Ukurasa wa mbele
Gazeti la injili
Nyimbo za Munishi
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail
Tuma SMS duniani
Sema nami
Sikiliza waongo
Twende kanisani
Gazeti INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com
Or fmunishi@hotmail.com

CUF kujitoa katika muafaka

Na Mwandishi wetu, Zanzibar

Chama cha CUF kimetishia kujitoa katika muafaka baina yake na CCM ikiwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itafanya mabadiliko katika vipengere vya muswada wa kuundwa kwa Tume ya Kusimamia Utekelezaji wa muafaka huo. Muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa katika Baraza la Wawakilishi baadaye mwezi huu. Tishio hilo lilitolewa jana na Katibu Mkuu wa CUF, Bw. Seif Sharrif Hamad kufuatia habari kuwa serikali hiyo imevifanyia marekebisho baadhi ya vipengere vya muafaka katika muswada huo.’

Hata hivyo Bw. Hamad alisema kitendo chochote cha kubadili vipengele katika muswada huo ni kinyume cha makubaliano ya Kamati ya muafaka. “Wakibadili hatukubali... Huyo Idd Hassan Pandu (Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar) kapata wapi mamlaka ya kubadili muswada huo,” alihoji Alisema muswada huo ni sehemu ya muafaka na kwamba kuufanyia mabadiliko ni kuvunja makubaliano.

“Kubadili muswada huo wa muafaka ni kuvunja makubaliano ya muafaka tuliotiliana sahihi Oktoba 10 mwaka huu....mabadiliko yoyote lazima yawahusishe wajumbe wa Kamati ya Muafaka,” alisema Bw. Seif. Hata hivyo, alisema CUF haijapata taarifa rasmi za mabadiliko ya muswada huo na kwamba itajaribu kuwasiliana na uongozi wa CCM.

Kuna habari za kuaminika juu ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kufanya marekebisho katika muswada huo. Marekebisho hayo ni pamoja na kuondoa kifungu kilichokuwa kinaipa uwezo tume ya pamoja ya kusimamia utekelezaji kumfunga jela mwaka mmoja au kulipa faini ya sh. 500,000 mtu atakayetoa maelezo ya uongo au kupotosha muafaaka huo.

Pia maoni ya wanachama wa CUF yanatofautiana kuhusu muafaka wengi wanasema Hakuna muafaka kama CCM bado wako madarakani. Akiongea na gazeti la INJILI bwana Jumbe Ramadhani mwanachama wa CUF alisema: "Eti Muafaka? Hakuna muhafaka bila CCM kutoka madarakani. Iliwaweka watu kizuizini kinyume cha sheria, na sasa inataka kuwaachia kama sharti la kutimiza muafaka? Walioachiwa ni haki yao maana hawakufanya kosa. Ikiwa kusema uchaguzi urudiwe ni kosa la jinai basi hakuna muafaka bila uchaguzi kurudiwa.Wanajua wako madarakani isivyo halali,Dawa ni kutoka."

Naye Mwanasheria Mkuu wa SMZ amesema muafaka huo ni mkataba wa vyama vya siasa na kwamba serikali kwa upande wake ina haki ya kufanya marekebisho. Mwanasheria huyo Bw. Idd Hassan Pandu alisema “SMZ ina haki ya msingi ya kuvifanyia marekebisho vipendele vya muafaka pale inapohisi kuwa maslahi ya taifa hayakuzingatiwa.”

Wengi wameyapinga maoni hayo kwa kusema kwamba muafaka ni mbinu za CCM kupoteza muda ili malengo muhimu ya kuwatoa madarakani yasifikiwe. Waliongeza kuwa Amerika ilimsaidia Mkapa ashinde uchaguzi kwa njia zisizo halali. Masharti ilikuwa awathibiti waislamu, na hasa wa Zanzibar. Kwa kiburi serikali ya CCM iliwaua waislamu zaidi ya 70 huko Zanzibar.Amerika ilimkingia kifua Mkapa, badala ajiuzulu aliwapandisha vyeo polisi walioua.Sasa Amerika maji yako shingoni.Mkapa anataka mapatano na waislamu bila kutoka madarakani.Sawa hiyo? Waliulza wanachama hao walioonekana kuchukizwa na na mbinu za CCM kupoteza muda.

Wakati huo huo Mkutano Mkuu wa chama cha CUF, jana ulibadilika ghafla mjini hapa baada ya baadhi ya wajumbe wake kuwaweka ‘kiti moto’ viongozi wa juu kutaka kuelezwa hatma ya waathirika wa mauaji ya Januari 26 na 27 mwaka huu yaliyotokana na maandamano ya chama hicho. Hali hiyo ilijitokeza baada ya Katibu Mkuu wa CUF Bw. Seif Shariff Hamad, kumaliza kuwasilisha mada juu ya mwelekeo mpya wa kisiasa katika uendelezaji demokrasia kwa misingi ya utawala wa sheria.

Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Chake Chake Bw. Nassoro Juma, alisema kwamba Amerika walianza kumjenga Mkapa kwa damu ya waislamu hapa Zanzibar, Huyu tutambomoa bila kumwaga damu. Amerika walimjenga Osama Bin Laden wanataka sisi tumbomoe? Hatutaki, hatuwezi,tumekataa.Walimjenga kwa damu ya Warusi,Siyo vibaya wakimbomoa kwa damu yao wenyewe.Wamezoea kujenga kwa damu.Walimjenga Saddam Hussein kwa damu ya Wairan na sasa wanambomoa kwa damu ya Wairaq.

"Hadi sasa familia za watu walioathirika na mauaji hayo hazina msaada wa kutosha kutoka kwenye chama licha ya viongozi kuelewa tatizo hilo. Mwenyekiti huyo alisema familia hizo hazielewi hatma ya maisha yao, kutokana na wazazi wao kupoteza maisha. Alisema lazima ikumbukwe kwamba ngome ya CUF iko kisiwani Pemba na lazima viongozi wawe karibu na wanachama ili wajue matatizo katika ngazi za utendaji katika chama. Pia walitilia mkazo suala la viongozi wa CUF kuwa macho na ujanja wa CCM." Hawa CCM ni waongo na mnajua hivyo, shauri yenu mkikubali kudanganywa."

 

 
| http://munishi.netfirms.com |
 
<<Back  |  Home |  Gazeti La Injili | Injili2 | Nyimbo Za Munishi | Next >>