Ukurasa wa mbele
Gazeti la injili
Nyimbo za Munishi
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail
Tuma SMS duniani
Sema nami
Sikiliza waongo
Twende kanisani

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Gazeti INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com
Or fmunishi@hotmail.com

Siasa na Dini Zitenganishwe?
Ni kweli Serikali hazina dini?

2

 

Munishi: "Jamani Tutenganishe"
Kuna msemaji mmoja amesema DINI ni chama. Sasa maoni yangu ni kwamba mtu awe mwanachama wa chama kimoja tu. Yaani kama ni muumini wa dini basi asiwe mwanachama wa chama cha siasa.

Ili wanasiasa watafute watu wasio na dini wawe wanachama wao. Wakiunda serikali waseme haina dini. Hakuna atakayewapinga kwa hilo. Kwa sasa hawawezi kusema serikali haina dini, maana waliounda serikali ni watu na dini zao. Na hawajawahi kuzikana dini zao. Kwa nini serikali inawasaidia kukana kwa niaba yao?
Wewe Unasemaje?

Pope asema "Hapana"

waliounda serikali wana dini zao binafsi lakini unaposema kuwa serikali ina dini ni kuwa labda imo chini ya dini fulani labda uislamu kama Misri au Ilivyokuwa Afghanstan au ilivyo Vatican lakini hii ya kwetu ina WAUMINI WA DINI TU ILA SERIKALI HAINA DINI WAL HAIFUATI DINI YEYOTE.....
Wewe Unasemaje?

Munishi asema "Hapana"
Sina maana hiyo ila serikali haiwezi kusema haina DINI Labda waseme serikali ina dini zote za waliounda serikali hapo nisingekuwa na utata.
Wewe Unasemaje?

Pope afurahia ushindi

BASI INAWEZEKANA TATIZO HAOPA NI LUGHA NA SIO UELEWA . TEH TEH TEH !!!!!!!! KWA KUWA TOFAUTI YA UTAWALA WA DINI NA SIASA NI KWAMBA KUNA DINI NYINGI TOFAUTI ZENYE VIONGOZI TOFAUTI KATIKA NCHI MOJA (Mfano: kadinali, padri na askofu na wakatoliki wake, sheik na kadhi na waislamu wao, wabudha wahindu wapagani, walokole nk) NA KUNA SERIKALI MOJA ISIYO NA DINI YENYE KIONGOZI MMOJA SIJUI UNANIELEWA HAPO?

Sasa linapokuja suala la kiutawala Serikali inatawala na baadae kuwaruhusu watu kila mtu kuwa na dini yake na hili ni kwa nchi zisizo na serikali ya dini lakini kama hakutakuwa na na mtawala mmoja hapo nani atamsikiliza mwenzie?
Wewe Unasemaje?

Siasa inanyanyasa DINI: Munishi

Wakisema serikali ina dini zote, na kiutendaji iwe hivyo. Siyo watu wa dini kuonekana duni mbele ya serikali. Nadhani waliosema serikali haina dini lengo lao lilikuwa kuwadhalilisha wenye dini ili maamuzi ya serikali yasipingwe na watu wa dini.

Wakibadili lugha kama unavyosema, basi dini itajihusisha moja kwa moja na mambo ya kisiasa. Jambo ambalo serikali nyingi hazitaki.
Wewe Unasemaje?

Hapa kwetu haiwezekani: POPE
Ndugu munishi ni lazima ujue kuwa Sisa nayo ni mfumo wa Maisha wa Kiutawala tofauti na Dini you talk about Faith na sehemu ambazo zinatawaliwa na serikali ya dini labda sehemu kubwa uwe ni dini tawala lakini kama hapa kwetu kwenye dini kubwa mbili ya ukristu na uislamu hapatawaliki asikudanganye mtu.
Wewe Unasemaje?
Munishi asema Inawezekana
Ndio maana nilisema kuwa siasa haiwezi bila dini, lakini dini inaweza bila siasa.

