![]() ![]() |
![]() |
|
|
Gazeti
INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com Or fmunishi@hotmail.com Ukurutu Apendekeza Mi mawazo yangu ni kuwa Mzee Small au King Majuto au
Jangala mojawapo angefaa sana kuwa rais. Kwani ukizingatia hali halisi
ya ukapa iliyopo Tanzania hivi sasa tunahitaji Rais atakayerejesha
Kicheko majumbani. Mi naenda zangu ----- Lets Be Honest --------------------------------------------------------------------------------
Total Posts: 10 | Joined Nov. 2001 | Posted on: 8:42 pm on Nov. 19,
2001 | IP Ima Amuunga Ukurutu Mkono Mheshimiwa ukurutu, hapo umenena! Na hasa haswa akiwa
mzee small. Nadhani tutasahau ukapa wote!. --------------------------------------------------------------------------------
Total Posts: 5 | Joined Nov. 2001 | Posted on: 10:54 pm on Nov. 19,
2001 | IP Mchunguzi Awachunguza Wote Kama kawaida yake akiona mambo yanaenda asivyotaka huingilia kati. ukurutuu samahani mh .... nadhani walioanzisha
bodi hii walikuwa na lengo tofauti kidogo na wewe. ndio maana
kukawa na mgawanyiko wa hoja mbali mbali ..siasa na mengineo .
sasa mheshimiwa utanisamehe nikitumia usemi wa mvunja nchi ni
mwana nchi na hii inajithihirisha pale ninapozichambua kauli zako.
mh ukurutuu lazima tukubali wakati mwengine kutoa point za changamoto
ni muhimu na sio kila kitu ni utani tuu. naweza kusema sio kila
lazima mtu uzungumze tuu hata kama huna cha kuzungumza ..wakati
mwengine nakubaliana na wahenga waliosema kuzungumza ni kipaji
. mh lazima tuwe serious .kama ujisikii kuandika kaa kimya haitakupunguzia
kitu . asalaam ----- BY MCHUNGUZI --------------------------------------------------------------------------------
Total Posts: 33 | Joined Oct. 2001 | Posted on: 12:01 pm on Nov.
20, 2001 | IP Ukurutu Achachamaa Unaonyesha ulivyo na utumwa wa Mawazo. Hivi unaifahamu
katiba ya nchi kweli wewe Mchukuzi? Kumradhi Mchunguzi. Kwanini
Umeona Kuwa ni Kioja kwa Mzee Small au King Majuto kuwa rais.
Kwani wale sio watanzania wenye akili timamu? Nimefanya makusudi
kwani nimesoma porojo za kuwataja watu hawa na wale kisa alikuwa
Waziri zamani au ni Mbunge, Mmesahau kuwa Tanania in maelfu ya
watu wanaweza kuwa rais. Sijui Tanzania itabadilika lini. Mimi
namsifu Mmoja hapo juu aliyesema tusitaje majina bali tukuze Democrasia.
Mwisho naomba uniombe mimi na niliowataja radhi, kwani kusema
mimi ni mvunja nchi ni kunidhalilisha mimi na wale niliowataja.
Au umeona wana kasoro gani ukilinganisha na uliowataja wewe? Au
kuna mtu maridhawa kakutuma umpigie vingoma nini?. (Edited by
ukurutuu at 7:48 pm on Nov. 20, 2001) (Edited by ukurutuu at 7:55
pm on Nov. 20, 2001) ----- Lets Be Honest --------------------------------------------------------------------------------
Total Posts: 10 | Joined Nov. 2001 | Posted on: 7:59 am on Nov.
21, 2001 | IP Munishi Aangusha Bomu Kiafrika
Mtu akishakufa siyo vizuri kuusema ubaya wake maana mwenyewe hayuko
kujitetea. Lakini anapokuwa hai, hata kama ni uhai unaosaidiwa
na mitambo, bado watesi wanaruhusiwa kuusema ubaya wake ili akipona
ajirekebishe.Na asipopona basi itawabidi watesi wanyamaze kimya
wawasikilize mashabiki wake wakisema uzuri wa Mwalimu wa kuwakomboa
Watanzania kutoka katika minyororo ya ukoloni wa Waingereza na
kuwaigiza kwenye ukoloni mwingine wa Julius Kambarage Nyerere.
