![]() ![]() |
![]() |
|
|
Gazeti
INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com Or fmunishi@hotmail.com
Askofu
Kulola huipigia debe CCM
Kulola Amtimua Mchungaji Arusha Na Mwandishi Wetu Arusha Aliyekuwa Askofu wa jimbo katika kanisa la EAGTkatika mtaa wa Elerai Arusha Mchungaji Jackson Peter, amejiengua kutoka kanisa hilo na kuanzisha kanisa jipya. Sababu? Bado hicho ni kitendawili ambacho wanaoweza kukitegua ni askofu mkuu Moses Kulola na yeye mwenyewe mchungaji J.K.Peter.
Askofu Jack ambaye pia alikuwa akisimamia kanisa la Elerai mjini Arusha amelihama kanisa hilo katika mazingara ya kutatanisha. Washirika waliohojiwa na gazeti la mtandao walisema kwamba mchungaji aliamua kuachia ngazi baada ya kutokuelewana na uongozi wa kanisa hilo,huku wengine wakisema kuwa ameachishwa kazi na uongozi wa kanisa hilo kwa sababu zinazojulikana na uongozi wa kanisa hilo la EAGT. Kanisa la EAGT linaongozwa na Askofu mkuu Moses Kulola, ambaye hakuweza kupatikana mara moja kukanusha au kukubaliana na habari hizi.Juhudi za mwandishi wa habari hizi kujaribu kumpata Askofu kulola hazikuweza kufanikiwa kwani kila mara alipopiga simu aliambiwa hawezi kuongea na Mtumishi wa Mungu kwa wakati huo. Naye mchungaji Jackson Peter hakuweza kupatikana kukanusha au kukubaliana na habari hizi. Lakini watafiti wa wa habari katika makanisa wanasema kuwa, mambo ndani ya EAGT siyo mazuri kwani kuna baadhi ya wachungaji ambao hawapendezwi na hatua ya kiongozi wa kanisa hiloBishop Kulola kumtawaza mtoto wake Dani Kulola huduma ya uinjilisti, na kuwasahau wengine ambao wanafikiri kuwa wanaweza kuliko huyo anayetawazwa.Kwamba hiyo ndiyo sababu iliyomfanya mchungaji Jackson Peter aachie ngazi, tunasubiri kusikia kutoka kwa Bishop Kulola.
Kutoka kwa Mhariri . Bado Hatujasikia kutoka Kwa askofu Kulola, Lakini wasomaji wameanza kutoa maoni yao. Yafuatayo ni maoni ya wasomaji kama walivyoyaandika. Gazeti la mtandao halihariri maoni ya wasomaji bali huyatoa kama yalivyoandikwa. EAGT Dodoma Kunafuka Moshi watu wanahoji uko Dodoma kuhusu kanisa la E.A.G.T kuwa kuna mch. wa uko Dodoma eneo la Makole anatuhumiwa kuzaa nje ya ndoa na kuna vikao vinaendelea kama atengwe au namna gani. Ambacho watu watu wanahoji ni kwamba kucheleweshwa kwa hukumu kunatokana na sela ya upendeleo ambayo imeligubika kanisa hilo. Habari tulizopata hapa nikwamba askofu mkuu anamtetea huyo bwana kwa sababu wanahudumu naye. Yeye ndie anaye pambisha pambio za kushusha utukufu. Hofu ni hii kuwa kama askofu atakubari atengwe italeta maswali kuwa kama amekuwa anahudumu kwenye mikutano ya bishop je Bishop hana macho kiroho mpaka huyo mtu amedumu katika dhambi ya kupelekea kuzaa mtoto nje ya ndoa. Na wangine wanahoji kuwa kama Akina Mwasumbi alitupwa nje na Mwasota kwa nini pia Huyu asishugulikiwe. Ninaendelea kulifuatilia jambo hili ingwaje ni kazi ngumu kidogo kama unavyojua wa EAGT ni wapole kama mzee kulola kila unapohoji jambo wao hunyamaza kimya na kukuambia kwa kweli sijui. Lakini hizo ni habari ambazo tumepata
nje ya kanisa hilo ila kutoka kwa watu wa karibu sana na huyo Mch.
kama unavyojua wachungaji hupenda kushirikisha watu wanao waamini
juu ya majaribu yao ili wawaombee wanasahau kwamba wale wanowaamini
nao wana watu wao ambao ndio sisi.
