![]() ![]() |
![]() |
|
![]() Nyerere Anaona Haya
![]() Nyerere Anaona Haya |
Gazeti
INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com Or fmunishi@hotmail.com Nyerere
Msingi aloujenga Haufai Tuubomoe?
Sina
matatizo na watu waliomuogopa Nyerere, au tuseme waliompenda
kwani ilikuwa haki yao kufanya hivyo. Kwetu sisi ambao
hatukumuogopa, tunajisikia kuonewa kama hatutapewa nafasi
ya kujadili yale yaliyotufanya tusimuogope Nyerere , japo
wengine wanatuelewa vibaya kwamba hatukumpenda Nyerere.
Malisa Apinga hoja Mwalimu alikuwa kinara katika kuiletea uhuru Tanganyika, sijui kama hilo ni kushindwa, tena bila kumwaga damu. Miaka kumi ya uhuru viwanda vingi vilianzishwa, tuliweza kupata elimu bure hadi chuo kikuu, matibabu ya litolewa bure hata wanyonge waliweza kutibiwa. Mimi nilifanya kazi wakati wa Mwalimu serikalini, niliweza kutumia mshahara wangu kwa mwezi na kutosheleza mahitaji yangu. elimu ilipewa kupaumbele katika wakati huo hata elimu ya watu wazima. Tanzania ukiondoa Cuba, ilikuwa nchi ya kwanza duniani kufuta ujinga, tulifika mahali aslimia 80 ya watanzania wote walijua kusoma na kuandika. Huwezi kupuuza ukweli kwamba chini ya uongozi wa Mwalimu, Tanzania iliweza kuzisaidia nchi nyingi za Afrika kujipatia uhuru wake. Afrika ya Kusini ni mfano. Wakati Afrika ukabila unaleta vita visivyo kwisha, Tanzania imeweza kuunganisha makabila za ya 120 chini ya lugha moja na taifa moja. Na yote haya bado tunasema Nyerere alishindwa? Hivi kumbe angeshinda alitakiwa kufanya nini cha zaidi? Leo Tanzania ni moja ya nchi chache Afrika ambako viongozi wanabadilishana madaraka kwa amani (japo ni wana CCM tu). Lawama kubwa kwa Mwalumu ni juu ya uchumi na vijiji vya ujamaa. Vita vya Uganda vilichangia kuleta matatizo ya uchumi hata watu kukosa vitu madukani. Ieleweke kuwa matatizo ya uchumi haya letwi na ujamaa. Amerika ambayo ni mama wa ubebari duniani wamekuwa na matatizo ya uchumi vipindi mbali mbali kwa mfano The Great Depression of 1930's na 1980' chini ya uongozi wa George Bush Sr. China ambayo bado ni nchi ya kikomunsti ndio yenye uchumi unao kua kwa kasi kuliko nchi yo yote duniani kwa sasa. Mwalimu alipoondoka madarakani viwanda vilikuwa vinafanya kazi karibu vyote. Huyo Mwinyi anaedaiwa kukabidhiwa nchi isiyokuwa na kitu, wakati huo dollar moja ya Kimarekani ilikuwa Tshs.24. Alipomkabidhi Mkapa dollar isha fika Shs 600. Wale wenye kumbukumbu wanajua miaka ya 70 na 80 mwanzoni rushwa ilikuwa adimu, haikuwa kawaida kwenda hospitali na utoe rushwa ndipo utibiwe, lakini wakati wa Mwinyi rushwa ilisambaa kila mahali mpaka serikali ikashindwa kabisa kukusanya kodi. Shinikizo la kimataifa lililazimisha Marehemu Kigoma Malima atolewe wizara ya fedha na Jakaya Kiketwe aingie ili serikali iweze kukusanya tena kodi. Kuna mengi ya kusema na nafasi hairuhusu.
Mimi sikubaliani na sera na utendaji wa serikali za Mwinyi
na Mkapa, kwani wamechangia kwa kiasi kikubwa sana kubomoa
yale yaliyojengwa toka tupate uhuru. Upinzani juu ya Nyerere
unatokana na aidha kutojua ukweli au kukataa kuuona ukweli.
