Ukurasa wa mbele
Gazeti la injili
Nyimbo za Munishi
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail
Tuma SMS duniani
Sema nami
Sikiliza waongo
Twende kanisani
http://munishi.netfirms.com
Gazeti La Injili

E-mail: munishifaustin@yahoo.com
Au fmunishi@hotmail.com

http://munishi.netfirms.com

Apollo Joo Afariki
Ni baada ya kuugua kwa muda mfupi

Marehemu Apollo Joo

Tumezipokea kwa majonzi na masikitiko makubwa habari za kifo cha mmoja kati ya waanzilishi wa makanisa ya kipentekoste Kenya, mchungaji Justus Odera Oyombe, maarufu kwa jina la apollo Joo

Atakumbukwa zaidi kwa mahubiri yake ya kusisitiza msimamo katika ukristo.Majuma machache kabla ya kufa kwake Apollo alisema.Eee Yesu mwana wa Mungu uliye hai. Nimefanya kazi yako tangu ujana wangu, na kama binadamu nilikukosea mengi.

Neema yako imekuwa ikinifunika na kunihakikishia kuwa bado hujaniacha pamoja na udhaifu wangu kama Apollo.Ikikupendeza nije kwako, basi ya nini mateso haya mwilini?

Kazi uliyonipa nimeifanya kwa kadiri ya uwezo wangu kama binadamu.Makosa yote niliyokukosea Naomba unisamehe na na uwasaidie wote niliowakosea neema ya kutosha kunisamehe kama na mimi ninavyowasamehe wote walionikosea.

Nijalie usingizi mwema nkingoja siku ile utakayomwamsha kila aliyelala katika wewe ili auingie ufalme wako wa milele.

Atakumbukwa daima kwa Imani yake kwa Mungu kupitia mwanawe Yesu Kristo.

 
| http://munishi.netfirms.com |
 
<<Back  |  Home |  Gazeti La Injili | Injili2 | Nyimbo Za Munishi | Next >>