Ukurasa wa mbele
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail

Gazeti la INJILI
Kwenye Internet

http://www.munishi.com

Tel. 254722602445 E-mail:munishi@munishi.com Or
info@munishi.com


Hawa wanafanya nini pamoja? Mmoja ni mwanasiasa, na mwingine ni mfanyikazi katika ukumbi wa habari na {MAELEZO}.

Mheshimiwa Augostine Lyatonga Mrema, Ambaye ni Mwenyekiti wa TLP { Tanzania Labour Party}Kushoto, akiwa na mfanyikazi wa cheo cha juu katika ukumbi wa habari na maelezo jijini Dar,
Wakati akitoa habari za mateso ya mtoto wa Nyerere Marekani. Huo ulikuwa mkutano wake Mrema na waandishi wa habari. Kinachowashangaza wengi, ni kwamba mfanyikazi wa cheo cha juu ukumbini hapo, naye aliketi na Mrema. Siyo kutoa habari, bali kuchuja atakayosema Mrema. Inasemekana kwamba mtu akienda kukodi ukumbi huo ili aongee na waandishi wa habari, Lazima kwanza awekwe kiti moto na huyo jamaa na ikiwa bahati aruhusiwe kuukodi ukumbi kwa masharti kwamba naye atakuwepo kuhakikisha uliyomwambia, ndiyo utakayowaambia waandishi wa habari bila kupunguza wala kuongeza. Na huo ndio uhuru wa kutoa habari na maelezo Tanzania. Tena Mrema mpizani, ndiye anayetoa habari za mateso ya "mtoto wa baba wa Taifa" hicho nacho ni kitendawili. Alitumwa Amerika na CCM? Vichwa havikosi kuuma Tanzania wanapojiuliza kama kweli Mrema ni Mpinzani au Pandikizi la CCM. Malalamiko yake makubwa yalikuwa kuteseka kwa mtoto wa Nyerere, Leticia nchini Marekani. Ila hakusema kama mateso hayo ni pamoja na kuosha vyombo kwenye mahoteli Marekani, lakini alisema anateseka.

WAPINZANI TANZANIA MNAPINGA NINI?

Ikiwa lengo la wapinzani ni kuitoa CCM madarakani watafanikiwa kwa kazi hiyo wakati wanapomuenzi Nyerere na kwenda kaburini kwake kuomba mizimu? Au watawaambia watanzania zidumu fikra za Nyerere zilizoiharibu Tanzania na kuwaomba wawapigie kura badala ya CCM?

Ikiwa viongozi wa upinzani wanamuenzi Nyerere, kuna haja gani ya kuanzisha vyama vya upinzani? Si Nyerere wanayemuenzi ndiye mwenyekiti wa CCM akiwa kaburini? Sasa wanamuenzi mwenyekiti wa chama huku wakipinga chama chake?

Hata sera zao hazina tofauti na zile za mwenyekiti wa CCM Nyerere. Kama zingekuwa na tofauti basi wangempinga Nyerere kwanza ndipo waweze kutuambia kwamba sera zao zitaleta maendeleo aliyoshindwa kuyaleta Nyerere.

Je wananchi wanawaamini wapinzani? Nionavyo mimi na mnikosoe, ni kwamba hawaoni tofauti ya upinzani na CCM. Utapingaje kitu ambacho hujakipinga? Au niseme vinginevyo. Wapinzani wanapinga nini Tanzania kabla hawajampinga Nyerere?

Wanampinga MKAPA? Mkapa ni mbwa mwitu anayekula mabaki ya fisi. Wanapinga nini? Watuambie. Mboni ya jicho la CCM ni Nyerere. Bila yeye hawaoni mbele wala nyuma. Swali la kujiuliza ni je kweli bado jicho linaona wakati Nyerere yuko kaburini? Jibu wanalo wenyewe CCM.

