www.munishi.com/mobile
Site Loading. PleaseWait. Rich in Images

MUNISHI'S VIDEO ON YOUTUBE - GTV
Munishi aachilia DVD Mpya. Ni nyimbo za kitambo Lakini ametengeneza Video yake na kuzifanya mpya tena. Inaonekana nyimbo za msanii huyu hazitishwi na muda. Badala yake zinashamiri kila miaka inavyopita. Zilirekodiwa 1990 na 2008 Video yake imetoka. Ina viwango vya kimataifa. Picha ya cover inazungumza yenyewe. Imechomolewa kwenye video yenyewe. GTV tv ambayo bado ni ndoto za Munishi ndiyo iliyofanya kazi ya kuitengeneza video hii. Inasifika kwa kutengeneza VOL 7 na 6, na sasa imekuja na Vol. 3. Utaipenda. Itafute. MATANGAZO YUKO WAPI?


CBC CHURCH NAKURUEast Africa Gospel Artists Tanzania

Gazeti INJILI
Kwenye Internet
-
http://www.munishi.com

Tel. 254722602445 E-mail:
munishi@munishi.com or info@munishi.com
Kenedy Ochieng Asema ana UKIMWI Mugabe na Mkapa lao moja
Gospel tape banned by Dar officials Vituko Makanisani Sokoni Gikomba
Munishi Magazetini


Kikwete akiwatapeli Media. Ni kawaida yake kukutana na wahariri wote wa vyombo vya habari na kuwaarifu kile anachotaka kipewe kipaumbele kwenye MEDIA. Kazi ya msemaji wa serikali, anaifanya Rais mwenyewe. Katika kujifanya kujua kila jambo, siku hiyo kikwete alitoa matamshi yaliyoonyesha kwamba Tanzania inataka kuivamia Uganda. Habari Zaidi VIDEO



TVT wapiga debe wa CCM


Wanahabari Tanzania, hasa wale wanaofanya kazi katika vyombo habari vya serikali, ni vibaraka wa serikali. Wanaegemea upande wa serikali hata kama serikali husika inakiuka haki za binadamu. Tangu enzi za Nyerere vyombo vya habari Tanzania viligeuzwa kuwa wasemaji wa serikali. Nyerere aliitumia sana redio Tanzania Dar es Salaam kueneza injili yake ya ujamaa na kujitegemea. Matokeo yake yakawa ni kushindwa vibaya kwa siasa ya ujamaa jambo lililopelekea afya ya Nyerere kuzorota na hatimaye kuiaga dunia. Soma Zaidi


Waciama Kutua London kwa kishindo

Kiboro ametoka Nation yakarabatiwa


Gazeti la Nation kwa mara nyingine wamegeuza sura, Baada ya mkurugenzi wa zamani bwana Wilfred Kiboro kunyeshwa mlango. Mkurugenzi mpya amekuja na mbinu mpya. Ana kibarua kizito kurudisha heshima ya Nation kama gazeti linalozingatia maadili ya taaluma ya uandishi habari Soma Zaidi

Nani angewahi kufikiri kwamba Kibaki siku moja angewahi kuwaamuru Polisi wamrushie mabomu ya machozi Raila Odinga? Mtu aliyesema KIBAKI TOSHA na akatosha. Kweli katika siasa chochote chweza kutokea. Na hatujui ni mengine gani yatakayotokea tunapoelekea uchaguzi mkuu Kenya. Ulikuwa mkutano wa Maombi ambao wahusika walikuwa na nia ya kuiombea Kenya iondokane na kivuli cha ukabila kinachotishia kuifunika Kenya. Serikali ilitumia Polisi kuupiga marufuku mkutano huo dakika za mwisho, jambo lililopelekea wahusika kuikaidi amri ya polisi na kuzusha rabsha zilizowaacha wengi wakiwa wamejeruhiwa. Je kwa nini serikali isingeruhusu mkutano huo na watoe ulinzi badala ya kuusambaratisha? Serikali inadai Usalama Nairobi umezorota na hawataruhusu mikutano yeyote jijini. Habari Zaidi



Msafara wa Moi ajalini


Rais Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Daniel Toroitich Moi, akiuguza majeraha aliyoyapata kwenye ajali iliyohusisha msafara wake, lakini gari iliyogongwa ni ile iliyokuwa imembeba yeye.Maswali mengi yameulizwa, lakini majibu yake yatatoka kwa mkuu wa Polisi. Iweje gari iliyombeba RAIS igongwe wakati zile za walinzi ndizo zilizopaswa kugongwa zikimlinda RAIS? Je lilikuwa jaribio la kuyakatiza maisha ya Moi? Kibaki Rais wa sasa Kenya analionaje hilo? Marekebisho gani serikali itayafanya katika kikosi kinachomlinda Rais wa zamani? Kuna mtu atakayefutwa kazi kufuatia ajali hiyo? Habari zaidi

