-
“Injili”ni
gazeti linalohubiri maneno ya Mungu kwa watu wa dini zote na pia
kwa wale ambao hawana dini. Gazeti hili huandikwa na kuhaririwa
na Mwinjilisti na mwimbaji wa nyimbo za Injili Munishi F. Munishi.
-
Zifuatazo
ni sera au kanuni za gazeti letu “Injili.” Tunaamini ya kwamba
Mungu ni mmoja mwenye nafsi tatu yaani Baba Mwana na Roho Mtakatifu.
Tena tunaamini kwamba kuna Mbingu na jehanamu kwamba Mbinguni
wataingia Watakatifu na jehanamu wenye dhambi.
-
Tunaamini
kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu aliyetumwa ulimwenguni kuwaokoa
wenye dhambi ambao wa kwanza wao ni waandishi na wahariri wa gazeti
hili. Kwamba yeyote atakayemwamini Yesu Kristo na kuzitubu dhambi
zake ataokolewa na kuwa na hakika ya wokovu akiwa hapa hapa duniani.
-
Pia
tunaamini kwamba Yesu akiwa Mungu alizaliwa kama binadamu na Bikira
Maria akateswa, akafa akafufuka siku ya tatu kama yanenavyo maandiko,
akapaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Baba akituandalia
makao, na atarudi tena kutuchukua.
-
Gazeti
la “Injili”linaamini kwamba kila mtu ana haki ya kuamini dini
anayoitaka, na kwa kuheshimu haki hiyo gazeti hili halitakashifu
dini yeyote, bali litamfundisha kila anayetaka imani ya Mungu
kwa kupitia kwa Yesu Kristo, na Injili kama ilivyoandikwa katika
Biblia msahafu ambao gazeti hili linauamini.
-
Kwa
upande wa siasa tunaamini kwamba Injili na siasa ni vitu viwili
tofauti ambavyo haviwezi kuchanganywa,kwani Injili ni maneno ya
Mungu na siasa ni maneno ya mwanadamu. Vitu hivyo viwili ni kama
mafuta na maji havichanganyikani.
-
Isitoshe
tunaamini kwamba Mungu alimuumba Mwanaume kwanza na baadaye Mwanamke
si kwamba mmoja ni bora kuliko mwingine, lakini makusudi ya Mungu
ni kwamba. Mwanamke atabaki kuwa mwanamke, na Mwanaume vivyo hivyo
atabaki kuwa Mwanaume.
-
Upande
wa sayansi na nishati, Injili inaamini kwamba dunia pamoja vyote
vilivyoko ni mali ya Mungu na vilifanyika kama Biblia ianvyosema,
na siyo kama wanasayansi wanavyosema.
-
Tena
wanadamu wote ni sawa machoni pa Muumba bila kujali rangi Dini
au Nishati na utajiri wa nchi fulani. Na kwamba mali zote za dunia
hii zitufae sisi sote,siyo wengine wawe wadaiwa na wengine wanaodai
kana kwamba mali hizo walizipata kwenye sayari nyingine ambayo
haikuumbwa na Mungu Baba yetu sisi sote.
-
Na
hii ndiyo imani yetu kwamba dunia itaongozwa na amri kumi za Mungu,
na siyo amri kutoka kwa matajiri wa dunia hii ambao utajiri wao
mbele za Mungu ni ubatili mtupu. Kwani Utu wa Mtu haupimwi na
vitu maana Mtu ndiye hufanya vitu na siyo vitu kumfanya Mtu awe
Mtu. Kwa maneno mengine Mtu ni Mtu hata kama hana vitu.
-
Na
mwisho tunaamini kwamba imani ya Mungu huja kwa kusikia au kusoma
Injili ya neno la Mungu. Na ya shetani pia huja kwa kusikia au
kusoma vijigazeti vinavyoandika uongo wa shetani.
-
Dunia
imesikia mabaya, ikaamini mabaya na ndio maana inatenda mabaya.
Gazeti la Injili linataka dunia isikie maneno ya Mungu, iamini
mazuri,na mwisho itende mazuri.
Ni
matumaini yetu kuwa gazeti la Injili litakuwa chaguo lako.
Hayo
ndiyo maono yetu, mwanzo wa kila kitu huwa mgumu, lakini kwa sababu
tumethubutu kuanza tunaamini tutaendelea. Tuombee,na utusaidie kwa
hali na mali.
Anwani
yetu ni, Injili S.L.P. 11213. Simu 224092 Nairobi Kenya. Na nambari
yetu ya Fax ni 224092 Nairobi.Mungu akubariki na tunatarajia kusikia
kutoka kwako. Mhariri wa injili Munishi.