Ukitaka CCM waamke na wakae chini, gusa mboni ya jicho lao Nyerere. Ukitaka wababaike wapande na kushuka, mkosoe Nyerere. Ukitaka mate yawatiririke mdomoni, sema Nyerere alikuwa mpumbavu. Ukitaka wainame kisha wainuke, sema sera za Nyerere ziliharibu Tanzania. Na ukitaka wakuite majina yote mabaya ya mizimu, waambie waachane na ukiritimba wa Nyerere. Watakuita mwizi, jambazi, kwapuzi, mbakaji, tapeli, mwisho wa yote watasema huna elimu lakini umewababaisha kiasi cha kukosa usingizi.

Ni mbinu iliyo wazi na inashangaza kwa nini wapinzani Tanzania hawaitumii. Siasa za Tanzania ni Nyerere. Kuzipinga lazima umpinge Nyerere. Sijui wapinzani Tanzania wanapinga nini. CCM? Sasa watapingaje CCM bila kumpinga Nyerere? Ndiyo maana nautilia mashaka makubwa upinzani Tanzania.

Mtu kama Mrema sijawahi kuamini kwamba ni mpinzani. Hatujaonana hatujuani lakini anisamehe kwa tathimini yangu hii. Kama kuna mtu amewahi kuwa karibu na Nyerere ni Mrema. Anazijua siri nyingi za Nyerere kuliko yeyote Tanzania. Amewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani, na mafaili yote ya siri za Nyerere anajua yako wapi. Kuanzia yale ya kumuua SOKOINE pamoja na viongozi wengi tu walioonekana tishio wakati wa Nyerere.Hakuna mtu mwenye ushahidi wa karibu kuliko Mrema.

Kwamba yuko kwenye kambi ya upinzani na hajawahi kumshambulia Nyerere kwa lolote, hiyo inatupa mashaka. Sisemi aropoke maneno yasiyo na msingi kumhusu Nyerere, bali atoboke ukweli ambao utawafanya CCM wainame na kuinuka. Yaani wakae chini halafu wasimame.Tena wasikie kwenda haja lakini isiwatoke. Lakini Mrema kimya!!! Isitoshe huenda kaburini kwa Nyerere kuomba mizimu ya huko. Kama hakuhusika moja kwa moja na madhambi ya Nyerere, basi anamfichia siri kwa sababu anazozijua yeye Mrema. Ndiyo maana wengi tunajiuliza kuna upinzani Tanzania au kifumba macho tu?

Tangu mfumo wa vyama vingi uanze Tanzania, Mrema amekuwa akitoka chama hiki na kuingia kingine kwa sababu zinazokaribia kufanana. Lengo likiwa ni kuudhoofisha upinzani nchini kuliko kufanya uimarike. Mrema amekuwa akikwamisha kila juhudi zinazofanywa na vyama vya upinzamni kuitoa CCM madarakani. Ndiyo maana tunakubaliana moja kwa moja na wale wanaomuona Mrema kama pandikizi la CCM kwenye upinzani kwa lengo la kuuharibu upinzani.

Kila chama alichojiunga Mrema, kiligawanyika mara mbili kama siyo mara tatu. Kazi yake kubwa ni kupima mahesabu ya wapinzani, na kuchukua hatua za haraka kuwakwamisha. Kuna habari kwamba wapinzani wanataka kumteua mgombea mmoja wa kiti cha urais. Hatua hiyo ni nzuri sana. Lakini kama kawaida yake, Mrema ndiye wa kwanza kuipinga na kutangaza kwamba anapinga hatua hiyo hata kama angeteuliwa yeye.

Mrema Awapongeza Afghanistan

Na Mwinjilisti Mwazembe Dar

Mwenyekiti wa TLP Mheshimiwa Mrema juzi tarehe 8-11-2001 Aliwaunga mkono Afghanistan kwa msimamo wao dhidi ya mashambulizi ya Marekani.

Aliyasema hayo juzi alipo kuwa anahutubia mkutano wa hadhara katikati ya jiji la Dar. Amesema kuwa japo ni Nchi ndogo lakini imeonyesha msimamo kwa kwa kuwa tayari kupambana mpaka damu ya mtu wa mwisho kwa kutokubali kile ambacho alikiita" vita ya Marekani dhidi ya Uislam." Amesema iliwapasa Self na Lipumba viongozi wa juu wa CUF kama kweli ni waislam kuiga mfano huu ili kupambana na ukafiri wa CCM.

