Ukurasa wa mbele
Gazeti la injili
Nyimbo za Munishi
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail
Tuma SMS duniani
Sema nami
Sikiliza waongo
Twende kanisani
Gazeti INJILI http://munishi.netfirms.com
E-mail: munishifaustin@yahoo.com
Or fmunishi@hotmail.com

MaranduTL Ajitoa Kwenye "Forum"

 

Mheshimiwa Marandu T.L leo ametangaza kujiondoa kwake katika bodi ya majadiliano kwenye Internet. Baada ya kutumiwa kwa muda kuchangia mada katika "Foram" ambayo inalenga kumfanya Mkapa pamoja na CCM kuendelea kuitawala Tanzania kwa mabavu.

Akitangaza kujiuzulu kwake, Mheshimiwa Marandu alieleza masikitiko yake jinsi bodi hiyo isivyo na uhuru wa kutoa mawazo. Alisema hakuna sababu ya kuwaalika watoe mawazo wakati mawazo yanayotakiwa yapo."Ikiwa mlikuwa na mawazo tayari, mngeyaandika na sisi tuyasome kuliko kutuita tuchangie mawazo yetu ambayo hamtaki kuyasikia.

Ifuatayo ni sehemu ya "Forum" hiyo bila kuhaririwa.

Marandu T.L Ajiuzulu

Mheshimiwa Mmoja Mgeni amenishauri Kuwa Niache kabisa Kutumnia "Offensive Language" Ili kunusuru wanaotaka Kutoa Hoja katika Ukumbi Huu. Mimi naona situmii Lugha ili kumuudhi Mtu ila ni Mambo yananichukiza kupita Kikomo. Hata hivyo Kwa Kujali wengine, na kwa kujiepusha mwenyewe na Repacations zisizo na Manufaa. Naomba Administrator aniondoe na Nitakuwa Msomaji tu wa Hoja. Kwa Masikitiko Makubwa Natoa Shukurani na Pongezi kwa Wote. Hasa nimpendelee AIKA ameniipress sana kwa Hekima zake. Kwaherini. -------------------------------------------------------------------------------- Total Posts: 60 | Joined Oct. 2001 | Posted on: 7:38 pm on Nov. 30, 2001 | IP

Mbongo Amliwaza Marandu

Pole sana bwana Marandu TL uchungu unaokupata, si wewe tu tupo wengi lakini hatuna option zaidi ya kuangalia jinsi ya kurekebisha matatizo haya kwa sababu tukiyaachia mwisho wa siku yatatuumiza zaidi ya sasa hivi. Hivi lakini hebu tuliza hasira kidogo, kwanza nakushukuru kwa data zako nzuri sana na kutupa reference ya website ya http://www.tanzam2000.com kuhusu nchi inavyochukuliwa utajiri wake kijinga, labda nikuulize, hivi ukisikia kwa kutupa reference hii na baada ya mwaka mmoja, miwili au mitatu watu wamezifanyia kazi data zako na sirikali yetu ikarekebishwa na madini haya yakaisaidia nchi yako kwa vizazi vya baadaye vyoooote, utajisikiaje kwa kamchango kako haka? Au ukakaa kimya na hizo data na baada ya muda wa miaka kumi au ishirini ijayo wakati wewe jua limeshaanza kuchwea(kuzeeka) ukawa unawaona vijukuu vyako visivyo na hatia vinateseka na kuonewa sana na kuanza kukulaumu kwa nini ulikuwa unawanyamazia hawa waliokuwa wanaiharibu nchi yetu, utajisikiaje? Umesema vizuri sana kwenye moja ya mchango wako kuhusu madini kuwa maji yakimwagika hayazoleki la muhimu ni kuangalia mbele, wazungu wanasema "you better learn through mistakes cause most of us keep on repeating the same mistakes we have been doing". Nafikiri wewe na mimi na sisi sote ni resources nzuri sana kwa kuweza kuleta mabadiliko kwa nchi yetu, kama utakubali kuacha kutoa mchango wako na kweli uwe tayari usilaumu na wala usijelaumu na wala ya kujisikia guilty kwa matatizo yote yatakayokupata either wewe, watoto wako, vijukuu vyako au hata vizazi vyako vijavyo. Matatizo yeko, yangu na sisi hakuna atakayeyatatua hata siku moja zaidi ya wewe, mimi na sisi. Hivi vichwa vyote hapa vinavyotafakari mambo haviwezi kuleta japo kibadiliko chochote kwa nchi yetu? kama sio leo basi kesho au keshokutwa tutaweza kuleta maendeleo japo kidogo. Tuliza hasira kidogo, twende kwenye mapambano sasa, kweli huu ndio utu uzima, tutafika tu, usiwasikilize wanaotaka kurudisha nyuma mapambano haya, aluta continua!!!! (Edited by mbongo at 8:26 pm on Nov. 30, 2001) -------------------------------------------------------------------------------- Total Posts: 15 | Joined Oct. 2001 | Posted on: 8:23 pm on Nov. 30, 2001 | IP

