoni yake kuhusu serikali. Kama hilo ni kosa linalostahili kifo, basi wa kufa ni yeye, na siyo wananchi wasio na hatia. Munishi anaiagiza serikali iache mara moja kuwasumbua watanzania wanaouza au kusikiliza kanda hizo. Ni haki yao kikatiba kufanya hivyo, na serikali haina haki ya kuwabuguthi.
Habari Zaidi


Gazeti la NATION likiripoti jinsi CCM inavyowatesa wasanii Tanzania

Nao PEOPLE wasema toleo nambari saba la Munishi ni kiboko yao.

Gazeti la NIPASHE nalo linapasha.

Munishi atangaza kuwania URAIS. Linaarifu NYAKATI

Mwanaspoti nalo halikuachwa nyuma

SIJUTI KUGOMBEA URAIS


Sijuti kugombea kiti cha urais Tanzania, Bali namshukuru Mungu kuniwezesha kufanya hivyo. Mungu ni HAKI tupu na ndani yake hakuna hata chembe ya udhalimu. Hatuwezi kudai kumcha Mungu huku tukiunga mkono udhalimu wa CCM. Wanaoiunga mkono CCM dhalimu, watuambie wanamwabudu nani kama siyo shetani baba wa udhalimu wote. Tusidanganyane. Huwezi kuwa mtumishi wa Mungu na ukose kuyaona MAOVU ya CCM. Watumishi wa shetani ndio wanaoyafurahia maovu kwani, yanatimiza lengo la shetani la kuchinja, kuharibu, na kuua. Tunaipinga CCM Tanzania sawa na tunavyompinga shetani duniani kote. Dunia ni mali ya Mungu, na Tanzania ni sehemu ya dunia. Hatuwezi kumpinga shetani duniani huku tukimruhusu aweke kambi Tanzania, akitumia Chama Cha Majambazi CCM. Haiwezekani, Tumekataa, Hatutakubali, na hatutaki.

Ni agizo la Mungu kwamba wale wanaomtumikia, Wayahubiri maneno yake kwa walimwengu wote. Kila atakaeyaamini maneno ya Mungu, Sifa ya kwanza ni kuyakataa maovu yote. Atafanya kila lililo ndani ya uwezo wake kuwasaidia, Kuwatetea, na kuwakomboa wanadamu wanaonyanyaswa chini ya utawala dhalimu wa CCM. Akifanya hivyo, anatimiza agizo la Mungu. Akifanya kinyume na hayo, Atakuwa hajatimiza wajibu wake kama mtumishi wa Mungu.

Watumishi wa Mungu ni wale wanaomwamini Mungu. Haijalishi wanatoka dini gani, hata kama ni dini za kienyeji,  Ilimradi wanamwamini Mungu, Basi wamehitimu kuitwa watumishi wa Mungu. Hatuwezi kuwahukumu watu kutokana na tofauti za kidini, Badala yake tunawahukumu kutokana na matendo yao. Wakitenda mema ambayo asili yake ni Mungu,  Tutawaita watumishi wa Mungu. Hata kama dini zao ni za kiasili. Huwezi kuwaita vinginevyo. Ni watumishi wa Mungu. Wakitenda maovu ambayo asili yake ni Shetani, Tutawaita waabudu Shetani hata kama dini yao inatoka Marekani. Katika hilo watumishi wa Mungu ni dhahiri. Yaani wale wanaochukia maovu na kuyakemea, hata kama maovu hayo ameyafanya Mkapa na serikali yake inayowaua wale wanaosema kwamba CCM imezeeka, Iliharibu Tanzania, hawaitaki. Kuna kosa gani kusema hivyo wakati ni ukweli usiopingika?

Wakati umefika kwa watumishi wa Mungu kuwakomboa watu wa Mungu. Wameteseka vya kutosha. CCM imewaibia, na hata wengine imewaibia uhai wao. Mungu anasema "IMETOSHA. LAZIMA WATANZANIA WAKOMBOLEWE KUTOKA MAKUCHA YA CCM." Kwa Mungu hakuna lisilowezekana. Mungu siyo sawa na mwanadamu. Akisema saa imefika Watanzania wakombolewe ANAMAANISHA NA ITAKUWA HIVYO. Nilianza kuyasema haya mwaka 2000, wengine wanauliza mbona ni muda mrefu na hakuna dalili za njia ya kuwakomboa watanzania? Mungu hatawaliwi na muda. Muda wote ni wake. Kifupi ni kwamba Mungu hachelewi wala hawahi. Hufanya vitu kivyake ili abaki Mungu nasi tubaki wanadamu. Mwaka elfu mbili nilisema ole wao wanaosimama kuyazuia mapenzi ya Mungu Tanzania. Mkapa alisema yeye ni mbabe na akashupaza shingo. Leo hii anatembelea magongo akielekea kaburini. Haijalishi watatumia pesa ngapi kujaribu kumtibu, Lakini lazima mapenzi ya Mungu yatendeke ili iwe funzo kwa wengine wasijaribu kushindana na Mungu. CCM mwisho wake umefika. Mungu anajua atatumia njia gani kuzima kiburi cha CCM. Kazi yangu ni kuwatayarisha watanzania wawe tayari kuyaona makuu ya Mungu Tanzania. Baada ya kila kitu kutendeka na CCM iwe ni historia, Watanzania tutayainua macho yetu juu na kumtukuza Mungu aliyetenda maajabu machoni petu. Kuna wengi hawataishi kuyaona hayo.

Sera za Mungu ni "ANZENI NA MIUJIZA ITAWAFUATA." Ni vigumu watu kuifuata miujiza ya Mungu, Lakini ni rahisi watu walioamua kufuatwa na miujiza ya Mungu. Kwanza wanaihitaji kuliko wale ambao hawajaamua. Tangu tulipoamua kuipinga CCM na sera zake mbovu, Mungu ametenda miujiza mingi. Mkubwa kuliko yote ni ule wa kumwangusha mbabe wa CCM DIKTETA Nyerere pamoja na  Nduli Benjamin Mkapa ambae atafuatia karibuni.  

Kwa sasa CCM ni sawa na nyoka aliyekwisha pondwa kichwa na kilichobaki ni kutikisika kwa mkia. Suala kama la kuibadili katiba ili iniruhusu kugombea bila chama cha kisiasa, siyo tatizo kubwa kama linavyoonekana. Wengine wanaliona hilo kama bahari kubwa mbele yetu.  

Yangu ni kuwaambia kwamba waamini tu na watauona muujiza wa Bwana. Kama wana wa Izraeli walivyopita katikati ya bahari ya Shamu kama nchi kavu, Ndivyo Watanzania tutakavyolivuka tatizo la katiba. Mungu mwacheni abaki Mungu.

Arafat kufa siyo mwisho wa mapambano


Arafat amekufa. Wapalestina wanaomboleza, Israeli wanashangilia. Ni mapema sana kushangilia. Sharon aliamini kwamba Arafat akifa, amani itainyeshea Israeli kama mvua. Kinyume chake ndio sahihi. Watamkumbuka Arafat japo sasa hawaombolezi kifo chake. Serikali ya Mkapa Tanzania inaamini kwamba Munishi na nyimbo zake ni mwanzo wa kuvurugika kwa amani Tanzania. Kinyume chake ndio sahihi. Amani ilivurugika pale Mkapa alipowaamuru Polisi wawaue Wazanzibari zaidi ya 70 kwa sababu za kisiasa. Majeshi Tanzania walikasirishwa sana na jambo hilo,na walikuwa tayari kuipindua serikali ya Mkapa. Munishi akaimba wimbo "MPENDE ADUI YAKO", Mkapa badala ajue kwamba wimbo huo ulikuwa ukimsaidia yeye ili serikali yake isipinduliwe na kisha afunguliwe mashitaka ya kuwaua raia wasio na hatia, Aliupiga marufuku wimbo huo na kuamuru polisi wamsake Munishi. Iko siku Mkapa atamkumbuka Munishi. Ngoja kipindi chake cha urais kimalizike, na tunaomba kimalizike salama, halafu Mkapa awe raia wa kawaida. Kombe aliyemwamuru amsake Munishi, ndiye atakayeamriwa amtie Mkapa mbaroni ili ajibu mashitaka ya kuua na kupora mali ya umma pamoja na kuiuza nchi kwa makaburu. Habari zaidi
Censorship turning systematic in Tanzania

Hii ni kanda mpya ya video katika VCD, ambayo Mchungaji Munishi aliitoa mapema mwaka 2004 na ilipoanza kusambaa Tanzania serikali ikaipiga marufuku. Ndani ya video hiyo kuna maneno kama CCM chama cha majambazi na wauaji.Pamoja na nyimbo mpya. Jipatie kanda hiyo uonje UHONDO.

Upande wa nyuma wa kasha la video mpya ya Munishi.

CCM WENGINE WANAKIITA CHAMA CHA MAJAMBAZI

SIKU YA KUFA NYANI MITI YOTE HUTELEZA

http://www.munishi.com

Siku ya kufa nyani, Miti yote huteleza.
CCM ni sawa na nyani ambaye siku ya kufa kwake imekaribia. Kila mti wanaojaribu kuuparamia unateleza. Ujuzi wa CCM kuparamia miti ni wa miaka mingi. Lakini sasa miti yote inateleza na kufa watakufa.

Utafiti uliofanywa na BBC Tanzania unaonyesha kwamba ukimwi umesambaa Tanzania kwa kiwango cha kutisha. Nchini Tanzania inasadikiwa kwamba wenye madaraka ndio wanaoongoza katika kuusambaza ukimwi. Kwingine wanadai ngono kama hongo, na mara nyingine wanapewa kama zawadi kwa sababu wana pesa nyingi walizojipatia wakiwa madarakani. Usijali kama walipata kwa halali mapesa wanayotumia, lakini ukweli unabaki kwamba wenye madaraka Tanzania ndiyo wanaoongoza katika kuusambaza ukimwi. Nani wamekuwa kwenye madaraka Tanzania kwa zaidi ya miaka arobaini kama siyo CCM?

 Hao ndio nambari wani kwa kila kitu, hata kuusambaza ukimwi ni nambari wani. Hata bila upinzani, ukimwi unatosha kuisambaratisha CCM. Msidanganyike kwamba CCM ni chama imara. Kama kuna chama kisicho na matumaini ni CCM.

Ni ukweli walikuwa wamejiimarisha katika kila kona ya nchi, lakini nguvu zao ndizo zimegeuka kuwa maangamizo yao. Huzuni yetu ni watanzania wasio na hatia ambao itawabidi wapoteze maisha yao.

Nchi nyingi barani Afrika wameutangaza ukimwi kama janga la kitaifa, Lakini Tanzania ndio kama hakuna ukimwi kabisa. Vigogo wanaokufa kwa ugonjwa huo wanatafutiwa majina ya kitaalamu kufunika isieleweke walikufa kwa Gonjwa la Ukimwi.

Utasikia kwamba ilikuwa ni kansa ya damu, wengine watasema kwamba moyo ulishambuliwa, na siyo ajabu ukasikia wakisema kwamba damu za waadhirika zilitengeneza mabonge ya barafu ya damu, na ilipokataa kuyeyuka ndipo kifo kikatokea. Kwamba nchi imekataa kukubali ukweli kwamba ukimwi unaua hata viongozi hilo ndilo linalotisha kuliko Ukimwi wenyewe. Hatulifurahii, kwani hatujui wanaosambaza wamefikia wapi katika zoezi lao. Siyo ajabu miaka kumi ijayo Tanzania ikawa na watu wachache sana.

Kama CCM wanaongoza kueneza ukimwi? KANISA NI SALAMA?
Lakini tusisahau kwamba maaskofu na mapadri wanakufa kwa ugonjwa huo wa UKIMWI.
Kwamba hata hao wanaondoka tena kwa kasi ya ajabu, huo ni ushahidi tosha kwamba wengi katika jamii hawawezi kuachana na UFUKSA. Sasa je tuwaache waende kaburini kichwa kichwa? Wanaohubiri kwamba KONDOMU inakinga kwa asilimia mia  moja wanakosea, na wanaosema kwamba watu wasitumie kondomu kabisa wanakosea zaidi. Mbaya zaidi ikiwa wanaosema hivyo ni kanisa Katoliki ambalo linajulikana kwa mmomonyoko wa maadili kuanzia makadinali maaskofu mapadri na watawa wa kike.

Siyo siri tena kwamba ufuksa kwenye kanisa hilo ni wa hali ya juu, hasa ule unaohusisha watu wa jinsia moja. Kisa na sababu ni sera ya kanisa ya kutowaruhusu watumishi wa kanisa kuoa na kuolewa. Ikiwa wenyewe  ni MAFUKSA YA KUTUPWA, kuna kosa gani mtu akiwapa mipira kujikinga angaa kidogo? Kwa wale waliowahi kupanda ndege, kila siku ni lazima atokee msaidizi katika ndege hiyo ili kuwaelezea jinsi ya kutumia mpira wa kujiokoa wakati wa ajali. Watu wote husikiliza kwa makini sana maneno yake, japo hakuna ukweli ni kwamba inapotokea ajali ya ndege wengi hufa. Na wale wanaopona mara ngingi huwa hawakusaidiwa na mipira hiyo. Japo kuna wachache ambao imewasaidia. Pointi hapa ni kwamba tusikatae kabisa kondomu. Nakataa kwamba kondomu itachochea ufuksa. Kuna majaketi ya kujikinga na risasi, na sioni watu wakiyanunua ili waende mahali polisi na majambazi wanapofyatuliana risasi.

Kwa kuwa ushahidi wa kutosha upo kuonyesha kwamba watu wameshindwa kuacha ufuksa, tusipinge kila juhudi zinazochukuliwa kuwasaidia wale walioshindwa kujizuia. Ukimuona mtu kapanda kwenye jengo ndefu na anataka kujirusha chini, siyo vibaya kutafuta magodoro mawili matatu ili akifika chini asijipigize sana kwenye lami. Nani ajuae? unaweza kuyaokoa maisha yake hata kwa kujaribu kumdaka kama mpira.Ninachotaka kusema hapa , ni kwamba kila juhudi zifanywe kujikinga na janga hili la ukimwi. Niliwahi kuimba na kusema kama polisi wanawashika wauza bangi, kwa nini wasiwakamate wauza miili wanaoeneza ukimwi? Wengine walisema BOLTI  nne zimefunguka kichwani mwangu. Cha ajabu niko hapa, na hakuna aliyejaribu kukaza hizo BOLTI kama alivyosema Bwana Njiraine. Pengine hawana spana saizi ya bolti hizo. Lakini hata PLAYAS inaweza kujaribu kukaza.

Suala siyo nani aliyeleta UKIMWI. Ila kwa kuwa uko nasi, tusizuie kila juhudi zinazofanywa na kila taasisi au watu binafsi kujaribu kupigana na janga hili ukimwi. Unafiki kama unaoonyeshwa na kanisa katoliki hautosaidia chochote. Wale wanaoweza kuachana kabisa na ufuksa hawawezi kushawishiwa na kondomu kujiingiza tena kwenye ufuksa. Wakifanya hivyo, wajilaumu wenyewe na siyo makampuni yanayotengeneza KONDOMU. Tuelezeni nini kitumike  badala ya kondomu  lakini siyo kukazania mambo ambayo hatuna hakika kama kweli mnayaweza mnayosema. Hata kama tuna hakika mia kwa mia kwamba Moshi na Mdada hawajihusishi na ufuksa, hiyo haitufanyi tuache kuwasaidia wale ambao hawakubahatika kushinda mtihani huo.

Kila la kheri na mjichunge jamani!!! Mambo siyo mazuri. kumeharibika. Hizo ndizo ligha za mitaani siku hizi.

MSINGI MBOVU WA NYERERE TUTAUBOMOA
Suala la wanawake wa Tanzania kuolewa na raia wa nje siyo tatizo. Mradi nia iwe walipendana siyo kisingizio cha kupata uraia. Hiyo itakuwa kazi ya idara ya uhamiaji  kujua.  Natilia maanani kubadilishwa kwa katiba kwani ndiyo itakayowawezesha wananchi kutoa maoni yao jinsi wangependa waongozwe. Porojo za vyama vya kisiasa huwa lengo lake ni kupata kura waingie madarakani. Wakishaingia msishangae wakifanya vinginevyo. Sitaki kuwatapeli wananchi wa Tanzania nitafanya hili na lile. Kazi yangu ni kuwaonyesha makosa ya serikali iliyotangulia ili wakati wa kuibadili katiba waondoe vipengele vilivyowakandamiza.

Mfano msingi aloujenga Nyerere Tanzania lazima tuubomoe. Haufai, na ni makosa kuendelea kujenga juu ya msingi mbovu.

Sina matatizo na watu waliomuogopa Nyerere, au tuseme waliompenda kwani ilikuwa haki yao kufanya hivyo. Kwetu sisi ambao hatukumuogopa, tunajisikia kuonewa kama hatutapewa nafasi ya kujadili yale yaliyotufanya tusimuogope Nyerere , japo wengine wanatuelewa vibaya kwamba hatukumpenda Nyerere.

Hata kama tungempenda Nyerere kuliko wakereketwa wake, isingekuwa sababu ya kutetea hata yale Nyerere mwenyewe aliyokiri kushindwa. Huwezi kumpenda mtu zaidi ya alivyojipenda mwenyewe. Watanzania wengi wanajidanganya kuwa walimpenda Nyerere kiasi cha kuyapenda mpaka yale ambayo Nyerere mwenyewe aliyachukia. Huo siyo upendo tena mnisamehe nikiuita wendawazimu.

Nyerere anaitwa mwanzilishi wa taifa la Tanzania sina utata hapo. Msingi alioujenga na baadaye akakiri kushindwa ndio ninaotaka tuujadili hapa.

