Ukurasa wa mbele
Gazeti la NYAKATI
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail

Gazeti la INJILI
Kwenye Internet

http://www.munishi.com

Tel. 254722602445 E-mail:munishi@munishi.com Or
munishifaustin@yahoo.com

Amerika wapata kipigo Iraq



Kumbe hata wanajeshi waliofundishwa kuua nao huogopa kufa? Waangalie. Wote nyuso zao zina hofu ya kutisha. Bush yuko ikulu anakula vinono, na watoto wa wenziwe anawatuma Iraq kuuawa. Sawa hiyo?

War mongers’ changing lingo

Five days into the Gulf War II, it is no longer necessary to argue about the legitimacy or otherwise of the war.

The fact, grim, brutal, and even ironical, is that the United States and its ally, Britain, has forced the world into a war whose toll is beginning to tell.

Where President George W Bush revelled in a war that would be precision-guided, electronically-driven and a war in a magnitude the world has never known, now he is realising that the US may have “e-bombs”, but it is not prepared for ground warfare. With increasing toll in weaponry and soldiers, the allies are beginning to differentiate between fantastic war adventures of the Hollywood type and the reality of imposing regime change in the Arabian desert.

Just five days away from the start of the war, the allies are counting at least four aircraft downed, 12 US marines killed, 16 British soldiers killed in what has been described as ‘friendly fire’, and several allied soldiers being displayed as prisoners of war.

The toll could be higher, given that this information comes to the world through the Western media, sympathetic to allied adventures.

Where Bush talked of fast ‘decapitation’ and rapid ‘regime change’, he is now pleading with the Iraqi regime not to “mistreat allied prisoners of war.”

Where Bush talked of a fast take-over and control of Iraqi oil fields, he is preparing Americans for a not-so-flattering rendezvous with reality.

Now he is saying this war could “take much longer than expected, given the rough terrain in a country larger than their California.”

Where initially US and Britain talked of “pockets of resistance”, now the military parlance is graduating into a lingo much more realistic. It is now “fierce resistance”, rather than “pockets of resistance”.

What has not changed, however, but certainly will sooner than expected, is the allies recognising the fact that the Iraqis, energised by a growing anti-war sentiments internationally, are fighting for the sovereignty of their country, rather than “surrendering, defecting, deserting, or capitulating” as initially expected.

Even though the much-talked of Iraqi “weapons of mass destruction” have not been unleashed by Saddam Hussein in defence of Iraq, the world is yet to be convinced that the regime is capable of destroying in mass US and its allies.

Nothing so far as destructive as allied weapons of mass destruction has been deployed in defence of the Iraqi sovereignty. The crave to secure oil fields is beginning to tell why the Gulf War II had to be.

AMERICA IS NOT SUPER POWER


Evangelist Faustin Munishi:The first bomb which America will drop any where will decide who is with America and who is not.This is what I told America. Change your foreign polieces and no one will ever hurt you. It seems to me that they dont want to change and they want to fight a new war which they know nothing about. They will lose.


Mr. Bush: Either you are with us or with terrorist


Evangelist and Gospel Singer Munishi: Sorry Mr Bush. I am not with America, and for that matter I am not with terrorists of which America is nomber one. If someone using a knife can hijack a US plane, what about someone who has an arrow? He can easily overthrow the US goverment. America should stop thinking that they are super power. They are not, and they will not be. The only SUPER POWER is GOD.

Its now official that the US army can shoot down US plane, full of US citizens, in US air space. What a foolish idea. And what is US Media doing? Printing flags Intead of telling their goverment to change its foreign polieces which was a major contrubitor of what happened in September 11th 2001


Osama Bin Laden: If Iam the terrorist, What is the diffret between me an Mr Bush? They killed innocent people in Afghanistan than thoose now claming I killed.

Tatizo siyo Osama Bin Laden, bali tatizo ni Amerika. Osama na wote wanaodhaniwa kuwa maghaidi wakifa leo tatizo la ughaidi haliwezi kwisha duniani. Ughaidi ni matunda ya sera mbaya.Huwezi kuumaliza ughaidi bila kumaliza sera mbaya.Kila mtu anaweza kuwa ghaidi kulingana na mahali alipo na hasa kama anahisi kunyimwa haki zake za msingi.