Sisemi kwamba Mwalimu hakufanya makosa, na sikubaliani nae
kwa kila kitu, bali pale ambapo mtu amefanya kweli ni lazima
kukiri. Lengo letu ni kuendeleza Tanzania na sio kujenga hoja
za chuki binafsi au kutafuta umaarufu kwa kumponda hata yule
ambae kuna ushahidi wa wazi kwamba alijitahidi. Hatari ya
upinzani wa namna hii ni kubomoa nchi, kupandikiza mgawanyiko,
na kuwakatisha tamaa wale wote wanao jitahidi kujenga nchi
yao kama wewe na mimi.
Mazuri ya Nyerere? Alikuwa msemaji mzuri aliyeweza kuutetea uongo ukafanana na kweli.Aliwatisha viongozi waliokuwa chini yake na kuwafanya wamwabudu kama mungu wao. Alikuwa na nguvu ya kushawishi akaitumia vibaya kuwashawishi watu wahamie kwenye vijiji vya ujamaa. Alikuwa msomi aliyengangania sera zake hata kama sera hizo zinaonyesha kila dalili ya kushindwa. Kwa hili alikuwa mpumbavu. Ni wapumbavu tu ndio wasiobadili mawazo. Melisa umejiita "DR" sijui ni wa binadamu au wanyama? Au ni "DR" wa mitishamba? Umenilazimisha nirudie yale ambayo hukuyasoma. Kiafrika Mtu akishakufa siyo vizuri kuusema ubaya wake maana mwenyewe hayuko kujitetea. Lakini anapokuwa hai, hata kama ni uhai unaosaidiwa na mitambo, bado watesi wanaruhusiwa kuusema ubaya wake ili akipona ajirekebishe.Na asipopona basi itawabidi watesi wanyamaze kimya wawasikilize mashabiki wake wakisema uzuri wa Mwalimu wa kuwakomboa Watanzania kutoka katika minyororo ya ukoloni wa Waingereza na kuwaigiza kwenye ukoloni mwingine wa Julius Kambarage Nyerere. Ukoloni wa kwanza haukuwa mbaya kuliko huu wa pili,ila tofauti yake ni kwamba ukoloni wa pili uliongozwa na Mwafrika kutoka Butiama, na ule wa kwanza uliongozwa na mzungu kutoka Uingereza. Kwa hiyo tofauti ilikuwa ni viongozi wa ukoloni, na Watanzania hawakutoka katika minyororo ya ukoloni, bali walibadilika kutoka ukoloni huu kungia mwingine ambao ndio unaowatawala mpaka leo. Kwa watu wenye mawazo kama mimi, ni heri tungebaki kama tulivyokuwa maana msaada wa kweli ungetoka popote, kuliko kujidanganya kuwa tulikuwa salama na kumbe ukweli wa mambo ni kwamba tulikuwa pabaya kuliko mwanzo .Ilikuwa kama kukimbia mvua na kuingia kwenye kibanda cha nyasi kinachovuja. huwezi kueleza tofauti maana bado unanyeshewa. Na mpaka leo Watanzani kama mimi hatujui tofauti ya kuwa huru na kutawaliwa. Ikiwa kuwa huru ni kumruhusu Nyerere kujaribia mawazo yake ya siasa ya ujamaa kwenye maisha yetu na baada a miaka 30 atuambie mawazo yake yalishindwa kwa sababu alikosea, na adhabu tuliyompa ni cheo cha baba wa Taifa, basi mtanisamehe nikisema kuwa mwacheni