Hayeshi afurukuta Nimekusikia mheshimiwa Munisi lakini bado kuna
mambo sikubaliani na wewe kuhusu mzee Nyerere.Kila binadamu anaouwezo
wa kufanya makosa ,sio mzee Nyerere peke yake.Kuhusu matatizo
yanayoikabibli Tanzania kwa wakati huu ,hapo umeweza kufafanua
kiundani na kiukweli pasi na kufanya upendeleo wa aina yeyote.Lakini
swali je wewe kama rais utawezaje kutatua haya matatizo yaliyopo
nchini?. ----- www.lycos.com(/D) --------------------------------------------------------------------------------
Total Posts: 64 | Joined Oct. 2001 | Posted on: 12:58 am on Nov.
22, 2001 | IP Marandu Akosa Subira Mimi nashauri hoja ya Ndugu Munishi iondolewe
kwani imechukua nafasi kubwa sana katika ukumbi huu lakini density
yake ni ndongo mno. labda angesamaraizi na kisha akaondoa hutwo
twumatangazo twake. vinginevyo imekaa kama Hekaya za Abunuwasi
Simulizi za Esopo au Alfa Lela Ulela. Ni hoja au niite hotuba
pengine mahubiri. Na hii sii sehemu ya mambo hayo. --------------------------------------------------------------------------------
Total Posts: 65 | Joined Oct. 2001 | Posted on: 6:03 am on Nov.
22, 2001 | IP Eriksen Amkwepa Munishi Kuna mheshimiwa mmoja au wawili wanaelekea kuwa
na mawazo ya kujenga demokrasia; na siyo kumtaja mtu binafsi kugombea
uraisi. Hakuna ubaya wowote kumtaja mtu. Tunataka mtu ambaye atapanua
na kuimarisha demokrasia; na hasa kutuletea maendeleo. Halafu
hayo maelezo ya Munishi inakuwaje? Hapa sio mahali pa mahubiri.
Hayavutii kusoma. Kwa maana hiyo hayatawafikia walengwa wote.
----- Eriksen --------------------------------------------------------------------------------
Total Posts: 29 | Joined Oct. 2001 | Posted on: 6:13 am on Nov.
22, 2001 | IP Pope Ampuuza Munishi Kwa kweli huyu Mheshimiwa sana huyu (siwezi kumuita
Muinjilisti) Anatubadili muelekeo kabisaaaa hajui anataka kusema
nini wala anacho kiongea tutawakilisha maoni kutayarisha Board
kwa ajili ya mahubiri. Naomba turudi kwenye Mada Hii ni mada Serious
kuliko wanavyo fikiria watu kama Munishi Good Day --------------------------------------------------------------------------------
Total Posts: 50 | Joined Oct. 2001 | Posted on: 8:30 pm on Nov.
22, 2001 | IP Mtu Kwao Awatoa Tongotongo Nani awe Rais Tanzania ni swali ambalo kwa mtazamo wa haraka linaonekana ni rahisi kujibu na ndio maana wengi wameanza kurembea majina kama vile kwipikwipi la kupopolea embe; chochote kinachoanguka ni sawa tu. Kwanza inabidi kuelewa Rais tunamzungumza ni wa Jamhuri ya Muungano na si wa Tanganyika wala Zanzibar. Pili ni kuhakikisha kuwa Rais huyo ana uwezo na akili timamu itakoweza kumuwezesha kuleta maendeleo na kuwaondoshea dhiki wananchi na sio kuwaongezea mzigo wa maisha na kuwa ombaomba mitaani. Hivyo tunahitaji kuangalia mtizamo wake wa kisiasa wa mtu huyo. Histora inaonyesha kuwa chaguo la mwalimu Nyerere huwa karaha na kero kwa watanzania. Maendeleo yanayoonekana sasa ni mtirirko wa uongozi bora wa Mzee Ali Hassan , kama vile kuporomoka kwa elimi Tanzania tunaouona sasa ni sera mbovu za elimu za Nyerere. Inachukua muda kujua na kuonja matunda ya maendeleo. Lakini baya zaidi nikufanya Tanzania kutawaliwa kwenye misingi ya Kifalme(Kisultani mambo leo). Mfano Baba alikuwa Rais na mtoto nae na shemeji na mjomba. Hatuendi. Mambo ya akina Warioba msiyalete. Lakini kubwa zaidi tusijifanye kusahau kuwa hii ni jamhuri ya muungano na hivyo wazanzibari nao wanahaki ya kuwa rais wa Tanzania na kwa kweli historia inajionyesha wazanzibari ni wazuri sana katika uongozi na hasa wa kisiasa. Nahata haya tunayojivunia sasa bara ni matunda yalioletwa na siasa safi za rais Mzanzibari. Mengi yamechafuliwa baada ya kuondoka. Huu ukumbi tunojitapa sasa kufanya mijadala ni matunda ya Mzanzibari,Mzee Ruhsa. hatutaki kupelekwa tena kule tulikotoka na kuanza kupekuana mifukono kusachi kama unayo Colgate umeficha! Sasa ni zamu ya Zanzibar,iwe imo kwenye katiba au la! mangapi hayamo kabisa kwenye katiba ya jamhuri ya muungano na yamepindwapindwa kunufaisha upande mmoja wa muungano na yamefanyika. Nitakupeni mfano mdogo na ambao si nyeti sana. Ushirikiano waKimataifa si suala la muungano. Hivyo Zanzibar kwa kutambua hivyo waliweza kushirikiana na mataifa ya nje nakuweza kuptamisaada mingi ya kuendesha nchi yao. Bara kuona hivyo Zanzibar inanufaika ,wakaigeuza
Wizara ya mambo ya nje kuwa Wizara ya mambo ya nje na ushirikiani
wa Kimataifa na hivyo kuipiga FULL STOP Zanzibar katika harakati
za kujinasua kiuchumi. Missada sasa ikija inaishia bara. Hitimisho
RAIS ATAKEKUJA ATOKE ZANZIBAR ----- Kiroboto --------------------------------------------------------------------------------
Total Posts: 22 | Joined Nov. 2001 | Posted on: 10:39 pm on Nov.