Amerika wana vita vya mafuta na waarabu.Hakuna dini hapo. Ni mafuta.Wasitudanganye kwamba wanapigwa vita vya kidini.Wamalize vita vyao huko Amerika na Uarabuni.Wasiingize dunia kwenye mzozo ambao wanaweza kuumaliza wenyewe.Hatuwataki Waamerika watusaidie kuutetea Ukristo.wasiutumie ukristo kulinda maslahi yao.

Walokufa Amerika hawana hatia? Wana hatia kama walikubaliana na sera za serikali yao kuwanyanyasa wengine.Mimi ni Mkristo mwananchi wa Tanzania na sikubaliani na sera za serikali yetu kuwanyanyasa waislamu kwa sababu ya dini yao.Wakati umefika wananchi wa Amerika kupinga kwa nguvu zote sera za serikali yao.Wasipofanya hivyo wana hatia.

Kwa nini mnawaogopa amerika? Sera zao ni mbaya na hamtaki kuwaambia wajirekebishe.Tatizo siyo walikufa wangapi,bali mauaji yataisha lini.Sera za Amerika ni mbaya,na hakuna anayewakemea. Amerika ilikosea kwa kiburi, waliowaua wakakosea, na sasa Amerika inataka kukosea tena.Makosa yataendelea mpaka lini?

Maadui wa Amerika siyo waislamu kama wanavyotaka tuamini.Mungu hapendezwi na kiburi cha amerika.Wanasema ni vita ya waovu juu ya wema.Wanakosea.Waamerika siyo wema kama wanavyofikiri.Kama ni dini, ukristo hauhitaji kutetewa na Amerika

Amerika ilijitengenezea maadui zake yenyewe kwa sera zake mbovu za kutaka kuitawala dunia ya Mungu bila idhini ya Muumbaji.Sasa wanaitaka dunia iwasaidie kupambana na maadui zao.Lazima wakubali kuwa wao siyo bora kuliko wanadamu wengine.Wajirekebishe kila upande, na hakuna atakayewadhuru.

Paka ni mnyama wa kufugwa, na hana madhara kwa mwanadamu.Lakini mwanadamu akimpiga paka kwa sababu yoyote na awe amefunga mlango, paka anageuka chui na kuwa madhara kwa mwanadamu.Amerika imewapiga wengi duniani kwa sababu wanazozijua wao,na sasa inakuwa vigumu kujua ni nani aliyegeuka kuwa chui na kusababisha madhara makubwa namna hii kwa Waamerika.

Hakuna SUPER POWER duniani.Ikiwa watu wanaweza kutumia visu kuziteka nyara ndege za Amerika na kuzitumia kama mabomu kuwalipua waamerika, basi tumefikia mahali pa kujiuliza kama tunahitaji silaha zote kali tulizojiwekea kujilinda.Wote tuko sawa. Tuliwaogopa bure kumbe kisu tu kinatosha.Sera za kuwanyanyasa wengine hazitalisaidia taifa lolote duniani.Sijui kama Mkapa anayasikia haya.

Mkapa alisema atatumia nguvu za dola kuwaweka sawa wale anaowanyanyasa. Kama ni nguvu za dola Amerika ni zaidi ya TZ mara mia moja.Tunasubiri tuone atafika wapi na nguvu za dola.Haki kwa kila mtu ndiyo silaha kwa sasa.Bila haki, Nguvu za dola ni Bure.Waliouawa Zanzibar ni watu, ndugu zao wapo,wanaoendelea kupigwa marungu ya Polisi ni watu,na wanaowekwa ndani na kuteswa bure ni watu.Yakiwafika shingoni sijui watafanya nini.Tunao muda kuyarekebishe yasitufikishe pabaya

Siungi mkono mauaji hasa ya raia wasio na hatia,au ya watu wasiohusika na mzozo wenyewe kama mabomu yaliyolipuliwa Nairobi na Dar,Lakini inapofikia kwamba wauaji ni watu walio tayari kufa, ni vizuri kujiuliza kile kinachowafikisha katika maamuzi ya namna hiyo, ili juhudi zifanywe kuepusha maafa kwa watu wasio na hatia.

Inashangaza kuona kwamba hakuna kiongozi Afrika aliyepeleka misaada ya chakula na nguo huko Amerika.Ni wanadamu.Wakati huu wa maafa wanahitaji kila msaada. Mablanketi, kandambili, na watu wa kusaidia kuwatoa wale ambao bado wameshikiliwa kwenye mabaki ya kuta zilizowaangukia.Sote ni wanadamu tunahitajiana mmoja kwa mwingine.