Tukitilia maanani kanuni za ujenzi kama anavyotueleza mtaalam wa mambo ya ujenzi.

Katiba ni MENU ya msingi wa nchi. Ndiyo inayosema msingi ulichimbwa kiasi gani na unaweza kubeba ghorofa ngapi kwenda juu.Pia inatueleza kokoto saruji na mchanga zilichanganywa sawa au la. Ukiisoma katiba utajua ni kwa nini nyumba hii tunayojaribu kuijenga ina nyufa kiasi hicho na ni karibu kuanguka.

Ikiwa tumeisoma katiba ituambie kila kitu kiliwekwa sawa halafu tukijaribu kuongeza ghorofa inaporomoka, Kitaalam tunamwita mhandisi wa kwanza atueleze kama kweli msingi ulijengwa sawa na Katiba inavyosema akisema ndivyo tutamuuliza mbona nyumba ina nyufa? Aseme sijui muulizeni mhandisi wa pili maana mimi niliweka msingi na kujaribu kuijenga kwa miaka zaidi ya 30 ikanishinda nikampa Mhandisi wa pili.

Kitaalam hatutachoka ila tutamwita mhandisi wa pili na tumuulize vipi mbona pamoja na "ruksa" nyumba bado ilikuwa na nyufa? Aseme Nilimwambia mhandisi wa kwanza msingi ulichimbwa vibaya kwa hiyo ilitakiwa uende chini mpaka ufikie MWABA. Na kwa sababu msingi uko kwenye jiwe jepesi linaloitwa ujamaa na kujitegemea bila Mwamba ambao ni Mungu ndio maana nyuma haikosi nyufa. Nilimwambia tuvunje nyumba na tuchimbe msingi upya akaninyooshea kifimbo na kuniambia thubutu!!! Mhandisi wa pili aendelee kusema alijitahidi hivyo hivyo kuziba nyufa na kuendelea kujenga lakini aliruhusu vijengo vingi vya chini ili kuepusha kuporomoka kama angeendelea kujenga kama mhandisi wa kwanza alivyotaka ajenge. Amalize kwa kusema jitihada zake za kujaribu kurekebisha hazikumaliza nyufa, na kwa sababu ya kujaribu kutumia akili yake ili kuiokoa nyumba isiporomoke walitofautiana na huyo mhandisi wa Kwanza aliyemwambia kuwa ameigeuza ikulu yka kuwa mahala pa biashara. na isitoshe anaongozwa na mwanamke. Kwa hasira huyu mhandisi wa pili alimjibu kuwa huwezi kunitukana matusi ya nguoni. Nyumba uliiharibu wewe na ulisema wazi kwamba ulikosea, ukaniita niirekebishe, na tayari nimekuambia inataka nini ili irekebike, na wewe hutaki niirekebishe bila ruksa yako. sasa mawili chukua nyumba yako uendelee kuijenga mwenyewe.


Kama Nyerere alikosea, tukisema inawauma nini? Makosa ya mtu ni makosa hata kama mwenyewe alikufa. Kwamba sasa hayuko duniani ndio wakati mzuri wa kujiuliza kwa nini alikuwepo, na dunia ilipata faida gani kuwa naye. Na sasa hatunaye, dunia ina pengo gani kumkosa ? Tamzania na dunia nzima haina pengo kumkosa Nyerere bali inapumua kwamba mwiba mguuni umetutoka. Nyerere hakuwa na haya kuutetea uongo ufanane na kweli. Nje kwenye vyombo vya habari alijionyesha kama mpenda haki na mpigania uhuru, lakini kwa ndani alikuwa akifanya kinyume chake. Huwezi kuwa mpigania haki wakati unawanjima watanzania haki ya kuyatoa mawazo yao. Ndivyo alivyofanya Nyerere, na kuna watu wanauita huo ni uzalendo. Kwao uzalendo ni kuwaweka watu kizuizini na kutunga sheria ya kuwashitaki wakati wako kizuizini.

Je nimsifu Nyerere? Ndiyo nitamsifu. Alikuwa KIONGOZI. Sifa ya kuwa kiongozi siyo lazima iambatane na MZURI. Katika hili Nyerere alikuwa KIONGOZI MBAYA. Ubaya wa Kiongozi siyo lazima uwe kwenye sura na maumbile, japo wako wengine wa hivyo. Sera za Nyerere za ujamaa na kujitegemea ndizo zilizokuwa mbaya. Akaambiwa sera ni mbovu, naye akautumia uongozi wake na sura na maumbile yake ya kuvutia kuzitetea sera zake mbovu mpaka zikaiharibu Tanzania. Kwamba aliweza kuzitetea sera zake mbovu kwa mbinu na hila zote hizo ndizo sifa zinazomstahili. Binafsi sioni sifa nyingine ya Nyerere.

Mbinu mbaya ambayo inanifanya nitamani kwamba mifupa yake ipelekwe gerezani, ni hii ya kuhakikisha kwamba Tanzania inabaki bila KIONGOZI kwa miaka mingi baada yake.Alitengeneza wale aliowaona wanafaa kuiongoza Tanzania baada yake na akahakikisha siyo viongozi. Kiongozi ni yule anayeweza kutengeneza njia mpya, na ikakosa mahali pa kutokea, na akarudi akatengeneza nyingine. Kifupi ni kwamba kiongozi ni yule anyedhubutu kuanzisha kitu kipya. Tanzania tulikuwa na Nyerere akaanzisha kitu ambacho hakikuwa kipya sana, ila alikipaka rangi kionekane kama ni chake. Kilipokwama hakuwa na ujasiri wa kuanza kingine mapema, bali alipoteza muda wa WATANZANIA kuyatetea mawazo mabovu. Alipomwachia Mwinyi, hakumwacha naye aanzishe kitu kipya kama kiongozi, bali alimtaka afuate nyayo zake ambazo zilikuwa zikielekea porini bila matarajio ya kuyafikia malengo. Mwinyi alipojaribu kufuta nyayo na kuandika zake, Nyerere alimkemea hadharani kana kwamba siyo yeye aliyemweka madarakani. Sasa tuna Mkapa aliyewekwa na huyo huyo Nyerere, lakini kwenye ramani ya dunia ni kama TANZANIA haiko. Nchi ikikosa kiongozi huwa haisikiki kwa shari wala kwa kheri. Tanzania kwa sasa haina kiongozi, na ikiwa wananchi hawatafanya mageuzi ya kweli, tutabaki bila kiongozi na sijui ni kwa muda gani.

Mkapa siyo kiongozi kwani kwa miaka kumi hajaanzisha kitu Tanzania kilichoshindwa wala kufanikiwa. Yuko tu. Hajulikani yuko upande upi. Tunajua kwamba yeye ni mkomunisti kama aliyemuweka madarakani, lakini hataki kujionyesha wazi kulingana na wakati huu wa soko huria.  Kutokana na hali ya nchi yetu kukosa kiongozi, pia inakosa sera. Watanzania hawawezi kuonyesha kwamba hii ndiyo sera yetu kama nchi. Yaani tuko tuko tu.

Wakati umefika kwa Watanzania wenyewe kujichagulia KIONGOZI wa kuwaongoza na siyo mtawala wa kuwatawala. Wafanye hivyo haraka kabla nchi yetu haijafutwa katika ramani ya dunia. Ni jambo gumu linalohitaji baraka za MAULANA RABUKA kuliwezesha. Watanzania wote ni waumini wa dini mbali mbali jambo litakalopelekea zoezi zima kuwa rahisi kuliko tulivyotegemea. Kila mmoja katika madhehebu ya dini yake amwombe Mungu atupe kiongozi atakayetuongoza kuyafikia maendeleo hapa duniani, na baadaye tuingie kwenye ufalme wake wa milele mbinguni.

TATIZO LA TANZANIA NI CCM

Matatizo ya Tanzania ni CCM. Miaka arobaini madarakani, wameharibu kila kitu. Utalaumu nini Tanzania ukose mkono wa CCM?

Kichwa kuuma, husababishwa na mengi. Utakosea sana kununua "HEADACHE" kutuliza maumivu ya kichwa, kumbe macho ndiyo sababu kichwa kuuma. Bila kutibu macho, utajisumbua bure lakini kichwa bado kitaendelea kuuma, na kinaweza kusababisha viungo vingine mwilini kuuma.

CCM ndio chanzo cha matatizo yetu Tanzania. Hakuna marekebisho bila CCM kutoka madarakani. Utaanzia wapi?

Ni kweli kwamba CCM ni chama tu, na watu ndani ya chama hicho ndio waliotunga sera mbovu  zilizoipelekea Tanzania kuwa ilivyo. Sambamba na hilo, ndiyo maana tunataka KATIBA ibadilishwe ili  Munishi niingie madarakani  bila chama.

Ni katiba mpya ndiyo itakayotengeneza mazingara mazuri  ya watanzania kuongozwa kujiongoza. Na mtu tayari kufanya yote hayo ni mimi Munishi. Kama kuna wengine siyo kazi yangu kuwatafuta, wajitokeze hapa kwenye ukumbi huu wamwage siasa zao hapa. Mimi siyo mwanasiasa na sitarajii kuwa mmoja. CCM wakitoka madarakani baada ya katiba waliyoiharibu kurekebishwa na kuwa katiba ya wananchi iliyo na mawazo ya wananchi kwa ajili ya wananchi, kila kitu kitakuwa shwari. Uchumi wetu unaweza usiwe kama wa Marekani kwa mwaka mmoja, Lakini utakuwa ukielekea huko. CCM Kiini cha matatizo Tanzania kitakuwa kimetoka.

Huitaji kuwa msomi wa chuo kikuu kujua kwamba CCM ndio chanzo cha kila tatizo Tanzania. Lakini kama wewe ni msomi na hujagundua kwamba CCM ndio chimbuko la matatizo Tanzania, nakupa pole. Nchi masikini duniani haziongozwi na CCM, lakini Tanzania ilitokea kutawaliwa na CCM kwa zaidi ya miaka 40 na watanzania wana kila sababu ya kutaka CCM itoke kwenye maisha yao. Je itamaliza matatizo yao? Ndiyo. Wengine watafaidi matunda ya ukombozi, na kuna wale dhaifu ambao hawataishi kuonja matunda ya ukombozi. Lakini haitukatishi tamaa ya kujikomboa.

Gari ambayo mitambo yake ya kujaza betri moto ni mibovu, inahitaji mitambo mingine na siyo betri mpya. Ukikosea uweke betri mpya na yenyewe itamalizwa nguvu kwani mitambo ya kuijaza nguvu imekufa. Tanzania iliwekwa betri mpya yaani Mwinyi na MKAPA, na zote zimenyonywa  moto zikawa hazifai.
Ndiyo maana Tanzania inahitaji mitambo mipya  inayozalisha sheria na utengamano. Hii ni KATIBA MPYA itakayoketa uongozi mpya, utakaoleta ENZI MPYA, itakayoleta maisha mapya, yatakayoleta maendeleo, yatakayorekebisha hali ya uchumi wetu, utakaosababisha kila kitu kurekebika na kuwa jinsi ambavyo hakikuwa wakati wa CCM. Hata makovu ya Munishi usoni msishangae kuona yamerekebishiwa Muhimbili na siyo Uswiss kama anavyofanya MKAPA. Mmewahi kujiuliza kwamba MKAPA anatumia milioni ngapi kwa siku huko anakotibiwa? Msiombe kujua maana machozi yatawatoka.

TANZANIA ILIANZA VIBAYA INAELEKEA PABAYA


Tanzania ilianza vibaya ndiyo maana inaelekea pabaya. Kuanzia wakoloni na Nyerere waliotutawala, Wote waliifanya Tanzania kuanza vibaya. Lazima tuanze upya vizuri, ili tuelekee pazuri. Watanzania tumechoshwa  na sera za kwenye vitabu, lakini kwenye maisha yetu hazitekelezeki. Tumepotezewa muda mrefu ambao tungeutumia vizuri leo hii hali yetu kimaisha ingekuwa tofauti na ilivyo sasa.

Lakini yote hayajapotea kwani tuna muda wa kuanza upya. Hatutakuwa na muda wa kupoteza kwani tayari tumepitwa na wakati. Tutaanzia tutakapoikuta nchi yetu na tuendelee mbele. Muhimu hatutarudia makosa ya zamani. Tutarekebisha yanayoweza kurekebishwa haraka ili angalau tupumue hewa yenye mabadiliko.

Tutaanza na kodi. Wananchi watapunguziwa mzigo wa  kodi, na  tutabadili mfumo wa kuikusanya. Tofauti na ilivyo sasa kodi kidogo sana itatozwa katika bidhaa muhimu, na nyingine hazitatozwa kodi kabisa. Badala ya kuwafanya wananchi wa kawaida masikini kwa kuwatoza kodi nyingi, tutaruhusu watu watoe michango ya hiari kusaidia taasisi za umma. Serikali na wananchi pamoja tutalijenga taifa letu kwa moyo wa kizalendo.

Kupigana na RUSHWA tutaimarisha taasisi za sheria nchini kwa kuinua kiwango cha mishahara kwa watumishi katika taasisi zote za kisheria. Polisi hali yao ya maisha itainuliwa na nyumba wanazoishi kufanyiwa ukarabati na mpya kujengwa haraka kukithi mahitaji yao ya nyumba. Suala la familia mbili au tatu kushiriki chumba kimoja litakuwa historia katika kikosi cha polisi.

Majeshi yetu yatarekebishwa kutoka yale yanayongojea vita mpaka kuwa mahali pa kufikiri na kugundua vitu kwa ajili ya ujenzi wa Taifa. Pia mishahara yao itarekebishwa ili ikithi mahitaji yao ya kila siku. Majaji nao wataongezewa mishahara ili iwe vigumu wao kupokea rushwa na kupindisha ukweli mahakamani. Tunajua hakuna kiasi cha pesa kinachotosha mwanadamu akose vishawishi, lakini kwa kiasi kikubwa tutapunguza rushwa katika taasisi zetu za kisheria.

Mipango yetu itakuwa ya kudumu na hakutakuwepo na  oparesheni za kushitukiza ambazo ni sawa na kuhamisha rushwa kutoka taasisi moja kwenda nyingine. Pia wote watahesabiwa ni wananchi wa Tanzania bila kujali walihusika vipi katika serikali ya CCM iliyokuwepo madarakani. Kifupi hatutapoteza muda kwa yaliyopita bali tutakaza mwendo kwa yaliyo mbele yetu.

Tunajua kuna watu wenye majumba makubwa waliyojenga kwa pesa za rushwa walipokuwa madarakani, Lakini serikali yetu haitawabomolea watu hao majumba kwa kisingizio kwamba zilijengwa kwenye sehemu za barabara, Badala yake tutawaonyesha jinsi mtu anavyoweza kuwa tajiri kihalali bila rushwa au kuwathulumu wengine. Kwao hilo litakuwa somo kubwa maishani kujifunza. Kwa hiyo badala ya kuanza kukimbiza pesa zao nje wakidhani serikali yetu itawanyanganya kama walivyonyanganya, Watulize roho.

Pesa ni za watanzania. Wakizitumia Tanzania ni bora zaidi kuliko wakizipeleka nje ya Tanzania. Hapo washike neno langu. Mimi siyo mtu wa kuyatafuna niliyokwisha sema.



Kuhusu ELIMU tayari watanzania mlizoea elimu ya bure ambayo ilizalisha wasomi duni. Serikali yetu itaruhusu ushindani katika sekta ya elimu ili ubora wa elimu udumishwe. Taasisi za kidini na zile za watu binafsi zitaruhusiwa kuendesha mashule lakini kwa utaratibu urtakaowekwa na serikali yetu. Moyo wa kujitolea kutoka kwa wananchi pamoja na serikali, utahakikisha kwamba hakuna mwanafunzi wa Tanzania anayekosa elimu kwa sababu tu wazazi ni masikini hawawezi kulipa gharama za shule. Huo utaitwa moyo wa ENZI MPYA.

MATIBABU nayo yatakuwa sawa na elimu. Lakini kila juhudi zitafanywa kuhakikisha hakuna anayefukuzwa kwenye hospitali kwa kisingizio cha kukosa malpo ya hospitali. Serikali itakuwa bega kwa bega na taasisi za kibinafsi pamoja na zile za kidini. kuwahudumia wananchi wa Tanzania kiafya na kielimu. Mahospitali yaliyoko yataimarishwa na mengine mapya kujengwa. Pia vifaa vya kiafya vitaboreshwa kuyafanya mahospitali yetu yaweze kuwahudumia watu wa aina zote.

Hali ilivyo sasa mahospitali yetu yameachwa kiholela kwani wakubwa hutibiwa hata mafua nje ya nchi. Mamilioni yanayotumika kuwatibu viongozi nje ya nchi yanaweza kabisa kutumika kuyaboresha mahospitali yetu , Na hata kujenga mengine mapya.

Kwa mfano matibabu ya Mheshimiwa Mkapa hivi karibuni, Yameligharimu Taifa mamilioni ya shilingi kama siyo mabilioni. Hawatasema gharama halisi kuogopa aibu, Lakini watafiti wanasema ni kitita cha pesa.

Ajabu ni kwamba aliyofanyiwa huko, yangewezekana kabisa kufanyika nchini pamoja na hali duni za hospitali zetu. Mimi siyo muuguzi, lakini najua upasuaji unahitaji dawa ya kumfanya mtu alale ili kisu kiingie bila mgonjwa kusikia. Je dawa hiyo hapa nchini hakuna? Na kisu je, hata hicho hatuna?

