![]() ![]() |
![]() |
|
|
Gazeti
INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com Or fmunishi@hotmail.com Taliban Wamefanya Kiungu, Amerika ilifanya kishetani Waamerika walioachiwa huru wamshukuru Mungu kwani ndiye aliyeigeuza mioyo ya wale waliokuwa wamewakamata. Serikali yao ilikubali wauwawe lakini Mungu wanayemwamini akaamua vinginevyo.Tangu wakati wa Daniel Meshack na Abednego, hakujawahi kutokea tendo linalomhusisha Mungu kwa karibu kama hili. Limeinua imani zetu Wakristo, Tulijua waislamu siyo adui zetu. Taliban wamefanya Kiungu, kuwaachia huru Waamerika waliotuhumiwa kuhubiri Ukristo Afghanistan. Kitendo hicho kimewagusa watu dunia nzima. Wameonyesha kwa vitendo kumpenda adui yao. Kwa upande wa imani Talibani wameishinda. Wafghanistan wana ushahidi wa kutosha kuwa Amerika inawaua kwa kuwaonea kwani hawakuhusika na tukio la September 11. Bush anaona haya kukutana na Waamerika walioachiwa huru na Taliban. Kisa? Anajua kuwa alikuwa amewaua kwa uamuzi wake wa kuishambulia afghanistan huku akijua kufanya hivyo kutapelekea Taliban kuwaua washukiwa hao. Kwa Bush ni kama anaona watu waliofufuka kutoka katika wafu. Kwa Waamerika waliochiwa, wanaichukia nchi yao na wamesema watarudi Afghanistan nyumbani. Mwendawazimu anapofanya kiwazimu, haishangazi kwani angefanya nini badala yake? Lakini mwenye akili timamu akifanya kiwazimu, basi kila mtu anamshangaa. Amerika ilifanya kiwazimu kuwashambulia na kuwaua raia wasio na hatia wa Afghanistan.Walikuwa na kilio Amerika, na wakati Waafghanistan wanawafariji wakawashambulia na kuwauwa.Kukawa na kilio pande zote.Sasa dunia inaifariji Afghan. Mmoja kati ya askari waliokuja kumkamata Yesu alikatwa sikio na mwanafunzi wake. Yesu aliokota sikio lenye damu na kulirudisha mahali pake na kumkemea mwanafunzi aliyefanya hayo. Taliban ni waislamu, lakini wamefanya kama Yesu Kristo. Tendo lao la kuwaachia huru Waamerika na huku uongozi wa Bush unawaua ndugu zao, limewafanya kuwa Wakristo kuliko Amerika. Ukristo si maneno!! Dunia haiwahurumii Amerika, sasa inawahurumia wananchi wa Afghanistan wanaouawa na Amerika bila hatia.Maghaidi waliowaua Waamerika September 11 walikufa pamoja nao,wakati maghaidi wanaowaua raia wa Afghanistan wako hai na tunawaona.Maghaidi wa kwanza unaweza ukawaita wendawazimu,walevi,au ambao hatujui walifanya hayo wakiwa katika hali gani kiakili.Maghaidi wa sasa ambao ni Amerika wanafanya hayo wakiwa na akili timamu tena kwa makusudi. |
||||||||||||
|
|
|
|