UJAMAA ULISHINDWA TANZANIA

Ikiwa ndio kwanza inajitayarisha kurusha matangazo yake, GTV imekuwa tishio kwa Serikali Tanzania. Aliyekuwa Rais wa kimabavu nchini humo William Benjamin Mkapa aliamuru polisi wawatie mbaroni wote watakaopatikana na VCD za GTV. Kisa ni kwamba Gospel Television ilikuwa imezungumzia uwezekano wa Mkapa kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa kutumia madaraka vibaya. GTV ilikuwa imedai kwamba, Mkapa akiwa madarakani aliwaamuru POLISI wawaue Wazanzibari zaidi ya 70 kwa kosa la kusema CCM Chama Cha Majambazi hawakitaki. Pamoja na mambo mengine GTV ilipendekeza tume ya kumchunguza Mkapa iundwe na akipatikana na makosa sheria ichukue mkondo wake. Pia GTV ilidai kwamba Mkapa aliitawala Tanzania kama mali yake binafsi kwani hakutaka ushauri wa mtu yeyote. Bado msimamo wa GTV ni huo na hatuombi msamaha kwa Mkapa wala CCM. Habari Zaidi

Machozi ya Uhuru


Kiongozi wa Upinzani Kenya Bwana Uhuru Kenyata akilia machozi ya Uhuru
Tatizo la wachuuzi halitafutiwi dawa makusudi. Wanasiasa huwatumia wachuuzi wakati wa uchaguzi.Wengi wa wapiga kura katika nchi za Afrika ni masikini wanaojitafutia riziki kwa njia za kuchuuza biashara ndogondogo. Siyo dhambi kufanya hivyo. Wafanyibiashara wakubwa huanza kwa kuchuuza kwanza. Kwamba wanasiasa watawaamuru polisi wawamiminie wachuuzi risasi za moto vichwani, hilo linatisha. Sambamba na hilo, hatuungi mkono hatua ya wachuuzi kulipiza kisasi kwa kumuua askari polisi. Wote wamekuwa wauaji. Lakini haiingii akilini kuona polisi wa Kenya wakiwaua raia wa Kenya kwa kosa la kujitafutia riziki zao za kila siku. Hata kama Nairobi inatakiwa kuwa safi, lazima usafi huo uwe wa kiwango cha nchi changa za kiafrika ambazo umasikini uko kwa kiwango cha kutisha. Kuigiza usafi wa miji ya nchi zilizoendelea, kutaigawa nchi katika matabaka ya matajiri wachache wasiotaka kuona masikini karibu nao. Tunaomba isifikie mahali pa kutungwa sheria inayosema kuwa masikini ni kosa linalopaswa kuadhibiwa kwa kupigwa risasi kichwani au kifuani? Habari Zaidi



Kikwete Sera Mbovu
Anaendeleza mbinu za Nyerere kuwatisha raia

Miezi mitatu madarakani, Kikwete ameanza kutumia mbinu za Nyerere kuwatisha raia Tanzania. Anawatuhumu wananchi kwamba mali walizo nazo hawakuzipata kihalali. Hii ni mbinu ya Serikali kuhakikisha mali zote Tanzania ziko mikononi mwa watu wanaodhaniwa siyo tishio kwa CCM. Ni zoezi la kisiasa kukiimarisha chama tawala. Kwamba Kikwete anatumia mbinu hizo wakati huu, inashangaza. Nchini Tanzania wenye mali kihalali ni wanachama wa CCM na viongozi wake. Wengine wote hata kama siyo wanachama wa chama chochote cha kisiasa, wakiwa na mali CCM hawalali usingizi. Watatunga mbinu za kuwaita majambazi wakati wenyewe ni majambazi nambari wani.




Kikwete Azimia
Azimia Jangwani kwenye mkutano wa lala salama, Magazeti yaandika ana UKIMWI, Wengine wasema Mwisho umeifikia CCM. Wengine wasema ni Mkono wa Mungu kuwafundisha adabu CCM

Walikuwa wakimsikiliza Kikwete kwa makini. Uwanja ni Jangwani jijini Dar. Ilikuwa siku moja kabla ya uchaguzi. Akiwa katikati ya hotuba yake iliyokuwa ikirushwa moja kwa moja kwenye TV na Redio Tanzania, Kikwete aliomba maji. Kabla ayafikishe mdomoni, magoti yalililegea na kuuacha mwili wa Kikwete kupigiza chini kama nyani aliyekosea tawi. Mkapa na walinzi wa kikwete walipigwa na butwaa kiasi cha kubaki midomo wazi. Umati ulionekana kuchanganyikiwa wasijue cha kufanya. Walinzi walikurupuka kumkimbilia Kikwete ambaye tayari alikuwa chini. Waliwaamuru wapiga picha waelekeze kamera zao kwa wananchi wakihofia kwamba Rais mtarajiwa ameiaga dunia. ITV kibaraka wa CCM walikatiza matangazo yao. TVT TV ya Propaganda za CCM nayo haikuwa na jinsi ila kuwatangazia watazamaji kwamba Kikwete alikuwa mzima na wasiwe na wasi wasi. Bila kujua kwamba matamshi hayo ndiyo yaliyowapa watanzania wasiwasi. Hata Kikwete alipoongea masaa mawili baadaye, watu hawakuamini ni yeye. Ndiyo maana wana CCM wengi hawakujitokeza kupiga kura wakihofu watakuwa wakichagua kivuli na siyo Kikwete. Kwa sasa mtizamo wa Watanzania ni kwenye AFYA ya Kikwete. Je ni mgonjwa kama ilivyodhaniwa? Habari Zaidi