Jogoo naye Awika mchana

muheshimiwa MarandoTL ningekuomba ufikirie upya uamuzi wako,mimi nimejifunza mengi kutoka kwako na nadhani hata wanabodi wengine ni hivyo hivyo,wewe ni msomi na unaelewa mambo mengi,utakua unatunyima busara na hekima zako,kuna msemo wa kiswahili kwamba mwanao akijisaidia kwenye mkono wako huukati bali utauosha na utamuosha na yeye. -------------------------------------------------------------------------------- Total Posts: 31 | Joined Nov. 2001 | Posted on: 10:25 pm on Nov. 30, 2001 | IP

Mchunguzi Alia Machozi ya mamba

HAYA MH MARANDU NAONA KASAFARI KAMEANZA...TEH TEH NDIO WALE WALE !! WATANZANIA WASIOPENDA KUKOSOLEWA BALI HUPENDA KUKOSOA WENZAO. MTU YOYOTE HAPA DUANIANI HAWEZI KUWA PERFECT HUNDERED PERCENT . NDIO MAANA NAKUMBUKA KALE KA USEMI KA BABU YANGU .. KUWA BINADAMU TUNAISHI KWA KUTEGEMEANA.. NAFANYA HILI UNANI-ELEKEZA / KUNIPONGEZA /KUNIONYA KUTOKANA NA JAMBO NILILOFANYA .. HII NDIO MISINGI YA KIBINADAMU. SASA NAPENDA KUSEMA JAMBO MOJA MAENDELEO NI MATOKEO YA CONTRADICTION BILA YA KUWA NA CONTRADICTION IWE MTU BINAFSI AU KIKUNDI CHA WATU HUWEZI/HAMWEZI KUWA NA MAENDELEO. NI LAZIMA KAMA MTU UJIULIZE MBONA MIMI NIKO HIVI YULE YUKO VILE AU ANAKILE NDIO UWEZE KUJITAHIDI KUFIKIA PALE ALIPO WENZAKO/MWENZIO. KWA MSINGI HUO BASI ... WENGI WAMEKIMBIA HUMU UKUMBINI ...LAKINI NASEMA KWA JINSI NIONAVYO MIMI MTU YOYOTE ASIYEKUBALI CONTRADICTION NI MTU WA KUOGOPA KAMA UKOMA.. MHESHIMIWA MARANDU MSALIMIE NDUGU YAKO MWINJILISTI ( MUNISHI)NADHANI NAYE KAINGIA MITINI KWA KUTOTAKA KUPIGWA ..JETUTAFIKA??? "NO DOUBT TANZANIA ITAJEGWA NA WENYE MOYO" (Edited by MCHUNGUZI at 11:14 pm on Nov. 30, 2001) ----- BY MCHUNGUZI -------------------------------------------------------------------------------- Total Posts: 33 | Joined Oct. 2001 | Posted on: 11:11 pm on Nov. 30, 2001 | IP

