![]() ![]() |
![]() |
|
Rev. Kulola amtimua Mchungaji Arusha. Study The Bible Nation Yasema Kenya Imekosea kutangaza msimamo haraka Kwa Nini Waislamu wanalalamika? Maombi
Ili Mungu Aiangushe |
http://munishi.netfirms.com
Tell.254-72-602445
Gospel tape banned by Dar officials
Moi
Aombewa Amalize Vizuri Rais Daniel Toroitich Arap Moi Na Mwinjilisti Faustin Munishi Kanisa la CBC Kenya yaani Christian Brotherhood Church limeanza maombi maalum kumuombea Rais Moi ili amalize ngwe yake vizuri. Pamoja na kumuombea Mheshimiwa Rais kanisa hilo pia litawaombea wakenya kwa ujumla ili wapite katika kipindi hiki cha mpito salama bila umwagikaji wa damu. Hayo yalitangazwa na askofu mkuu wa kanisa hilo Geofrey Litunya Buliba kwenye makao makuu ya kanisa hilo huko Nakuru. Bishop Buliba aliwataka wakenya kuwa watulivu na kuachana na uvumi kwamba kutatokea machafuko Moi akiondoka madarakani.
"Mungu alitupa Moi baada ya Kenyatta, Bado atatupa mwingine baada ya Moi." "La muhimu ni wakenya tumuombe Mungu kwa bidii ili atupe kiongozi hasa yule anayemcha Mungu." Aliongeza kusema kuwa kila kitu kina wakati wake duniani. Ilimpendeza Mungu tuongozwe na Moi kwa kipindi chote hiki, na sasa ikimpendeza Mungu atatupa kiongozi mwingine. Askofu Buliba aliwataka wakenya wayatupie macho mazuri ya Moi ambayo ni mengi, kuliko kuyaangalia mabaya yake ambayo ni machache. "Hakuna mwanadamu aliye mkamilifu aukose ubaya katika maisha yake. Na Moi ni mwanadamu kama wale wengine." Askofu huyo alimaliza kwa kusema: "Tumeanza Maombi ili Mungu atupe kiongozi, lakini hatuombi tupewe malaika ila mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke.Kile tunachotaka ni mcha Mungu ambaye atajirudi haraka akikosa, kuliko yule anayeyatetea makosa kwa kufanya kosa.
Huyo hatumtaki na ndiyo maana tunamuomba Mungu atuangazie mwanga ili tumpate mtumishi wake atutumikie na sisi.Hatutaki mtawala, bali tunamtaka kiongozi.Atuongoze katika kila jambo. Akisema tusiibe, aongoze kwa kutokuiba. Akisema tujihadhari na ukimwi, aongoze kwa mwenendo mwema. Akisema tuwe wasafi, aongoze kwa kuwa msafi wa mwili na mavazi. Akisema tuwasaidie masikini, naye awe anaongoza kutoa ili kuwasaidia wasiojiweza katika jamii. Akisema tufanye kazi kwa bidii, naye awe kielelezo kwa kufanya kazi kwa bidii. Moi aliongoza katika hayo yote ndiyo maana tunakuomba mwingine kama au wa kuzidi Moi, lakini siyo wa kiwango cha chini ya Moi. Alimaliza Askofu huyo. |
Nyerere Msingi aloujenga Haufai Tuubomoe? Marandu T.L Ajitoa Kwenye "FORUM" Majira Wajaribu Kumzima Munishi? Taliban Wamefanya Kiungu, Amerika walifanya kishetani WorldSpace
Hawajui Wamlenge Nani Gospel tape banned by Dar officials Rodnat Mwenda Ashambulia Munishi Majambazi Wamvamia Munishi Nyumbani Free
Translation |
|||||||||||
|
|
|
|