Kibaki ajenga Hospitali ya kisasa Nairobi

Dr. Dan Gikonyo na mkewe Betty, mbele ya hospitali ya kisasa iliyojengwa katika mtaa wa Karen Nairobi. Dr. Gikonyo ni daktari binafsi wa Rais wa Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki. Hospitali hiyo yenye mitambo ya kisasa, inasadikiwa kuwa ya kipekee Afrika. Inaweza kufanya mambo mengi ambayo viongozi wa Afrika hulazimika kwenda ngambo kutibiwa. Kwamba Kibaki alifikiria kujenga hospitali kama hiyo Kenya, ni hatua inayostahili kupongezwa. Lakini gharama za matibabu katika hospitali hiyo ni za juu kiasi kwamba matajiri tu ndio watakaoweza kumudu. Itambidi Kibaki afikirie jinsi ya kuiboresha hospitali ya Kenyatta ambayo ndiyo hospitali ya rufaa nchini Kenya ili wananchi wa kawaida waweze kumudu gharama za matibabu. Vinginevyo itaonekana kwamba matajiri pekee ndio wanaostahili kuishi Kenya, na wengine wapotelee mbali. Zaidi

Gharama ya kuwa na gari Nairobi


Siku hizi ukifanya kosa barabarani, utakutana na hawa jamaa. Watakupiga, halafu wataamua wakushitaki kwa kosa gani, na kisha upelekwe mahakamani kama hutaongea lugha wanayoijua. zaidi

Nyumba yageuka KABURI Nairobi

Back to School But...

Anaitwa Ruth Wanjiru. Anamlilia mama asimwache Shuleni. Mpiga picha BONIFACE MWANGI alipokuwa katika ziara ya shule za Nairobi, alimkuta Ruth akijigaragaza chini akilia.Kwake, ni nani kama mama? Japo jina la Shule ni GLAD TOTO NURSERY SCHOOL, ikimaanisha toto lenye furaha, Wanjiru alionekana kutokuwa na furaha siku yake ya kwanza Shuleni hapo. Sababu ni kwamba kuna watu walioamua kumtoa nyumbani na kumpeleka shuleni bila matakwa yake. Haijalishi wazazi wanapenda kiasi gani watoto wao waende shule, Lakini kama watoto wenyewe hawajui maana ya shule, watakuwepo kuwaridhisha wazazi, na elimu ya kweli wataipata watakapohitaji au watakapolazimishwa na hali ya maisha. Je tuwaache watoto mpaka watakapoiona maana ya elimu ndipo tuwapeleke Shule?
Habari Zaidi

"CCM Wakiniua Mnizike Kenya

"CCM Wakiniua, Mnizike Kenya." Asema Munishi. "Siyo kwamba nimebadili uraia, wala sitarajii kufanya hivyo.Mimi bado ni Mtanzania. Sikuchagua kuzaliwa Tanzania, lakini nitachagua pa kuzikwa.Serikali za CCM zimenifanya nisiwe na mahali ninapoweza kupaita nyumbani ndani ya nchi yangu. Kosa langu ni kusema CCM sera zake zimeiharibu Tanzania, na hawafai kuwa madarakani.Makachero wa Tanzania wamekuwa wakitumia kila mbinu chafu kuwasumbua na hata kuwaua wote walio na uhusiano wa karibu na Munishi. Ajabu ni kwamba Munishi mwenyewe akienda Tanzania wanafuatilia nyendo zake bila kutishia kumuua. Akiwa Kenya ambako ndipo sanaa yake ilimpatia uwezo wa kununua nusu ekari ambapo amejenga nyumba ya mabati kujisitiri na jamii yake, bado makachero hawaishi kumvamia kama majambazi, na kutishia kumuua. Munishi akiwaeleza wanahabari kwamba wavamizi walidai kutumwa, wao wanaandika kwamba ni majambazi wa kawaida. Walijuaje kama ni majambazi wa kawaida? Tena wangejuaje kwamba siyo majambazi wa kawaida? Basi kwa nini waandike ni majambazi wa kawaida? Mbaya zaidi wanasema Munishi ndiye aliyewaambia wakati sivyo. Mtu akikuuliza je! unaona waliokuvamia kama ni washindani wako kibiashara? Na jibu likawa ni vigumu kujua kwa hakika wavamizi wangu ni kina nani, Lakini walidai kutumwa na watu ambao hawakuwataja. Je hapo utakuwa umesema kwamba majambazi hawakuwa washindani wangu kibiashara bali ni wa kawaida? NATION wanapaswa mara moja kumjibu Munishi kwani mahojiano aliyanakili kwenye simu yake Habari Zaidi

KIBAKI AJICHIMBIA KABURI KISIASA
Kosa la Simba kumwachia fisi windo lake
WAKENYA WASEMA NO KWA KATIBA KIELELEZO- PIGO KWA KIBAKI