huyo mzee apumzike kwa amani kutoka katika dunia hii, ili akapate nafasi ya kukutana na Muumba wake ambaye akiamua kumsamehe amsamehe. Na pia akiamua kumhukumu yote ni sawa, lakini siwezi kumwomba Mungu amponye Nyerere aje kufanya nini? Ambacho hakukifanya kwa miaka yote 77 aliyoishi duniani? alitumia nusu ya maisha yake kufanya majaribio na Watanzania, na sasa Mungu atatushangaa kwamba tunamsumbua amponye. Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu, na hawezi kukubali kushiriki utukufu wake na Nyerere.Amewaona Watanzania wanamwabudu Nyerere kuliko yeye na ameamua kumchukua ili wajue kuwa wanaweza pasipo Nyerere. Tena Yeye Mungu pekee ndiye Baba wa vyote. lakini wanadamu wanamwita mwanadamu baba wa taifa? hiyo ni kufuru. Elimu ni nzuri, lakini ile inayotoka kwa Mungu.Hii ya wanadamu mara nyingi inakuwa na kasoro nyingi.na wale waliyo nayo husahau kumtegemea Mungu,na kuitegemea elimu yao ambayo mara nyingi inashindwa kuwatatulia matatizo. Elimu ya madarasani na uongozi ni vitu viwili tofauti lakini wanadamu huvutiwa sana na viongozi waliosoma wanasahau kuwa uongozi unatoka kwa Mungu. Na mara nyingi hawa viongozi waliosoma hawaongozi vizuri. Tuna mifano mingi, lakini Nyerere ni mmoja wa hao viongozi wasomi ambao hawakuongoza vizuri. Hotuba nzuri, maneno ya kushawishi akili na kupendwa na waandishi wa habari siyo cheti cha kiongozi mzuri. Na Nyerere anasifiwa kwa hiyo. Lakini ukija kwenye matendo ya zile hotuba nzuri hakuna hata kijiji kimoja cha maonyesho kuonyesha kuna msomi mmoja aliyewahi kufikiri kuhusu vijiji vya ujamaa na hiki ni kimoja ya vijiji alivyovianzisha, na watu katika kijiji hiki wanafurahia mawazo ya msomi huyo. Lakini Tanzania nzima hakuna hata kijiji kimoja cha ujamaa kilichobaki kama maonyesho ya mawazo ya msomi Nyerere badala yake Tanzania ni moja kati ya nchi masikini duniani. Na yote hayo ni matunda ya msomi mmoja waliyemwita Mwalimu wa umasikini. Sasa mambo yakiwa hivyo najiuliza kwa nini alipoteza muda kwenda Makerere kupata shahada ya DR. ambayo haikumsaidia kuifanya Tanzania mahali pazuri pa kuishi? Bado nasita katika njia mbili, sijui nimpeleke mtoto wangu Makerere apate shahada kama ya Nyerere ndipo aje agombee uongozi wa Tanzaia, au tumtegemee Mungu atupe kiongozi ambaye ataongoza vizuri hata kama hana karatasi ya chuo kikuu? Na kama Mungu anaweza kutupa kiongozi basi hata mimi niko tayari maana kile ambacho sina ni karatasi ya chuo kikuu tu.na kama Nyerere DR. anaweza kushindwa mambo mengi hivyo, basi nina hakika siwezi kushindwa kama yeye.