Wengine wanasema Mkapa ni BONGE LA JITU Tena mtumiaji mzuri wa vileo kwa hiyo pengine dawa zetu za kumfanya alale zisingefua dafu. Sawa. Kama tunaweza kumfanya Tembo mzima alale na ahamishwe kutoka Ziwa Manyara hadi Ngorongoro, Je hata hiyo Mkapa angewekewa dozi moja asingelala?

Wengine wanasema hatuna madaktari bingwa wa kuweza kumhudumia RAIS. Mbona basi aliandamana nao huko alikotibiwa? Au walienda kufanya nini? Kuwatizama mabingwa wenzao wa nchi za nje  wakimhudumia rais wao? Kuna malalamiko kutoka baadhi ya madaktari bingwa nchini kwamba viongozi wanawapuuza wakati wana elimu sawa na ya wenzao wa nchi za nje.

Wanadai kwamba elimu ya udaktari haina njia fupi kwa daktari wa Amerika na yule wa Tanzania. Wote inabidi wapitie mafunzo mamoja na kuhitimu kumoja. Tatizo ni kwamba wenzetu wana nyenzo za kisasa wakati Tanzania tunatumia nyenzo za kizamani.

Lakini pia wanaliona hilo siyo tatizo kubwa kushindwa kulishughulikia tatizo kama la Mheshimiwa Mkapa nchini. Japo hawakutaka kutajwa, walijigamba kwamba wakati wa ajali ya TRENI Dodoma, walihusika katika kuwahudumia majeruhi waliokuwa katika hali mbaya mara kumi ya Mkapa na wakapona kabisa.

Hawaoni sababu yeyote ya Rais kutumia pesa za walipa kodi nyingi kiasi hicho kufanyiwa kile ambacho wenyewe wangeweza kukifanyia hapa nchini kwa gharama ndogo. Kuongezea uzito hoja yao wanasema, mbali na vyombo vya kisasa, dawa za kutuliza maumivu ni zile zile walizo nazo hapa nchini. Hata zile za kuzuia INFECTION nazo hazina tofauti na zile walizo nazo Tanzania.

Tofauti ni kwamba kwa sababu Mkapa ameziacha dawa hizo Tanzania, Amekwenda kulipa mamilioni kununua kile ambacho angeweza kukipata kiurahisi Tanzania.

Mwisho walimalizia kwa kusema kwamba haijalishi ni dawa gani utakazotumia. Kama nguvu ya mwili kupambana na madadhi imekufa, madaktari wanaweza kufanya sufuri kumfanya mgojwa apone.

Walisisitiza kwamba dawa husaidiana na mwili kupambana na maradhi. Walidokeza kwamba watu wengi wanakufa kwa magojwa yanayotibika kwa sababu uwezo wa kupambana  na maradhi mwilini umekufa. Walitumia lugha ya kitaalamu na kusema Upungufu wa Kinga Mwilini {UKIMWI} unawamaliza wengi japo dawa na mashine za kisasa wanazo.

Walionya kwamba viongozi wetu wanatakiwa waige mfano wa Rais wa Kwanza Kenya Mzee Jomo Kenyatta ambaye asliwaamini madaktari wa nchi yake na hakwenda ngambo kutibiwa. Alikufa usingizini Mombasa alipokuwa amekwenda kusheherekea sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya. Alikufa kishujaa nchini mwake chini ya uangalizai wa madaktari wazalendo wa Kenya.

Tanzania inawadhalilisha madaktari wake na kuonekana duni mbele ya wenzao wa ULAYA, lakini bado viongozi wetu wanakufa wakiwa mikononi mwa mabingwa hao. Walitoa mfano wa Nyerere kama kiongozi wa Tanzania aliyewahikufa mikononi mwa madaktari bingwa wa nchi za nje. Wanadai kwamba hata kama wanatoa mawazo wakati mgonjwa yuko nje ya nchi, Mawazo yao hayasikilizwa, jambo linaloleta lawama baadaye kwamba kama wangesikilizwa pengine Nyerere angekuwa hai leo.

Mambo hayatakuwa hivyo katika serikali ya ENZI MPYA. Tutaheshimu madakrari wetu, na watapewa kila motisha kuyaokoa maisha ya watanzania na viongozi wake wa ngazi zote. Hakuna sababu ya kutumia pesa za walipa kodi kuwaelimisha madaktari ambao kazi zao hazithaminiwi na viongozi.

Ndio maana wengi wa madaktari kutoka Tanzania wamehamia huko wanakokimbilia viongozi kwa matibabu. Inaelekea siku moja watakutana nao huko kama madaktari bingwa kumbe ni wale wale kutoka Tanzania na elimu ile ile waliyoidharau viongozi wetu.

Kuna wengine wanaohoji kwamba viongozi ni watu muhimu katika taifa na ni lazima kila hatua zichukuliwe kuchunguza afya zao.  Hatuipingi hoja hiyo, ila tunasema yote hayo yafanyike Tanzania..

 Wanataaluma hiyo wapo. Kwa nini viongozi waharibu pesa tunazozihitaji zaidi kwa yale yanayowezekana hapa? Kama ni ajali na iwe kiongozi kapoteza sehemu ya ubongo, halafu wajaribu kurudisha waliouokoteza chini zoezi hilo liwashinde, Hapo itaeleweka watakapotumia ndege yeyote hata kama ni ya jeshi kumkimbiza kiongozi husika kunakoweza kupatikana msaada wa haraka.

Lakini suala la Mkapa ni tofauti kabisa. Hata kama angehitaji vipimo vya mifupa vifanyiwe nje ya nchi, ilikuwa rahisi.Upasuaji ungefanyiwa Tanzania, na sehemu ya mfupa ipelekwe nje ya nchi kwa ucvhunguzi zaidi na majibu yangekuja mapema. Bado Rais angekuwa Nyumbani, angekunywa uji wa mbege kusaidia kujenga mifupa, na watu wangemuona kirahisi MUHIMBILI au IKULU kumtakia dua apone haraka.

Yale aliyokataa kuyafanya ndiyo anayoyafanya sasa. Bado inasemekana hajapona kabisa, na dawa bado anatumia tena kwa wingi. Nitashangaa zaidi nikisikia kwamba bado dawa anaagiza ngambo wakati zipo hapa TZ.

MKAPA NA MUNISHI WAPATANISHWE

Malumbano yanayoendelea kati ya Mchungaji Munishi na Mheshimiwa Rais Mkapa siyo mazuri kwa nchi yetu. Afrika tunajua kuitisha mikutano ya upatanishao wakati damu nyingi sana imeshamwagika. Hatuna hekima ya kuzuia kabla ya madhara makubwa kufanyika. Mizozo yote huanza na malumbano kama haya mnayoyaona hapa. Kila upande ukidai kunyimwa haki na upande wa pili. Tusipoziba ufa hapa tutajenga ukuta. Malumbano yakizidi na yakomae kabisa, huzaa magomvi ambayo nayo huzaa vita.

Hakuna vita inayoanza kama vita.  Huanza kama maneno ya chokochoko kama hizi mnazozisikia hapa. yasipozimwa au kupatanishwa huzaa vita. Ni muhimu sana kuwapatanisha Mheshimiwa Mkapa na Mchungaji Munishi. Nionavyo mimi Munishi hana historia ya kulumbana na serikali. Malumbano yalianza pale serikali ilipoipiga marufuku kanda toleo la saba ya mchungaji Munishi. Sababu hasa zilikuwa kisiasa kuliko vinginevyo. Sijui serikali walisikia nini kwenye kanda hiyo na kuamua kuipiga STOP, Lakini mimi sioni chochote ndani ya kanda hiyo ambacho kingeifanya serikali kuhamaki kama ilivyohamaki.

Baada ya kukurupushani za kuweka watu ndani na habari za kutafutwa Munishi kusambaa, ndipo Munishi alipotoa taarifa kwa vyombo vya habari kwamba maisha yake yalikuwa hatarini kufuatia zoezi la serikali kuzikamata kanda zake. Sina data zaidi ya hapo, lakini nafikiri kuwa malumbano yalianzia hapo. Kama sikosei pia ndio sababu kubwa ya Munishi kuanzisha Web Site yake ambayo wengi tunaiona kama mahali pa kutolea malalamiko yake kuhusu hatua ya serikali. Anahisi kaonewa.

Serikali nayo kwa upande wake imeendeleza ukimya ambao siyo wa kawaida. Ni kama wanadharau. Kama kanda tulizuia na watu tukawaweka ndani, SO WHAT? Mtaifanya nini serikali yenye ridhaa ya wachache ambayo siyo butu? Kwangu msimamo huo hauisaidii serikali. Unathibitisha jinsi ambavyo viongozi wa Tanzania wanavyodhamini ubabe wa vyombo vya dola.Wanaweza kumfanyia mwananchi chochote na wasipelekwe popote. Hata kama simba aliumbwa ale nyama ya swala, lakini swala hawajui hilo. Ndio maana kila inapobidi, swala hutimua mbio. Vinginevyo kizazi cha swala mwituni kingekuwa kimemalizika. Kwamba swala bado wapo mwituni pamoja na wingi wa simba, hiyo inaonyesha serikali haina nguvu inazofikiri kuwa nazo.

Nashauri kwamba Munishi na Mkapa wakae pamoja kutatua tatizo ambalo linakua kila kukicha. Ubabe hautasaidia katika hili. Msisahau kwamba nchi za magharibi huifurahia mizozo ndani ya Afrika. Huitumia kama soko lao la kuuzia silaha. Ninachosema hapa ni kwamba ni rahisi sana kwa nchi za magharibi kutoa misaada ya silaha kwa yeyote anayeonekana mpinzani wa serikali. Siyo ajabu wakatumia mzozo huo kumpa mpinzani silaha bure, huku wakiidanganya serikali inunue silaha kwao kupambana na mpinzani. Mwisho wa kila kitu mnauana wenyewe, na silaha mnazilipa kwa njia moja ama ile nyingine. Tuyatatue matatizo yetu wenyewe. Tena kabla hayajatuletea madhara. Hii ni tathmini yangu mwenyewe kuhusu malumbano kati ya Munishi na Mkapa.

DINI ISIWE KIGEZO MNINYIME KURA

Dini yangu isiwe kikwazo mninyime kura. Badala yake iwe kivutio michague kwa wingi. Watu wa dini zote mpeni nafasi Mungu aingilie kati uongozi wa nchi yetu. Mungu aliwekwa kando tangu mwanzo Tanzania. Kilichoongoza ni mawazo potovu ya Nyerere yaliyotaka kuchukua nafasi ya Mungu. Yalishindwa vibaya kwani mwanadamu hawezi kushindana na Mungu. Hata leo Tanzania mtajidanganya ikiwa mtairudisha siasa madarakani. Mambo yatakuwa mabaya kuliko awali. Kwani mmeonyeshwa njia na makusudi mkaikataa. Ni matumaini yangu kwamba watanzania wataitikia wito wa kumchagua Munishi kama rais wa kwanza kuchaguliwa bila kuwa mwanachama wa chama cha kisiasa.

Dini yeyote ikitumiwa kuongoza nchi mafanikio huwa mengi. Watakaoyapinga ni waumini wa dini nyingine. Na watafanya hivyo kwa kutokuijua dini yao sawasawa. Mwinyi alikuwa mkweli kwa imani ya dini yake.Wakati wa uongozi wake misikiti mingi ilijengwa, mashule mengi ya kiislamu yalianzishwa, na wakristo wasioijua dini yao waliliona hilo kama tishio kubwa kwao.

Mafundisho kamili ya dini ya kiislamu ni kutenda haki kwa kila mtu, kutokunywa pombe, na mengine mengi. Ikiwa mtu wa dini nyingine atawafundisha watu kutenda hayo, mimi nitafurahi kwamba yale niliyotaka kuwafundisha watu, sasa yanafundishwa. Sitojali anayeyafundisha kama ni mtu wa dini yangu. Wakati wa Mwinyi watu walikuwa wacha Mungu sana. Uongozi wake uliegemea sana mafundisho ya dini aliyoiamini, jambo lililonifanya nami kuongeza bidii katika kumcha Mungu kutumia dini niliyoiamini. Na karibu kila dini iliyouona uislamu kama tishio wakati wa Mwinyi ilifanya hivyo. Hali hiyo ilipelekea Tanzania kama taifa kumcha Mungu kwa mioyo yao yote. Nini kingezuia baraka za Mungu kumiminika Tanzania? Zikamiminika baraka mpaka watanzania wakashindwa kuyaamini macho yao.

Sasa tuna Mkapa Mkristo  kwa jina kama alivyokuwa Nyerere. Anaiongoza nchi siyo kutumia misingi ya dini yake, bali porojo za siasa. Kwenye siasa uongo na ujanja ujanja ndivyo vinavyotawala. Nini kitawazuia watanzania nao kuwa waongo na wajanja wajanja? Wanayaona kwa viongozi nao wanafanya yayo hayo. Ndiyo maana rushwa, wizi, magendo vimeshamiri na vilishamiri wakati wa Nyerere na Mkapa. Sisemi wakati wa Mwinyi hakukuwepo na hayo, lakini si kwa kiwango hiki. Baba mlevi na mvutaji wa sigara hawezi kuwa na sababu za kutosha kumwelezea mtoto wake asilewe wala kuvuta sigara. Haijalishi sheria kali atakazojaribu kuweka, zitavunjwa zote. Makapa anaweka sheria kali kuwazuia watu wasifanye maovu ambayo yeye na serikali yake wanayafanya. Nani mjinga atii sheria hizo? Ndio maana utaona kwamba maovu badala ya kupungua yanaongezeka.


Imani ya Mungu ni suala la mtu binafsi na Mungu, lakini mtu huyo akiwa kiongozi haimuondolei haki yake ya kumwabudu Mungu kama dini yake inavyomfundisha. Hata akiwafundisha watu yale anayoyaamini kwa dhati kutoka moyoni mwake hafanyi kosa. Tatizo hutokea wakati kiongozi anapojaribu kuwabudu Mungu kwa kutumia imani ya dini zote. Hawezi , na haiwezekani ndio maana wengi huamua kusahau imanizao za kidini na kuitumia siasa pekee kuongoza. Kwa sababu siasa ni uongo, inashindwa kabisa kumaliza maovu nchini. Matokeo yake nchi inaongozwa kwa mbinu za nani kamzidi nani kwa kiwango gani cha uongo.

Ndiyo dini haiwezi kabisa kumaliza maovu yote, wala haitakiwi ifanye hivyo. Inachotakiwa kufanya ni kuwafundisha watu wawe waaminifu katika imani zao, na wawafundishe wengine kuyashika yale wanayoyaamini kwa hiari yao wenyewe. Kifupi tunataka nchi iwe na ushindani wa kumcha Mungu bila kulazimishana kufanya hivyo. Baraka amani, utulivu uponyaji, na  miujiza Mungu atakayoitenda maishani mwa mtu, ndiyo itakayokuwa changamoto ya kumfanya kila mtu awe na bidii ya kumcha Mungu kwa moyo wake wote.

Nchi inapokuwa na wacha Mungu wa kweli, ndipo kiwango cha maovu kinapoweza kupungua kama siyo kwisha kabisa. Lakini lazima ianzie kwa viongozi na hasa rais. Kiongozi akiwa mcha Mungu na siyo mnafiki, ni rahisi kuiambukiza nchi nzima. Siko hapa kuhukumu nani mcha Mungu na nani siyo, lakini nijuavyo mimi ni kwamba kila mcha Mungu atafanya kila linalowezekana kuwaelezea wengine yale anayofaidika nayo akiwa mcha Mungu. Ndiyo maana sioni makosa ya mwinyi kufanya mengi kuwasaidia waislamu wakati wa uongozi wake. Alifanya kama binadamu yeyote na hakuficha kama Nyerere alivyofanya kwa kanisa katoliki lakini kwa siri. Hiyo ni kuonyesha kwamba hakuwa na hakika na imani aliyoiamini ndiyo maana hakuthubutu kujionyesha hadharani kwamba ana upendeleo wa kidini. Pia hata hao aliowasaidioa hawakuweza kuitumia nafasi hiyo kumcha Mun\gu kwa dhati bali waliitumia nafasi hiyo kupata mali na viwanja vingi pamoja na waumini wengi ambao hawana msimamo na imani yao.

Waislamu na wakristo ni dini ambazo haziwezi kufutika katika uso wa dunia. Ni makosa na tena kupoteza muda kujaribu kutafuta misaada ya kuifuta dini nyingine duniani. Ni sawa na kujilisha upepo. Muhimu ni kila dini kuamka kutafuta nafasi ya kuongoza nchi. Wanasiasa wameharibu nchi kwani wao hupenda kuabudu vitu kuliko Mungu. Mimi ni mkristo, na sioni haya kusema kwamba nchi nyingi zinazodai kuwa ni za kikristo ndizo zinazoongoza katika maovu ya kila namna.Kosa lao ni moja tu. Kutokuruhusu viongozi waongoze sawa na imani zao kwa Mungu.

Kiongozi anapomcha Mungu na kutumia uchaji wake Mungu kuongoza, Mungu huongoza kupitia yeye. Na Mungu akiliongoza Taifa, nini kitakachomshinda? Kwa sababu wale wanaotuongoza siyo wachaji Mungu, mnajua wazi wanamcha nani. Vitu siasa, na shetani mwenyewe ambaye ndiye baba wa uongo wote. Mkiacha shetani aongoze nchi, kwa nini mnashangaa maovu wizi, rushwa na matambiko mengi ya kumwaga damu nchini? Hayo ndiyo matunda ya kazi za shetani. Tuungane dini zote kumwondoa shetani madarakani. Tanzania anatawala akitumia jina la CCM, lakini ni shetani mwenyewe.