Wahenga zamani walisema, Simba ni mwindaji hodari.Akifanya kosa la kumwachia fisi windo lake, Basi mafisi wataitana kwa kicheko, na kabla simba ajue nini kinaendelea, wingi wa fisi utamzuia kujaribu kudai windo lake. Pengine arudi msituni akawinde, au afe njaa. Kusema ajaribu kunyakua windo mdomoni mwa fisi, atahatarisha maisha yake. Isitoshe mabaki aliyoacha fisi, hayafai kuliwa na yeyote.Mfupa uliomshinda FISI hata simba hauwezi. Bora akawinde. Inaonekana Raila ameamua kuwinda na tayari amepata. Kama kawaida KUNGURU Fisi na Mbwa mwitu wanajiandaa kujaribu bahati yao ili wapewe ngaa mnofu kidogo.Swali ambalo wengi wanajiuliza ni je safari hii atakubali kuachia windo lake kwa yeyote? Tunasubiri tuone.Habari zaidi

Mchungaji Alaani Mauaji Zanzibar

Mchungaji Mmasi wa TAG Kibosho Moshi nchini Tanzania, Amelaani vikali mauaji ya kisiasa yaliyofanyika Zanzibar hivi karibuni. Akiongea na GOSPELGTV mjini Nairobi, Mchungaji Mmasi alisema kwamba serikali ina mkono mrefu, lakini mkono huo unapotumika kuwanyamazisha wapinzani kwa gharama yeyote, hapo ndipo serikali inapokosea. Aliitaka Serikali ya CCM ijue kwamba mkono wa Mungu ni mrefu kuliko wa serikali. Habari Zaidi


CCM Wameanza tena kuua
Nchini Tanzania Wanaopinga CCM chama kinachotawala kwa mabavu, Wanauawa.


Chuki ambayo Serikali ya CCM inaipanda mioyoni mwa Watanzania, siku moja watavuna matunda yake. Mkapa anamaliza muda wake vibaya. Asifikiri wale anaowatesa akiwa madarakani, watamwacha aishi salama wakati atakapoachia madaraka. Pesa alizowaibia Watanzania zitakuwa chungu kila senti. Inashangaza Amerika wanamsakama Saddam Hussein na wanamwacha Mkapa awaue Watanzania apendavyo.
Mungu atatulipizia kisasi.
Chuo Kikuu waikana CCM
Wasema hawaoni sababu ya kuwarudisha CCM madarakani

(Picha na Mroki Mroki)
Wanachuo wa Chuo Kikuu Dar es Salaam UDSM wakiandamana Dar kupinga sera za Serikali ya CCM.
Wanaitaka Serikali kupitia bodi ya udhamini wa wanafunzi wa elimu ya juu HESBL, Kuwalipa haraka pesa zao za kujikimu.Walidai hiyo ni haki yao na hawaoni sababu ya Serikali kutumia pesa za walipa kodi kufanyia kampeni za CCM, huku wanafunzi na wananchi wakishindwa kujikimu kimaisha.Walisema Tanzania siyo mali ya CCM na TRA, bali ni ya Watanzania wote na wanachuo wakiwemo. Waliongeza kwamba hawaoni sababu ya kuirudisha CCM madarakani ikiwa mbinu zao ni kuitumia TRA kama silaha ya kuwatisha wananchi ili iwaibie mali zao. Walisema kwamba wanafunzi na wananchi wamekondeana kwa njaa, huku viongozi wa CCM na wafanyikazi wa TRA wakivimbisha matumbo kwa pesa za umma. Walionya kwamba wizi huu wa mchana lazima ukome. Habari zaidi

'Arusha Times' waiba Story ya 'NATION'
Kumbe magazeti huibiana habari?

Ajabu ni kwamba STORY iliandikwa kwanza na Daily NATION, na badala AT waseme waliikopi kutoka Nation, wao wanajifanya kwamba story ni yao, tena wanadai imeandikwa na Staff Reporter wao.Waandishi wa habari wanapoibiana habari, nini hawawezi kuiba? Gazeti la waswahili wanaoandika kiingereza, siyo ajabu wakiamua kuwa majambazi waibe story zilizoandikwa kwa kiingereza sanifu.Kama kizungu kinawapiga chenga, si wawasiliane kwa lugha wanayoijua kuliko kuamua kuwa majambazi wa habari? Habari Zaidi

Meet The Kioko's

Mr and Mrs Kioko in Nairobi
Bwana anapofanya kazi tofauti na mkewe, lakini bado wanakuwa na lengo moja. Habari Zaidi


TV zinaposhindana
Vs

NTV Wavuta viatu badala ya Soksi
Kuboresha NTV Haimaanishi kupora watangazaji kutoka KTN. Badala yake inaonyesha uvivu wa kutengeneza watangazaji wenu, au kuwatafuta wapya.
Baada ya kurupushani na Lucy, sasa Nation wanaonekana kushika adabu. TV yao wanasema itatuwasha badala ya sisi kuiwasha.Wengi wametafsiri hiyo kama ongezeko la vipindi vinavyohusiana na "ngono" Tayari wameanza kuonyesha nyimbo ambazo waimbaji na wachezaji wako nusu uchi kama siyo uchi kabisa. Ikiwa walimaanisha kuiwasha jamii kwa jinsi hiyo, basi wamekosea. Tunatakiwa kulaani vipindi vya ngono kwenye TV. Na Nation wajue hivyo..Habari Zaidi