Kwa Watanzania ni vizuri Nyerere aondoke ili tuwe na mawazo
mapya na mbinu mpya za kuikomboa kikweli Tanzania.Hata Musa
alipokufa ,Yoshua alifanya makuu kuliko Musa Na Yoshua wa
Tanzania ni mimi Faustin S. Munishi . Malisa
"DR" Akasirika Ndugu Munishi, Tunaweza kulumbana mpaka siku Bwana Yesu anarudi na kila mmoja akabaki na msimamo wake kuhusu Mwalimu Nyerere. Na sijui hii ni kwa faida ya nani? Sitapoteza muda wangu katika hili, kazi kubwa ni kuingo'a CCM ambayo ni kikwazo kikubwa. Jambo moja ambalo nataka liwe wazi kwa wasomaji wote ni pale unapojiita Yoshua wa Tanzania. Ulinikejeli kuhusu tilte ya DR, nami sipendi kujisifu bali nataka wasomaji wajue kwamba hayanitakayo yasema kwa sehemu yanatokana na taaluma yangu katika theolojia na falsafa vilivyonipatia shahada ya juu ya udaktari hivi karibuni. Kwa wasomaji wa Biblia wanajua kwamba Yoshua ni mtumishi wa Mungu alie waingiza wana wa Israeli katika nchi ya ahadi baada ya kifo cha Musa. Munishi kama anajita Yoshua badala ya Faustin hilo halinihusu, mtu anauhuru wa kubadilisha jina lake. Lakini kujiita kwake Yoshua ana maaana ya Kujilinganisha na Yoshua wa kwenye Bibilia. Kwanza ieleweke kwamba jina Yoshua ni jina la kiebrania au kiyahudi na huandikwa Yeshua. JIna hili kwa kiyunani hutamkwa Yesu, na maana yake ni mkombozi. Yoshua aliteuliwa na Mungu kuwaingiza wana wa Israeli katika nchi ya Kaanani. Tunasoma "Yoshua mwana wa Nuni asimamaye mbele yako ndiye atakayeingia mtie moyo kwa kuwa yeye atawarithisha Israeli".Kumb.1:38 Ili kuwa Yoshua ni lazima uwe msaidizi wa Musa alie chaguliwa na Mungu. Mwalimu Nyerere kuna wakati aliwahi kuitwa kwa kejeli Musa. Sasa Munishi lini ulikuwa msaidizi wa Nyerere na sasa amekufa kwa hiyo wewe umepewa jukumu lakuwaingiza watanzania katika nchi ya ahadi? Yeshua tunajua ni Yesu, sasa ndio tuseme wewe ni Yesu wa Tanzania? Yoshua alikuwa mtii kwa Musa na alijifunza toka kwa Musa. Yoshua aliendeleza yale alioanza Musa, je wewe unataka kuyaendeleza ya nani, ikiwa huyo Nyerere kwako ni mpumbavu? Kujiita Yoshua ni kujiita Yesu unless unataka kubadilisha jina lako na kujulikana kama Yoshua Munishi. Wasomaji wenyewe wataelewa wana deal na mtu wa aina gani hapa! Ndugu
Munishi nakusifu kwa ujasiri wako, lakini ujasiri bila maarifa
ni sawa na kujaribu kukamata upepo, na sababu ya kusema hivi
inatokana na ukweli kwamba mambo mengi unayosema hayana uchambuzi
wa kutosha na mengi ni Hear say. Kwa mfano unasema Nyerere
alipata shahada ya DR. kule Makerere. Hiyo si kweli Mwalimu
alipata diploma pale Uganda na baadae akaenda Uingereza alikopata
degree ya M.A. Mwalimu hakuwahi kupata an "academic doctorate".
Degree ya Udaktari alipewa kwa heshima "Honarary Doctorate".
Ingawa wewe mwenyewe unakiri kwamba huna elimu ya chuo kikuu
bado huja chelewa. Itakusaidia na kukuwezesha kupangilia hoja
zako na hatiamae kutimiza lengo lako. Usiwachukie wasomi kwa
sababu wewe hujasoma. Nafasi bado ingalipon Munishi Ajibu Mashambulizi Tatizo la watu wanaodhani kuwa wamemaliza kusoma hupenda kujionyesha kila mahali kwamba wao wana PHD au "Parmanent Head Damage." Kwenye ukumbi huu tuna wachangia mada tu, na kuhitimu kufanya hivyo huitaji PHD au "DR" kama Malisa anavyotaka kutuogopesha na "udaktari" Na sijui kama ni udaktari wa mifugo au ule wa mitishamba. Kila mtu hapa ana elimu yake na matisho ya "DR" hayakufanyi uwe mchangiaji mzuri. Historia inaonyesha kuwa watu waliofanya makuu duniani hawakuwa na