22, 2001 | IP Mchunguzi Akurupuka Mtukwao kweli inabidi tumshukuru mzee mwinyi katika kuleta maendeleo kwa upande mmoja . Lakini mkuu napenda kukupinga vikali kabisa kuwa mzee nyerere ndio chimbuko la kuporomoka kwa elimu katika Tanzania . Mheshimiwa mtukwao, naomba ufanye uchunguzi wa kutosha . Mwalimu Nyerere atakumbukwa na kila Mtanzania katika swala la elimu . jamani mwalimu amefanya makubwa katika nchi hii sio mtu wa kumzungumza zungumza tuu. kuhusu mzee ruska ... mheshimiwa naona kicheko kama umemwona mzee ruska na serikali yake walikuwa ni viongozi bora.kwa dondoo zifuatazo naomba uniambie kama mbado upo mbado umesimama katika fikra zako. 1. mheshimiwa mtu kwako, katika serikali ya mzee ruska kulikuwa kumekithiri rushwa na uonevu uliokithiri serikali ilikuwa imeenda likizo kabisa.mfano mdogo tuu ni hawa watu wa tume ya jiji walivyokuwa wakituchanganya katika kutugawia watu watano watano kiwanja kimoja . kulikuwa hakuna utu bali fedha. 2. mheshimiwa mtu kwako ,serikali ya mzee ruska ilikuwa iliendeshwa kiswahili mno.serikali ilikuwa aina fedha kabisa . Bajeti ya serikali ilikuwa ikipagwa kwa miezi mitatu mitatu .. hivi serikali gani duniani inafuata utaratibu huu.. 3.mheshimiwa mtu kwako,serikali ya mzee ruska ilimsahau kabisa mtu wa kawaida watu kama kina Dewji ,Raza na Gulamali walikuwa majina ya kuogopwa na walikuwa na uwezo wa kufanya lolote. 4. mheshimiwa mtu kwao, serikali wakati wa mwinyi ilikuwa imeenda likizo ,kulikuwa na magulio tuu na kila mtu alikuwa na wazo moja tuu la kuchukua chake mapema... 5.Mheshiwa mtu kwao, serikali ya mzee ruska ilitutesa sana katika kutulipa mishahara yetu , bila kuwasahau waalimu waliumia mno mheshimiwa mbado upo? 6. mkapa amerudisha kitu kilikuwa kimepotea kitu kinachoitwa SERIKALI ...... Mheshimiwa mtukwao ,naomba kutoa hoja kuwa wakati umefika wa kumfikiria kiongozi atakayeweza kuendesha serikali katika karne ya ishirini na moja, nikiwa na maana kiongozi mwenye vision, mkapa kazi yake ilikuwa kurudisha heshima ya kitu SERIKALI nadhani ndio maana anabana sana wananchi. WAKATI UMEFIKA WA kumjenga mtu atayeongoza Tanzania katika msingi ya maendelo ,usawa ,haki na uhuru wa kweli sambamba na matarajio ya kila mwananchi . MUNGU IBARIKI TANZANIA ............ (Edited
by MCHUNGUZI at 11:22 am on Nov. 22, 2001) ----- BY MCHUNGUZI
--------------------------------------------------------------------------------
Total Posts: 33 | Joined Oct. 2001 | Posted on: 11:33 pm on Nov.
22, 2001 | IP
|
||||||||||||
|
|
|
|