CCM sasa ni 'Mzoga'

Yalianzia viwanja vya KARIMJEE Dar es Salaam, na kumalizikia Mnazi Mmoja. Yalikumba wa kila rika.Walisema ni maandamano ya kuchangia watoto yatima, Lakini ujumbe kutoka mioyoni mwao ni kwamba CCM OUT.Watanzania wengi wamechoshwa na KERO za CCM. Woga unawafanya waseme wasiyomaanisha.Siku ya kufa nyani, miti yote huteleza. CCM ni Nyani ambaye siku ya kufa kwake imefika. Haijalishi ujuzi wa miaka arobaini kuparamia miti, Lakini safari hii miti yote inateleza. Watapigiza chini kwa kishindo, na ndio mwisho wao. Watanzania tunataka ENZI MPYA bila CCM. Habari Zaidi

Mkurugenzi wa EATV afariki
Je alitolewa sadaka kwa Shetani?
Web Site ya Gospel kusheherekea machungu ya wengine?


Mkurugenzi mtendaji wa East africa TV na Redio bwana Rodney Mutie Mengi amefariki mjini Dar es salaam Oktober 6 2005. Bwana Mengi mwenye umri wa miaka 31, atakumbukwa na wapenzi wa muziki katika EATV. Akiwa mkurugenzi, EATV pamoja na redio yake ilishika kasi katika miji mikuu ya mataifa ya Afrika ya Mashariki. TV hiyo ambayo imekuwa maarufu kwa kuonyesha miziki ya kidunia inayotukuza ngono na ufahari, ilikuwa kero kwa waumini wa dini. Haikujulikana mara moja kilichosababisha kifo chake, ila Taarifa tuliyoipata kutoka gazeti la NIPASHE, ilimkariri baba wa Marehemu ambaye pia ni mmiliki wa utitiri wa vyombo vya habari akisema kwamba mwanawe ameiaga dunia. Tangu kifo chake, Vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Mengi baba wa Marehemu, vimekuwa vikiripoti watu mashuhuri waliofika kutoa rambirambi zao badala ya kuelezea kilichosababisha kifo cha Mkurugenzi huyo. Tayari kuna uvumi mitaani, lakini GOSPELGTV inawaomba wanaoeneza uvumi waache. Wakati huu wa majonzi utumike kuwapa pole jamaa na marafiki wa marehemu, ili kama EATV itampata mkurugenzi mpya, asikie kilio cha wengi kwamba TV hiyo inaupotosha umma kwa miziki yao inayotukuza picha za ngono. Ikiwezekana wazipatie nyimbo za GOSPEL kipau mbele na Mungu atawabariki. Hata hivyo GOSPELGTV tunawapa pole jamaa na marafiki wa marehemu. Mungu anajua pa kuiweka Roho ya Marehemu. Maombi yetu hayatabadilisha hilo.Habari Zaidi


Rufftone wapambana na Ringtone
Walipotangaza vita magazeti yote yaliandika. Sasa wanadai kupatana, magazeti yote kimyaaaa!!

Rafftone wakiwa na Ringtone Kisii

Roy Smith Mwatia na Alex Apoko
Ni MARAPA wa Gospel.Usijali majina yao ya Kiluhia na Kikisii, Lakini wanajulikana kama Rufftone na Ringtone.Kila mmoja anadai kumzidi mwenzake katika kurap Gospel.Wanachosahau ni kwamba wote ni mapandikizi ya vyombo vya habari. Siku Media itawaweka chini, Huo utakuwa mwanzo wa mwisho wao.Pengine wajikaze kiusanii wakite mizizi yao wenyewe. Lakini kwa mtindo huu wa kujiona wamefika, tena mbaya zaidi wanajilinganisha na wasanii wa nchi za magaribi wakati unga wa ugali kumudu ni shida,Tunasubiri tuone. Habari Zaidi

Tanzania wabadili pasipoti tena
A country without National IDs, but they keep on changing passports every now and then.
What a SHAME?

Wenye pasi wanatakiwa kuomba upya, na kutimiza masharti yote ikiwa ni pamoja na kulipa shilingi elfu nne za Kenya. Isitoshe kila mwombaji lazima achukuliwe alama za vidole vya mikono yote miwili. Wadadisi wa mambo ya kisiasa wanahoji uhalali wa serikali kubadili pasipoti wakati huu wa uchaguzi. Wengine wanaliona hilo kama mbinu ya serikali ya CCM kutafuta pesa za kuugharamia uchaguzi. Pasipoti ambayo ilikuwa ikigharimu shilingi elfu tano za Tanzania, sasa inagharimu zaidi ya shilingi elfu hamsini za Tanzania. Je mwananchi wa kawaida Tanzania atapata wapi TSHS.50,000? Habari Zaidi