hizo PHD. Pia historia hiyo hiyo inatuonyesha kuwa watu waliofanya madudu katika maisha yao ni wale waliofikiri kuwa wanajua na kumbe hawakujua iwapasavyo kujua. Nyerere, Kaunda, Obote, wote walikuwa na kitu kilichoitwa "DR". Angalia walivyofanya madudu. Hata kama ingelikuwa ni sheria kila mwana bodi aonyeshe vyeti vyake vya masomo, hiyo isingenizuia kumuuliza Melisa atueleze ni "DR" wa aina gani, na alihitimu kutoka chuo gani. Ndivyo yafanyavyo makampuni yote kabla ya kuwaajiri watu walio na vyeti vya "PHD". Hii inatokana na udanganyifu hasa kwa hao wanaodai kuwa ni "DR" kwani wengi hupata vyeti hivyo kwa njia ya udanganyifu. Unafikiri kwa nini makampuni hupoteza muda kuwahoji watu kabla ya ajira? Sina tatizo na wasomi, kwani wasomi hasa hufanya kisomi balala ya kupoteza muda kujitangaza kuwa wao ni wasomi. Ninapomuona mtu anayetanguliza "DR" kama kinga ya kuandika hoja kwenye ukumbi huu kama alivyofanya Malisa, ninakuwa na kila sababu ya kushuku huo u "DR" wake. Mfano mzuri ni Marandu TL Kama angetanguliza kujiita DR. na pengine yeye ni DR. wa kweli, halafu awatangazie watu kuwa ana WEB SITE yake aliyoitengeneza mwenyewe inayoitwa http://www.geocities.com/tlekundayo Na kisha baada ya kuitembelea akute madudu aliyofanya hapo, moja kwa moja atamdharau. Lakini kwa kuwa hukutanguliza majivuno ya kujiita DR. mtu anaelewa kuwa ana shida kidogo na HTML na akijifunza ataboresha WebSite yake.
Elimu ni mchanganyiko wa mambo mtu anayoyaelewa kumsaidia
maishani, na siyo lazima aipate darasani. Utaratibu wa shule
ni kiwango cha wanadamu kupima ni nani kahitimu nini na wapi,
lakini utaratibu huo nao una matatizo yake kwa hiyo siyo kila
aliyepitia utaratibu huo anaweza kuitwa ameelimika. Kuna wanaosukumwa
na pesa kupita na wengine wanasukumwa na wanasiasa kwa malengo
siyo ya kupata elimu, bali kupata ushahidi wa karatasi ya
kuwawezesha kuajiriwa labda kwenye mashirika ya kiserikali,
au kugombea nafasi za kisiasa. Ndiyo maana tuna watu wengi
wanaofanya madudu katika taasisi mbali mbali. Siyo kwamba
hawana shahada, bali wana shahada bila elimu ifananayo na
shahada wanazotaka kila mtu ajue kuwa wanazo. Nasikitika kusema
kuwa Melisa ameanza kuonyesha kila dalili za kufanana na hao.
MaranduTL Abadili Msimamo Tanzania Ilipata Uhuru Wake 1961 na Rais wa Kwanza wa Tanzania alikuwa ni Mwalimu Julius K. Nyerere. Mwalimu alikuwa Rais Akiwa na Umri wa miaka 39 na alitawala kwa miaka 24 Mfululizo Mpaka alipojiuzulu hapo 1985. Kwa Kweli Yapo Mambo ambayo Nyerere aliyofanya katika Utawala wake Mazuri kupita mfano. Mfano sahihi wa kazi hizo ni Kama Jitihada za Kampeni za Kufuta Ujinga. Kwa Hili Nyerere alifanikiwa sana. La Pili ni Kutetea Uhuru wa Afrika kutoka kwa Wakoloni. mfano Namibia ,Angola, Zimbabwe Afrika ya Kusini Nk. Sioni mengine ,Kama yapo wasomaji wataniambia.
SHUTUMA ZANGU KWA NYERERE. 2) Nyerere Hakupenda kuwapa watu uhuru wakati wa utawala wake. i) Ilikuwa ni Vigumu mtu kuwa na television 2) Hata mtu kuwa na Pass ya kusafiria ilikuwa ni kazi sana. 3)Hakuruhusu Democrasia ya kweli wakati wa utawala wake. Mambo kama kutawala vipindi viwili yalikuja baada ya yeye kuondoka. 4) Vyama Vingi Vilianzishwa kwa Hila chini ya Ushauri wa Nyerere ..."Msipoanzisha Mageuzi na kuyaratibu!, yatakuja kwa nguvu na CCM Mtaondoka, lakini mkianzisha mageuzi hayo kama CCM, Vitaanza utitiri wa Vyama na vitakufa Natural death..." Hii sii kauli ya Mpenda Demokrasia. Ndio alitaka Vife.