Wakishindwa kuifanya siasa na dini zitawale pamoja na hapa nina maana maamuzi makubwa yafanywe na dini, basi waachie ngazi dini zitawale. Zinaweza kufanya hivyo bila siasa.

Kama yote hayo yatawashinda, basi tusidanganyane. Tutenganishe. Na kutenganisha ni rahisi. Waumini wa dini wakome kuwa wanachama wa siasa, na wanasiasa watafute wale wasio na dini wawe wanachama wao. Halafu tuone kazi hapo.

Mimi mwenyewe siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa na sitarajii kuwa hivyo. Lakini hii hainiondolei haki yangu ya kuiongoza jamii. kwa sababu siasa imejitwika jukumu hilo ikashindwa, ituachie wenyewe kwani jukumu la kumwongoza mwanadamu tangu mwanzo lilikuwa la Mungu akiwatumia watumishi wake aliowateua.

Katika hilo mimi ni mteule wa Mungu kwa Tanzania. Pope unaonekana ni msomaji mzuri wa BIBLIA. Basi wewe siyo mgeni wa haya niyasemayo. Waambie akina Kimeta Jr. haya watafurahi kusikia.
Wewe Unasemaje?
Ndani ya DINI iko siasa- Al Melech
Ndani ya dini iko siasa, Vatican iko siasa, Anglican iko siasa. Wale ambao wanataka kuongoza kidini huwa wana campaign ili wachaguliwe. Hata pope alipigiwa kura, na hao hutumia siasa chafu.
Wewe Unasemaje?

Eriksen Aungana na Al Melech
Al Melech nakusikia walonga. Siasa chafu ndio siasa gani? Tufafanulie kidogo hapo.
Wewe Unasemaje?

Pope amuona mwokozi - Al Melech
Haya Al Melech na mimi pia nilipigiwa kura ?!!!. Ohooo kumbe Pope John Paul nikidhani ni mimi Pope Pius haya ni siasa gani chafu hizo ndugu yangu maana mhh umenigusa pahala yakhe......
Wewe Unasemaje?

Mavuto Agonga msumari kwa mbali
Yale yale afadhali ndugu yangu Munishi amenyamaza akisema kitu hapa nitawasikia watu fulaniiii!!!!
Wewe Unasemaje?

Al Malech anogewa, Sasa ni kizungu
People live in boundaries. These boundaries are not just countries, but also beliefs, organizations, sporting groups, religions etc. there is leadership in all these bounds. How to lead and gain leadership within these "places" is what i refer to as politics au siasa na Kiswahili.

Before an anglican archi-bishop gets his position he must have vied for it; he must have been elected. sometimes they are unopposed but ofte, there are others in hot pursuit for the position. I see them slanderously accuse their opponents, na kupakana matope.  Vatican hivyo hivyo.  Pope J. Paul II alichaguliwa na watu, ikiwa campaign yake haikuwa kali, angeshindwa na mwingine angekuwa pope.  katika haraati ya kuwaania kiti cha uongozi, mwanadam wa kawaida hufanya "all manner" to get there. Wana PIGANIA cheos. Dini zote ambazo nimeona, ni hivyo hivyo

Hiyo kupakana matope, vita, uongo ndio SIASA CHAFU.

Munishi asema siasa haiwezi bila dini, na dini inaweza bila siasa.

Basi
sikiliza:
Siasa ni watu; mawazo yao, iko na wafuasi, kama hakuna watu hakuna siasa.
Dini iko na watu - waumini. kama hakuna watu hakuna dini.
Zote hizi mbili siasa na dini haziwezi bila watu.|
Wewe Unasemaje?

Sehemu Ya Tatu

 
| http://munishi.netfirms.com |
 
<<Back  |  Home |  Gazeti La Injili | Injili2 | Nyimbo Za Munishi | Next >>