Kimurgor Ameuawa

Aliyekuwa Mlinzi mkuu wa Moi Bwana Kimurgor, ameuawa mjini Nairobi. Commando aliyesomea Israel, pia aliwahi kuwa mkuu wa kikosi cha GSU wakati wa utawala wa Rais mstaafu Moi. Wakati serikali ya Kibaki ilipochukua madaraka, Bwana Kimurgor alistaafishwa na kuwa raia wa kawaida. Mpaka siku ya kufa kwake, alikuwa ofisa ulinzi katika kampuni binafsi ya ndege. Inasemekana kwamba alikuwa akiendesha mwenyewe ndani ya gari yake aina ya TOYOTA PRADO katika mtaa wa Fedha Estate, alipokutana na watu watatu wenye silaha.Aliposimamishwa na watu hao, alihisi hatari na kukaidi amri yao. Aliendesha kasi kuwapita lakini commando safari hii hakuwa na bahati kwani walimfyatulia risasi zilizoyakatiza maisha yake papo hapo.Polisi wameanza msako mkali, huku vyombo vya habari vikiripoti kwamba wauaji wake walikuwa majambazi wa kawaida. Ila hakuna chochote kilichoibiwa kutoka kwa marehemu. Hata silaha yake aina ya pisto ilikutwa ikiwa sawa na risasi kumi na moja ndani yake, jambo linaloonyesha kwamba commando hakuweza kuitumia silaha yake kujikinga na watu waliopania kumuua. Habari Zaidi


MatangazoHabari Zaidi

Aibu Yaifunika Tanzania

Serikali ya Mkapa imefanya kosa la kiistoria pale ilipowafukuza waandishi wa habari wa nchi jirani ya Kenya. Waliyataka wenyewe, na yalipokuja sasa wanayakimbia. Baada ya gazeti la "Mwananchi' kuuzwa kwa kampuni ya 'NATION", Wakenya waliwekeza mabilioni ya dola za Kimarekani katika sekta ya habari na utangazaji nchini Tanzania. Kile ambacho hawakukijua, ni kwamba sekta hiyo haijawahi kuwa huru Tanzania. Walipoanza kuandika habari kulingana na taaluma yao, gazeti la 'Mwananchi' lilianza kuchanja mbuga Tanzania, na kuwa moja kati ya magazeti yanayoongoza nchini humo. Serikali ikaliona hilo. Kama kawaida yao kuthibiti habari, walijaribu kulitumia gazeti la 'Mwananchi" liwapigie debe CCM wakati huu wa uchaguzi. Inasemekana wanataaluma hao waliikatalia serikali usoni, jambo lililosababisha kutimuliwa kwao. Mkapa ameithihirishia dunia kile ambacho walikuwa wakikijua tayari. Kwamba Tanzania hakuna uhuru wa kutoa mawazo. Na kwamba utitiri wa vyombo vya habari Tanzania ni kifunga macho ili jumuia ya kimataifa ione kwamba kuna uhuru wa habari, kumbe asilimia 99 ya vyombo hivyo humilikiwa na serikali pamoja na maajenti wake. Inasemekana Mkapa mwenyewe anamiliki zaidi ya magazeti 8 yakiwemo yale ya kidini ambayo hayaachi kuweka picha yake mbele. Anapomaliza urais na kuirudia kazi yake ya uandishi, Mkapa atakumbukwa kama mwanahabari aliyepata madaraka yakamlevya, kisha akaanza kuwatesa wanahabri wenzake.


Serkali ya Tanzania inaongozwa na wahuni. Usipounga mkono maovu yao, basi watakufanya chochote. Watatumia kila chombo cha dola. Idara ya UHAMIAJI ikiwa mojawapo. Ni kawaida yao. Wamezoea. Na hawapelekwi kokote. Kinachoniumiza moyo, ni mabilioni ya shilingi za Kenya "NATION walizotapeliwa na Serikali ya Tanzania. Kwamba sasa wanawatimua, Mtu anaweza jiuliza kwa nini waliwauzia kampuni hiyo ya "MANANCHI" ikiwa kuwapa vibali ni vigumu? Hata kama wewe ni Mtanzania usishangae kuitwa mkimbizi kutoka Zambia. Wana habari wa "NATION" wako Tanzania kufanya kazi kulingana na taaluma yao na siyo kuipigia debe CCM. Kama Mkapa alifikiri kwamba "NATION" ni "UHURU" na "MZALENDO" magazeti ya chama, atakiona kilichomnyima kuku kutoa maziwa anyonyeshe vifaranga. Namshukuru Mungu kwamba "NATION" wamejionea wenyewe yale ambayo nimekuwa nikiyalalamikia kwa miaka mingi. Kanda yangu ilipigwa marufuku kwa kusema "CCM aliyoanzisha Nyerere imezeeka, Sijui "MWANANCHI" walisema nini. Lakini Wahuni wa DAR, wameanza fujo zao. Safari hii wameuma kubwa kuliko uwezo wao kutafuna. Pengine wateme. Wakimeza itawakwama kooni.Jipeni moyo "NATION" Mungu ni mkuu kuliko CCM na Mkapa mwanahabari anaewatesa wanahabari..Habari Zaidi

Tuzo la Mwanzo wa Mwisho?