5) Bila Kujali Mateso yatakayowapata Wananchi alifanyia majaribio
Siasa yake ya Ujamaa na Kujitegemea, hata pale aliposhauriwa
sana madhara yake. 7)Utawala wa Kidemokrasia unakuwa na Mihimili Mitatu ya Madaraka, 1)BUNGE 2)MAHAKAMA 3) SERIKALI, Nyerere aliweka sumu ambayo Mpaka sasa ipo, serikali na Rais ndiyo kinara, Mara kadhaa Nyerere aliwahi kulivuja Bunge, na Katika Kipindi cha awamu ya Pili Malecela akiwa Waziri Mkuu wameshachezea sana Maamuzi ya Mahakama. Hata sasa Mnaona Vyombo vya Dola kama Polisi na Mgambo wanavyogandamiza wananchi, hii ni tabia ya siku nyingi waliyorithi kwenye Utawala wa Nyerere. 8) Kwa Kifupi Pamoja na Mambo Machache Mazuri aliyofanya Nyerere, Amefanya Pia Mambo mabaya sana, mengine kwa Kutokujua au mengine kwa Ubinafsi ambayo Matatizo yake Huna haja ya Kunirukia Tazama Katiba ya Nchi, hila zote, ujanja-ujanja wote uliopo Umesababishwa na Nyerere. Angalia hata Raff alizocheza 1995. Kwa Kuhitimisha Niseme Kuwa Matatizo Makubwa ya Kikatiba, Haki za binaadamu na Matatizo ya Kidemokrasia yaliyopo sasa tusingeyaona kama Nyerere alikuwa ni Kiongozi mwadilifu (
Hakuheshimu haki ya Mtanzania). WEWE UTANIAMBIA ,"MARANDU
UNAWAZIMU NINI? NYERERE ALIKUWA MWADILIFU MNO" JIBU LANGU
NI KATIBA ISINGEKUWA HIVI. MIMI NISEME NYERERE HAKUWA NA TAMAA
YA KUJITAJIRISHA LAKINI ALIKUWA NA TAMAA KUBWA YA KUABUDIWA
NA KUTUKUZWA, INFACT ALITAKA AWE KAMA AKINA MAO NA KINA KIM. Kimeta Jr Ampinga MaranduTL Ni kosa kwako kubadili msimamo kwa sababu tu Mwalimui, kwa madai yako alipenda kuabudiwa. Kila kiongozi yupo hivyo. hata wewe marandu natumaini utapenda kuabudiwa baada ya kuona you are the highest authority. Lakini ningesema tu kuwa mwalimu unashindwa kumuelewa. Mambo mengine unayomshutumu kwayo aliyafanya siyo kwa nia mbaya ila kwa sababu ya muda wenyewe na hali ya kisiasa ya dunia. Mimi nitamlinda JK Nyerere kwa nguvu zangu zote. Suala la katiba siyo tatizo la nyerere pekee ni tatizo la kila mtu. Sasa hivi nyerere hayupo, wewe Marandu na watu wenye mtazamo kama wako kwa mwalimu hawajafanya lolote kubadili. Kumbuka, katiba kama dira ya nchi inaendana na matakwa ya jamii na wakati. Siamini kuwa katiba na ubaya wote ilionao ni kwa sababu ya Nyerere tu. Ni kwa sababu ya waTanganyika na baadaye watanzania wote walioitunga, kuipitisha na kuitumia. Kumlaumu JK ni kuatafuta kisingizio tu cha uvivu wa watanzania.ni suala la mbaazi ukikauka husingizia jua. Kwa hiyo bwana Marandu you were wrong from the beginning. Nyerere peke yake siyo Tanzania. Wala mwalimu hakuwa mfalme kiasi kwamba haukuweza kumpinga. Suala la vyama vingi na democrasia: mimi sielewi ni democrasia ipi unayoizungumzia. Kama ni hii democracia ya US na nchi za ulaya ni ujinga mtupu. Uchaguzi hata hapa marekani is simply a drama! vyama vingi havina maana kama nchi yenyewe na watu wake hawakotayari kwa msingi huo unaouita democrasia.