Kimeta nae Ajiengua

Mimi nina lalamika kwa sababu watu wanaondoa komments zangu.Bila shaka hao ni moderators tu.sas kama umoderator wenyewe ndiyo wa kufuta mawazo ya wengine nawashauri kujiondoa kabisa.Mimi ni wa kwanza kukupongeza kwa kujiondoa .Maana naona wengine humu ,kama kwenye ile topic ya Nani anafaa kuwa Rais baada ya mkapa wanataka tuandike mawazo yao.hao ni kina Errcksen,pope na wenzake. kama hamtakai mawazo yetu kwa nini basi mlialika watu waandike?si muandike kila kitu ninyi na sisi tuwe tunasoma tu? lakini ninafikiri moja ya tabia za binadamu mzuri ni kukubai hoja za mwingine hata kama zinachoma kama ndimi za moto. Nimechukia kuona watu sasa siyo wanamoderate ila wanataka tuandike wanachopenda..kwa maana hiyo ukumbi huu hautakuwa na maana kama hakuna uhuru wa kutoa hoja binafsi ila tu zile wale wanaojiita moderators wanziaona za msingi. kwa maneno haya najitoa kutoka kuandika kwenye ukumbi huu.Ntaandika sehemu nyingine ambako free speech is protected not abused on personal whims!. Kimeta Jr. -------------------------------------------------------------------------------- Total Posts: 14 | Joined Nov. 2001 | Posted on: 11:15 pm on Nov. 30, 2001 | IP

Mchunguzi Amwambia Nenda Salama

MH KIMETA WASALIMIE WAFUATAO HUKO UENDAKO
1. mh Munishi ( asiyekubali kupigwana kuamua kujitoa)
2. Mh marandu ( never contradiction) ----- BY MCHUNGUZI -------------------------------------------------------------------------------- Total Posts: 33 | Joined Oct. 2001 | Posted on: 11:24 pm on Nov. 30, 2001 | IP

Marandu Amjibu mchunguzi

Ndugu Mchunguzi Siondoki kwa Kuogopa Kukosolewa Kama unavyosema. Malalamiko Yaliyotolewa na Member mmoja Juu ya Kutumia Lugha ya Kuudhi yamenistua sana. Sidhani kama Ukisema Wanasiasa watanzania wamefanya "UJINGA" au ukisema Kuuza nchi ni "USHENZI AU UPUMBAVU" Unalenga Kuudhi. Kwanza Kumuudhi nani hasa au tuseme Katika Ukumbi Huu kuna wahusika Hao. Ni baada ya Kuona Hiyo hatari ya Kunyoosheana vidole hapa Ndani na ndiyo maana nimeona nitoke. Kama ni Kukosolewa nimekubali mara kadhaa kukosolewa bila ya Kunung'unika. -------------------------------------------------------------------------------- Total Posts: 60 | Joined Oct. 2001 | Posted on: 1:33 am on Dec. 1, 2001 | IP

Jogoo Lawika Tena

Bwana MaranduTL nafurahi kukuona tena,lakini kama kuna member kakulalamikia kama unavyosema hayo ni maoni yake, si lazima awe sahihi ,ni sahihi kwake yeye jinsi alivyoona,mshawishi kwa hoja ili akubaliane na wewe,ndio mjadala wenyewe. -------------------------------------------------------------------------------- Total Posts: 31 | Joined Nov. 2001 | Posted on: 4:27 am on Dec. 1, 2001 | IP

POPE Arudi Tena

Kwanza nasikitishwa na uamuzi wa Marandu T.L kama tulivyomzoea lakini huu uamuzi wako ndugu umekuwa wa jazba mno na hatujui huyo mheshimiwa kwa kukurekebisha lugha kama amekosea sana, naomba Mheshimiwa uwe na moyo wa kukosolewa, Sasa hebu fikiria kama wewe ndo ungekuwa rais wa nchi na umekosolewa hivyo na chama cha upinzani na uamuzi wako ukawa huo ni wazi watakao umia ni wengi na hautakuwa na manufaa kama wako, Katika mjadala wetu wa nani anayefaa kuwa rais nafikiri niongeze kuwa hatutaki rais mwenye jazba kama wewe mheshimiwa Marandu T.L ambaye atajiona kuwa yeye yuko perfect alwayz, No capital Nooooo. Nilikuzoea sana na mara nyingi sana nilikuwa nakimbilia kusoma post zako hata kama ni za mwiso na kurudia nyingine ila kama huo ni uamuzi wako naomba uufikirie tena.