Mapenzi ya Mungu yatendeke

Munishi sijawahi kuwa Jambazi. Tena Munishi nina elimu ya kutosha. Kwamba kuna watu wanaongangania kigezo cha elimu na ujambazi ambao hawana ushahidi, hiyo inaonyesha jinsi ambavyo CCM wako tayari kubaki madarakani kwa gharama zozote. Maisha yangu yako wazi kwa umma tangu mwaka 1980 nilipoanza kumtumikia Mungu kwa njia ya nyimbo. Umri wangu wakati huo ulikuwa miaka ishirini.

Wanaodai kwamba nilikuwa jambazi, waseme nilifungiwa katika magereza ipi Tanzania. Ama waonyeshe alama zangu za vidole kutoka makao makuu ya CID. Sijawahi kwenda jela, sijawahi chukuliwa alama za vidole kama ilivyo kawaida ya majambazi sugu. Sasa sijui huo wizi Tanzania niliufanya wakati gani. Wacheni kunizulia mambo yasiyo na msingi. Kama hamnitaki niwe rais semeni na mtoe sababu nyingine. Hii ya wizi na kukosa masomo naona kama itawageuka na kuwapiga wenyewe kwani ni uongo mtupu.

Niliwahi kukiri kwamba elimu ya kukaa darasani ni ya darasa la saba. Elimu ya kujiendeleza mwenyewe ni nyingi kiasi kwamba sijui kipimo chake. Katika hilo wanaoonekana kutoelimika ni wale wanaojaribu kunishambulia kwa hilo. Elimu haina mwisho, bali ina mwanzo. Mimi nimetaja mwanzo wa elimu yangu, wengine wakapata mtaji wa kujengea hoja. Sasa kila wanapojaribu kunipinga wanajenga hoja kwenye elimu na ujambazi. Haya hiyo wananchi wameisikia, na bado wako tayari kunipa kura niingie ikulu. Hakuna sababu nyingine? Kama hakuna basi thibitisheni kwamba sina elimu kivipi. Na tena mthibitishe kwamba mimi ni jambazi niliiba wapi, na nilimwibia nani, na hukumu ilikuwa miaka mingapi jela, nambari ya kesi ilikuwa ngapi, Kituo gani cha polisi kilipeleleza wizi huo, mwisho onyesheni picha yangu kutoka CID nikiwa nimebeba bango la kuonyesha mimi ni jambazi, pamoja na alama za vidole.

Naheshimu uhuru wa watu kutoa maoni yao hapa, lakini uhuru huo usitumike kuniharibia jina kwa tuhuma za uongo. Nisemayo hapa ni kweli Tena ninamaanisha na ndiyo maana nimeamua kutumia jina kamili. Pamoja na kwamba siwajui majina yenu, na sitaki kuyajua, Nawaomba msiniharibie jina kwa tuhuma za uongo. Pinga hoja yangu kwa hoja. Ikikushinda nyamaza kuliko kuanza kuniharibia jina. Kuwa rais ni maji ambayo tayari mwenzenu nimeshayavulia nguo. Lazima niyaoge. Pengine iko siku nanyi mtataka kugombea kiti ninachogombea. Ikiwa mnataka watu wawazushie mambo mengi ya uongo basi msinizushie na mimi. Naomba nieleweke hapa. Siyo kwamba sitaki kupingwa. Pingeni mkiwa na sababu za kweli kufanya hivyo.

Nasikika kama ninaeomba. Hapana. Mara nyingine mwanadamu unaweza kukosa maneno ya kujitetea wakati unajua wazi tuhuma dhidi yako ni uzushi na uongo mtupu. Mwenzenu nimefika hapo.Je nikae kando kama anavyoshauri mwendawazimu fulani hapa? Hapana. Bado niko Imara. Mengine Mungu atashughulika nayo. Mimi nitajitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu kuwaeleza watanzania kwa nini CCM haitufai, na mimi ndiye Mkombozi Mungu aliyenituma kuikomboa Tanzania kutoka katika makucha ya CCM. Kama alivyosema Yesu, "IKIWEZEKANA KIKOMBE HIKI KINIEPUKE, LAKINI SIYO KAMA NIPENDAVYO MIMI, BALI MAPENZI YAKO YATENDEKE."
Katika hili la kuikomboa Tanzania nisingependa watu kuniita mwizi wakati sivyo, lakini kwa sababu ni lazima nikinywee kikombe hiki cha mateso, basi nami nasema mapenzi ya Mungu yatendeke.

CCM NDIYO KIINI CHA MATATIZO YETU TANZANIA

Machozi yananitoka nikiyakumbuka mateso ya CCM Tanzania. Wananchi tulifanywa watumwa wa CCM katika nchi yetu. Michango ya lazima ilikuwa ni kawaida. Walisema wanataka pesa za chama. Ukisema wewe siyo mwanachama wanasema watanzania wote ni CCM wapende wasipende.  

Viongozi wa CCM walionekana kama miungu wadogo. Nasema hata sasa wanaonekana hivyo. Dola ndiyo iliyoogopewa Tanzania. Polisi na viongozi wa CCM waliogopewa kuliko moto wa Jehanum. Wenyewe walihesabiwa kuwa JEHANAMU Tanzania. Wangeweza kumkamata wamtakaye, wakamtesa wakamfungulia kesi bandia, wakamfunga jela. Hata kutokuwa na kazi ilikuwa ni kosa la jinai.

Kazi waliziharibu wenyewe, halafu wakatunga sheria ya kuwakamata wasio na kazi. Waliwaita wazururaji. Nasikitika kwamba sheria hiyo inayokiuka haki za binadamu bado inatumika hadi leo. Kazi ya serikali yangu itakuwa kutengeneza mazingira yatakayozalisha kazi nyingi kwa watanzania, na siyo kujinaisha kutokuwa na kazi. Mtu kukosa kazi siyo kosa lake. Kwa nini afungwe jela kwa kukosa kazi?

CCM walitaifisha mashirika yote na kuyafanya mashirika ya UMMA. Madudu yaliyofuatia wenyewe mliyaona. Mashirika yote yalikufa. Majumba yote yalitaifishwa na kuitwa MSAJILI WA MAJUMBA.

Watanzania walinyimwa haki yao kujijengea nyumba. Hata waliojaribu kujenga walijenga mabanda kuepuka usumbufu  wa serikali ya CCM wakati huo ikiongozwa na Nyerere. Hata leo makazi ya watanzania yanatisha. Mashamba kama ya kahawa moshi yalitahifishwa na kufanywa mashamba ya Umma.

Wazungu waliokuwa wakiyamiliki mashamba hayo walitimuliwa na Nyerere akaweka Wazanaki wenzake wayasimamie mashamba hayo. Leo hii siyo mashamba tena bali ni mbuga ambazo hazina wanyama pori. Ajira ngapi za watanzania zilipotea kwa sera mbovu za CCM? Leo hii Mkapa anawatimua watanzania kwenye machimbo ya dhahabu MERERANI na kuwauzia Wazungu. Anadai kwamba watanzania hawana nyenzo za kuchimba madini. Watazipata wapi wakati tangu mwanzo walilemazwa na CCM wasifanye chochote katika nchi yao?

CCM wamejua mwisho wao umefika ndiyo maana wanauza kila kinachouzika wajiwekee akiba tutakapowavua madaraka. Wanajisumbua.

Mkapa anajitahidi kukusanya kodi na kuzidi kuwadidimiza watanzania walionyanyaswa na CCM kwa miaka arobaini. Kwangu mimi Mkapa hajafanya chochote Tanzania zaidi ya kuiuza nchi yetu kwa mabepari ambao watanzania hatuwezi kushindana nao kibiashara. Hii ni kutokana na sera za CCM zilizotangulia kuwadumaza watanzania katika kila kitu. Ndio maana tumegundua kwamba CCM ilishusha Jehanamu Tanzania, na tunataka mabadiliko Tanzania na tunayataka sasa.

Nyerere alikosea, na Mkapa bado anakosea

Serikali ya Tanzania inakosea kuuza mashirika ya umma kwa watu binafsi. Siasa ya ujamaa ambayo hatujaikana hadharani inakataza hilo. Wananchi wanapolalamika kuhusu soko huru wana haki ya kufanya hivyo kwani hawajatayarishwa kuingia katika mfumo wa soko huria.Wanachokijua ni mfumo wa kuingoja serikali iwafanyie kila kitu. Hata kuwatoza Watanzania kodi ni makosa. Kodi ni pato la ziada kutoka katika biashara. Kama watanzania hawajaingia kabisa katika ushindani wa kibiashara katika soko huria, kuwatoza kodi ni kuzidi kuwadidimiza na kuwafanya watoke kabisa katika huo UTANDAWIZI wa SOKO HURIA.

Unaitwa UTANDAWIZI yaani wizi uliotanda. Kabla ya kuwafundisha watanzania hu UTANDAWIZI, kuwalazimisha kuingia ndani yake ni sawa na kumtosa mtu asiyejua kuogelea baharini. Matokeo wote tunayajua. ATAZAMA. Watanzania tangu waingizwe kwenye soko huru, wanazama na hawawezi kupiga mbizi. Afrika ya kusini ndio wanaofaidi. Makampuni mengi ya kigeni yamechipuka, hata yanayouza mchicha kutoka Afrika ya kusini. Wakulima wetu hawana soko la kisamvu, kwani kisamvu kutoka afrika kusini kinauzwa kwenye maduka makubwa yaliyojengwa kisasa, tofauti na mchicha wetu ambao hutandikwa chini katika soko la kariakoo.

Bado hatujajua madhara ya mazao yanayokuzwa na kemikali nyingi, lakini subirini mtaona. Mayai ya kuku wa kienyeji anayejiokotea chakula chake mwenyewe ni bora kuliko yale ya kuku wa KISIASA. Nawaita wa KISIASA makusudi japo najua jina wanalotumia ni kuku wa GREDI . Siasa inaingia pale ambapo wanasiasa wanalinda maslahi ya wafanyibiashara, hata kama biashara yenyewe ina madhara kwa wananchi. Hapa ninalenga machungwa maembe vitunguu, nyanya na mazao yote kutoka South Africa. Yanalimwa katika mashamba makubwa ya MAKABURU, na wanatumia chochote ili wazalishe haraka kwa ajili ya biashara. Nasikia kwamba wenyewe wala hawawapi mifugo wao mazao hayo wachilia mbali kujaribu kuyatumia kama chakula.

Mkapa naye anatuambia ni UTANDAWIZI na amewaruhusu MAKABURU kujaza nchi yetu mazao ambayo kiafya siyo mazuri kwetu. Tukilalamika anasema sisi ndio hatujui maana ya soko huria. Hata kama tunajua UTANDAWIZI kuliko makaburu na Mkapa, haitaondoa ukweli kwamba hatuhitaji machungwa kutoka afrika kusini wakati Tanzania ina machungwa ya kuitosha na mengine yanauzwa KENYA. Afadhali nao Afrika ya kusini wayakubali machungwa ya BONGO kuuzwa CAPE TOWN. Pengine yanauzwa huko mimi ndio sijui. Lakini nina mashaka. Jamani! hata mchicha sasa unapatikana SUPER MARKET? tena siyo mchicha wa Tanzania, unatoka nje ya nchi. Sawa. Huo ndio UTANDAWIZI Mkapa na serikali yake wanataka tuupigie makofi.

Hapana hatuwezi kushangilia wakati tunaona wazi kwamba wananchi wanaumizwa na sera mbovu za serikali anayoiongoza Mkapa. Tanzania ina mali nyingi za asili lakini zote Mkapa amewakabithi wageni kwa kigezo cha SOKO HURIA. Madini ya Tanzanite hupatikana Tanzania pekee, lakini Kenya ndio waliopata zawadi kwa kuongoza katika kuyatoa mawe hayo. Kilichofanyika ni kwamba Tanzanite yote ilinunuliwa na Wakenya na kupelekwa kwenye soko la kimataifa kupitia Kenya. Siyo madini tu, hata mlima Kilimanjaro watalii wengi wanajua kwamba uko Kenya. Yaani kiutalii wenzetu Kenya wamejitangaza na sasa wanatangaza mlima Kilimanjaro pamoja na mbuga zetu za wanyama lakini wanasema ziko kwao. Masai Mara inajulikana kuliko Serengeti na watalii wanaposisitiza kwenda serengeti wanaambiwa waache kila kitu Kenya kwani huko wanakokwenda ni vichakani sana na watu wa huko ni wa ajabu sana wanaweza kuwaibia pesa na vitu vyao. Watalii wanapitishwa Namanga kwenda kuona mbuga zetu wakati matumizi mengi wameyatumia Kenya. Tena wanapita Namanga wakitumia gari la Kenya, ndani wana maji ya kunywa kutoka Kenya na watakacholipa Tanzania ni kiingilio kwenye mbuga za wanyama na kurudi kuimalizia safari yao Kenya. Mkapa hata hiyo anataka tumsifie kwamba sekta ya utalii ameiinua vilivyo.
Siyo nia yangu kukosoa kila kitu, lakini kukiwepo la kusifu nitasifu. Kwenye Serikali ya Mkapa na CCM sioni la kusifia na siwazuii wanaoliona kulisifia.

Kama kuwaua watu huko Zanzibar kunastahili kusifiwa basi mkapa apokee sifa kutoka kwenye gazeti la UHURU na MZALENDO na siyo kutoka kwenye gazeti la INJILI ninaloliandika mimi Munishi. Ikiwa kuwaruhusu Makaburu watuuzie hata mchicha nayo inastahili kusifiwa, basi nitamsifu nikiwa kaburini. Tena kama nchi inayoongozwa na mwandishi wa habari MKAPA ndiyo inayoongoza katika kuwanyanyasa waandishi wa habari, na mnataka tumsifie Bwana Mkapa basi kalamu zetu zimekataa kuandika sifa hizo. Ikiwa mnataka tumsifu Mkapa kwa kuingia kwenye mijadala ya Internet na kujiita BIG BOY Huku akiwatusi watu matusi ya nguoni ili wasitoe hoja za kumkosoa yeye na serikali yake, basi sifa hizo atazipata kutoka kwa wendawazimu kama yeye. Watu ambao hawalali bila kumwaga damu ya wananchi waislamu wasio na hatia. Wanatekeleza agizo la mabwana zao Amerika bila kujua lkwamba Marekani wana malengo yao ya kumiliki mali zote asili duniani. Waarabu ambao wengi wao ni waislamu wana kitu ambacho Marekani wanakimezea mate. Wanawaletea UTANDAWIZI ili wawaibie katika huo wizi uliotanda.

NAKANUSHA UVUMI UGONJWA WA MKAPA

Kwanza kabisa  napenda kukanusha uvumi ulioenea Tanzania. Wengi wanasema Nyerere ndiye anayesababisha ugonjwa wa mheshimiwa Mkapa. Wanadai kwamba kuyauza mashirika ya umma kwa mabepari, ndiyo sababu Nyerere anataka kumwita Mkapa kuzimu haraka. Wanaendelea kudai kwamba ujamaa ambao Nyerere aliuingiza ndani ya mifupa ya Mkapa, ndio unaopingana na utandawizi na soko huria ndani ya nyama na mishipa ya Mkapa. Wanasema mifupa inauma kwa sababu ujamaa hautaki kutoka, pamoja na shinikizo unaowekewa na mishipa ya damu. Wanasema ndani ya Mkapa damu imeiwekea mifupa shinikizo ili iutoe ujamaa ndani, na mifupa imekataa hilo katakata. Matokeo mifupa inasagana yenyewe. Huo ndio uvumi ulioenea katika kila kona ya Tanzania.Wengine wanasema Waislamu waliouawa wakati wa uchaguzi uliopita ndio wanaomtesa Mheshimiwa Mkapa. Kuna wanaosema kwamba pengine ndugu wa jamaa waliowahi kuuawa au kuteswa na CCM ndio waliomloga Rais.

Mimi kama mchungaji  napinga uvumi huo kwa nguvu zangu zote. Mtu akisha kufa hana uwezo wa kurudi duniani kwa njia ya roho aje afanye lolote kwa walio hai. Hizo ni imani potovu za kishirikina ambazo hazina msingi wowote katika maandiko ya neno la Mungu. Pia siamini kwamba Mkapa amelogwa. Kwa maoni yangu Mkapa anaumwa kama kawaida ya wanadamu kuumwa. Maadui zake watakosea kufurahia kuugua kwa Mkapa, kwani hata akifa siyo adhabu tosha ya makosa aliyoyafanya. Adhabu inayomtosha ni kuwa hai maadui zake wamsamehe, na wamtendee mema badala ya mabaya aliyowatendea. Nakubaliana na maoni kwamba wote tunatakiwa kumuombea Mkapa apone haraka. Lakini kama ikishindikana, tutasema MAPENZI YA MUNGU YATENDEKE.

Binafsi ningependa kuendelea kupinga sera za CCM ambazo nazichukia sana na Mkapa akiwa hai. Nilipoanza kumpinga Nyerere mwaka mmoja kabla ya kifo chake, vyombo vya habari havikuandika. Nilipotoa kanda baada ya kifo chake Nyerere, wengine walinisakama kwamba Mbona alipokuwa hai sikusema lolote? Unaweza kuwahesabia haki kwa hilo lakini si kweli kwamba niliogopa kumkosoa Nyerere akiwa hai. Nilifanya hivyo. Lakini jinsi alivyokuwa amethibiti vyombo vya habari ungesemea wapi kwamba Nyerere alikuwa mwendawazimu? Sitaki wanaonipinga wawe na sababu ya kusema namkosoa Mkapa akiwa marehemu, ndio maana inanilazimu niombe apate nafuu.

