Ukurasa wa mbele
Gazeti la injili
Nyimbo za Munishi
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail
Tuma SMS duniani
Sema nami
Sikiliza waongo
Twende kanisani
Gazeti INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com
Or fmunishi@hotmail.com

Waziri Idi Simba Amejiuzulu

 

Name: Rev.Leonard S.Mwazembe
Homepage
: http:/munishi.netfirms.com
Hometown: Dar es salaam
Sent: 11.47 - 8/11

Ninapenda kutoa maoni yangu kuhusu kujiuzulu kwa Mr.Idd Simba ambaye alikuwa waziri wa viwanda. Ni baada ya tume kuwakilisha ripoti yao na waziri kuonekana anahusika kuchukua rushwa kuhusu tuhuma ya sukari. Cha ajabu ni kwamba wakati wabunge wamekabidhiwa ripoti siku ya alhamisi ili weekend waweze kuuipitia na kutoa uamuzi siku ya jumatatu tarehe 5-11-01 tayari wabunge wa ccm walifanya kikao chao na kumlazimisha Mr.Simba kujiuzuru.

Na mimi nasema hivi mtu anapotuhumiwa hatimaye kujiuzuru maana yake ni kweli alihusika. Sasa cha ajabu ni kwamba ripoti ya tume imemuona mhe kuwa amejihusisha na vitendo vya rushwa na kumtaka ajiuzulu kwa masrai ya taifa. maana yake ni muhujumu na muhujumu huyo huyo anapotangaza kuachia ngazi Mhe.Rais anapokea kwa masikitiko barua ya kujiuzuru kwake. swali je Rais alipendezwa na kitendo cha huyu Bwana na kwa hiyo alitaka aendelee kula rushwa?

Kiini macho ni kwamba pamoja na huyu Bwaana kupatika na rushwa Rais amempa zawadi ya kumpongeza kuendelea kuwa waziri mpaka tarehe 16-11 na kumtuma nje ili akamalizie biashara zake za sukari. Kwa nini Rais asimuenzi baba wa Taifa Nyerere kwa kufanya kama yeye alivyo kuwa anafanya kwa mtu kama waziri Simba ni kwamba angemfikisha mahakani na mahakama ikimpata na hatia basi ahukumiwe. Lakini kwa mchezo huu ni kama wanatuchezesha mazingaombwe.

Nawapongeza wabunge kutoka vyama vya upinzani ambao wametaka bwana Simba ashitakiwe. Mwisho nawapongeza pia wabunge wa Ccm kwa msimamo wao wa kuondoa ouvu ndani ya chama chao.

 
| http://munishi.netfirms.com |
 
<<Back  |  Home |  Gazeti La Injili | Injili2 | Nyimbo Za Munishi | Next >>