Let us not copy everythig fro US, Uk or wherever. Tunahitaji
kumlauma mwalimu kwa kungalia vigezo vya nchi yetu na nchi
nyingine za kiafrika hata za ulimwengu, lakini siyo kuiga
tu na kudai kuwa mwalimu hakuwa na ufundi wa kuiga kama sisi
kina Marandu. Hiyo unayodai ndiyo democrasia ndiyo inayoua
watu burundi ,Kenya, Kongo na sehemu nyingi, kwa sabau tu
watu kama wewe wamenakili kama kasuku anavyonakili . Mimi
nampongeza mwalimu kwa kuwa mbunifu kuliko viongozi wengine.
Mzee
Hayeshi Auliza majibu Je mchungaji Munishi ni utawala gani unaouona bora au utainufaisha Tanzania?.Inavyoonekana wewe huwezi kumkubali kiongozi yeyote atakayekuja nchini sasa unaanza kudai kuwa nchi inatakiwa kutawaliwa na mungu je ni nani atakayekuwa kiongozi wetu?. Ninavyojua mimi Tanzania inao waumini tofauti je ni dini gani unayofikiria itatutawala?. Tunataka utupe mifano ili ujaribu kuzilinda hoja zako kwani katika historia ya kiafrika hakuna nchi ambayo inajitawala kwa misingi ya kidini .Nchi kama Sudan au Nigeria wao wanasema kuwa wanatawala kidini lakini kwa kweli kitu kama hicho hakiwezi kufanya kazi na ndio maana tunaona mifano katika nchi hizo ya vita visivyoisha na kuchukiana . Hali kadhalika Zambia ingawaje nchi yenyewe ni asilimia karibu tisini na tisa na kitu lakini bado wanapata taabu kuongoza kidini.Sasa kwa kufuata mifano hiyo je wewe huoni kama unamawazo potofu sana ambayo yanaweza kuleta mifarakano katika nchi yetu?. Wakati mwingine mimi nafikiri lazima tuwe wakweli na makini wakati tukichangia hoja yaani tujaribu kuandika vitu ambavyo vinavyowezekana . Mimi siwezi au sina ruhusa yeyote ya kukubadilisha msimamo wako kuhusu mzee Julius ,lakini kwa ukweli mpaka hivi sasa hakuna kiongozi kama mzee Nyerere na kama kuna mtu aliyefanya vibweka zaidi ya mzee ,tafadhali tueleze na mimi nitakueleza vibweka vya mzee Julius. Lazima tumtazame huyo mzee kwa undani sana ,la hatuwezi kuelewa kabisa nini alijaribu kukifanya ingawaje kuna mambo hayakwenda sawa lakini cha msingi ni nia yake ambayo ninaamini ilikuwa safi ,hivyo ndivyo ninavoamini mimi kwa hiyo sijaribu kwakataza watu katika fikra zao kuhusu mzee Julius. Ukurasa wa Nyerere ulipita na hivi sasa tunaukrasa mpya ambao ndio tunahitajika kuusoma na kuukosoa kama kuna makosa yeyote yanayofanywa,lakini tuking'ang'ana na kuzungumzia mambo yaliyopita sifikiri kama tutafika popote .
