|
|
Gazeti
INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com Or
fmunishi@hotmail.com
Amri Kumi
za Mungu
-
Mimi
ni Bwana Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri katika nyumba
ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi.
-
Usijifanyie
sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni,
wala kilicho chini duniani,wala kilicho majini chini ya dunia.
Usivisujudie wala kuvitumikia; Kwa kuwa mimi Bwana Mungu wako,
ni Mungu mwenye wivu; Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata
kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu
elfu wanipendao, na kizishika amri zangu.
-
Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia
kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
- Ikumbuke siku
ya sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
lakini siku ya saba ni sabato ya Bwana Mungu wako, siku hiyo usifanye
kazi yoyote, wewe, wala mnyama wako, wala binti yako, wala mtumwa
wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni
aliye ndani ya malango yako. Maana kwa siku sita Bwana alifanya
mbingu na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya
saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya sabato akaitakasa.
- Waheshimu
baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi
upewayo na Bwana, Mungu wako.
- Usiue
- Usizini
- Usiibe
- Usimshuhudie
jirani yako uongo.
- Usiitamani
nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa
wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake,wala punda wake, wala
chochote alicho nacho jirani yako
|
|