Ndugu Lemomo Amlaumu Mhariri wa Gazeti la INJILI Name: Joseph lemomo
Mwinjilisti Mwazembe Amtetea Rev.Kulola Name: Leonard S. Mwazembe
Nimepitia habari kadha katika gazeti la mtandao la injili ila napenda kutoa maoni yangu kuhusu kufukuzwa kwa mch arusha. Ni kweli inawezekana kutofautiana maono lakini zipo njia nzuri za kiblia za kuachana zenye kumpa Mungu utukufu. Mf.wa Paulo na Banaba pia Rutu na Ibrahimu hawa waliachana kwa utukufu wa Mungu na wengi ne wengi. Ningependa pia kusema kama sio kutofautina maono ila ni kwa sababu tu za kibinadamu basi hatari. Ninasema za kibinadamu kwa sababu tayari nasikia wengine hawaridhiki na kuteuliwa kwa mtoto wa askofu kuwa mwinjilisti Tufahamu kua uinjilisti sio cheo wala sio biashara ni wito wa kuwafikia wenye dhambi ambapo kibiblia wote tuliookoka tumeitwa kuufikia ulimwengu wa wenye dhambi. Sasa sioni shida mtoto wa askofu kuchukua nafasi ya kutangaza injili ya ufalme na kama watu wanaokoka na wewe unampinga hiyo ni roho ya dini. Mwaka huu nilikuwepo kwenye mkutano wao wa pasaka alihubiri mtoto wa askofu na watu wengi waliokoka na wengi kufunguliwa kutoka katika nguvu za giza je hiyo sio baraka? Na unapo pinga hiyo kazi tukuite nani? Inakupasa ujifunze kwa wanafunzi ambao walitumwa na Bwana Yesu wakakuta mtu mwingine anafanya kazi ile ile ambayo wao walijiona wanafaa kuifanya wakamzuia Bwana akawambi msimkataze asiye kinyume chenu yuko upande wenu. Mimi nasema hivi huyo mtoto wa askofu yuko upande wao
na kama wakimpinga basi wanitumikia dini au shetani maana dini na
shetani ni mke na mume kazi yao kubwa ni kupinga injili ya wokovu
na nguvu za Mungu. Pili injili sio mashindano kuwa nani zaidi sio simba na yanga. namtia moyo mtumishi wa Mungu Dan Pamoja askofu Kulola asitishwe na mawazo ya kidini. Hata Musa wa biblia alitumwa na ndugu zake wa tumbo moja Miriamu pamoja na Haruni Kut 7:7. Sasa hiyo sio sababu ya mtu kuhama kama ni moja wapo. Kubwa ya kibiblia iwe ni kutofautiana maono ambapo lengo liwe ni lile lile la kumtwanga shetani. Mungu awabariki sana popote ambapo maoni haya yatawafikia. Mwinjilisti Mwazembe Dar Bwana Mwakipesile Ampinga Mwazembe Name: Mwakipesile Ndugu Mwazembe!! Pengine wewe ni mgeni hapa Tanzania na hulijui vizuri kanisa la EAGT. Kulola ndiyo EAGT na EAGT ni Kulola. Naweza kuliita kanisa linalojihusisha na kulinda maslahi ya mtu mmoja. Waangalie wachungaji hasa wa Mbeya.Hali yao kimaisha inatisha. Lakini mwangalie Kulola. Michango yote ya kanisa nchi nzima ni yake.Akija kwenye mkutano atazikandia pesa na kusema kuwa hazipendi. Baada ya mkutano, sadaka yote anakabidhiwa yeye. Bila kusahau vitenge wanavyonunua walala hoi kumpa mke wa Kulola.
Kwa ujumla hali ya washirika wa kanisa la EAGT haiwezi kufananishwa na hali ya maisha ya askofu wao. Hatusemi wafanane kabisa, lakini ionekane kidogo wanajaribu kuinuka kimaisha.Miaka nenda miaka rudi washirika wanalipishwa michango ya kuufanya mkutano wa kulola ufanikiwe kuwakusanya watu ambao watakuja kutoa michango mingine. Siyo vibaya kufanya mikutano ya Injili,lakini mikutano ya Kulola haiwalengi wenye dhambi, bali wale ambao tayari wamekwisha amini tayari. Nasikitika kusema kwamba hata wanaojifanya kulia pale mbele ili kuleta hisia kwamba mapepo yanawatoka, ni waumini wa kanisa hilo ambao wengi wao huwa wanazililia shida na matatizo ya maisha na siyo mapepo.
Hakuna maana ya kuwakusanya watu na kuwafanya walie,halafu uwachangishe pesa na kuwaacha katika hali ile nile ya umasikini wa kutupwa. Safari zote za Kulola hutumia ndege kutoka mkoa huu kwenda mwingine na inasadikiwa kuwa kanisa hilo lina uhusiano wa karibu sana na chama kinachotawala CCM.Linatumiwa na serikali kulinda maslahi ya serikali. Moses Kulola mwenyewe ni CCM Damu.Anawakemea wote wanaoikosoa serikali na kusema wanachanganya siasa na dini.Ukweli ni kwamba WANAOKUBALIANA NA MAOVU YA SERIKALI NDIO WANAOCHANGANYA SIASA NA DINI. Ndugu Mwazembe fanya utafiti kuhusu EAGT na utagundua kuwa ni kanisa la kikabila na Wasukuma ndio wanaoliona kama ni kanisa lao.Pamoja na kwamba sisi Wanyakyusa tupo,lakini hatusikiki.Mtu wetu akijaribu kuinuka kidogo Wasukuma wanamwambia Kulola amtupe nje ya Kanisa.
Mfano ulio Hai ni Mchungaji Emanueli Mwasota ambaye pamoja na kwamba alimsaidia Kulola sana wakati wa mwanzo, sasa Kulola amemsahau na kumtupa nje.Mwingine ni Mwasumbi. Naye yuko nje.Cha ajabu ni kwamba Kulola bado anawakandia kwa nguvu zote ili hata huko waliko waonekane kama wenye dhambi na Kulola aonekane Mtakatifu kuliko wote Tanzania Mwakipesile Mbeya Mwazembe Ajibu Mashambulizi Name:
Rev Mwazembe L.
Ev.And Gospel Singer Faustin Munishi |
||||||||||||
|
|
|
|