Wakati Mabomu yalipolipuka Nairobi na Dar,walisema Waafrika hawajajiandaa vya kutosha kutoa usaidizi wakati wa majanga.Sasa ni wazi kwamba hakuna anayeweza kujigamba kwamba yuko tayari kupambana na majanga .Polisi na wazima moto wa Amerika waliowahi kufika kwenye tukio walikufa wote. Zaidi ya 400.

Kama ni vita Amerika imeshindwa vibaya.Sasa wabadili sera zao ambazo zimechangia zaidi kusababisha haya. Kusema watalipiza kisasi hawawezi.Waliokufa ni wengi zaidi ya kulipiza kisasi. Kuchukua ndege na kuangusha mabomu Iraq au pengine popote haitasaidia. Na mbaya zaidi wote wataonekana wendawazimu.Wakubali kushindwa na wabadili sera zao sasa na siyo baadaye.

Maisha yetu wanadamu ni mali ya Mungu. Hakuna mwenye haki ya kuutoa uhai wa mwingine.Amerika ilikosea kwa sera zake ikasababisha uhai wa wengi kupotea duniani.Maghaidi wakakosea kuwaua waamerika, na sasa Amerika imekosea tena.Mbaya zaidi Bush anaitaka dunia iwe upande wake au Maghaidi.Hatoi nafasi ya tatu.Wote ni wauaji dunia isiwaunge mkono Amerika.

Mfa maji haachi kutapatapa.Amerika imemkanyaga Mungu pabaya, Pale ilipoitaka dunia iiabudu badala ya Mungu.Mungu ameruhusu maghaidi waifanyie Amerika kile Komputa ilichoifanyia Taipreta. Mbinu za vita zimebadilika,Silaha za kisasa ni bure,Na hakuna mwenye jeshi la kupambana vita hivi.Siyo Amerika wala Uingereza.

Mwisho Wa Amerika umefika. Walichokoza kwa zaidi ya miaka 20,na mwezi uliopita wakapigwa pigo moja la nguvu.Badala ya kuzika waliokufa,Amerika wametoka tena kuchokoza.Wamewaacha waliowapiga ndani, na wanakimbilia Afghanistan kuuwa raia wasio na hatia.Amerika itawaka moto, na waliotoka hawatarudi.Huo ndio mwisho wao.

Amerika walimjenga Osama Bin Laden wanataka sisi tumbomoe? Hatutaki, hatuwezi,tumekataa.Walimjenga kwa damu ya Warusi,Siyo vibaya wakimbomoa kwa damu yao wenyewe.Wamezoea kujenga kwa damu.Walimjenga Saddam Hussein kwa damu ya Wairan na sasa wanambomoa kwa damu ya Wairaq.Walianza kumjenga Mkapa kwa damu ya waislamu huko Zanzibar, Huyu tutambomoa bila kumwaga damu.

Amerika ilimsaidia Mkapa ashinde uchaguzi kwa njia zisizo halali.Masharti ilikuwa awathibiti waislamu, na hasa wa Zanzibar. Kwa kiburi serikali ya CCM iliwaua waislamu zaidi ya 70 huko Zanzibar.Amerika ilimkingia kifua Mkapa, badala ajiuzulu aliwapandisha vyeo polisi walioua.Sasa Amerika maji yako shingoni.Mkapa anataka mapatano na waislamu bila kutoka madarakani.Sawa hiyo?

Eti Muafaka? Hakuna muhafaka bila CCM kutoka madarakani.Iliwaweka watu kizuizini kinyume cha sheria, na sasa inataka kuwaachia kama sharti la kutimiza muafaka.Walioachiwa ni haki yao maana hawakufanya kosa.Ikiwa kusema uchaguzi urudiwe ni kosa la jinai basi hakuna muafaka bila uchaguzi kurudiwa.Wanajua wako madarakani isivyo halali.Dawa ni kutoka.

Vita Ya Amerika inawaadhiri wenyewe. Sasa hawasafiri kwa ndege,hawasomi barua,hawali vyakula vilivyofungwa kwenye paketi,Hawakai ghorofani,Hawaendi kwenye majumba ya starehe Na kadhalika.Kwangu mimi wanaendelea kushindwa vita vibaya.Waache makeke yao wainue mikono juu kama ishara ya kusarenda. Tuone kama maisha yao yatarudi kama kawaida kwa kiasi.

