Ukurasa wa mbele
Gazeti la injili
Nyimbo za Munishi
Soma barua Yahoo
Soma barua Hotmail
Tuma SMS duniani
Sema nami
Sikiliza waongo
Twende kanisani
http://munishi.netfirms.com
Gazeti La Injili

E-mail: munishifaustin@yahoo.com
Au fmunishi@hotmail.com

http://munishi.netfirms.com

Katiba Mpya Tanzania

Katiba ni MENU ya msingi wa nchi. Ndiyo inayosema msingi ulichimbwa kiasi gani na unaweza kubeba ghorofa ngapi kwenda juu.Pia inatueleza kokoto saruji na mchanga zilichanganywa sawa au la. Ukiisoma katiba utajua ni kwa nini nyumba hii tunayojaribu kuijenga ina nyufa kiasi hicho na ni karibu kuanguka.

Ikiwa tumeisoma katiba ituambie kila kitu kiliwekwa sawa halafu tukijaribu kuongeza ghorofa inaporomoka, Kitaalam tunamwita mhandisi wa kwanza atueleze kama kweli msingi ulijengwa sawa na Katiba inavyosema akisema ndivyo tutamuuliza mbona nyumba ina nyufa? Aseme sijui muulizeni mhandisi wa pili maana mimi niliweka msingi na kujaribu kuijenga kwa miaka zaidi ya 30 ikanishinda nikampa Mhandisi wa pili.

Kitaalam hatutachoka ila tutamwita mhandisi wa pili na tumuulize vipi mbona pamoja na "ruksa" nyumba bado ilikuwa na nyufa? Aseme Nilimwambia mhandisi wa kwanza msingi ulichimbwa vibaya kwa hiyo ilitakiwa uende chini mpaka ufikie MWABA. Na kwa sababu msingi uko kwenye jiwe jepesi linaloitwa ujamaa na kujitegemea bila Mwamba ambao ni Mungu Ndio maana nyumba haikosi nyufa.

Nilimwambia tuvunje nyumba na tuchimbe msingi upya akaninyooshea kifimbo na kuniambia thubutu!!! Mhandisi wa pili aendelee kusema alijitahidi hivyo hivyo kuziba nyufa na kuendelea kujenga lakini aliruhusu vijengo vingi vya chini ili kuepusha kuporomoka kama angeendelea kujenga kama mhandisi wa kwanza alivyotaka ajenge. Amalize kwa kusema jitihada zake za kujaribu kurekebisha hazikumaliza nyufa, na kwa sababu ya kujaribu kutumia akili yake ili kuiokoa nyumba isiporomoke walitofautiana na huyo mhandisi wa Kwanza aliyemwambia kuwa ameigeuza ikulu yake kuwa mahala pa biashara. Isitoshe anaongozwa na mwanamke. Kwa hasira huyu mhandisi wa pili alimjibu kuwa huwezi kunitukana matusi ya nguoni. Nyumba uliiharibu mwenyewe na ulisema wazi kwamba ulikosea, ukaniita niirekebishe, na tayari nimekuambia inataka nini ili irekebike, na wewe hutaki niirekebishe bila ruksa yako. Sasa mawili chukua nyumba yako uendelee kuijenga mwenyewe.

Ndipo mhandisi wa kwanza alipomwita kijana wake akamkabithi nyumba aendelee kuijenga siyo kama yeye anavyotaka bali asikilize kutoka kwa mhandisi wa kwanza. Kijana akajitahidi kukusanya kodi mpaka wananchi wanamwita Bwana kodi lakini nyufa bado ziko. Kwa bahati mbaya huyo mwanzilishi akafariki. Sasa kijana amechanganyikiwa hajui aanzie wapi.

Kitaalam tutamwambia aivunje nyumba yote na asiogope na aanze upya na tuweke katiba mpya. Pia msingi tuuchimbe mpaka ufikie MWAMBA . akianza kufanya hayo hata mimi nitamwita Rais wa jamhuri ya muungano wa TANZANIA. Ikiwa hajui atafanyaje niko tayari kumsaidia kwa kila jambo siyo lazima niwe Ikulu au kwenye baraza lake la mawaziri la hasha. Mimi nitabaki hapa hapa nilipo.

Kwetu kuna ndege ambaye akiona nyoka analia sana. Watu walio karibu wanaweza kufanya makosa ya kumfukuza huyo ndege maana kelele yake inawasumbua.Kumbe wanamfukuza mtu ambaye alitumwa na Mungu kuwaonya kuhusu hatari iliyo mbele.

Wakati wa kampeni ya uchaguzi uliopita .Mungu alinionyesha kwamba kuna hatari inayolijia taifa letu kwa hiyo niwaambie watawala nini cha kufanya. Nikajaribu kwenda Redio Tanzania nikiwa na CD yangu ya maonyo kwa viongozi. nilifukuzwa kama mbwa na kuambiwa chochote kinachohusu dini niwaone CCT kwanza ili wanipe ruhusa. nikaenda CCT wakaniambia hawaamini kuwa Mungu anaweza kuzungumza na mtu. Nikaenda ITV na wao wakasema chochote kuhusu dini hawagusi. Nikajaribu nimwone mwandishi wa habari mwenzangu ninyi mnamwita Rais Mkapa pale ikulu. FFU walipoiona benzi yangu ya zamani 1971 tena ikiwa na namba za Kenya walinitoa mbio na kuniambia mheshimiwa hawezi kuniona. Nikarudi Nairobi na kuamua kutuma FAX kwenye vyombo vyote vya habari Tanzania Kenya na nchi za magharibi. cha ajabu wote walipuuzia ujumbe huo.*(Sasa hapa naomba webmaster asisome maana atasema ninahubiri.)

Nikarudi Nairobi akili ikaniambia nitunge wimbo na ndani ya huo wimbo niweke maneno kwamba: CCM alianzisha Nyerere,Sasa imezeeka, Sera zake zimeharibu hii nchi, Msiwarudishe madarakani kabisa. Lengo lilikuwa wakubwa wasikie waliulize niweze kuwapa ujumbe niliokuwa nao. Matokeo yake Serikali ilipiga marufuku hiyo kanda na wote waliokamatwa na kanda hiyo waliwekwa ndani Zoezi hilo lilifanyika nchi nzima.

Hawakuniuliza hawajaniuliza na sijui kama wataniuliza. Uchaguzi ukafanyika waliosema wameshinda wakasema. na walioshindwa wakaandamana mauaji yakatokea. Hawakuniuliza hawajaniuliza na sijui kama wataniuliza. Hatari ile iliyokuwepo wakati ule bado iko tena ya sasa ni kubwa zaidi. Mungu ananionyesha yale yanayopangwa kufanywa nikiyaandika wengi hawanielewi.wengine wananituma Mirembe, wengine wanafikiri nataka kuwa Rais, yaani kila mtu anafikiri lake.

Nawashukuru waheshimiwa wananchi wote kwa kunisikiliza kwa leo nitakoma hapa. Singependa chochote kibaya kiipate Tanzania, kwani na mim ni mtanzania. Mimi ni mjinga ambaye akielimishwa anaelewa haraka. Mpumbavu ndiye asiyebadili msimamo.Ikiwa Mkapa atakubali kunisikiliza nitamwambia nini cha kufanya kuiepusha nchi na vita ya kidini ambayo inaonyesha kila dalili ya kuanza.

 
| http://munishi.netfirms.com |
 
<<Back  |  Home |  Gazeti La Injili | Injili2 | Nyimbo Za Munishi | Next >>