Siyo kwamba hata Mkapa akiwa hai watakosa ya kusema, Hapana. Watasema Mengi sana. Wengine wanasema sifai kuwa rais kwa sababu  nilikuwa jambazi. Ningekuwa jambazi sasa hivi ningekuwa jela. Hasa baada ya kuikosoa serikali kesi zote zingefufuliwa. Lakini wanajua kwamba sijawahi kuiba mali ya mtu ndio maana wanatapatapa kutafuta matope ya kunipaka.

Tukirudi kwenye hoja, CCM lazima watoke madarakani. Haijalishi mbinu gani watakazotumia kuwafisha moyo wanaharakati za mabadiliko, lakini kutoka watatoka.

Serikali yetu wananchi tutakayoiunda haitalipiza kisasi.  Macho yetu tutayaelekeza mbele kuiendeleza Nchi na siyo kutafuta Mkapa tumweke ndani. Kwa hiyo Mkapa asiwe na wasiwasi kwamba nikichukua madaraka UKONGA ndiko kutakuwa nyumbani kwake. Hapana. Ikiwa Mtu aliamuru watu zaidi ya sabini wakauawa kwa sababu za kisiasa, hata ukamchukua umkatekate vipande sabini bado haitoshi kugharamia maisha ya wale sabini. Isitoshe utakuwa umongeza kifo cha mtu ambaye angekufa tu hata kama hukumuua. Adhabu kali kwa Mkapa ni kuwekwa benchi wao na CCM halafu waone nchi ikinawiri kwa miaka miwili ya kwanza. Inazidi adhabu ya kifo kwao. Lakini mali za wananchi lazima warudishe. Majengo na viwanja vyote vilivyo katika jina la CCM siyo mali ya chama bali ni mali ya wananchi wa Tanzania. Hayo tutachukua. Pesa zote za wizi walizojiwekea nje ya nci tutazichukua.

Tutaiomba jumuia ya kimataifa itusaidie katika kuhakikisha kwamba pesa zote viongozi wa CCM walizoiba zinarudi mikononi mwa Watanzania. Kabla hawajatupa mikopo, tutawaomba watusaidie kurudisha kilicho chetu kwanza na mikopo ifuatie. Mikopo ina masharti, lakini pesa zetu CCM walizoweka kwenye mabenki yao hazina masharti kwani ni zetu. Wana CCM watakaoamua kubaki nchini baada ya mabadiliko hatutawasumbua bali tutawaambia wafungue macho waone kazi ilivyopaswa kufanywa.

Wananchi wapendwa Msife moyo na kejeli za CCM. Kazi iliyo mbele yetu ni moja nayo ni kuitoa CCM madarakani. Kura yako ndiyo silaha yako. Hakikisha unayo na uitumie vizuri.Penye nia pana njia. Msife moyo. Mungu yuko upande wetu. Milima mingine itayeyuka yenyewe na mtapita kukiwa tambarare. Bahari nyingine zitakauka zenyewe na mtapita kama nchi kavu. Tusimame kama Daudi. CCM ni GOLIATHI, lakini jiwe moja ndani ya kombeo lilimaliza kiburi cha Goliathi. CCM mnaowasikia leo wakitamba nitawaletea kichwa chao wakiwa wamenyamaza.Umoja wetu ndiyo nguvu yetu.

MKINICHAGUA NITAUINDA SERIKALI YETU  SIYO YANGU

http://munishi.com/

Kinyume na ilivyo sasa, Mkinichagua kuwa kiongozi wenu 2005 nitaunda serikali yetu. Katiba ya sasa inamruhusu rais kuunda baraza lake la mawaziri. Katiba mpya ambayo ndiyo ninayoipigania, Bunge ndilo litakalochagua mawaziri. Wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi, ndio watakaowachagua mawaziri wakitumia kura. Watakaogombea nafasi za uwaziri siyo lazima wawe wabunge, lakini ni lazima wawe wanataaluma katika wizara husika. Hakuna njia za mkato katika hili. Wananchi ndio watakaokuwa na uwezo wa kuwafuta mawaziri kazi, baada ya malalamiko yao kufanyiwa uchunguzi na mahakama. Hata majaji wa mahakama kuu watachaguliwa na bunge. Kila taasisi itakuwa huru kufanya sawa na taaluma zao bila kuingiliwa na wanasiasa. Kazi kubwa ya rais itakuwa kuwasikiliza wananchi wanataka waongozwe vipi, na kuangalia jinsi gani wananchi wenyewe wanaweza kusaidia katika kujiongoza.

Wakati wa kupoteza muda kujadili nani anayefaa kutuongoza umepita. Sasa tunataka nani tusaidiane naye kujiongoza. Badala ya kuwatukana watu ambao hawajaonyesha nia ya kuwania urais, ni wakati wa kumuuliza aliyejitokeza atafanya nini tofauti na serikali zilizopita. Nimesoma kwa mshangao jinsi watu fulani wanavyopoteza muda kutaja majina ya watu na kuyapaka matope. Utawasikia wakisema fulani hafai au anafaa kuwa rais. Mbaya zaidi wataanza kuwatusi waliowataja na wenyewe wala hawana ndoto za urais. Pengine wenyewe wanajiona duni hawawezi lolote mpaka wapate mtu wa kuwaongoza. Swali ni je! wenyewe wanafaa kuongozwa.

Katika serikali yetu tutakayoiunda, kila mtu ni muhimu.Tutampa kila mtu nafasi ya kujinadi nini anaweza kukifanya vizuri zaidi na kutumia kipawa hicho kulijenga taifa. Ushauri wangu kwa hawa wanaopoteza muda wakitauta nani anayefaa kuwatawala, waanze sasa kuonyesha wao wanaweza kufanya nini nami nitahakikisha taaluma na vipawa vyao vinatumika kulijenga Taifa. Rais hawezi kuwa mtu aliyesomea kila kitu. Na haitakiwi iwe hivyo. Mara nyingi taaluma ya rais siyo muhimu akishakuwa rais. Mfano ni Mkapa ambaye taaluma yake ni uandishi wa habari. Kinyume na ilivyotarajiwa, Yeye ndiye anaewatukana waandishi na kuwaita wajinga, isitoshe wengine anawaweka ndani  kutumia serikali yake kuzifungia kazi zao.

Wakati wa rais kuunda baraza la mawaziri akitumia ndugu na marafiki zake umeisha. Serikali zilizopita watu walikuwa wanasimamia wizara tofauti na taaluma zao. Mtu anaweza kujiuliza kwa nini serikali ilitumia pesa nyingi kuwasomesha na baada ya kuhitimu  wasipewe nafasi ya kuonyesha umairi wao katika taaluma zao? Siyo ajabu kila wizara ilikuwa "inaboronga."

Kama nilivyotangulia kusema, nitakuwa rais asiye na madaraka mengi kama ya Mkapa. Bunge ndilo litakaloamua mambo mengi ya kiserekali, na wananchi ndio askari wa kuangalia utekelezwaji wake. Wananchi ndio watakaokuwa na madaraka kuliko viongozi serikalini. Ulinzi mkubwa watapewa wananchi na mali zao, kinyume na ilivyo sasa ambapo wanasiasa ndio wanaolindwa kuliko wananchi. Siyo ajabu mkaniona mitaani baada ya kunichagua niwe rais wenu. Sitawaogopa kwa hiyo sitakuwa na ulinzi kama alio nao Mkapa. Sina madaraka mengi kwa hiyo maadui zangu watakuwa wachache. Mkapa analindwa kwa sababu mtu akiweza kumuua serikali yake imekwisha. Mimi haitakuwa hivyo. Kwanza serikali ni yetu, na mmoja wetu akiondoka serikali inabaki kwa sababu ni yetu.

Utendaji katika ofisi zote kuanzia ikulu utakuwa rahisi. Mafaili ya ikulu yatapungua kwani kila wizara itapewa nguvu ya kufanya mambo yake. Isitoshe IT ndiyo itakayopewa kipaumbele katika uongozi wetu. Badala ya mafaili kibao, kutakuwa na kompyuta chache kutunza data za kila wizara. Wananchi watawezeshwa kujua nini kinaendelea katika ofisi yeyote ya serikali kwa njia ya Redio TV na Internet. Kila juhudi zitafanywa kufikisha habari kwa wananchi ili wafanye maamuzi baada ya kuelewa. Ndugu wananchi nina mengi, lakini nikomee hapo ili niruhusu maswali. Naweza kuendelea na kuendelea kumbe ninayogusia hayakuhusu ulipo wakati huu. Nangoja kusikia kutoka kwenu. Usiogope kuuliza lolote ili unipe kura yako baada ya kuelewa nitafanya nini nikisaidiana na wewe kuifanya Tanzania mahali pazuri pa kuishi tofauti na serikali za awali.

NYUMBANI NI NYUMBANI
Lakini CCM ni wauaji

Pamoja na kwamba unaweza kupata mali na utajiri ugenini, lakini huwezi kupata kila kitu ugenini. Ndio maana Nyumbani ni nyumbani hata kukiwaje. Sera zangu kuhusu Watanzania walio nje, ni kuwaomba warudi nyumbani tuijenge Tanzania. Hata ukiwa na nini ugenini huwezi kuthaminiwa kama ukiwa nyumbani. Kuna mengi ugenini ambayo kila kukicha yatakukera. Swali kwamba utarudi lini kwenu, ni mojawapo ya mambo yanayokera. Hata ukipewa uraia wa kujiandikisha, huwezi kupewa uzito sawa na wazawa wa huko. Ombi langu kwenu Watanzania mlio nje: Karibuni nyumbani kwani CCM iliyoharibu nchi mwisho wake umefika. Leteni mali zenu na hakuna atakayewasumbua. Tutawapa nafasi za kwanza za uwekezaji katika nchi yetu.

Mimi mwenyewe nimekaa ugenini kwa muda mrefu. Japo ni taifa jirani ambalo hatupitani sana katika mila na utamaduni, hukosi ya kukukera kama mgeni. Mfano niliwahi kushinda nishani ya mwanzilishi wa kuimba nyimbo za injili (SOLO) Lakini kwa sababu sikuwa raia, vyombo vya habari vilisema kwamba nishani hiyo apewe mzawa. Wakampa nishani kwa sababu ni mzawa lakini mwanzilishi ni mimi. Vitu vidogodogo kama hivyo vinakukumbusha nyumbani.

Pamoja na kwamba Mkapa na CCM walikuwa wameniwekea ukuta nisikanyage Tanzania, mwenyewe niliamua liwalo na liwe na nikarudi nyumbani.Nilifurahi sana kuwaona wazazi, ndugu na jamaa zangu ambayo zaidi ya miaka kumi tulikuwa hatujaonana. Japo nilifuatwa kila nilikoenda na watu tofauti, haikuniondolea furaha yangu ya kuwa nyumbani. Sitaki kuongeza chumvi niseme kwamba nilikamatwa na kusumbuliwa, lakini nyendo zangu zote zilifuatiliwa.

Kilichonihuzunisha ni habari za kukamatwa kwa wenye maduka ya kanda za muziki. Kosa lao lilikuwa kuuza kanda ya Munishi toleo la saba kwa jina "MPENDE ADUI" Ilidaiwa kwamba ndani ya kanda hiyo kulikuwa na maneno "CCM aliyoanzisha Nyerere, Sasa imezeeka. Sera zake zimeiharibu Tanzania, Na Ujamaa ulishindwa kabisa, Watanzania Msiirudishe CCM madarakani." Hayo ndiyo maneno yaliyodaiwa kuwa  ya "UHAINI."  Wenye maduka nchi nzima waliwekwa ndani kwa kile kilichodaiwa "AMRI KUTOKA JUU" Wengine waliachiliwa baada ya kukaa mwezi kwenye CELL za polisi bila kufikishwa mahakamani. Wengine walitoa rushwa ya malaki ya shilingi za kitanzania kununua uhuru wao. Wengine walionywa vikali kutouza kanda zozote alizoimba Mwinjilisti Munishi.


Hii ndiyo kanda ambayo Serikali ya CCM iliipiga marufuku

Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, kuna mama mmoja ambaye sakata hiyo haikumwendea vizuri na hivi tunapozungumza ni marehemu. Walikuwa wakimwita Mama Tony, mkazi wa Kindi chini Muyuni kilomita mbili kutoka  sekondari ya wasichana "WERUWERU." Bila kujua kwamba kanda ya Munishi imepigwa marufuku na serikali, yeye alikuwa akiziuza kwenye duka lake lililoko soko kuu la Moshi. Duka lake liko kwenye mlango wa kuingilia sokoni, na pengine ndiyo sababu likawa maarufu.

Ilifika siku ya siku, ambapo maofisa kutoka kituo cha polisi Moshi wealifika dukani kwake wakiwa wamevalia kiraia. Waliikuta kanda hiyo inaimba kwani ilikuwa haibanduki kwenye kinanda hasa ikizingatiwa kwamba ndiyo kwanza ilikuwa imetoka jikoni na ilikuwa inauza kama keki moto. Maofisa walijifanya kana kwamba hawaijui kanda yenyewe na wakauliza wapewe kanda ya Munishi kwa jina Mpende Adui. Walipopewa moja, walisema kwamba waongezewe tatu kwani walikuwa wanne. Baada ya kupewa walidai risiti na wakalipa pesa. Kilichofuatia hata wewe unakijua.

Walimuamrisha huyo mama kufunga duka, na wakaandamana naye kituoni. Alishinda huko mchana kutwa, na usiku wake wakaandamana naye nyumbani kwake kufanya upekuzi bila kibali kutoka mahakamani. Hawakupata walichokitafuta, kwani kanda zote zilikuwa dukani, na tayari walikuwa wamezibeba. Chini ya godoro walikuta pesa taslimu milioni tano za kitanzania. Waliuliza kwa nini pesa kiasi hicho ziko nyumbani na siyo benki? Majibu waliyoyapata yaliwasisimua zaidi. Mama Tony aliwajibu kwamba mume wake yuko Mererani kwenye machimbo ya dhahabu na kwamba shimo lake lilikuwa limetoa mawe. Pesa nyingine zimewekwa benki na hizi milioni tano ni matumizi ya nyumbani na dukani.

Walibishana wenyewe kama wabebe pesa ziwe kielelezo cha kesi ya kanda, na baada ya kubishana wao kwa wao pesa ziliachwa nyumbani na wakaandamana na Mama Tony kituoni.Usiku wa manane, askari wale wale walirudi nyumbani kwa mama Tony wakidai walisahau kitu fulani ndani ya nyumba. Walimkuta msaidizi wa nyumba, na walipofunguliwa breki ya kwanza ikawa ni kwenye chumba cha kulala na wakapekua godoro ili waone kama mzigo wa pesa bado uko. Walipoambiwa kwamba pesa zimepelekwa kwa mzee Mererani usiku huo, unajua jinsi walivyojisikia. Waliondoka shingo upande na kuwaacha wanakijiji waliogubikwa na woga wa magari ya polisi kijijini usiku wa manane ambapo siyo kawaida ya kijiji hicho kutembelewa na wageni kutoka serikalini.

Asubuhi yake Mzee mwenye nyumba aliwahi mapema polisi kuanza jitihada za kumtoa mke wake ndani hata kwa dhamana. Mikwala aliyowekewa ilikuwa babu kubwa. Kwanza aliambiwa kwamba shauri lao kubwa sana kwani amri ilitoka juu. Mzee wa kichagga kutoka Mererani akaanza kutumia pesa kumtoa mke wake. Aliongea na wazee maafande wadogo karibu wote bila mafanikio. Usisahau kwamba maongezi yanafanyika baa na bili zote za pombe pamoja na miguu ya mbuzi anayelipa ni Mzee wa Mererani. Wiki tatu zikakatika na mama Tony bado yuko ndani. Baada ya kuuliza nini kinachotakiwa ndipo alipoelekezwa amuone mkuu wa kituo. Aliyempa ushauri huo ni afande ambaye cheo chake ni koplo jina lake tunalo. Alimwambia mkuu wa kituo cha  polisi Moshi siyo mtu rahisi kuona kwa hiyo lazima mipango dhabiti ifanywe ili mkutano wake na mkuu wa polisi ufanikiwe. Mzee alikubaliana na kila kitu ili mradi mke wake atoke.

Hatimaye alifanikiwa kukutana na mkuu wa kituo cha  polisi Moshi.Mkutano ulifanyika kwenye hoteli kubwa kuliko ile waliyokuwa wakikutana na maafande, kwa hiyo bili za vinywaji na vyakula zilikuwa kubwa kuliko awali. Mzee wa Kichagga alichanganyikiwa alipoambiwa kwamba shauri lake hata mkuu wa kituo haliwezi, kwani hata yeye alipokea amri kutoka makao makuu Dar kwamba wote watakaokamatwa na kanda za Munishi wawekwe ndani hadi uchaguzi umalizike. Mwezi ukaisha na mama Tony bado alikuwa kituo cha polisi Moshi. Ilimbidi mzee wa Kichagga atumie kila pesa aliyokuwa nayo kununua uhuru wa mke wake. Hatimaye alifanikiwa kumtoa katika kituo cha polisi, na alipokuwa akiongea nami hakumbuki ni pesa ngapi alizotumia katika harakati za kujaribu kuununua uhuru wa mkewe, lakini alisema ni mamilioni ya shilingi. Mama Tony alitakiwa kuripoti polisi mara mbili kwa wiki na alifanya hivyo kwa mwaka mzima. Mpaka wakati walipoambiwa kwamba faili ya kesi yao imefungwa, Maisha yao hayakuwa sawa tena. Pesa zilikuwa zimewapungukia. Biashara ilikuwa imezorota, Bado maofisa wa polisi walikuwa wakija dukani na nyumbani kwao kila wanapoamua kufanya hivyo.