Anguko la Amerika litakuwa kubwa, na kishindo chake kitasikika dunia nzima.Ole wake atakayejaribu kuishikilia Amerika isianguke!! Atasagwa kama panzi. Mungu ameikataa Amerika kwa kujiinua kwao na kiburi.Lakini wakijirudi,warekebishe sera zao Mungu mwenye huruma atawasamehe.Wasipofanya hayo,Ole wao

Dini misingi yake ni haki kwa watu wote.Nani anayechanganya dini na siasa? Ni yule anayepingana na udhalimu wa wanasiasa? au ni yule anayekubaliana na udhalimu huo? Mkapa alipowanyima waislamu zaidi ya 70 haki yao ya kuishi, Wenye dini wanafiki walikubaliana naudhalimu huo. Hao ndio wanaochanganya dini na siasa.Wanaowapinga wanasiasa, wanatenganisha siasa na dini.

Wanaojiita "wasomi" wanajaribu kuninyamazisha nisiyakemee maovu.Mungu yuko upande wangu sitowaogopa waovu.Wakitaka tusiwakemee watende mema nasi tutawasifu.Mkapa awalipe fidia jamaa wa marehemu waliouawa Zanzibar,Tunajua hakuna kiwango cha pesa kutosha kulipa uhai wa mwanadamu, lakini ni kuonesha nia njema.Watoke madarakani na uchaguzi urudiwe.

Viongozi wa dini wanafiki, wanaitwa ikulu na kupewa ploti na pesa kidogo,wakitoka huko wanamwabudu "rais" kuliko Mungu.Wanabeba picha walizochukuliwa wakiwa ikulu kumwonyesha kila mtu.Wakikusikia unawakemea wanasiasa wanakukemea.Siyo kosa lao, wamesahau wao wanamtumikia Mungu Mkuu kuliko wanasiasa.Badala wanasiasa kushukuru kuwa na bahati ya kukutana na mtumishi wa Mungu, imekuwa kinyume chake.

Propaganda za America zinawadhuru wenyewe.Maghaidi waliofanikiwa kuwaua Waamerika zaidi ya 10,000 kwa pigo moja lenye nguvu leo shambulio lao la pili litakuwa ni unga kwenye bahasha? Tena unga wenyewe unatumwa kwa mkikuyu huko Moranga? Sijui mnasemaje, lakini mimi siamini kwamba shambulio litakalofuata litakuwa unga kwenye bahasha.

Ukweli unabaki kweli bila kujali unasemwa na nani,nao uongo unabaki hivyo hata kama wanaousema ni Bush na Blair.Hakuna ushahidi wa kutosha kumhusisha Osama na mauaji ya September 11,lakini waamerika bado wanamimina mabomu Afghanistan ambayo yanazidi kuwauwa raia wasiyo na hatia.Cha ajabu viongozi wenzangu wa makanisa hawakemei hilo.Wanadanganyika kuwa Amerika wanatupigania wakristo.Mungu tunayemwamini ana nguvu za kutosha na haitaji kusaidiwa na Amerika.

Baada ya vita historia itaandikwa Amerika. Kwamba utawala wa Bush uliwatuma wanajeshi wa Amerika kuua waafghanstan wasio na hatia, huku wakijua wazi hawawezi kushinda vita dhidi ya ughaidi kwa kufanya hivyo.Waliwageuza wanajeshi wao kuwa maghaidi hatari kuliko wale wanaojifanya kupambana nao.Baada ya kuua, waamerika walirudi kwao kungoja kuuawa.

Vita ni mchezo mbaya wa kuuana, na unanoga wakati kila mmoja anapoogopa kufa na kujitahidi kwa kila mbinu ili asiuawe na adui yake.Lakini wakati upande mmoja unapoonyesha kuwa haupigani ili kuishi,basi mchezo umeisha. Na kama utaendelea kuchezwa, basi utamu wa mchezo unakuwa haupo.Amerika wanapigana ili waishi kuulinda utajiri wao, wakati maghaidi wanapigana ili wafe.Wanaposema wametangaza vita na maghaidi ina maana kwamba hawajui vita ni nini.Na kama kweli wametangaza vita, kwa nini hawataki kuuawa kwa kila njia inayofaa kuua?Wanaua kwa mabomu,kwa nini wasiuawe kwa kutumia ndege zao? Amerika Waache kuua na mchezo umeisha.Hakuna atakayewaua.