Ester Wahome Mwimbaji wa nyimbo za Injili akipokea tuzo la KISIMA kutoka kampuni ya "Nation" Pamoja nae ni mwimbaji wa nyimbo za dansi Saimoni Kihara maarufu kwa jina la Musaimo. Kwamba makanisa yamewatupa waimbaji wao mpaka kufikia hatua ya kupewa tuzo na watu wasio wa Kanisa tena kwenye vilabu vya usiku, hiyo ni aibu kwa Kanisa pamoja na waimbaji wanaokubali kuidhalilisha Injili. Tuzo la waimbaji wa Injili liko mbinguni. Lakini haya matuzo ya kina "Nation" na mengine ya watu 'Wa Kora", yanawafaa wenyewe. Ndio maana kila mwimbaji wa Injili aliyekubali kupewa tuzo za kidunia, inakuwa huo ndio mwanzo wa mwisho wake. Tunaomba mambo yasiwe hivyo kwa Ester Wahome. Habari Zaidi

GTV ON YouTube
Munishi Rais wa Tanzania?


Mchungaji Faustin Munishi amesema hakuna Uchaguzi Tanzania bila Katiba mpya. Akiongea katika Gospel GTV Pastor Munishi alivitaka vyama vya upinzani Tanzania kuususia uchaguzi kwani CCM wakitumia katiba ya sasa wameumaliza upinzani Tanzania. Kwa sasa ni sawa na hakuna upinzani. Kuingia kwenye uchaguzi ambao CCM hawaruhusu wengine waseme, ni sawa na kuwafunga vifaranga wa kuku na kuwashindanisha na mwewe. Matokeo mnayajua. CCM wanajua walichofanya Tanzania kwa miaka zaidi ya arobaini, ndiyo maana wananunua kila mtu. Pesa zilizo haki ya mikoa kimaendeleo, zinatumika kuinunua mikoa iiunge mkono CCM. Alisema lazima Katiba ibadilishwe kuwaruhusu wagombea binafsi ndipo upinzani wa kweli utakapoonekana Tanzania. Alielezea nia yake ya kugombea Urais Tanzania bila chama cha kisiasa. Mchungaji Munishi alisisitiza kwamba "Siasa ni uongo na hawezi kujiunga na uongo ili awatoe waongo." Alisema kwamba endapo CCM watakaidi kuibadili Katiba, basi wafuasi wake watamtangaza rasmi kuwa Rais wa Gospel Tanzania. Kwa mara ya kwanza Tanzania itakuwa na marais zaidi ya kumi. Huko ndiko tunakoelekea ikiwa CCM watawaburuza watanzania kwenye uchaguzi bila KATIBA mpya. Habari Zaidi



Padre Atuhumiwa kwa UBASHA

Padre Sixtus Kimaro Akiwa mahakamani Kisutu Dar.
Ameshitakiwa kwa tuhuma za kumlawiti mvulana wa miaka 17
Kasisi Kimaro alionekana mtulivu Mahakamani, Lakini aliufunika uso wake usichukuliwe picha na Wanahabari waliokuwa wamefurika mahakamani HABARI ZAIDI


Polisi Nairobi wampiga mchungaji risasi: Ni Rev. David Jesse wa Kwanza

Lucy kiboko yao

Haki ya magazeti kuandika, inaishia pale haki ya Lucy kupinga inapoanzia. Tena haki ya Lucy kulala usingizi inaishia pale haki ya jirani yake kusheherekea inapoanzia.
Vyombo vya Habari Kenya vimekiona cha mtema kuni vilivyojaribu kutoka katika mifuko ya wanasiasa ambamo vimekaa kwa muda mrefu. Kama kuonyesha kwamba wamenunuliwa, Lucy Kibaki mke wa rais wa Kenya, aliingia katika jumba la Nation bila woga kwani kwake hilo jumba pamoja na waandishi ndani yake ni mali yake. Anawalipa wasiandike mabaya yake wala mumewe, na alishangaa kuona wamekiuka maagano. Watamsema sana mama Lucy, lakini ukweli unabaki kwamba amewasaidia kuuza magazeti ambayo watu walikuwa wameyasahau kama bado yako. HABARI ZAIDI


 

POLICE ON KILLING MISSION

Wanasema Cheruyot alikuwa muuaji na jambazi hatari. Walipompata, waliwaita waandishi wa habari na kumuua Cheruyot mbele yao. Yaani waandishi wa habari pamoja na Polisi waliungana katika zoezi la kuua. Inawezekana Cheruyot alikuwa muuaji, Lakini hakuwahi kuwaita waandishi wa habari na kuua mtu mbele yao. Kati ya Cheruyot, Polisi na waandishi wa habari, nani MKOMBOZI? Machoni pa Mungu wote ni WAUAJI. Moja kati ya amri za Mungu inasema usiue. Ukiua kwa sababu unayemuua aliua, hiyo haikufanyi wewe usiwe muuaji.