Amesema CUF kwa kukubali muafaka na CCM ni sawa sawa na kuunga mkono ukafiri na kuusaliti uislam kwani CCM haina Mungu. Amesema CCM inamkataa Mungu na ndio maana juzi imepitisha sheria kuwa mtu yeyote akisema Yesu sio Mungu ufungwe.

Wakati ni haki ya muislam kusema Yesu sio Mungu na kama ilivyo haki ya Mkristo kusema Yesu ni Mungu Kama pia Ilivyo kuwa Zamani kwetu sisi Wachaga kabla ya kumjua Kristo au Muhamed mlima kilimanjaro ulikuwa mungu wetu kwa hivyo ilikuwa ni haki yetu kusema mlima huu ni mungu.

Kwa sababu muislam akisema Yesu ni Mungu kwake ni kukufuru kwa hiyo CCM inawalazimisha waislam wote kukufuru. Amesema muislam yeyote mwenye kadi ya CCM anaenda motoni kwa sababu CCM ni makafiri .

Akaongeza kwa kusoma kifungu kutoka katika Quran kinacho wataka waislam wasishilikiane na makafiri maana wakifanya hivyo hawatafika peponi. Mwenekiti huyo wa TLP amehoji kweli kwamba wakati ule wa maandamano yaliosababisha mauji makubwa ambayo hayajawahi kutokea hapa nchini Ingetokea kuwa na mke wa Self angebakwa kweli angekubali muafaka? Ukweli ni kwamba wengi wake zao walibakwa kwa sababu ya kusimama na CUF na kuipinga CCM.

Hii nini wananchi kama Self sio mbinafsi. Mrema anasikitika kwa kuchoma mwizi wa kuku, na mwizi wa urais anachwa. Akauliza mkutano tunapochoma mwizi wa kuku na wa urais tumfanye nini?

Akasema hivi sasa kuna muislamu anatumikia kifungo cha miaka 15 kwa sababu aliowa binti wa miaka chini ya 18 Huyu mtu kwa mujibu wa sheria za kislam hana makosa maali alilipa na shehe alitoa baraka.

Lakini CCM kwa sababu hawaiamini Quran Tukufu wamemfunga mtu huyu hii nini wanainchi kama sio kupinga uislam. Je mke wa mtume wa pili alimuoakiwa na miaka mingapi? watu wakasema 9 Akauliza je mtume alibaka wakasema hapana sasa kwa nini huyu afungwe? Amesema CCM wamedharau uislam kwa kufuta Kadhi mkuu. Amesema sasa CUF ni CCM B kwa hiyo akawataka wana chama wa CUF kujiunga TLP.


Contact us/ Tuandikie

Your full Names
Your E-mail
Subject
Message
   
 
Comments
Name Edwin Eliakim
Email kiedwel@yahoo.com
Subject maoni
Mzeemrema mimi ni kijana wako na nimekuwa mfuasi wako kwa muda lakini sasa nitakuchoka. Inakuwaje ufanye kazi ya kufuatilia maisha ya watu? Ina maana huyo mtoto wa nyerere ndiye mtanzania anayeteseka kuliko watanzania wote au kuna kitu unatafuta hapo mzee. Jambo la pili mzee mambo ya Quran na CCM mbona ni mambo mawili tofauti sana? Je kwa kuchukia muafaka wa CUF na CCM huoni kwamba wewe ndiye utakayeenda jehanamu? Biblia inasema heri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa mungu. Inavyoelekea kuna kila sababu ya wewe mwenyewekuona kwamba siasa zimekushinda hivyo urudi kijijini ukalime.hoja zako hizo zinakudhalilisha sana.Kama huna cha kuwaeleza watanzania kaa kimya kuliko kujichafulia jina lako ulillijenga kwa miaka mingi.
Hayo ni maoni yake Bwana Edwin Eliakim.Wewe unasemaje? Tuandikie nasi tutachapisha maoni yako hapa. Ikiwezekana taja mahali ulipo.
 
| http://munishi.com |