Amerika wana zana za kivita, lakini siyo wapiganaji.Historia inaonyesha kwamba hawajawahi kushinda vita.Walienda Somalia kujaribu kuonyesa ubabe wa kivita, waliuawa na kuburuzwa kwenye barabara za Mogadishu.Walienda Iraq kumtafuta Saddam,walirudi mikono mitupu.Sasa wako Afghanistan kumtafuta Osama,wakati maghaidi wamewaacha New York.

Kama dunia imeungana kupambana na ughaidi, kwa nini tusianze na Amerika ambao ndio maghaidi wakubwa duniani. Ikiwa ughaidi ni kufanya vitendo viovu kuyafikia malengo halali, basi Amerika ilianzishwa kwa ughaidi.Waliwachukua mababu zetu kama watumwa kuwajengea, na sasa wanachukua mali zetu za asili ili waendelee kuwa matajiri.

Wataalam wa vita niambieni mpaka sasa nani mshindi katika vita ya Amerika na maghaidi? Maghaidi wakitumia visu vya plastiki waliteka ndege za Amerika na kuzielekeza katika majengo makubwa ya Amerika na kuua waamerika zaidi ya 10,000. Nayo Amerika kujibu mashambulizi inaangusha mabomu ambayo gharama yake inaweza kuijenga Afghanistan mara mia moja.Tena yanaangushwa jangwani.

Waamerika walioachiwa huru wamshukuru Mungu kwani ndiye aliyeigeuza mioyo ya wale waliokuwa wamewakamata. Serikali yao ilikubali wauwawe lakini Mungu wanayemwamini akaamua vinginevyo.Tangu wakati wa Daniel Meshack na Abednego, hakujawahi kutokea tendo linalomhusisha Mungu kwa karibu kama hili. Limeinua imani zetu Wakristo, Tulijua waislamu siyo adui zetu.

Taliban wamefanya Kiungu, kuwaachia huru Waamerika waliotuhumiwa kuhubiri Ukristo Afghanistan. Kitendo hicho kimewagusa watu dunia nzima. Wameonyesha kwa vitendo kumpenda adui yao. Kwa upande wa imani Talibani wameishinda. Wafghanistan wana ushahidi wa kutosha kuwa Amerika inawaua kwa kuwaonea kwani hawakuhusika na tukio la September 11.

Bush anaona haya kukutana na Waamerika walioachiwa huru na Taliban. Kisa? Anajua kuwa alikuwa amewaua kwa uamuzi wake wa kuishambulia afghanistan huku akijua kufanya hivyo kutapelekea Taliban kuwaua washukiwa hao. Kwa Bush ni kama anaona watu waliofufuka kutoka katika wafu. Kwa Waamerika waliochiwa, wanaichukia nchi yao na wamesema watarudi Afghanistan nyumbani.

Mwendawazimu anapofanya kiwazimu, haishangazi kwani angefanya nini badala yake? Lakini mwenye akili timamu akifanya kiwazimu, basi kila mtu anamshangaa. Amerika ilifanya kiwazimu kuwashambulia na kuwaua raia wasio na hatia wa Afghanistan.Walikuwa na kilio Amerika, na wakati Waafghanistan wanawafariji wakawashambulia na kuwauwa.Kukawa na kilio pande zote.Sasa dunia inaifariji Afghan.

Mmoja kati ya askari waliokuja kumkamata Yesu alikatwa sikio na mwanafunzi wake. Yesu aliokota sikio lenye damu na kulirudisha mahali pake na kumkemea mwanafunzi aliyefanya hayo. Taliban ni waislamu, lakini wamefanya kama Yesu Kristo. Tendo lao la kuwaachia huru Waamerika na huku uongozi wa Bush unawaua ndugu zao limewafanya kuwa Wakristo kuliko Amerika. Ukristo si maneno!!

Dunia haiwahurumii Amerika, sasa inawahurumia wananchi wa Afghanistan wanaouawa na Amerika bila hatia.Maghaidi waliowaua Waamerika September 11 walikufa pamoja nao,wakati maghaidi wanaowaua raia wa Afghanistan wako hai na tunawaona.Maghaidi wa kwanza unaweza ukawaita wendawazimu,walevi,au ambao hatujui walifanya hayo wakiwa katika hali gani kiakili.Maghaidi wa sasa ambao ni Amerika wanafanya hayo wakiwa na akili timamu tena kwa makusudi.Habari Zaidi

Contact us/ Tuandikie

Full Name
E-mail
Subject
Message
   
   

 

 
| http://munishi.com |