Cheruyot kabla, na baada kuuawa. Habari Zaidi


Censorship turning systematic in Tanzania

Nyerere Aililia CCM akiwa kaburini


Wengine wanakiita Chama Cha Majambazi. Washirikina Wachawi, Wauaji. Chama kilichoharibu maisha ya watanzania kwa zaidi ya miaka arobaini.CCM wanatumia mbinu zote kubaki madarakani. Pesa walizoiba miaka zaidi ya arobaini ndizo wanazotumia kununua kila anayekubali kununuliwa., Je Tufanyeje kuitoa CCM madarakani?
Hotuba ya Munishi kwa TAIFA 'Ujamaa ulishindwa'


Serikali ya Mkapa Tanzania inaamini kwamba Munishi na nyimbo zake ni mwanzo wa kuvurugika kwa amani Tanzania. Kinyume chake ndio sahihi. Amani ilivurugika pale Mkapa alipowaamuru Polisi wawaue Wazanzibari zaidi ya 70 kwa sababu za kisiasa. Majeshi Tanzania walikasirishwa sana na jambo hilo,na walikuwa tayari kuipindua serikali ya Mkapa. Munishi akaimba wimbo "MPENDE ADUI YAKO", Mkapa badala ajue kwamba wimbo huo ulikuwa ukimsaidia yeye ili serikali yake isipinduliwe na kisha afunguliwe mashitaka ya kuwaua raia wasio na hatia, Aliupiga marufuku wimbo huo na kuamuru polisi wamsake Munishi. Iko siku Mkapa atamkumbuka Munishi. Ngoja kipindi chake cha urais kimalizike, na tunaomba kimalizike salama, halafu Mkapa awe raia wa kawaida. Kombe aliyemwamuru amsake Munishi, ndiye atakayeamriwa amtie Mkapa mbaroni ili ajibu mashitaka ya kuua na kupora mali ya umma pamoja na kuiuza nchi kwa makaburu. Habari zaidi


Amerika Wafundishwa Adabu Iraq


Wimbo mpya "Nateseka Natukuza"

Habari na Maelezo:
Watanzania hawana Uhuru wa kutoa maoni.

Hawa wanafanya nini pamoja? Mmoja ni mwanasiasa, na mwingine ni mfanyikazi katika ukumbi wa habari na {MAELEZO Tanzania.}Walinaswa pamoja na mpiga picha wetu kwenye mkutano na waandishi wa habari. HABARI ZAIDI

Munishi jamaa na marafiki miaka 16 iliyopita Katika picha


Redio Injili FM

Sasa unaweza kuisikiliza redio INJILI FM On Line



GTV Online

Gospel Television ambayo Studio zake ziko Nairobi Kenya, Sasa itaanza kurusha matangazo yake kutumia Internet. Mipango yote imekamilika na tuko mbioni kukamilisha ile ya kiufundi ili tuwe Online ulimwenguni kote. Endelea kuutupia macho ukurasa huu. Kwa sasa unaweza kuisikia sauti ya GTV. Habari zaidi

Yesu Anaponya Bure


Habari nyingine MOTO MOTO


DNG, ABURA washinda tuzo la watu wa"KORA"

Habari Zaidi

Usafiri Nairobi-MATATU

Kila kitu ndani ya Matatu ni haraka. Kuingia haraka, kulipa haraka, na kushuka haraka. Ukifika Nairobi usisahau haraka ya Matatu. Wao husema Haraka ina baraka. Sera mpya za usafiri Kenya zinaonekana kuhamisha tatizo kutoka kwenye MATATU na kulihamishia kwenye Treni. Sijui watakapolihamisha kwenye Treni tatizo sugu la usafiri wataliahamishia wapi? Habari zaidi

Nation Lageuka kuwa Gazeti la chama na serikali

Rev.Wachira asema magazeti yanapaswa kuikosoa serikali, kwani hata kama serikali ingeundwa na malaika, bado inahitaji chombo cha kuikosoa isiende mrama. Ni makosa kufikiri kwamba serikali mpya haijafanya makosa. Kwangu tayari wamefanya makosa mengi kwa mwaka mmoja madarakani. Mwaka wa pili utakuwa kuvunja rekodi ya makosa yaliyofanywa na serikali za awali.Tusubiri hadi wavunje rekodi ndipo tuikosoe?
Habari zaidi
Nyerere aliiharibu Tanzania

Mwalimu Nyerere: Sera za ujamaa zilishindwa kabisa Tanzania

"Too appalling this letdown, Ndugu Mkapa"

Mr Philip Ochieng.

Habari Katika Picha

Kiraeli Carol 1989, Munishi 1974, Sister to Kiraeli 1989, Salelo, Mojashi 1995
Contact us/ Tuandikie

Your full Names
Your E-mail
Subject
Message
   
   

Twende nikutembeze Nairobi



Siku ya kufa Nyani miti yote huteleza. CCM ni Nyani ambaye siku ya kufa kwake imekaribia. Haijalishi uhodari wa CCM kuparamia miti zaidi ya miaka arobaini, lakini safari hii miti yote inateleza. Watapigiza chini kwa kishindo, na huo ndio utakuwa mwisho wao. Watanzania tunataka ENZI MPYA bila CCM Habari Zaidi

Soma Magazeti ya kila siku Hapa

Nation Media
Nation Kenya


IPPMedia TZ


BCSTIMES TZ


Standard Kenya



Vision Uganda


Monitor Uganda

Matangazo
Kifo

Biashara

Study The Bible

Passage (eg. John 3:16):

Search word(s) (eg. saved):


Read Bible



Faustin Munishi Tell. 25472602445 Nairobi Kenya East Africa
E-mail: fmunishi@hotmail.com  |  munishifaustin@yahoo.com

Check mail at Hotmail
Check Mail at Yahoo