Afya ya mama Tony ilianza kuzorota japo hakudai kuteswa alipokuwa kituo cha polisi kwa muda mrefu. Mwenyewe alisema hakuwahi kupigwa na askari wakati wote akiwa rumande ya polisi, lakini anasahau kwamba haikumpasa awe hapo zaidi ya masaa ishirini na manne bila kufikishwa mahakamani.  Mwezi wa nane mwaka huu 2003 Mama Tony aliaga dunia baada ya kulalamika kwamba kichwa kinamuuma siku moja kabla ya kifo chake. Siyo nia yangu kukihusisha kifo chake na serikali ya CCM, lakini msomaji unaweza mwenyewe kuangalia mchango wa CCM katika kifo cha mama Tony na ufukara wa mume wake.

Alikuwa milionea wa Mererani, lakini baada ya serikali kuyaingilia maisha yake sasa hana pesa. Hata nauli ya kwenda Mererani kujaribu bahati siku hizi anaomba. Mbaya zaidi amempoteza mke wake mwaka huu. Watoto yatima, Baba mjane, na kanda zake hawakumrudishia. Kanda alikuwa amezinunua kutoka kwa wakala aliyekuwa amezifuata Nairobi. Hii ndiyo CCM ambayo kila nikisema haifai kuwa madarakani wengine hawanielewi. Nashukuru wengi wananielewa hasa wale waliowahi kukutana ana kwa ana na mateso ya CCM. Jamaa na marafiki wa Waislamu zaidi ya sabini waliouawa Zanzibar wakati wa uchaguzi uliopita watanielewa nisemapo CCM ni chama cha wauaji. Wenye maduka ya kanda walionyanganywa kanda walizonunua kwa pesa taslimu, watanielewa kwa nini nasema CCM ni Chama cha Majambazi.

Dawa ni kuitoa CCM madarakani kwa njia ya kura. Kura yako ndiyo uhai wako. Usikubali kuiuza kwa pesa au ahadi za uongo kutoka CCM. Wakikupa pesa kula lakini kura yako usiwape CCM. Nasema pesa pokea kwani ni mali yako. CCM hawana kilicho chao bali kila walicho nacho waliwanyanganya wananchi wa Tanzania. Mungu amesikia kilio cha watanzania na ameanza kutusaidia kuufikia ukombozi wetu. Mungu wabariki wananchi wa Tanzania. Wasaidie kuitoa CCM madarakani bila umwagikaji wa damu. Watanzania walio nje wape moyo wa kurudi kuja kuijenga nchi yetu ya Tanzania. Tumeomba machache katika jina la Yesu. AMEN.

MUHIMU NI MABADILIKO SIYO UDINI NA UKABILA

http://www.munishi.com/


http://www.munishi.com/

Dini Kabila. itikadi za kisiasa siyo muhimu kwa sasa. Muhimu ni kuitoa CCM madarakani.Wengine wanasema ni mlima mrefu kupanda. Watanzania tumeamua kuupanda mlima huo. Nia sababu na uwezo tunao. Hakuna litakalotuzuia. Tunataka mabadiliko ya kuitoa CCM madarakani TOSHA. Mengine tuongee baada ya kibarua hicho. Hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Tukimwachia Mungu, kwa imani yote yawezekana.

Vipingamizi ni vidogo. Kama KATIBA ni moja ya vipingamizi. Tunajua wazi kwamba serikali ya CCM haitakubali kuirekebisha KATIBA waliyokwisha iharibu ilinde maslahi yao. Lakini nguvu ya wananchi kuamua ni sawa na maji mengi ambayo yamefurika mabadiliko. Yatazoa kila kitakachojaribu kuyazuia yasiende yalikokosudia. Nchini Kenya wananchi waliamua wamechoka na KANU. Hawakujali kwamba KATIBA yao inasema hakuna ruksa muungano wa vyama kuunda serikali. Nia yao ya kuitoa KANU madarakani, ilifanikiwa japo katiba inasema wako madarakani isivyo halali. Nani anajali? Hata KANU ilikuwa na uhalali gani kuwa madarakani kuwatesa Wakenya?

Siyo kwamba hatupendi kufuata sheria. Ndiyo maana tunapendekeza kwamba KATIBA yetu lazima irekebishwe kabla ya uchaguzi. Tunajua wazi kwamba CCM hawawezi kutengeneza mazingira ya kufanikisha hilo. Hata wakijaribu, ni kununua muda tu na kutafuta sababu za kukwamisha zoezi zima. Je katika mazingira hayo mnatarajia Munishi na watanzania wanaotaka mabadiliko wafanyeje? Lazima tuanze mikakati ya kujikomboa hata kama ni kinyume na KATIBA ya CCM ambayo ndiyo wanayoiita KATIBA ya Tanzania.

Ni kweli kwamba Tanzania kuna mfumo  mbaya wa utawala na siyo mfumo wa uongozi. Tunataka mabadiliko tuwe na mfumo mzuri wa uongozi. Siyo lazima mimi niwe Rais ndipo hayo yatekelezeke. Mtanzania yeyote mwenye mawazo ya kutengeneza mfumo mzuri wa uongozi Tanzania nitamuunga mkono.Na kuna ubaya gani kama Watanzania watasema ni mimi? Lakini siyo CCM. Sijali dini au kabila la kiongozi husika lakini najali chama kisiwe CCM. Wamekuwepo miaka zaidi ya arobaini, kama kutengeneza muda waliokaa madarakani ungetosha kufanya hivyo. Kwamba matunda ni umasikini na hali duni za kutisha, inanipa sababu ya kesema CCM wamezeeka na hawawezi kujifunza mbinu mpya.


Mimi siyo mwanachama wa chama chochote cha kisiasa na sitarajii kujiunga na Mtikila wala chama chochote cha kisiasa. Wala sitarajii kuunda chama cha kisiasa. Lakini nataka mimi na Watanzania wengi wasio wanachama wa vyama vya kisiasa wawe huru kugombea uongozi wa nchi yao bila kuzuiwa na chochote kama katiba ya CCM. Tunataka katiba irekebishwe iseme hivyo. Tanzania ni ya Watanzania na siyo mali ya Rais aliyeko madarakani. Tunataka KATIBA irekebishwe ili madaraka mengi aliyo nayo rais yapunguzwe. Madaraka yote yawe kwa wenye nchi ambao ni watanzania, halafu lifuate Bunge na ndipo rais. Tunataka katiba inayompa Rais nguvu za kuwaongoza watanzania wapendavyo na siyo apendavyo Rais. Marais watakuja wakienda, na wengine watakufa, lakini Tanzania itabaki. Tutengeneze katiba inayowalenga watanzania na vizazi vijavyo. Katiba tuliyo nayo inalenga CCM na rais anayetawala. Ndiyo maana Rais ana mamlaka ya kuvunja Bunge, isitoshe anaweza kuwapeleka vijana wetu vitani apendavyo. Nyerere aliwapeleka vijana wetu Uganda kujaribu kumsaidia rafiki yake Obote arudi madarakani. Hatutaki upuuzi kama huo urudiwe na Rais yeyote Tanzania. Ndiyo maana kuyapunguza mamlaka ya Rais ni Muhimu kwa Tanzania na vizazi vijavyo.

Siombi kura kwa mtindo huu, lakini sera zangu naziamini kiasi kwamba masanduku ndiyo yatakayokosekana. Katiba irekebishwe, na nguvu ya hoja ndiyo itakayomimina kura upande wangu.  Nataka niwe kiongozi nisiye na madaraka mengi kama ya Mkapa. Hivi amelazwa Watanzania matumbo ni moto japo wana Bunge na viongozi wengine. Haipaswi kuwa hivyo. Ndiyo maana mara nyingi tunafichwa hali za kiafya za watawala wetu. Wana madaraka mengi, kiasi kwamba walitakiwa wasiugue. Hata wakiugua tunafichwa. Tunapoambiwa ni wagonjwa ni wakati maji yamezidi unga. Walipokubali kwamba Nyerere anaumwa ambaye hakupaswa kuugua kulingana na madaraka yake, Mwezi haukwisha aliaga dunia. Tunataka katiba irekebishwe tuwe na rais mwanadamu anaeugua na kuuguzwa kama wanadamu wengine. Kwani kuna kosa gani mtu kuugua? Watanzania tupo. Ndiyo maana walimwomboleza Nyerere kwa muda mrefu. Hawakuamini kwamba kweli yule mwenye mamlaka karibu ya Mungu ametuacha. Tunataka Tanzania mpya na KATIBA mpya tusiyarudie makosa ya awali. Ikiwa makosa yaliyofanywa na wingi wa madaraka ya Rais wa kwanza Nyerere yametufikisha tulipo, Je akitokea mwendawazimu mwingine Tanzania itakuwa wapi? Mwenye sikio asikie neno hili ambalo Roho wa Mungu anawaambia Watanzania.

HOTUBA YANGU HAIKUMAANISHA VURUGU

Jamani Hamjambo? Mimi siyo mtu wa kuchochea vurugu na sipendi kabisa vurugu. Nisemayo ni kwamba CCM aliyoanzisha Nyerere sasa imezeeka. Sera zake zimeiharibu nchi yetu ya Tanzania. Ujamaa ulishindwa kabisa na haifai kurudishwa madarakani.

Nakubaliana na hoja kwamba huwezi kuwaridhisha watu wote. CCM haijawaridhisha watanzania kwa lolote. Imekuwa ikitumia mabavu kwa kila kitu. Mbaya zaidi Nyerere alisema CHAMA KINASHIKA HATAMU ZOTE NA KUUA TAASISI ZOTE. Kila kitu Tanzania kilifanywa siasa na siasa kuwa kila kitu.

Hakuna mabadiliko Tanzania bila kuitoa CCM madarakani. CCM ni sawa na kansa kwa watanzania. Dawa yake ni kukata sehemu iliyoharibiwa na kansa hiyo na kuzuia isiendelee kusambaa. CCM walitumia pesa za umma kujitanua kila kona ya Tanzania kuendeleza maovu yao. Michango ya lazima kutoka kwa wananchi ndiyo iliyowafikisha CCM walipo. Wanaoridhika na CCM ni wale wanaokula kwenye sahani ya CCM iliyojaa pesa za wizi.

Watanzania tunachotaka ni mabadiliko ya kuitoa CCM madarakani. Tutafanya hivyo kulingana na sheria lakini siyo sheria za CCM. Ikiwa CCM wakitumia mwenyekiti wake wa zamani Nyerere, Waliweza kucheza na katiba ya nchi ili ilinde maslahi yao, nani atakayeweza kusema kwamba Tanzania kuna sheria? Sheria Tanzania ni CCM na CCM ndiyo sheria. Katika mazingira kama hayo mnategemea  watanzania wafanye nini? Waendelee kukaa chini ya utawala dhalimu? HAPANA. Liwalo na liwe. CCM sasa basi.Wametuibia vya kutosha, Wametuchangisha kwa nguvu vya kutosha, Tumetozwa pesa za michango ya mafuta ya mwenge vya kutosha, Sasa tunataka mabadiliko. Tusiibiwe tena, tusilipe pesa za mafuta ya mwenge tena.

Umewahi kuhudhuria tamasha la mahali mwenge unapolala? Mambo yote ya kishetani hufanyika hapo. Ulevi wa kupindukia usiku kucha, Ubakaji, na mambo mengi maovu hufanyika kwa kisingizio cha mbio za mwenge. Walitudanganya kwamba Mwenge unaleta amani pasipo na amani. Mbona wasiupeleke Rwanda na Burundi? Tena kwa nini hawakuupeleka Somalia ukaleta amani huko? Nani wanaouhitaji mwenge zaidi, Watanzania au nchi ambazo hazina amani? Sasa tunakubaliana na wale wanaosema kwamba Mwenge ulikuwa uchawi wa kizanaki kuwafumba macho watanzania. Tunakemea pepo hili la Mwenge pamoja na shetani mwenyewe CCM  kwa jina la Yesu washindwe.

Mwisho wa kuwanyanyasa watanzania umefika. Nuru ya Mungu imeanza kuiangazia Tanzania. Wanaosema hakuna kiongozi atakaweza kuongoza bila kulaumiwa, waachie ngazi nichukue hatamu za uongozi na watakaolalamika ni vigogo wa CCM waliozoea vya bure.

Uongozi wangu utaheshimu Taasisi na kila mtu atapewa uhuru wa kufanya kazi kwa bidii na alifurahie jasho lake. Kinyume na ilivyo sasa Watanzania wengi wanatumia msemo usemao MPANDA NGAZI HUSHUKA. Hawataki kufanya bidii ya kujitoa katika umaskini, kwani serikali inawasaidia kuwashusha waliopanda ngazi kwa njia ya kuwatoza kodi. Kodi siyo mbaya. Lakini inapotumika kama ujamaa mamboleo ndipo tunapokuwa na kila sababu za kuwakosoa watoza kodi.

Mkapa ni mwanafunzi mzuri wa Nyerere. Na itakumbukwa kwamba Nyerere hakuwahi kuukana  ujamaa hadharani. Mkapa pamoja na na kuyauza mashirika ya umma kwa mabepari, mwenyewe ni mjamaa mpaka ndani ya  mifupa yake. Hajawahi kuukana ujamaa hadharani. Kutokana na hayo Tanzania inabaki na sera  kama za popo ambaye siyo mnyama wala siyo ndege. Sera za Tanzania Siyo wajamaa wala siyo mabepari, Lakini watanzania wenyewe walilazimishwa kuwa wajamaa kwa miaka yote ya utawala wa Nyerere. Na mniambie kama Tanzania sasa inaongozwa na nani kama siyo Nyerere akiwa kaburini.

Baada ya kuyasema hayo naomba nieleweke kwamba mimi sipingi kodi. Ninachopinga ni kuitumia kodi kama kama njia ya kuwakomoa matajiri. Na ndivyo kodi inavyokusanywa Tanzania. Nikisema inatumika kuwakomoa matajiri inasikika vizuri. Lakini ukweli ni kwamba kodi inatumika kuwazuia watanzania kuwa matajiri. Mtanzania anayeuza vitu vidogo vidogo kwenye duka lake dogo, anapotozwa kodi za ajabu ajabu, basi lazima atafunga duka lake. Kwa sababu ya kasumba za kiujamaa alizotuachia Nyerere, Mtanzania mwenye kaduka ka nguo na gari moja TOYOTA CHASER pamoja na nyumba ya kulala na familia yake, huyo ni tajiri kulingana na serikali ya Tanzania. Ataandamwa na maofisa wa kodi mpaka afunge duka lake.

Je huo ndio utawala wa kufuata sheria au ni kunyanyasana? Nchini Kenya walifuata sera za kibepari tangu wapate uhuru, jambo linalowapa uwezo wa kupambanua nani tajiri na masikini. Nchini Kenya ukiwa na viduka vya nguo hata kumi pamoja na vigari hata vitatu, kisha uwe na vinyumba hata kumi vya kupangisha bado unawekwa kwenye kundi la Jua kali, yaani watu wanaojitafutia maisha, na siyo matajiri. Tatizo la Tanzania ni kwamba Nyerere hakuruhusu matajiri wawe matajiri. Serikali inapowasumbua walalahoi wanaojitafutia maisha kwa kodi kibao, huo ni ukandamizaji.

Serikali yangu haitafanya hivyo. Sera za serikali yangu zitakuwa kuwaruhusu wananchi watajirike wawezavyo mradi tu wanafanya kazi au biashara halali. Matajiri wataruhusiwa kuchangia mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na ustawi wa jamii. Kodi zitatozwa kulingana na mapato ya wahusika na siyo njia ya kujipatia pesa za kampeni za uchaguzi. CCM weanafanya kila wawezalo kupata pesa za kuwanunua wananchi katika uchaguzi ujao. Lakini watashangaa kujua kwamba wananchi safari hii watapokea pesa lakini watachagua mabadiliko. Pesa siyo kila kitu, Msemo huo utakuwa na maana kubwa kwa CCM watakapowekwa BENCH.


Mwinjilisti Faustin Munishi
Hotuba Kwa Taifa
"Maovu ya CCM sasa basi"

CCM imeleta Jehanamu Tanzania. Watanzania watakaoingia Jehanamu, Itabidi Mungu awapunguzie ukali wa moto kwani tayari wameungua vya kutosha chini ya utawala dhalimu wa CCM. CCM ni wanyanganyi. Walianza kuwanyanganya wananchi mali zao wakitumia azimio la Arusha, na sasa Mkapa anatunyanganya mali akitumia ukusanyaji wa kodi. Anatumia TIN kama nambari 666 ya mpinga Kristo kutunyanganya mali zetu. Je Roho ya mpinga Kristo inafanya kazi ndani ya CCM? Kila dalili zinaonyesha hivyo.

Wananchi wapendwa yangu ni machache sana leo. Maisha yetu na watoto wetu ni muhimu kuliko chama chochote cha siasa. Hakuna sababu ya kuwa mwanachama wa chama cha kisiasa, wakati chama husika ndicho sababu ya kuharibika kwa maisha yetu ya sasa na baadaye. Nazungumza kuhusu CCM. Inasikitisha kuona kwamba wananchi Tanzania wameyazoea maovu ya CCM kiasi cha kukata tamaa ya kujikomboa.

Kwao maovu wanayofanyiwa ni kawaida iliyozoeleka, na hawaoni sababu ya kufanya chochote kujitoa kwenye makucha ya CCM. Niko hapa kuwapa sababu za kuanza harakati za kujikomboa. Tunataka ukombozi kwa sababu ni haki yetu. Lazima tujikomboe kwani tusipofanya hivyo hakuna atakayefanya kwa ajili yetu. Maisha yetu ndiyo yanayoharibiwa, kwa hiyo hakuna mhadhiriwa nambari moja kama mwananchi wa Tanzania. CCM inawatesa Watanzania, wengine inawaua kosa lao ni kusema CCM itoke madarakani kwani sera zake zimeiharibu Tanzania.