Munishi: "Miaka 40 ilitosha kujua kama Nyerere Hafai " Miaka 40 ilitosha kumpima Nyerere na kumkuta kuwa alikuwa hafai. Ukurasa wa Nyerere Tanzania haujafutika ndiyo maana bado kuna watu wanaofikiri kuwa Nyerere alistahili sifa zozote. Aliharibu Tanzania na lawama ndizo zinazomstahili. Najua kwamba kumlaumu mfu hakusaidii, lakini kuuvunja msingi alioujenga kutawasaidia wale wanaojaribu kujenga juu yake. Haijalishi mbinu gani watakazotumia, lakini kwa sababu msingi wa Nyerere ni mmbovu tena haufai, kila kitakachojengwa juu yake kitabomoka. Wengine wanasema ana mawazo potovu anayejaribu kuwaonya watu wasifanye kazi bure ya kujenga juu ya msingi mbovu. Naona kuwa wao ndio wamechoka kufikiri. Miaka yao haikubali mawazo mapya. Wanafikiria kufa kuliko kuishi. Kila kitu kwao ni "HAIWEZEKANI." Wanamshuku hata Mungu mwenyewe. Ni watu wa ajabu sana. Wanaogopa msingi ukivunjwa tutaanzia wapi kujenga msingi mpya? Hawaioni nishati ya kisasa kwani wao waliishi nyakati giza. Nuru pekee kwao ilikuwa Nyerere. Alifikiri na kuwaza kwa ajili yao. Aliwaambia wasifanye chochote kwani serikali itafanya kila kitu. Wakamwamini walikosea. Wanaogelea kwenye dimbwi la umasikini ambao Nyerere aliwafundisha kukubaliana nao. Yeyote aliyejaribu kujitoa katika dimbwi hilo, aliitwa mhujumu wa uchumi ambao uliharibiwa na sera zake mbovu. Aliziamini sera zake na kuwataka watanzania waziabudu kuliko Mungu ambaye ndiye muweza wa kila kitu. Mawazo yake potovu aliyaweka kwenye kibuyu kwa jina TANU na sasa CCM. Aliwafanya watu waumini wa CCM kwa lazima kuanzia vijijini hadi mijini. Kwenye mashirika ya umma wimbo ulikuwa CCM. Majeshi yote saluti ilikuwa CCM. Na kuna wendawazimu wanaosema kuwa huo ulikuwa uzuri wa mwendawazimu mwenzi wao NYERERE. Sawa na iwe hivyo. Wana haki ya kuamini kiwazimu bila kuwazuia wengine kuamini KIUNGU. Mimi Faustin S. Munishi, nina maono na Tanzania. Kwamba Mungu anataka kuibariki Tanzania endapo tu watakubali kuyasikia mausia yake. Anasema kuwa kwa watanzania kumwamini Nyerere kuliko yeye walikosea. Watubu na waanze kumwabudu yeye, waone yale atakayowafanyia. Wasijali nani, wapi, aliyejaribu kuongoza kidini akashindwa, kwani yeye ni Mungu asiyeshindwa. Mungu hutumia watu, na katika maono haya ananitumia mimi. Binafsi mimi ni Mkristo, na siwezi kuukana ukristo kinafiki kama alivyofanya Nyerere. Alivaa kibagalashia cha kiislamu kuwadanganya waislamu kwamba yeye naye yumo. Kumbe Nyerere hakuwa Mwislamu wala Mkristo. Mwenyewe alijua kuwa alikuwa nini. Kwamba Tanzania kuna dini nyingi zinazomwabudu Mungu hiyo hainizuii mimi kusema maono yangu kwa Tanzania. Kwa sababu dini zinamwabudu Mungu na mimi nina maono kutoka kwa Mungu, sioni shida hapo. Dini zote zinazomwabudu MUNGU wa kweli tutakubaliana. Watakaoshindwa kunielewa ni wale wanaomwabudu shetani, na hao "TUTAPAMBANA" siyo kwa silaha, au mwili na nyama, bali katika ulimwengu wa kiroho. Uwezo wa kupambana nao tumepewa na Mungu. Uwezo wa kuwageuza mioyo ili warudiwe na fahamu zao wajue kuwa hakuna anayestahili kuabudiwa duniani wala mbinguni isipokuwa MUNGU peke yake, tunao. Sasa hapo ni akili kichwani mwetu tujue nini kianze! Kushawishi ? au MAPAMBANO? Lakini watu kama akina HAYESHI hao tayari ni wafuasi wetu. Wanahitaji kuoshwa kidogo bongo zao, ili kutu ya Nyerere itoke. |
||||||||||||
|
|
|
|