Nikirudi kwako Kimeta Jr, jana niljaribu kukujibu hoja yako ya kuondolewa post zako Technically lakini naona bado hukuelewa bado mimi nasisitiza kuwa mtu hawezi kutoa post yako kabisa na hata isionekane kabisa kitakachoonekana ni automatic generated message kuwa the post was edited by......... on......., tu so you can "ONLY EDIT IT NOT TO DELETE IT " nimeweka kidhungu kidogo kuonyesha msisistizo !! ,Na haiwezi kutoonekana kabisa labda ulipost vibaya na hata webmaster hawezi kufuta kabisa post yako bali anouwezo wa kufuta topic yote na hiyo hata moderator anaweza ila sio kufuta post Mheshimiwa Kimeta Jr, naongea hivyo kama mtaalamu wa computer na hii Board inkuwa powered by ikonboard.com tembelea humo soma vizuri kama hutaona hiyo !! Tufanye uchunguzi na tuwe na hakika na tunachokilalamikia waheshimiwa naona wiki mbili hizi ka board kamekumbwa na pepo mbaya, ashindwe kwa nguvu za ke mwenyezi. Asalaam alleykhum. (Edited by POPE at 9:26 am on Dec. 1, 2001) -------------------------------------------------------------------------------- Total Posts: 46 | Joined Oct. 2001 | Posted on: 9:21 am on Dec. 1, 2001 | IP

Emanuel Justin Ajitetea

Sijajua kama ni hoja yangu imeleta matatizo au vipi! na kama ni hivyo ni mimi ndio niayepaswa kujikata kama Mheshimiwa mmoja alivyfanya hivi karibuni serikalini. Lakini ningependa sana kuwaomba wachangiaji wenzangu jambo moja: hebu tutulieni kidogo, tuvute pumzi halafu tuendelee. Bwana Marandu pole sana kwa hoja yangu ilyoonekana kama inakushambulia wewe, sikua na lengo la kukufikisha hapo unapotaka kwenda ila nilishauri kwamba kwa kuwa tunajitahidi kuangalia matatizo mbalimbali ya jamii zetu, basi tuwe makini tu na approach zetu. Bwana Marandu wote wanaondika hapa wanajua uzito wa hoja zako na jinsi ambavyo unaonekana kuwa mtu ambaye una uchungu wa kweli wa nchi yako, hivyo naomba tuendelee na matatizo mengine tutayatatua taratibu on the way. Kikubwa tu ni kwamba tuwe makini. Nimeona umetoa mfano wa Yesu; inawezekana ni mkristo, kumbuka Yesu mwenyewe alisema ya kwamba "ninawatuma kama kondoo kwenye kundi la mbwa mwitu, iweni werevu.......kwa hiyo ndugu yangu ninaomba unielewe tunakuhitaji, na tunahitaji hoja zako-tukubaliane approach tu- naamini tutafika, ningepata muda mzuri ningekufafanuli zaidi ili tufikie muafaka na tuone mifano mingi ya wanamapinduzi katika historia za nchi mbalimbali waliotumia "Confrontation" za ukali na waliotumia "approach" tofauti: mafanikio yake, tofauti na madhara yake. ----- Immanuel -------------------------------------------------------------------------------- Total Posts: 8 | Joined Nov. 2001 | Posted on: 9:47 am on Dec. 1, 2001 | IP

Masai Na rungu Bodini

Basi.
Hata mimi tatoka hapa. Hii watu iko ubakusi ya viungo.
Kwa sababu meno yangu ni nyaupe kama masiwa na yao ina rangi ya shaba ndio haitaki mimi hapa.
Tena masikio yangu ni murefu kidogo, na ya kwao iko mufupi ndio maana imefuta mimi.
Basi.
Mheshimiwa marandu pole sana.
Hata mimi takaa kidogo nikiona inaendelea kufuta mawaso yangu nitakuja huko tukae pamoja.
Basi.
Lakini ukiamua kurudi, pia ni musuri tu maana ile mutu kumbafu ndio haiwesi kubadilika.
Basi.
Lakini wewe siyo kumbafu ndiyo maana hata ile moshungaji Monish ilikuwa imeweka katika timu yake.
Basi.
Ukiamua kukaa sawa. Ukiamua kwenda sawa. Ukiamua kurudi sawa tu.
Ukiamua kwenda upumusike kidogo halafu urudi, itakuwa sawa saidi. Basi.
----- Musee ya Boma -------------------------------------------------------------------------------- Total Posts: 28 | Joined Nov. 2001 | Posted on: 12:10 pm on Dec. 1, 2001 | Itaendelea

 
| http://munishi.netfirms.com |
 
<<Back  |  Home |  Gazeti La Injili | Injili2 | Nyimbo Za Munishi | Next >>