Maumivu Mateso Dhuluma Uonevu, na uchungu wote tunausikia, na mwisho wa kuvumilia umefika. Kifo mara nyingi huwa ndio mwamuzi kati ya uchungu na maumivu makali, huupumzisha mwili usiteseke tena. Tusipochukua hatua kwa kuogopa kuuawa, mateso na maumivu ya CCM yatafanya kile tunachokiogopa. Tayari yameua wengi, na wengi wako mbioni kufuatia mkondo huo.

Swali langu kwenu ni hili: Mnataka CCM iue wangapi ndipo mseme imetosha liwalo na liwe? Kwangu naona imetosha, SASA BASI. Liwalo na liwe, tutachukua hatua za haraka kujikomboa. Je tuchukue hatua gani? Kwamba tumefikia mahali pa kujiuliza swali hilo, hiyo ni hatua nzuri ya mwanzo. Nani anayeweza kusema kwamba mateso ya CCM hayajamhadhiri kwa lolote? Atakuwa anasema uongo. Kila Mtanzania mdogo kwa mkubwa, ameonja maovu ya CCM.

Siyo nia yangu kuamsha hisia zenu kinyume na CCM bali nia yangu ni kuwafanya muipende kiasi cha kuitoa madarakani. Kuitoa CCM ndani ya mawazo yenu ni rahisi kama ilivyoingia. Swali la kujiuliza ni Je CCM iliingizwaje kwenye mawazo na fikra zetu? Jibu lake ndiyo njia ya kuitoa na kuisahau. Sitaki tufanye kosa la kuitoa CCM kwa mbinu wanayoitumia kubaki madarakani. Tutakosea kwani tutakuwa tukifanya kile wanachokijua zaidi yetu. Kwa hiyo mawazo kwamba tutaitoa CCM kwa mtutu wa bunduki msahau.Tena hatuwezi kutumia chama kingine cha siasa kuitoa CCM, kwani hakutakuwepo na tofauti.

TUTAITOA CCM MADARAKANI BILA SIASA
" Siasa ni uongo, kwa hiyo hatuwezi kuutumia uongo kuwatoa waongo."

Siasa ni uongo, kwa hiyo hatuwezi kuutumia uongo kuwatoa waongo. Ndugu wananchi, asiwadanganye mtu. Hakuna siasa nzuri. Wanasiasa wote duniani mbinu zao zinafanana tofauti ni mahali mbinu hizo zinapotumika. Kwa hiyo rais wa Amerika hana tofauti yeyote na wanasiasa wetu hapa Tanzania sema kiwango cha uongo wanachotumia wanasiasa wa nchi zilizoendelea kinazidi kile kinachotumiwa na wanasiasa wa nchi zinazojaribu kuendelea.

Kifupi hakuna nchi iliyoendelea duniani.Kilichoendelea ni mbinu za kuwaibia wananchi walio wengi mali yao ambayo ni haki yao, na kuiingiza kwenye mkondo wa kisiasa ambao unalindwa na uongo pamoja na silaha kali. Kwa hiyo mbinu ya kwanza kuwatoa CCM madarakani ni kutambua kwamba wanasiasa wote duniani ni waongo. Pili ni kutokusikiliza uongo wao ambao hupeperushwa na vyombo vya habari kila siku. Ni vizuri mjue kwamba hakuna vyombo huru vya habari katika dunia inayoongozwa na siasa. Kwa hiyo someni habari magazetini, pia sikilizeni redio. Lakini mjue asilimia tisini ya yale mnayoona na kusikia kwenye vyombo vya habari ni takataka kama siyo uongo na mbinu za kuwafanya mnunue bidhaa. Kwa sababu wanasiasa wengi siyo waandishi wa habari, kazi hiyo hufanywa na wanataaluma hiyo kwa malipo.

Kwa hiyo hamtakosea kama mtasema kwamba waandishi wa habari wameshirikiana na wanasiasa kuifikisha hali yetu kimaisha ilipo. Uzuri wa waandishi wa habari, ni kwamba wanaweza kirahisi kurudiwa na fahamu zao, na kuwageuka wanasiasa na kuungana na sauti ya wanainchi. Tatizo ni kwamba walikuwa hawajui kama mnajua. Wakijua kwamba nimewaambia na mbaya zaidi wajue kwamba sasa mnajua yale waliyowaficha muda mrefu, watajikomba kuwaumbua wanasiasa. Hapo tuwe tayari kusikia mengi. Watakapogeukana hiyo ni furaha tele upande wetu.Tutakuwa tumempata msaidizi katika vita yetu ya kuwatoa CCM madarakani.

WANASIASA HUTUMIA VYOMBO VYA DOLA KUWANYANYASA WANANCHI "Kila inapobidi majeshi yote hutumika kulinda maslahi ya wanasiasa. "

Siyo rahisi wanasiasa warudiwe na fahamu zao, hasa ukitilia maanani kwamba wamezoea ukubwa na kutaka kuabudiwa kama 'miungu' wadogo. Kwa hiyo watatumia kila mbinu kubaki madarakani. Mbinu wanayoijua zaidi ni ile ya kutumia vyombo vya dola kama polisi na majeshi yote ya angani nchi kavu na majini, bila kusahau vikosi vya siri ambavyo hutumiwa kuwanyamazisha wapinzani.

KAZI IKO HAPA.

Wananchi wapendwa sipendi kuwaficha niwaambie kibarua kilicho mbele yetu ni rahisi. Nitakosea sana nikifanya hivyo. Jukumu langu ni kuweka wazi mbele yenu kila pingamizi tutakalokutana nalo, na kuwaeleza mbinu na njia sahihi ya kupambana na adui yetu. Majeshi yote yameundwa na wananchi wa TANZANIA. Polisi kwa lengo la kulinda mali zetu wananchi, na majeshi yale mengine wanasema lengo lao ni kulinda mipaka ya nchi yetu.

Hiyo ndiyo lugha wanayotumia wanasiasa kutuonyesha kwamba majeshi yako kwa ajili yetu wananchi kumbe ni kinyume chake. Kila inapobidi majeshi yote hutumika kulinda maslahi ya wanasiasa. Mnakumbuka yaliyowapata wananchi wa Zanzibar walipojaribu kuipinga CCM. Wananchi zaidi ya sabini walipoteza maisha yao, huku wengine wakikatwa viungo vya miili yao ili kuwafundisha adabu.

Yaani watanzania wako tayari kuua wenzao kwa ajili ya wanasiasa. Hiyo ndio kazi iliyo mbele yetu. Mjue kuna watu walio tayari kuua kwa ajili ya CCM na viongozi wake. Na tayari walifanya hivyo mchana jua linawaka bila kuogopa kamera za TV. Inataka moyo, lakini msisahau nguvu iliyo katika KWELI. Ukweli utatuweka huru mbali na wanasiasa waongo. Kweli ni NENO la Mungu ambalo ndiyo silaha yetu yenye nguvu zote.

TIINI MAMLAKA HATA CCM?
"Tuna haki na uhuru wa kuikataa CCM, na Mungu aliyetupa hawezi kutunyanganya haki na uhuru huo. Ni mali yetu, aliyetupatia ni Mungu na tumeamua kutumia haki na uhuru huo kuikataa CCM ya wauaji. "

Wacheni waje wakitumia silaha, sisi tutawakabili kwa NENO la Mungu. Kwa imani yote yawezekana kwa waaaminio. Imani yetu kwa Mungu tusikubali iyumbishwe na chochote. Siyo matisho ya CCM wala kejeli zao.Mara zote wananchi ndio wengi kuliko risasi zote CCM walizojilimbikizia. Sauti ya wengi ndiyo sauti ya Mungu.

Tukisema kwa sauti kubwa kwamba 'CCM CHAMA CHA MAJAMBAZI HATUKITAKI,' hiyo ndiyo itakayokuwa sauti ya Mungu. Na hakuna awezaye kushindana na MUNGU. Tuna haki na uhuru wa kuikataa CCM, na Mungu hawezi kutunyanganya haki na uhuru huo. Ni mali yetu, aliyetupatia ni Mungu na tumeamua kutumia haki na uhuru huo kuikataa CCM ya wauaji. Watakaopingana na uamuzi wetu kuikataa CCM, hao ndio watakaokuwa wakipingana na agizo la Mungu. Ndiyo watakuwa wameasi mamlaka ya Mungu. Kwa hiyo lazima waitii mamlaka yetu wananchi, kwani hiyo ameiweka Mungu mwenyewe. CCM iliwekwa na mtu mmoja, ni sawa ikitolewa na watu.

Walitudanganya kwamba wanafanya uchaguzi ili iwe kana kwamba iliwekwa na watu, lakini tumegundua janja yao.Maoni ya wengi hayajawahi kuheshimiwa katika uchaguzi wowote ule tuliowahi kuwa nao. Kwanza tulikuwa tukichagua nini kinyume cha nini? Uchaguzi lazima uwe kati ya Shetani na Mungu, na siyo kati ya shetani na mashetani. Chaguzi tulizowahi kuzifanya kabla ya vyama vingi vya siasa, zilikuwa kati ya Shetani na kivuli. Chaguzi tulizofanya wakati wa vyama vingi vya kisiasa, zimekuwa kati ya Shetani {CCM}na vijishetani {vyama vya upinzani} ambavyo navyo vitakua kumfikia Shetani mwenyewe. Sasa tunataka uchaguzi wa kweli. Tuchagua kati ya Shetani na Mungu. Duniani hakuna uchaguzi zaidi ya kuchagua MUNGU na Shetani. Hakuna kitu cha tatu wananchi msidanganyike.

GIZA NA NURU
" Msije mkanilaumu kwamba nilisema siasa ni dini ya shetani."

Dunia imekuwa na historia ya kupenda giza kuliko NURU, ndio maana wengi wanapenda siasa ambayo ni giza nene. Nuru ya injili sasa inaangaza duniani kote. Inatufundisha kuikataa siasa ambayo hutumiwa na shetani kuyatekeleza malengo yake ya kuharibu, kuchinja na kuua. Msije mkanilaumu kwamba nilisema siasa ni dini ya shetani. Lakini hata kama ulimi wangu ungeteleza niseme hivyo, ningekuwa nimekosea nini? Je sasa nimesema hivyo? Hapana. Nilichosema ni kwamba siasa ni chombo anachotumia sana Shetani. Hatuwezi kumkataa Shetani na kuikubali SIASA chombo anachokitumia. Tumkatae jongoo na mti wake. Wananchi! Siasa ni mbaya na hilo mnalijua fika. Wengi mtaniuliza nini mbadala wa siasa? Jibu langu ni KWELI. Neno la Mungu ndiyo KWELI.

UJAMAA NA UBEPARI
"Ujamaa ulisikika mzuri masikioni, lakini kwa sababu aliouleta alikuwa Nyerere mwanasiasa muongo, kila kilichovutia hakikutekelezeka."

Watu tofauti kwa nyakati tofauti wamekuwa na mawazo tofauti kuhusu mfumo gani unaofaa kumwongoza mwanadamu. Wengine waliufuata mfumo wa ukomunisti kama akina Nyerere, wakashindwa kabisa. Mbaya zaidi walitumia miaka zaidi ya 30 kuyajaribu mawazo yao ya ujamaa Tanzania. Matokeo yake yalikuwa kuiacha Tanzania ikiwa imeharibiwa na sera zao mbovu, na hata sasa hatuna sera kamili tunayoifuata.

Tanzania siyo mabepari wala siyo wajamaa kama alivyotaka Nyerere. Sisemi ubepari ni bora kuliko ujamaa, kwani sera zote hizo ni za kisiasa. Kwangu zote ni mbovu kwani zinakosa KWELI ndani yake. Ujamaa ulisikika mzuri masikioni, lakini kwa sababu aliouleta alikuwa Nyerere mwanasiasa muongo, kila kilichovutia hakikutekelezeka. Badala ya aliyeanzisha kukiri kwamba alikuwa amesema uongo, alitumia uongo mkumbwa kuutetea uongo mdogo aliouanzisha. Miaka ikapita na tulichoambulia watanzania ni umaskini wa kutisha.

Nyerere alitutaka tuamini kwamba dunia yote inapita kwenye matatizo kama yetu watanzania, na wakati huo huo polisi waliwakamata wananchi waliopatikana na sabuni, dawa za meno na mafuta ya kupikia kutoka Kenya. Ilikuwa ni sawa na kukamatwa na madawa ya kulevya. Wengi wakati huo tuilijiuliza: Ikiwa dunia yote ina mateso kama yetu, mbona hapa Kenya wao wanaogea sabuni? Tofauti na sisi tunaotumia maziwa ya mpapai kuogea? Tena mbona wenzetu wanatumia dawa za meno wakati Nyerere anaziita anasa? Kweli kuogea sabuni ya REXONA au kutumia dawa ya meno ya COLGET ni anasa? Nyerere mwanasiasa muongo alitutaka tuamini hivyo.

Wengi walimuamini na mpaka leo hawataki makuu. Waliukubali umaskini, na hawataki kuchukua hatua zozote kupambana nao. Japo Nyerere alisema adui zetu ni umaskini ujinga na maradhi, alitufundisha kuwapenda na kuwakubali maadui hao. Nasikitika kusema kwamba kuna watu waliomwamini Nyerere kinyume cha Amin wa Uganda. Waliomwamini Nyerere walikosea sawa na waliomwamini Amin. Watu hao wawili walileta madhara kwa nchi zao, lakini ya Nyerere Tanzania yalizidi.

Ninachotaka kusema ni kwamba mifumo yote ya siasa ilishindwa. Sasa tuufuate mfumo wa Injili ambao hauwezi kushindwa. Injili ni uwezo wa Mungu, sioni haya kusema Injili ndio mkombozi wa dunia. Itaikomboa dunia kutoka katika minyororo ya uongo ya wanasiasa. Lazima tuiamini Injili kama kweli tunataka ukombozi. Dunia ni ya Mungu na haiwezi kuongozwa kwa siasa za watu ambazo ni uongo. Dunia itaongozwa na KWELI ya neno la MUNGU.

WANASIASA NA MFUMO WA BIASHARA NCHINI
"Inasikitisha kuona wananchi ndani ya nchi yao wakiteseka, huku wanasiasa na wageni wachache wakimiliki njia zote kuu za uchumi."

Duniani kuna vita nyingi na tetesi za vita. Yote hayo ni matunda ya wanasiasa. Shetani anawatumia kuua na kuharibu maisha ya watu. KWELI imekuja ili tuwe na uzima, kinyume na shetani aliyekuja kuua. Utajiri wa dunia uko mikononi mwa wanasiasa. Mnajua ni kwa nini? Ili utajiri huo utumike kununua kila wanachokihitaji. Nanyi wananchi ni moja ya bidhaa ambayo wanasiasa hupanga kuinunua. Mnanunuliwa wakati wa kura ili kutia saini chaguzi ambazo washindi hujulikana kabla ya siku ya kura.

Hawataki mjiendeleze ili muwe rahisi kununuliwa. Ndio maana wengi wenu hamjiwezi kimaisha na hiyo haiwasumbui wanasiasa kwani wanapenda mbaki kama mlivyo ili wawatumie. Hata wale wanaojaribu kujipatia riziki zao za kila siku kwa kuanzisha biashara ndogo ndogo, bado wanasiasa hawaachi wafanye hivyo. Kila siku tume ya jiji hupewa kazi ya kuusafisha mji, na wafanyabiashara ndogo ndogo ndio uchafu unaotakiwa kusafishwa mijini. Siyo ajabu kwani huo ni mpango kamili unaolenga kuwanufaisha wafanyibiashara waliounganishwa kisiasa. Hawa ndio wale ambao hupewa tenda za serikali ili wagawane mapato na wanasiasa.

Kuna wengine wa asili ya kiasia ambao nao hupewa kumiliki maeneo yote muhimu ya kibiashara. Makubaliano ni kwamba mapato wayagawane na wanasiasa. Inasikitisha kuona wananchi ndani ya nchi yao wakiteseka, huku wanasiasa na wageni wachache wakimiliki njia zote kuu za uchumi. Hali hii haipaswi kuwa hivyo. Wananchi wanatakiwa wapewe uhuru wa kufanya biashara popote katika nchi yao. Udogo wa biashara usiwe ndio sababu ya kumsumbua mwananchi, kwani hata hizo biashara kubwa ziliaza zikiwa ndogo. Wananchi wanaoiamini KWELI wanatakiwa waruhusiwe kufanya chochote chema katika nchi yao.

Hali hiyo ndio itakayochochea ubunifu utakaopelekea kugunduliwa kwa vitu vingi kwa ajili ya maisha ya kila siku ya mwanadamu. Ugunduzi huo ndio unaoweza kuinua uchumi wa nchi husika kinyume na nchi nyingine, kwani "akili ni nywele na kila mtu ana zake." Na wale wanaogundua vitu, wanapaswa kulipwa sawa sawa na ugunduzi wao. Hapo taifa litakuwa limejitengenezea wanasayansi wake, wanaoweza kuvumbua vitu ambayo wengine hawana, na wakiviitaji taifa linapata pesa za kigeni kuinua uchumi wa nchi.

Sekta ya elimu nayo itakuwa imeboreshwa kwani elimu kwa watoto wetu itazingatia zaidi vitu tulivyogundua wenyewe, kinyume na elimu ya sasa ambayo misingi yake ni mengi yaliyofanywa na wengine, huku tukipima uwezo wetu katika kuyaiga. Ndiyo maana maisha ya waalimu katika nchi nyingi ni duni. Wanasiasa hufundishwa na waalimu, lakini kimaisha wametofautiana sana. Waalimu mishahara yao ni midogo sana kulinganisha na wanasiasa ambao kila kukicha hujiongezea mishahara na marupurupu mengi.

Katika nchi ambayo inaongozwa na KWELI bila siasa, waalimu ndio wanaotakiwa kupata mshahara wa kuwatosha kumudu maisha yao kama siyo uliowazidi wanasiasa. Hata kama watawazidi wanasiasa kimshahara kuna ubaya gani? Hilo ni swali tu. Msije mkasema niliwaambia mishahara ya waalimu izidi ya kila mtu. Lakini waalimu ndio humfundisha kila mtu. Sasa inakuwaje kila mtu anampita mwalimu kimshahara? Hapo nimetoka maana naona maswali hayaishi kichwani mwangu. Mengine mtajijazia wenyewe.

RAIS BILA WALINZI?
Watalinda nini wakati KWELI inajilinda yenyewe?

KWELI na uongo ni kama mafuta na maji. Huwezi kuvichanganya hata kama utajaribu kufanya hivyo. Kweli inajilinda yenyewe na haihitaji kulindwa na silaha kali. Uongo lazima ulindwe kwa kutumia silaha kali, kwani hawajui wale waliodanganywa wakierevuka watafanya nini. Ndio maana dunia nzima inafikiria kuhusu silaha kali kuliko chakula cha wanadamu wanaoikaa. Waangalie wanasiasa wanavyolindwa. Watu zaidi ya mia moja hawafanyi kitu kingine duniani ila kumlinda mwanasiasa.

Naheshimu kila taaluma ya mtu, lakini siwezi kumshauri yeyote awe mlinzi wa mwanasiasa. Kwa nini ufe kwa ajili ya uongo ambao hukuusema? Tena kwa mshahara gani basi? Yaani wenzio wako ndani wanakula vinono nawe unaungua jua nje? Sawa ni kazi yako. Unaipenda. Sina la kuongeza. Lakini ikiwa mimi ndiye nitakayekuwa kiongozi katika nchi itakayokuwa ikiongozwa na KWELI bila siasa, basi sitaki walinzi. Watalinda nini wakati KWELI inajilinda yenyewe?

Unamkumbuka mmoja wa wanafunzi wa Yesu aliyejaribu kufanya kazi ya kumlinda? Alikata sikio la mmoja wa askari waliokuwa wanamkamata Yesu. Aliambiwa aurudishe upanga wake kiunoni kwani YESU ni KWELI iliyotoka kwa Mungu na hakuhitaji kulindwa na mapanga au bunduki. Pesa wanazotumia wanasiasa kununulia silaha za kujilinda, zinatosha kumaliza baa la njaa duniani kote.

Yaani nina maana kila mtu duniani anaweza kula milo mitatu kwa siku. Tena chakula kizuri. Lakini pesa zote wanatumia wanasiasa kununulia silaha kali za kujilinda na wale waliowadanganya. Mwisho wao umefika. KWELI itawatoa madarakani bila kutumia silaha. Ole wao. Silaha walizojiwekea watazifanyia nini? Mbinu za vita zimebadilika. Hatutatumia mbinu walizozizoea.

Nguvu ya kweli ya INJILI itawakata makali yao. Injili ni NENO la Mungu ambaye ndiye KWELI yenyewe. Je wanasiasa watashindana, au kupigana na Mungu? Kila la kheri katika vita yao hiyo. Watatoweka mmoja baada ya mwengine. Hawatajua ilikuwaje, wala hawaruhusiwi kujua. Pesa na utajiri havitawasaidia wakati huo. KWELI haipimi uzito wa mtu kulingana na vitu alivyo navyo. Mtu ni mtu hata kama hana vitu. Mtu huunda vitu, lakini vitu haviwezi kuunda mtu. Vitu ni kwa ajili ya mtu, lakini siyo mtu kwa ajili ya vitu.

WANASIASA HUTUMIA DINI KUTAWALA
Makanisa mengi yameanzishwa na kufadhiliwa na wanasiasa kwa kwa lengo la kuyatumia kisiasa, wakati lugha yao ni kwamba chama na serikali havina dini.



Dini ni imani kwa Mungu wakati siasa ni imani kwa watu. Zote mbili ni itikadi zinazohitaji watu kufanikisha malengo yao. Ndio maana nawataka watu wa dini zote tuungane pamoja kuitoa siasa madarakani. Suala kwamba dini gani itatawala hilo lisitusumbue kwa sasa. Muhimu ni wote tutambue kwamba wanasiasa wanatutumia vibaya. Baada ya kutambua hayo tuachane kabisa na siasa. Kitakachofuata ni kila dini inayowania uongozi kujitokeza hadharani na kutangaza nia yao ya kutaka kuongoza. Wananchi wa dini husika, pamoja na wale wasio na dini, bila kuwasahau wale wa dini nyingine watakaoamua kujiunga na dini yenye sera nzuri kutoka kwa Mungu, Watachagua dini gani iongoze kwa kipindi kilichozoeleka cha miaka mitano.

Baada ya miaka mitano tutachaguana tena. Pamoja na kwamba kila dini itakuwa na katiba yake, lakini lazima tuwe na katiba moja ya pamoja. Nayo ni ile itakayozingatia Imani kwa Mungu ambayo ndilo lengo la kila dini. Pamoja na kwamba dini fulani itachukua uongozi kwa kipindi cha miaka mitano, bado kila dini itawakilishwa katika baraza la makuhani ambalo ndilo litakalohusika na kuhakikisha kwamba amri kumi za Mungu zinafuatwa kikamilifu. Kwa hiyo hofu kwamba kutatokea michafuko ya kidini msahau kabisa. Badala yake dini zote zitaingia katika ushirikiano ambao haujawahi kuonekana tangu kuumbwa ulimwengu. Bado kila dini itakuwa huru kuendelea kufanya mambo yake yenyewe, bila kuomba kibali kwa wanasiasa kama ilivyo sasa.

Hakutakuwepo na makanisa ua misikiti inayodhaminiwa na serikali. Makanisa mengi yameanzishwa na kufadhiliwa na wanasiasa kwa kwa lengo la kuyatumia kisiasa wakati lugha yao ni kwamba chama na serikali havina dini. Mambo yako hivyo karibu kila dini. Inasikitisha kuona kwamba wengine wanafikia mahali pa kudanganya kwamba watu wamepona kwenye mikutano yao ya kidini, kumbe ni waongo. Tayari tumewangundua kuwa ni wapambe wa CCM. Wanalindwa kama wanasiasa na huku wanajiita maaskofu. Wanatembelea magari ya kifahari na huku waumini wao ni masikini wanaodanganywa kwamba wakitoa watabarikiwa. Tayari viongozi wa dini wanawasaidia wanasiasa katika kuendeleza ukandamizaji na uonevu kwa waumini wao, ili mradi tu waitwe ikulu na wapewe magari na pesa. Hawana tofauti na wanasiasa tunaotaka kuwatoa madarakani. Kweli ya Mungu ni taa. Ikiwamulika, matendo yao yataonekana na kila mtu. Hawa ndio watakaokwenda pamoja na wanasiasa wakati dini ya kweli itakapochukua madaraka.


MAUAJI YA KISIASA SIRI YAFICHULIWA

Wanasiasa kwa makusudi wameziharibu taasisi zote. Duniani taasisi zote hufanya kazi kwa ajili ya wanasiasa. Nchi zilizoendelea wameendelea katika kujaribu kuficho hilo lakini nchi zetu jambo hilo liko wazi. Kwamba wana mbinu kali za kulificha, haiwatofautishi na wenzao katika nchi zinazoendelea. Inabaki kwamba kila taasisi duniani inalinda maslahi ya wanasiasa kwanza. Mahakama mara nyingi zinaonekana kupindisha ukweli, hasa pale ambapo mwanasiasa anahusika. Hebu fikiri kuhusu gari lililotekwa nyara katikati ya mji.

Watekaji wanamlazimisha mwenye gari kuliendesha kuelekea wanakotaka. Baada ya safari ya kama kilomita mbili hivi, wanaacha gari la kwanza baada ya kulizinga jingine kwa mbele. Mwanye gari la pili anapigwa risasi na kuuawa hapo hapo baada ya kisichojulikana kuendelea kati ya watekaji na yeye. Wanayaacha magari yote mawili hapo baada ya kumwamuru mwenye gari la tatu kutoka ndani ya gari lake na kuwapa funguo. Wanaondoka na gari huku wakiwaacha wenye magari wote mahali pamoja, lakini mmoja ni marehemu na mwingine amebaki bila gari.

Baada ya dakika kama tano hivi, Polisi wanawasili mahali hapo. Wakiwa katika kuwahoji wenye magari wawili, waandishi wa habari wa magazeti TV na Redio wanawasili mahali pa tukio. Usijali wataulizana nini hapo, lakini sikiliza redio na utizame TV jioni, halafu usome magazeti asubuhi yake. Utakayemsikia akitajwa kwamba aliuawa na majambazi waliojaribu kumpora gari, ndiye aliyekuwa amelengwa na taaluma zote hizo. Yaani habari yenyewe itasomeka hivi. MAJAMBAZI WAMUUA BWANA XXXX Aliyekuwa mhubiri wa INJILI bwana XXXX amefariki dunia baada ya majambazi kumfyatulia risasi.

Wakiongea katika sehemu ya tukio, bwana JJJJ na bwana SSSS walisema kwamba walishuhudia majambazi wakimfyatulia risasi bwana XXXX baada ya mvutano ulioonekana kama Bwana XXXX alikataa kuwapatia majamabzi fungua za gari lake. Wakisimulia saidi kisa hicho, walisema kwamba walisikia mlio wa risasi mara mbili, na baadaye majambazi walitoka kwenye gari la huyo aliyekuja kujulikana baadaye kama Bwana XXXX. Walimwamuru Bwana SSSS atoke kwenye gari lake na awape funguo. Alitii, na majambazi waliondoka na gari lake ambalo mpaka sasa halijapatikana. Kwa sababu vyombo vyote vya habari vimelipa uzito suala hilo kwenye kurasa zao za kwanza, wananchi wanaiamini hadithi hiyo. Ndiyo lengo lilikuwa ifanyike hivyo ili wananchi waaminishwe uongo. UKWELI wa mambo ni kwamba bwana XXXX alikuwa mlengwa kwenye sakata yote hiyo.

Kuna mtu aliyejua kwamba atapitia barabara hiyo saa hizo baada ya kutafiti nyendo zake kwa zaidi ya miezi mitatu. Taasisi zilizotumika kuwadanganya wananchi nazo zilihusishwa wengine wakijua na wengine bila kujua. Walioporwa magari yao ndio ambao hawakujua nini kilichokuwa kikiendelea. Ilikuwa hivi: Bwana XXXX aliwaudhi wanasiasa kwa kujaribu kuwaambia kwamba wanasiasa hawawatendei mema wananchi walio wengi. Walipochukizwa naye wakaamua kwamba atauawa. Pesa nyingi zikatolewa kwa ajili ya kazi hiyo. Walitakiwa watu kutoka katika taasisi mbili nyeti. Polisi na vyombo vya habari vilitosha kukamilisha zoezi zima.

Kachero mmoja wa polisi alitumika kuzijua nyendo zote za Bwana XXXX, halafu mkuu moja wa kituo cha polisi alitakiwa kuwatoa vijana ambao watafanya kama wafanyavyo majambazi. Na huyo huyo ndiye aliyetakiwa kuvipigia simu vyombo vya habari kuviarifu kuhusu tukio, na jitihada zao za kuwafukuza majambazi.

Lengo likiwa kutekeleza mauaji ya kisiasa, na kuyafanya yaonekane kama ujambazi wa kawaida. Walikosea. Kwanza hakuna ujambazi wa kawaida. Kwamba kuna ujambazi hiyo inaonyesha kushindwa kwa wanasiasa kuwalinda wananchi pamoja na mali zao. Pili: Kwamba wanamuua mtu kwa sababu tu amewakosoa chama tawala CCM huo ni wendawazimu nambari ONE. Wananchi mfano huu unaonyesha jinsi wanasiasa wanavyoweza kuzitumia taasisi kuyaficha maovu yao. Hii ni siri iliyofichuliwa katika mijadala ya Internet huko BCSTIMES .COM baada ya siri hii kufichuliwa na mtu aliyejiita AISHA AIESHI. Unaweza kujisomea mwenyewe kisa hicho kwa KUBONYEZA HAPA. Kuna matukio mengi ya zamani na hivi karibuni yanayofanana kabisa na mfano huu. Mauaji ya watu zaidi ya sabini kule Zanzibar, Kifo cha SOKOINE aliyekuwa waziri mkuu wakati wa Nyerere. Kifo cha KOMBE aliyekuwa mkuu wa kikosi cha usalama wa taifa wakati wa Nyerere, na wengine wengi.


Mchungaji Faustin Munishi ambaye pia ni mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Afrika ya mashariki na kati, ametangaza azma yake kuwania kiti cha urais Tanzania katika uchaguzi ujao. Mengi yamesemwa kuhusu hatua ya mchungaji huyo, na hapa ni sehemu ya mjadala katika mtandao. Inasemekana serikali ilikuwa imeufungia mjadala huu usiweze kusomwa na Watanzania. Gazeti la Injili kwenye internet linakuletea mjadala huo bila kuhariri chochote.

SASA BASI INATOSHA

Ndugu wananchi yangu yalikuwa hayo machache. Msimame imara, wala msikubali kuyumbishwa na hawa wanasiasa. Mkatae kabisa mbinu zao za kutaka kuendeleza maovu yao kwa kuachiana viti. Nyerere alituachia MKAPA ili alinde madhambi yake.Naye Mkapa anataka kutuachia sijui nani ili alinde madhambi yake. Watalindana mpaka lini? Mwisho wao umefika.Sasa tunataka dunia isiyo na kitu kinachoitwa SIASA.

Wametudanganya vya kutosha, wakatuibia vya kutosha sasa tunataka KWELI ya neno la Mungu iongoze Tanzania. Mungu ni pendo na anaipenda Tanzania ndio maana amenituma mtumishi wake kuwaletea ujumbe huu. Msijali kufurukuta kwao kwani wangefanyaje nao wanakata roho? Watawapeleka kwenye madanguro yao kuwatesa lakini msikate tamaa. Watatumia kila mbinu ikiwepo ya kuwafungulia kesi za uongo, msijali kwani hayo yote hayana budi kuja. Nguvu ya dola ni ndogo sana ukilinganisha na nguvu ya wananchi wamoja.Umoja wetu na imani yetu kwa Mungu ndiyo silaha kubwa ambayo kila mmoja wetu lazima awe nayo.

Watahangaika kujua nani anayetupa nguvu tulizo nazo, lakini jibu watakalolipata litawarudisha hatua mia tatu nyuma. Wataanzisha magazeti kwa lengo la kuueneza uongo wao lakini watagonga mawe kwani wananchi tumeyashitukia magazeti ya hivyo. Watatumia pesa walizoiba kwetu kutununua kwazo, nasi tutatumia pesa bila kuwaunga mkono.Pesa ni zetu. Zikirudishwa hatuachi. Tutazitumia. Tuanze mara moja zoezi la kuchoma moto kadi za vyama vya kisiasa. Sisi ni waumini wa dini na hiyo inatutosha. Hatuwezi kuamini katika dini mbili, yaani siasa na INJILI. Moja ni ya shetani na nyingine ni ya Mungu.Sisi tumeamua kuwa upande wa Mungu. Mungu hawezi kutuacha watoto wake tuteswe na siasa za yule mwovu.

Hatua ya kwanza tutakayoichukua kuelekea ukombozi, Mungu atachukua hatua mia moja kutulinda na CCM pamoja na wanasiasa waovu. Mara zote Mungu hafanyi chochote kutulazimishia matakwa yake. Lakini tunapoamua kwamba tutaifuata njia hii, na kisha tuombe baraka na ulinzi kutoka kwake, mara moja Mungu hutujibu maombi yetu kwa kuanza kutulinda na kutupa ufunuo zaidi. Nilipochukua kalamu kuanza kuandika haya, ndipo ufunuo wote huu uliponijia kutoka kwa Mungu. Ningengoja ufunuo kwanza ndipo niandike, pengine mpaka mwaka 2080 ndipo ningepata ufunuo huu. Ni muhimu sana kutilia maanani ujumbe huu. Huwezi kuusoma popote kwani lengo kubwa la serikali ni kuwazuia wananchi kujua. Wanajua kwamba mkijua mtawauliza maswali wasiyopenda kuulizwa. Wana mengi ya kuficha na anayejaribu kuyafichua ni adui wao nambari moja. Kama hawatammaliza kibiashara au kisiasa, basi watapanga njama za kuutoa uhai wake. Wameuawa wengi ndiyo maana hatuchukulii kama mzaha matisho yao ya kuua. Bonyeza hapa usome yale waliyokusudia kumfanyia mwandishi wa hotuba hii.[/B][B]



Hii pia ni moja ya Kanda mpya ya video katika VCD. Ndani yake kuna vichekesho vya kuvunja mbavu. Bwana Godfrey Gathena Kuniara maarufu kwa jina la kisanii Ole Soipei ndiye msanii katika kanda hii.Usiikose.

Hapa kuna VCD mpya ya Waciama. Nyimbo ni kwa lugha ya KIKUYU. Picha pamoja na kuhariri vimefanyika Gospel Television.Utaipenda.

Jiandikishe Hapa
Hata kuishi Amerika ni haki yako

 
| http://munishi.com |